Usiku wa kuamkia leo kiungo wa Manchester city na timu ya taifa ya Hispania Rodri ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia ( BALLOON D'OR).Lakini maswali yamekuwa mengi kwanini Rodri na sio Vinicius Jr kama wengi walivyotarajia, hapa nimekusogezea baadhi ya vigezo vinavyoyumikia kumchagua mchezaji bora wa Dunia.
INDIVIDUAL PERFORMANCE ( Uwezo binafsi) Kwenye eneo hili Rodri amekuwa na kiungo bora sana akiwa na timu ya Taifa hata Klabu, amekuwa na muendelezo wa kiwango chake kile kile.
ACHIEVEMENT ( Mafanikio) Ukiachana na uwezo mkubwa ambao Rodri ameonyesha uwanjani,pia ni mchezaji ambaye amefanikiwa kwa upande wa kutwaa Mataji mengi ngazi ya Klabu na timu ya Taifa.Msimu uliyopita ametwaaa EPL, UEFA Super Cup, Euro akiwa na Hispania, Mchezaji bora wa mashindano ya Euro 2024, Klabu bingwa ya Dunia ngazi ya Klabu.Ukilinganisha na Vinicius Jr ambaye ameshinda UEFA na Laliga pekee huku kwenye ngazi ya timu ya Taifa akiwa hajatoa mchango mkubwa..
CLASS AND FAIR PLAY ( Daraja la kiwango na Uungwana Mchezoni)Kwenye upande wa daraja Rodri kwenye eneo la kiungo mkabaji amekuwa kwenye muendelezo wa kiwango kiasi Cha kukosekana kwake uwanjani unaona Manchester city inayumba kwenye eneo hilo au Hispania inavuja kwenye eneo la kati.Lakini upande wa Uungwana Rodri amempiga gape kubwa Vinicius Jr ambaye mara nyingi amekuwa akiingia kwenye migogori na wachezaji wengine uwanjani.
So far kwa upande wangu Rodri amestahili kutwaa tuzo hiyo, lakini pia ameenda kubadilisha mitazamo ya watu wengi ya kuamini mchezaji anayecheza eneo la ukabaji ni ngumu kushinda Ballon d'or, mara ya mwisho alishinda Fabio Cannavaro mwaka 2006.Lakini Rodri anakuwa Mhispania wa kwanza baada ya miaka 64 kupita kutwaa tuzo hiyo kubwa duniani.

Last edited: