Ligi Kuu Thread

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

YANGA KUCHEZA NA NAMUNGO KABLA YA KUIVAA SIMBA​


VIGOGO, Yanga SC watakuwa na mechi moja zaidi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara wiki ijayo kabla ya kukutana na mahasimu wao, Simba SC mwisho wa mwezi.
Yanga watamenyana na Namungo FC Jumamosi ya Aprili 23, kabla ya kukutana na mabingwa watetezi, Simba SC Jumamosi ya Aprili 30, mechi zote zikipigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

REFA KOMBA KUWACHEZESHA MAMELODI LIGI YA MABINGWA​


SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemteua refa Frank Komba wa Tanzania kuwa miongoni mwa waamuzi watakaochezesha mchezo wa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika, baina ya wenyeji, Mamelodi Sundowns na Petro Atlètico ya Angola Aprili 24, mwaka huu Uwanja wa FNB Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.


Kwa upande wake, Meneja Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto ameteuliwa na CAF kuwa Mratibu (General Coordinator) wa mchezo wa Robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Al-Masry SC na RS Berkane Ya Morocco Aprili 17, mwaka huu nchini Misri.


Naye Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo ameteuliwa kuwa Ofisa Habari wa mchezo wa Robo fainali Kombe la Shirikisho baina ya wenyeji, Simba SC na Orlando Pirates ya Afrika Kusini Aprili 17 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

NAMUNGO YAICHAPA RUVU 3-1 ILULU​


WENYEJI, Namungo FC wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Mabao ya Namungo FC yamefungwa na David Molinga ‘Falcao’ dakika ya 11, Hashim Manyanya dakika 35 na Emmanuel Charles dakika ya 88, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Saadat Mohamed dakika ya 64.
Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 20 na kupanda nafasi ya tatu, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 21 za mechi 20 pia nafasi y 12.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, bao la Oscar Paul dakika ya saba limeipa Tanzania Prisons limeipa ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Prisons inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 20, ingawa inabaki nafasi ya 15, ikiizidi pointi Mbeya Kwanza baada ya wote kucheza mechi 20.
Ikumbukwe mwishoni mwa msimu timu mbili zitashuka moja kwa moja na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MTIBWA SUGAR YAIBAMIZA DODOMA JIJI 2-1 JAMHURI​


WENYEJI, Dodoma Jiji FC jana wamechapwa mabao 2-1 na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Mtibwa Sugar yalifungwa na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ dakika ya tisa na Mururi Mayanja Brian dakika ya 26, wakati bao pekee la Dodoma Jiji lilifungwa na Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 83.
Mtibwa Sugar inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 21 na kusogea nafasi ya nne, wakati Dodoma Jiji FC wanabaki na pointi zao 21 za mechi 21 sasa nafasi ya 14.
Katika mchezo uliotangulia Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, wenyeji Kagera Sugar walilazimishwa sare ya 0-0 na KMC.
Kagera Sugar inafikisha pointi 26 nafasi ya tano na KMC pointi 24 nafasi ya nane baada ya wote kucheza mechi 20.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

TFF YAPANGUA KAMATI ZOTE ZA MAREFA​



KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imefanya marekebisho kadhaa katika Kamati za uongozi za Marefa ili kuboresha viwango vyao katika uchezeshaji wa mechi.




Nassor Hamdoun wa Kigoma (kushoto), ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi, Alfred Lwiza wa Mwanza ni Mjumbe wa Kamati Ndogo ya Kutunga Sheria. Mwingine katikati ni Marehemu Said Almasi wa Mwanza pia enzi zao wanachezesha miaka ya 1990.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MBEYA KWANZA YAICHAPA COASTAL UNION 2-0 SONGEA​


WENYEJI, wahamiaji Mbeya Kwanza wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Mabao ya Mbeya Kwanza leo yamefungwa na Hamisi Kanduru dakika ya 26 na Willy Edgar dakika ya 90 na kwa ushindi huo inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 21, ingawa inaendelea kushika mkia katika ligi ya timu 16, ikizidiwa pointi moja na ndugu zao, Tanzania Prisons ya Mbeya nayo, ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Coastal Union baada ya kipigo cha leo inabaki na pointi zake 21 za mechi 21 na kushukia nafasi ya 14.
Mbali ya timu mbili kushuka moja kwa moja mwishoni mwa msimu, mbili zitakwenda kucheza na timu za Championship kuwania
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

GEITA GOLD YAILAMBA KMC 2-0 NYANKUMBU​


WENYEJI, Geita Gold wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
Mabao ya Geita Gold ya kocha Freddy Felix Minziro yamefungwa na Amos Charles dakika ya 48 na George Mpole dakika ya 75 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 27 katika mchezo wa 20 na kupanda nafasi ya tano, ikizidiwa pointi moja na Azam FC ambayo hata hivyo ina mechi moja mkononi.
KMC baada ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 24 za mechi 21 ikishukia nafasi ya tisa.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

YONDAN NA NABI WAFUNGIWA, REFA YANGA NA GEITA KIKAANGONI TFF​



BEKI wa Geita Gold, Kelvin Yondan amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Sh. Milioni 1 kwa kosa la kumchezea rafu ya makusudi mshambuliaji wa Yanga, Mkongo Fiston Kalala Mayele kwenye mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).



 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

DODOMA JIJI YAZINDUKA, YAICHAPA MBEYA CITY 2-1​

WENYEJI, Dodoma Jiji jana wamezinduka na kuichapa Mbeya City ambao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mabao ya Dodoma Jiji yalifungwa na Augustine Nsata dakika ya pili na Seif Abdallah Karihe dakika ya 25, wakati la MCC lilifungwa na Samson Madeleke dakika ya 41.
Dodoma Jiji inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 21 na kusogea nafasi ya 10, wakati Mbeya Kwanza City inabaki na pointi zake 25 za mechi 20 sasa nafasi ya saba.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

KAYOKO KUCHEZESHA PAMBANO LA WATANI JUMAMOSI​



REFA Ramadhani Kayoko ndiye atakayepuliza kipyenga kwenye mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kayoko atasaidiwa na Frank Kombe, wote wa Dar es Salaam na Mohamed Mkono wa Tanga.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MBEYA KWANZA YAICHAPA TANZANIA PRISONS 1-0​


BAO la penalti la Deo Minga dakika ya 75 limetosha kuipa Mbeya Kwanza ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons leo Uwanja wa Maji Maji mjini Songea mkoani Ruvuma.
Mbeya Kwanza inafikisha pointi 21 katika mchezo wa 22 nafasi ya 15 kwenye ligi ya timu 16, ikiizidi wastani wa mabao tu Coastal Union inayoshika mkia, ingawa ina mechi moja mkononi.
Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 22 za mechi 22 sasa nafasi ya 14.
Ikumbukwe timu mbili zitateremka daraja mwishoni mwa msimu na mbili zitakwenda kucheza na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

RAIS SAMIA KUPOKEA KOMBE HALISI LA DUNIA​


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atalipokea rasmi na kulishika, Kombe la Dunia linalotarajia kuwasili nchini Mei 31, mwaka huu.
Kwa mujibu wa sheria za FIFA, ni Mkuu wa nchi pekee ndiye anayeruhusiwa kulishika kombe hilo, wengine watastahili Chu kulitazama na kupiga nalo picha.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ziara ya Kombe la Dunia nchini Tanzania, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, alisema kuwa Ujio wa Kombe nchini upo chini ya Kampuni ya vinywaji ya Coca cola.
“Napenda kuchukua fursa hii kuipongeza Coca-Cola kwa dhamira yake ya makusudi ya kuendelea kusaidia sekta ya soka na michezo kwa ujumla.
Fursa ya kuandaa ziara ya kombe hilo ni ishara ya kuiamini nchi yetu kuwa inapenda soka”."Ziara ya kombe itaiweka nchi yetu kwenye ramani ya kimataifa, kwa siku mbili kombe litakuwa hapa, dunia nzima itaiangalia nchi yetu.
Ningependa kuwahakikishia ushirikiano wetu na Coca-Cola wakati wote wa kampeni hii na hata kombe linapokuja na kuondoka. Pia nizisihi timu zetu za soka zichukue ziara ya kombe hili kama chachu ya kuwatia moyo kuweka juhudi zaidi na kuhakikisha kuwa ndoto yetu ya siku moja kushiriki mashindano ya kombe la dunia inatimia” aliongeza Mchengerwa.
Akizungumzia faida ya ziara ya kombe la Dunia katika maendeleo ya sekta ya michezo na Tanzania ni miongoni mwa mataifa 54 duniani na 9 barani Afrika kulikaribisha Kombe la Dunia chini ya ushirikiano wa Coca-Cola.
Wakati dunia ikisubiri kwa hamu mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA 2022 nchini Qatar mwezi Novemba, mashabiki wa soka na watumiaji wa Coca-Cola nchini Tanzania wanatarajiwa kuungana na nchi 54 duniani kote kulikaribisha Kombe la Dunia la FIFA nchini tarehe 31 Mei na Juni Mosi mwaka huu.
Kampuni ya Coca-Cola kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Duniani FIFA itawapa mashabiki wa soka nchini Tanzania fursa ya kipekee ya kuiona tunzo ya ngazi ya juu inayotamaniwa zaidi na wapenda soka duniani kwa kupata nafasi ya kupiga nayo picha wakati wa ziara yake.
Tanzania ni miongoni mwa nchi 54 duniani na tisa barani Afrika kupata fursa ya kuwa mwenyeji wa ziara ya kombe hilo baada ya miaka 8.
Ziara hiyo ni sehemu ya utamaduni wa Coca-Cola kusherehekea na kushiriki furaha ya kila mashindano ya Kombe la Dunia na mashabiki pamoja na watumiaji wake kupitia ushirikiano wake wa muda mrefu na FIFA.
"Huu ni wakati mzuri kwa bidhaa yetu, watumiaji na mashabiki wa soka nchini Tanzania, tunaposhiriki msisimko na kusherehekea kumbukumbu zilizoletwa na ziara ya Kombe la Dunia.
Hili litakuwa kombe la awali litakalowasilishwa kwa timu itakayoshinda nchini Qatar na tunafuraha kuwa sehemu ya masoko yaliyochaguliwa kuwa sehemu ya wakati huu wa kipekee,” alisema Unguu Sulay, Mkurugenzi Mkuu wa Coca-Cola Kwanza Tanzania.
"Kombe la Kombe la Dunia la FIFA linaleta matukio ya kukumbukwa na kusisimua zaidi kwa watumiaji wetu na mashabiki wa soka hapa baada ya miaka 8 tangu kombe hilo kuja Tanzania.
Tunaelewa jukumu la soka katika kuunganisha mamilioni ya Watanzania na ni wakati mzuri sana ambao tunauenzi na kuuthamini,” aliongeza Unguu Sulay.
Kombe la Dunia linatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere Mei 31 majira ya saa 11 asubuhi. Litakaribishwa na viongozi mbalimbali wa serikali na michezo akiwemo Waziri wa Michezo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, na uongozi wa Coca-Cola Tanzania.
Baada ya kutua, viongozi wachache wa serikali na wageni waliochaguliwa wataruhusiwa kutazama kwanza kabla ya msafara huo kuelekea Ikulu.
Mara ya mwisho kombe hilo kuzuru Tanzania ilikuwa mwaka 2013 ambapo liliandaliwa na aliyekuwa Rais wa nne wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Akizungumzia faida ya ziara ya kombe la Dunia katika maendeleo ya sekta ya michezo nchini Tanzania, Rais wa Shirikisho la SokaTanzania (TFF), Wallace Karia alisema:
“Kwa miaka mingi, Coca-Cola imekuwa mshirika wetu mkubwa katika kuendeleza soka na michezo nchini Tanzania. Sio tu kupitia ufadhili lakini pia kuanzisha mojawapo ya mashindano ya soka ya vijana kote nchini, 'Copa Coca-Cola'.
Michuano hiyo ilifungua milango kwa maelfu ya vipaji vya soka nchini Tanzania ambavyo leo vinatamba katika klabu kadhaa za soka za Ligi Kuu na Timu ya Taifa. Tunafurahi kwamba matukio muhimu kama ziara ya kombe la Dunia ni sehemu ya historia yetu kwenye soka.
Tofauti na miaka ya nyuma, watumiaji na mashabiki wa soka watakaopata fursa ya kulitazama kombe hilo na kupiga nalo picha na pia watakaochaguliwa kupitia uanzishaji wa mtandaoni ambapo watumiaji 2000 pekee ndio watapata nafasi ya kujishindia tiketi za dhahabu za VIP kuhudhuria utazamaji wa kombe hilo.Michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2022 itafanyika nchini Qatar kuanzia Novemba 21 hadi Desemba 18.
Afrika itawakilishwa na nchi tano katika mashindano hayo ambazo ni Senegal, Ghana, Morocco, Tunisia, na Cameroon.Kuhusu Ziara ya Kombe la Dunia la FIFAKombe Halisi la Dunia la FIFA hutunukiwa mshindi huku likibakia mikononi mwa FIFA.
Kombe hili limeundwa kwa dhahabu yenye uzito wa kilo 6.142, iliyoundwa kama muundo wa watu wawili wanaoshikilia ulimwengu juu yao. Muundo wa sasa wa Kombe Halisi ni wa mwaka 1974. Kama moja ya alama za michezo zinazotambulika zaidi duniani.
Kombe la Dunia la FIFA linaweza tu kuguswa na kushikiliwa na kikundi maalum cha watu ambacho kinajumuisha washindi wa zamani wa FIFA.
Kwa sababu kanuni zinasema kuwa Mashindano ya Kombe la Dunia ya FIFA yatabakia mikononi mwa FIFA.
Ziara ya Kombe la Dunia ni fursa ya kipekee kwa watu kuchukua sehemu ya historia ya soka na kushiriki mapenzi yao kwa ajili ya mchezo huo.
Hisia za kuona Kombe la Dunia la FIFA zitabaki kwenye kumbukumbu za mashabiki wa soka kwa muda mrefu.Kuhusu Kampuni ya Coca-ColaKampuni ya Coca-Cola ndiyo kampuni kubwa zaidi ya vinywaji duniani, inayoburudisha watumiaji.
Ikiongozwa na Coca-Cola, mojawapo ya bidhaa zenye thamani kubwa na zinazotambulika duniani, kampuni yetu ina bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 21, 19.
Bidhaa hizo ni pamoja na Diet Coke, Coca-Cola Zero, Fanta, Sprite, Dasani, vitaminwater, Powerade, Minute Maid, Simply, Del Valle, Georgia, na Gold Peak. Kupitia mfumo mkubwa zaidi wa usambazaji wa vinywaji duniani, sisi ni watoa huduma namba moja wa vinywaji vinavyometa.
Vinywaji vyetu hufurahiwa na watumiaji katika zaidi ya nchi 200 kila siku.Kampuni yetu inaangazia kuunda mazingira salama, jumuishi ya kazi kwa washirika wetu, na kuimarisha maendeleo ya kiuchumi.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

GWIJI WA UFARANSA, TREZEGUET KUMLETA MWALI WA QATAR 2022​


MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, David Trezeguet anatarajiwa kuwasili nchini na Kombe halisi la Dunia la FIFA Mei 31, mwaka huu.
Kwa mara ya nne mfululizo Tanzania imefanikiwa kuwa kati ya nchi 9 za Afrika ambazo kombe la Dunia litakuja nchini.
Akizungumza jana katika uzinduzi wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Coca cola nchini, Unguu Sulay alisema kwa mara nyingine Tanzania imefanikiwa kupata tiketi ya kulishuhudia kombe hilo kabla ya kuelekea nchini Qatar katika fainali za mwaka huu.
Sulay alisema ziara hiyo ni muendelezo wa kampuni yao kurudisha kiu na mipango ta Tanzania katika kusaka tiketi ya kushiriki kwa mara ya kwanza fainali hizo katika miaka ya baadaye.
"Sio kila Taifa linapata hii nafasi,Tanzania imekuwa ni tofauti tumepata nafasi hii kwa mara ya nne kulipokea kombe hili halisi na watu kupata nafasi ya kupiga nalo picha," alisema Sulay.





"Kombe hili litakuwa hapa nchini kwa siku mbili kuanzia Mei 31 na Juni Mosi na huu ni muendelezo wa kampuni yetu sio tu kuishia kuburudisha kupitia vinywaji bora lakini pia kujihusisha na moja kwa moja na msisimko wa kimichezo kupitia soka na burudani.
Naye mgeni rasmi katika uzinduzi huo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohammed Mchengerwa, robo tatu ya Watanzania wanapenda michezo na ziara hii inakuja kuwapa fursa watu wengi wenye rika tofauti kushuhudia kombe hili ambalo Tanzania inafanikisha ndoto za kuandaa fainali hizi.
"Serikali na wizara yetu ya michezo imefarijika na ziara hii ikiwezeshwa na ninyi Coca cola, Rais wetu (Samia Suluhu Hassan) anapenda michezo na tuna ndoto za siku moja tuje kuandaa fainali hizi ingawa kwanza tunatakiwa kuamini inawezekana na baada ya hapo tujenge miundo mbinu kama vile viwanja," alisema Mchengerwa....
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia alisema ziara hii ya kombe hili ni muendelezo wa ushirikiano bora kati ya kampuni hiyo na TFF katika maendeleo ya mpira.
" Coca cola imekuwa na mkono mzuri katika kuendeleza soka, sijui kama watu wanafahamu timu yetu ya Taifa Stars ya sasa ina wachezaji wengi ambao walizalishwa na mkakati wa kuzalisha vijana uliodhaminiwa na kampuni hii na ukaleta matunda bora kwa Taifa letu,"alisema Karia.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA NA YANGA ZATOZWA FAINI KWA MAKOSA TOFAUTI​



KLABU za Simba na Yanga zimetozwa faini kwa makosa mbalimbali ya kikanuni katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina yao ulionalizika kwa sare ya 0-0 Jumamosi iliyopita Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.




 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

NAMUNGO FC YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA SIMBA LINDI​


WENYEJI, Namungo FC wamelazimishwa sare ya 2-2 na mabingwa watetezi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Mabao ya Namungo ambayo mara mbili ilitangulia dhidi ya wazoefu wa Robo Fainali ya michuano ya klabu Afrika yamefungwa na Jacob Masawe dakika ya nane na Mzambia Obrey Chirwa dakika ya 54, wakati ya Simba yamefungwa na Shomari Kapombe dakika ya 42 na Kibu Dennis dakika ya 79.
Namungo wanafikisha pointi 30 katika mchezo wa 32, ingawa wanabaki nafasi ya tatu wakizidiwa pointi 13 na Simba ambao imecheza mechi ya 21 leo sawa na watani wao, Yanga wanaoongiza Ligi kwa pointi zao 55.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

RASMI, DTB NI TIMU YA LIGI KUU MSIMU UJAO​



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeithibitisha klabu ya DTB ya Dar es Salaam kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu unaitwa, 2022-2023.
Hiyo ni baada ya DTB kufikisha pointi 65 kileleni mwa Championship, tatu zaidi ya Ihefu inayofuatia na nane zaidi ya Kitayosce inayoshika nafasi ya tatu kuelekea mechi mbili za nwisho.
Timu mbili za juu Championship zitapanda Ligi Kuu moja kwa moja na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Ligi Kuu kuwani kupanda.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

COASTAL UNION YAICHAPA POLISI 1-0 MKWAKWANI​


WENYEJI, Coastal Union wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Bao pekee la Coastal Union limefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 21 na kwa ushindi huo Wagosi wa Kaya wanafikisha pointi 24 katika mchezo wa 22 na kupanda nafasi ya 12 kutoka mkoani.
Polisi Tanzania inabaki na pointi zake 25 za mechi 21 nafasi ya 10.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

RUVU SHOOTING YAICHAPA GEITA GOLD 2-1 MABATINI​


WENYEJI, Ruvu Shooting wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Mabao ya Ruvu Shooting yamefungwa na Hamad Majimengi dakika ya 53 na Elias Maguri dakika ya 87 baada ya Geita Gold kutangulia na bao la Offen Chikola dakika ya 24.
Kwa ushindi huo, Ruvu Shooting inafikisha pointi 25 katika mchezo wa 23 na kusogea nafasi ya 13, wakati Geita Gold inabaki na pointi zake 31 za mechi 23 sasa nafasi ya tano.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

KMC YACHAPA MTIBWA SUGAR 3-2 UHURU​


WENYEJI, KMC wameibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mchana wa leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya KMC yamefungwa na Matheo Anthony mawili dakika ya 21 na 81 na Hassan Kessy dakika ya 73, wakati ya Mtibwa Sugar yamefungwa na George Makang'a dakika ya 13 na Ismail Mhesa kwa penalti dakika ya 41.
Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 27 na kusogea nafasi ya 10, wakati Mtibwa Sugar inabaki na pointi zake 27 nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 23, wakitofautiana tu wastani wa mabao.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

KICHUYA APIGA ZOTE MBILI NAMUNGO YAILAZA BIASHARA 2-1 NYAMAGANA​



NAMUNGO FC imewachapa wenyeji, Biashara United mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Mabao ya Namungo FC yote yamefungwa na Shiza Ramadhani Kichuya dakika ya tisa na 67, wakati la Biashara United limefungwa na Ambroce Awio dakika ya 85.
Namungo FC inafikisha pointi 36 na kupanda nafasi ya tatu, ikiizidi pointi mbili Geita Gold baada ya wote kucheza mechi 24, wakati Biashara United inabaki na pointi zake 23 za mechi 24 sasa ikishukia nafasi ya 13.
Ligi Kuu inashirikisha jumla ya timu 16 na mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.