Simba Sports Club Thread

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA SC YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-0 DAR​


MABINGWA watetezi, Simba SC wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba yamefungwa na washambuliaji wake wa Kimataifa wa Tanzania, Kibu Dennis dakika ya 13 na Nahodha, John Bocco dakika ya 29 wote wakimalizia pasi za kiungo Mzambia, Rally Bwalya.
Kwa ushindi huo, Simba was SC inafikisha pointi 49, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi nane na watani wao, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 23, wakati Kagera inabaki na pointi 29 mechi 23 nafasi ya saba.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
𝐓𝐀𝐀𝐑𝐈𝐅𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐔𝐌𝐌𝐀. #NguvuMoja

FSoh4pIWQAMvuXY
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

SIMBA SC YAPIGWA FAINI MILIONI 23 KWA USHIRIKINA​


SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika (CAF) limeipiga Klabu ya Simba faini ya dola za Kimarekani 10,000 zaidi ya Sh. Milioni 23.2 za Tanzania.
Adhabu hiyo imetokana na Simba kufanya vitendo vya kishirikina kwenye ya marudiano Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Orlando Pirates Uwanja we Orlando Pirates Jijini Johannesburg, Afrika Kusini.
Simba ilitolewa kwa penalti 4-3 baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani.
Tayari Orlando Pirates imeingia Fainali baada ya kuitoa na Al Ahly Tripoli ya Libya kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 2-0 ugenini na kufungwa 1-0 nyumbani.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

GEITA GOLD YALAZIMISHWA SARE NA SIMBA 1-1 KIRUMBA​


WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya 1-1 na mabingwa watetezi, Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Dar es Salaam.
Geita Gold walitangulia kwa bao la mshambuliaji wake mahiri, George Enock Mpole dakika ya, kabla ya mshambuliaji mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya 20 Kongo (DRC), Kibu Dennis Prosper kuisawazishia Simba dakika ya 28.
Simba inafikisha pointi 51, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi 12 na watani, Yanga, wakati Geita Gold inatimiza pointi 35, nayo inabaki nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 25.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

SIMBA SC YAMTUPIA VIRAGO KOCHA PABLO​



KLABU ya Simba imeachana na kocha wake, Mspaniola Pablo Franco Martin baada ya makubaliano ya pande zote MBILI na kuelekea mechi zilizobaki kumalizia msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara timu itakuwa chini ya kocha Msaidizi, Suleiman Matola.
Pamoja na Pablo aliyejiunga na timu hiyo Novemba mwaka jana, Simba pia imeachana na kocha wa mazoezi ya viungo Daniel De Castro Reyes ambaye pia ni Mspaniola.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

KIBU DENNIS MCHEZAJI BORA SIMBA MEI​


MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Kibu Dennis Prosper ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Simba mwezi Mei.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

FUNDI RALLY BWALYA ALIBYOAGWA SIMBA SC​


KOCHA wa Simba, Suleiman Matola akimkabidhi jezi maalum kwa ishara ya kumuaga kiungo Mzambia, Rally Bwalya baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo dhidi ya KMC Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Bwalya anaondoka Simba kwenda kujiunga na Amazulu ya Afrika Kusini baada ya misimu miwili ya kuwa na Wekundu wa Msimbazi na ameaga vizuri akiisaidia timu kushinda 3-1 leo.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

SIMBA SC YAICHAPA KMC 3-1 BENJAMIN MKAPA​


MABINGWA wa zamani, Simba SC wametoka nyuma na kushinda 3-1 dhidi ya KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
KMC walitangulia na bao la Hassan Kabunda dakika ya 41, kabla ya Simba kutoka nyuma kwa mabao ya Kibu Dennis dakika ya 51, Msenegal, Pape Sakho dakika ya 62 na beki Mkongo, Henock Inonga dakika ya 65.
Kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi 57, ingawa kushika nafasi ile ile, ya pili ikizidiwa pointi 10 na mabingwa tayari, Yanga baada ya wote kucheza mechi 27.
KMC baada ya kichapo hicho inabaki na pointi zake 32 za mechi 27 ikishukia nafasi ya 10 kutoka ya tisa.