Rodri Abeba BALLON D'OR Mbele Ya Vinny Jr | Una Lipi La Kuzungumza Mwana Kijiweni?

Kijiweni

Administrator
Staff member
Nov 7, 2022
489
643
125
Usiku wa kuamkia leo kiungo wa Manchester city na timu ya taifa ya Hispania Rodri ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Dunia ( BALLOON D'OR).Lakini maswali yamekuwa mengi kwanini Rodri na sio Vinicius Jr kama wengi walivyotarajia, hapa nimekusogezea baadhi ya vigezo vinavyoyumikia kumchagua mchezaji bora wa Dunia.

INDIVIDUAL PERFORMANCE ( Uwezo binafsi) Kwenye eneo hili Rodri amekuwa na kiungo bora sana akiwa na timu ya Taifa hata Klabu, amekuwa na muendelezo wa kiwango chake kile kile.

ACHIEVEMENT ( Mafanikio) Ukiachana na uwezo mkubwa ambao Rodri ameonyesha uwanjani,pia ni mchezaji ambaye amefanikiwa kwa upande wa kutwaa Mataji mengi ngazi ya Klabu na timu ya Taifa.Msimu uliyopita ametwaaa EPL, UEFA Super Cup, Euro akiwa na Hispania, Mchezaji bora wa mashindano ya Euro 2024, Klabu bingwa ya Dunia ngazi ya Klabu.Ukilinganisha na Vinicius Jr ambaye ameshinda UEFA na Laliga pekee huku kwenye ngazi ya timu ya Taifa akiwa hajatoa mchango mkubwa..

CLASS AND FAIR PLAY ( Daraja la kiwango na Uungwana Mchezoni)Kwenye upande wa daraja Rodri kwenye eneo la kiungo mkabaji amekuwa kwenye muendelezo wa kiwango kiasi Cha kukosekana kwake uwanjani unaona Manchester city inayumba kwenye eneo hilo au Hispania inavuja kwenye eneo la kati.Lakini upande wa Uungwana Rodri amempiga gape kubwa Vinicius Jr ambaye mara nyingi amekuwa akiingia kwenye migogori na wachezaji wengine uwanjani.

So far kwa upande wangu Rodri amestahili kutwaa tuzo hiyo, lakini pia ameenda kubadilisha mitazamo ya watu wengi ya kuamini mchezaji anayecheza eneo la ukabaji ni ngumu kushinda Ballon d'or, mara ya mwisho alishinda Fabio Cannavaro mwaka 2006.Lakini Rodri anakuwa Mhispania wa kwanza baada ya miaka 64 kupita kutwaa tuzo hiyo kubwa duniani.
 
Last edited:
  • Like
Reactions: Scalion
Aug 3, 2024
12
3
5
𝗸𝘄𝗮𝗻𝗴𝘂 𝗺𝗶𝗺𝗶 𝗥𝗢𝗗𝗥𝗜 𝗮𝗹𝗶𝘀𝘁𝗮𝗵𝗶𝗹𝗶 𝗸𝗮𝗯𝗶𝘀𝗮 𝗵𝗮𝗺𝗻𝗮 𝗵𝘂𝗷𝘂𝗺𝗮 𝗶𝗹𝗶𝘆𝗼𝗳𝗮𝗻𝘆𝗶𝗸𝗮 𝗵𝗮𝗽𝗼 𝗛𝗶𝘀𝗶𝗮 𝗭𝗲𝘁𝘂 𝗻𝗱𝗶𝗼 𝘇𝗶𝗻𝗮𝗳𝗮𝗻𝘆𝗮 𝘁𝘂𝗼𝗻𝗲 𝗞𝘄𝗮𝗺𝗯𝗮 𝗺𝗱𝗼𝗴𝗼 𝗩𝗶𝗻 𝗷𝗿 𝗸𝗮𝗼𝗻𝗲𝗮 𝗯𝘂𝘁 𝘀𝗶𝗼 𝗸𝘄𝗲𝗹𝗶😎👊👊
 

Scalion

Mgeni
Sep 21, 2024
6
3
5
Kwakweli hiyo ipo wazi kwamba Rodri amestahili kutwaa hiyo tuzo kwasababu amekuwa na mchango mkubwa sana katika club yake na timu yake ya taifa kwangu mimi sipingi kutwaa kwake hiyo tuzo
 

Scalion

Mgeni
Sep 21, 2024
6
3
5
Watazamaji wa mpira wote tunajua vini ndo alistahili. ilikuwa wazi sana. hizi tuzo hazijaanza kuwa za kishenzi leo wala jana kwaio hatushangai
Mmhhh unaeza kunielezea japo kidogo Jr kwafanya kipi hii misimu kilicho mzidi Rodri?

Mimi binafsi nilitamani Jr Abebe hiyo tuzo lakini huo unakuwa ushabiki na sio mpira ndugu yangu angalia mchango wao hawa wawili wanapo kuwa kwenye timu za taifa na kwenye club zao
 

briX

Mgeni
Oct 29, 2024
5
3
5
kama ishu ni makombe na mafanikio wangempa carvajal. na ka timu ya taifa ina mchango mkubwa kiivo 2010 wangempa iniesta au sneijder. ivo vigezo hawaviangalii ata waache siasa. mpira tunaangalia wote
 
  • Like
Reactions: Baba Wawili

briX

Mgeni
Oct 29, 2024
5
3
5
v
Mmhhh unaeza kunielezea japo kidogo Jr kwafanya kipi hii misimu kilicho mzidi Rodri?

Mimi binafsi nilitamani Jr Abebe hiyo tuzo lakini huo unakuwa ushabiki na sio mpira ndugu yangu angalia mchango wao hawa wawili wanapo kuwa kwenye timu za taifa na kwenye club zao
Vini alishinda mchezaji bora uefa. rodri akiwepo. Rodri hakuwa ata mchezaji bora kwa city msmu ulopita wote tunajua foden ndo aliibeba timu. Kwa upande wa madrid wote tunajua ndo aliibeba timu kupata mafanikio yote walioipata. vitu viko wazi ivi
 
Oct 28, 2024
2
2
5
vin jr hajastahili bana, ni mchezaji mzuri ila kuna vijitabia ambavyo kimsingi sio sawa kwenue soka. na akiendelea hivi atalisikia tuu hilo dude kwenye bomba. to me Rodri alistahili hii tuzo
 
Aug 3, 2024
12
3
5
𝗛𝗮𝗿𝗮𝗳𝘂 𝗸𝗶𝘁𝘂 𝗺𝘀𝗶𝗰𝗵𝗼 𝗸𝗶𝗷𝘂𝗮 𝗯𝗮𝗿𝗼𝗻 𝗛𝗶𝗶 𝗶𝗻𝗮𝗽𝗶𝗴𝗶𝘄𝗮 𝗸𝘂𝗿𝗮 𝗸𝘄𝗮 𝘄𝗮𝗹𝗶𝗼 𝗳𝗮𝗻𝘆𝗮 𝘃𝘇𝘂𝗿𝗶 𝗦𝗼 𝗡𝗶 𝘀𝘂𝗮𝗹𝗮 𝗹𝗮 𝘄𝗮𝘇𝗶 𝘄𝗮𝘁𝘂 𝗪𝗮𝗺𝗲𝗽𝗶𝗴𝗮 𝗸𝘂𝗿𝗮 𝗸𝘄 𝗸𝗶𝗷𝗮𝗻𝗮 𝗥𝗼𝗱𝗿𝗶 𝗩𝗶𝗻 𝗮𝗻𝗮 𝗸𝗮𝘂𝗹𝗶 𝗺𝗯𝗼𝘃𝘂 𝗻𝗮 𝗹𝗮𝘄𝗮𝗺𝗮 𝗻𝘆𝗶𝗻𝗴𝗶 𝗮𝗻𝗮𝗷𝗶𝗼𝗻𝗮 𝘀𝗮𝗻𝗮 𝘂𝘆𝘂 𝗱𝗼𝗴 𝗻𝗱𝗶𝗼 𝗺𝗮𝗮𝗻𝗮 𝗻𝗶 𝘃𝗶𝗴𝘂𝗺𝘂 𝗸𝘂𝗺𝗽𝗮 𝗸𝘂𝗺𝗽𝗮 𝗸𝘂𝗿𝗮 𝗷𝘂𝘇 𝗸𝗮𝗺𝘄𝗮𝗺𝗯𝗶𝗮 𝗽𝗲𝗱𝗿𝗶 𝗮𝘁𝗮𝗰𝗵𝘂𝗸𝘂𝗮 𝗯𝗮𝗿𝗼𝗻 𝗸𝗮𝗺𝗮 𝘆𝗮 𝗯𝗮𝗯𝗮 𝗮𝗸𝗲 𝘃𝗶𝗹𝗲😂
 

Rweyemamu

Mgeni
Jun 9, 2024
16
4
5
Kuna mwamba anaitwa Martinez wa Inter msimu uloisha kakiwasha sana seria A na copa America lkn haonwi sijui ndio mambo ya nyota daaah