Simba Sports Club Thread

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA SC WALIVYOMKIMBUKA RAIS MAGUFULI​

110A4263-71AA-4478-947F-BBC9BA10C431.jpeg

MEI 19 mwaka 2018, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, DK John Pombe Magufuli akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa Nahodha wa Simba, John Raphael Bocco.
Tiara kumbuka daima Dk.John Pombe Magufuli. Pumzika kwa amani.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Pablo Awapa Majukumu Mazito Morrison, Sakho​

moriii.jpg

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco amesema amefurahishwa viwango vya mastaa wake hususani viungo, Pape Sakho na Bernard Morrison katika mchezo wao wa Jumapili iliyopita dhidi ya RS Berkane na anaamini nyota hao wataendelea kuwa na kiwango bora dhidi ya ASEC Mimosas, Jumapili hii.
Simba Jumapili iliyopita wakiwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Berkane katika mchezo wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, ushindi huo umeifanya Simba kuongoza msimamo wa Kundi D wakiwa na alama saba.
Jumapili hii Simba inatarajiwa kushuka Stade de l’Amitie nchini Benin, kwa ajili ya mchezo wao wa tano dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Mchezo huo unafanyika Benin kwa kuwa uwanja wa ASEC Mimosas nchini Ivory Coast uko kwenye marekebisho.
Katika mchezo huo, Sakho alifunga bao pekee la ushindi la Simba ambapo sasa anafikisha mabao mawili, huku Morrison ambaye mpaka sasa ana mabao matatu. Akizungumza na Championi Jumatano, Pablo aliwapongeza mastaa hao kutokana na msaada mkubwa ambao walionyesha kwenye mchezo dhidi ya Berkane.
“Nawapongeza sana wachezaji wangu kwa kupambana katika mchezo wetu wa Jumapili, nadhani kwa kiasi kikubwa walijitoa sana kuhakikisha tunapata matokeo, hususani Sakho aliyefunga bao na kina Morrison ambao waliingia kipindi cha pili na kuonyesha kiwango bora.
“Tuna mchezo mgumu wa ugenini Jumapili, ni mchezo ambao huenda ukatupa tiketi ya kufuzu robo fainali, hivyo natamani kuona wachezaji hawa wakiwa kwenye kiwango bora ili kuhakikisha tunapata matokeo,” alisema Pablo.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Mastaa Simba Waapa Caf​

simbasctanzania_276061385_121956527082098_6837536992516696653_n.jpg

BAADA ya kikosi cha Simba kutua nchini kikitokea nchini Benin walikokuwa kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas, mastaa wa timu hiyo wamepa ni lazima washinde mechi yao ya mwisho na kwenda robo fainali ya mashindano hayo.

Simba inatarajia kucheza na US Gendarmerie ya Niger Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, mchezo ambao ni lazima Wanamsimbazi washinde ili waende robo fainali. Mchezo uliopita Simba ilichapwa mabao 3-0 mbele ya ASEC ya Ivory Coast.

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema baada ya kurejea nchini jana Jumanne wakitokea Benin wachezaji walioitwa timu ya taifa wataenda kwenye majukumu na wale ambao hawajaitwa wataenda mapumzikoni.

“Naomba utambue kuwa baada ya kuwasili wachezaji walioitwa timu ya taifa wataenda kwenye majukumu yao na wasiokua na majukumu hayo wataenda mapumziko, ila Machi 27, mwaka huu, kikosi kinarejea kambini kuanza maandalizi ya mechi dhidi ya US Gendarmerie.

“Tunashukuru baada ya mchezo huo kupoteza wachezaji wote wameahidi kupambana katika mechi yetu dhidi ya US Gendamerie, ambapo kila mmoja amejipanga kupata pointi tatu muhimu, kwani siku hiyo mashabiki waje kushuhudia biriani la Caf ambalo limeandaliwa spesho.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA SC WAINGIA KAMBINI KUJIANDAA KUIVAA USGN​

772CEAAF-9766-473F-A4F8-1EAAFA693A80.jpeg

KIKOSI cha Simba kimeingia kambini leo kujiandaa mechi yake ya mwisho ya Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gendamarie ya Niger Aprili 3, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Simba inahitaji ushindi lazima katika mchezo huo ili kujikatia tiketi ya kwenda Robo Fainali.
00DA5C3D-6634-4660-B25B-EB67E52E0200.jpeg

6CA41314-B91B-46FD-A4C6-C5B6B8FB4712.jpeg
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

KUZIONA SIMBA NA GENDAMARIE BUKU TATU TU​

F211AC70-FAF9-408A-ADBD-766029BD0033.jpeg

KIINGILIO cha chini katika mchezo wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba was SC na US Gendamarie ya Niger Aprili 3, mwaka huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam ni Sh 3,000.
554F43F6-7C78-4468-8688-A489530C8AC6.jpeg

5D22B074-3701-4AB1-B684-11CFB32A36F0.jpeg
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Pablo Ajiapiza Robo Fainali Shirikisho Afrika
270778578_7099345533438811_5541774526876163966_n.jpg


KUELEKEA mchezo wao wa mwisho wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USGN, Kocha Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameweka wazi kuwa watafanya kila kinachowezekana kushinda mchezo huo, ili kutinga hatua ya robo fainali.
JUMAPILI ya Aprili 3, mwaka huu, Simba wanaokamata nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi D, wanatarajia kuwa wenyeji wa USGN katika mchezo huo wa sita wa hatua ya makundi unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
SIMBA ambao mpaka sasa wamefanikiwa kukusanya pointi saba katika michezo yao mitano waliyocheza, wanatakiwa kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya USGN ili ku[1]jihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.
AKIZUNGUMZA na Championi Ijumaa, kocha Pablo alisema: “Tulitamani kupata matokeo katika mchezo wetu uliopita dhidi ya ASEC Mimosas ili tusiwe kwenye presha kubwa katika mchezo huu wa mwisho dhidi ya USGN, lakini haikuwa hivyo. “Hayo yamepita na kazi kubwa iliyo mbele yetu kwa sasa ni kuhakikisha tunashinda mchezo ujao na kutinga robo fainali, tunacheza nyumbani mbele ya mashabiki wetu na hatima ya kufuzu kimchezo iko mikononi mwetu, hivyo tutafanya kila linalowezekana kufanikisha hilo kwa kuwa tunaamini hakuna sababu ya kushindwa.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA SC YATINGA ROBO FAINALI KWA KISHINDO​

5CFE7780-42EB-4118-99BB-EB6EDC9538C8.jpeg

MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya US Gendamarie ya Niger usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba inayofundishwa na kocha Mspaniola, Pablo Franco Martin yamefungwa na kiungo Mmali, Sadio Kanouté dakika ya 63, mshambuliaji Mkongo Chris Kope Mutshimba Mugalu dakika ya 68 na 78 na kipa Saidu Hamisu aliyejifunga dakika ya 84 katika harakati za kuokoa.
Sifa zimuendee winga Mghana, Bernard Morrison aliyeseti mabao mawili ya kwanza baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza.
Simba inamaliza na pointi 10, sawa na RSB Berkane wakilingana hadi wastani wa mabao na zote zinakwenda Nane Bora zikizipiku ASEC Mimosas ya Ivory Coast iliyomaliza na pointi tisa na Gendamarie pointi tano.
RSB Berkane wamefuzu baada ya ushindi wa nyumbani wa 1-0 dhidi ya ASEC leo Uwanja wa Manispaa y Berkane nchini Morocco.
Timu nyingine zilizokwenda Robo Fainali ni Al Ahli Tripoli ya Libya na Pyramids ya Misri kutoka Kundi A, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na Al-Ittihad ya Libya Kundi B, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Al Masry ya Misri Kundi C.
Droo ya Robo Fainali itapangw Aprili 5, mwaka huu makao makuu ya Shirikisho (CAF), Jijini Cairo, nchini Misri.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SERIKALI YAIPONGEZA SIMBA SC KUTINGA ROBO FAINALI​


WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa ameipongeza Simba SC kwa kufuzu Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibamiza US Gendarmerie ya Niger mabao 4-0 usiku wa jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mchengerwa ametoa pongezi hizo muda mfupi baada ya kumalizika kwa mpambano huo ambapo amesema ushindi huo ni ushindi wa kihistoria.
"Ninaipongeza Timu ya Simba kwa ushindi wa kishindo kuelekea kwenye Robo Fainali ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika. Kama Taifa, tunajivunia kwa ushindi huo mnono unaoitangaza Nchi yetu kimataifa." Amefafanua Mhe. Mchengerwa
Ameitaka Timu ya Simba kufanya maandalizi ya kutosha ili kuweza kufanya vizuri zaidi katika mashindano hayo hatimaye kuchukua kombe na kuendelea kuitangaza Tanzania duniani.
Simba kwenye michuano ya robo fainali inaweza kukutana na TP Mazembe(DR Congo), Orlando Pirates ( Afrika Kusini) na Al Ahly Tripoli (Libya).
Ukiachilia timu hizi nne(4) timu nyingine nne(4) ambazo zimefuzu kuingia robo fainali ya mashindano haya ni pamoja na RS Berkane (Morocco), Pyramids (Misri), Al-Ittihad (Libya) na Al Masry Misri.
Simba inatarajiwa kuanzia nyumbani Uwanja wa Mkapa
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 MKWAKWANI​


MABINGWA watetezi, Simba SC wamepata ushindi wa ugenini wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na winga Mghana, Bernard Morrison dakika ya 40 na mshambuliaji Mnyarwanda, mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere dakika ya 90 na ushei, wakati la Coastal Union limefungwa na mshambuliaji Mnigeria, Victor Patrick Akpan dakika ya 78.
Simba inafikisha pointi 40 baada ya ushindi huo katika mchezo wa 18, ingawa inabaki nafasi ya pili ilizidiwa pointi 11 na watani, Yanga ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
Coastal Union baada ya ya kichapo cha leo inabaki na pointi zake 21 za mechi 19 nafasi ya 12.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Sakata la Morrison Kuzuiwa Kuingia Nchini Afrika Kusini, Barbara Atamka Neno​

BERNARD-MORRISON.jpg

TAARIFA zilizothibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Soka ya Simba Barbara Gonzalez ni kuwa kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo Bernard Morrison hawezi kuingia ndani ya ardhi ya Afrika Kusini kutokana na kuwa na kizuizi cha kuingia nchini humo.

Morrison kabla ya kujiunga na vilabu vya Yanga na Simba tayari alishawahi kufanya kazi nchini Afrika Kusini katika klabu ya Orlando Pirates na aliondoka klabuni hapo kutokana na matatizo ya utovu wa nidhamu.

Pamoja na Morrison kutohusika katika mchezo huo wa marudiano hiyo haijashusha hamasa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu hiyo Barbara Gonzalez baada ya kudai kuwa Morrison atamaliza mchezo kwenye ardhi ya Tanzania katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
barbara.jpg

Droo ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika imetangazwa hapo jana ambapo Klabu ya Soka ya Simba ya nchini Tanzania imepangwa kumenyana na Klabu ya soka ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini.

Mchezo wa kwanza wa hatua hiyo ya mtoano unatarajiwa kuanza nchini Tanzania katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam ambapo wenyeji Simba wataikaribisha Orlando Pirates Aprili 17, wiki moja baadaye Orlando Pirates watakuwa wenyeji wa Simba katika dimba la Orlando Stadium jijini Johannesburg.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limekubali ombi letu la mashabiki 60,000 kuingia uwanjani kwenye mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Orlando Pirates. #NguvuMoja
Image
Image
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA SC YALAZIMISHWA SARE NA POLISI 0-0 MOSHI​


MABINGWA watetezi, Simba SC wamelazimishwa sare ya bila mabao na wenyeji, Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kwa sare hiyo inayoiongezea kila timu pointi moja, Simba inafikisha pointi 41 na wanabaki nafasi ya pili, wakizidiwa pointi 10 na watani wao wa jadi, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 19.
Polisi Tanzania inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 19 pia na kusogea kwa nafasi moja hadi ya nane.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

SIMBA NA ORLANDO KUSINDIKIZWA NA QURAN TUKUFU JUMAPILI​



MECHI ya kwanza ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba SC na Orlando Pirates ya Afrika Kusini itafanyika sambamba na mashindano ya Quran Jumapili ijayo.
Hayo yamesemwa na Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally katika mkutano wake na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam.
“Maswali yamekuwa mengi kuhusu Uwanja wa Mkapa sababu siku ya mchezo dhidi ya Orlando Pirates kutakuwa na mashindano makubwa ya Quran, na inafahamika kwamba uwanja unatakiwa kuwa wazi kwa masaa 72 kabla ya mchezo,”.
“Baada ya mazungumzo baina ya Simba, CAF, TFF na waandaaji wa mashindano ya Quran tumekubaliana matukio yote yatafanyika ndani ya siku hiyo moja na CAF wamebariki hilo,” amesema Ahmed Ally.
Mechi hiyo inatarajiwa kuanza Saa 1:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na timu hizo zitarudiana Aprili 24, Uwanja wa Orlando Jijini Johannesburg.
Msimu uliopita Simba ilitolewa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa kuifungia 4-0 Johannesburg na kushinda 3-0 Dar es Salaam, lakini safari hii Wekundu wa Msimbazi wamepania kutinga Nusu Fainali.
“Hii ni robo fainali ya aina yake, iwe mchana iwe usiku, Mnyama safari hii anaenda semi final, tumedhamiria hilo, tumejipanga kwa hilo ndio maana tunataka mashabiki mje kwa wingi,” alisema Ahmed Ally jana.

 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Simba Yapiga Marufuku Mashabiki Kupiga Tochi Mechi dhidi ya Orlando Pirates​


April 11, 2022 by cshechambo


WhatsApp-Image-2022-04-11-at-4.21.14-PM.jpg

Shabiki wa klabu ya Simba akimulika tochi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USGN uwanja wa Benjamin Mkapa.
UONGOZI wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC umepiga marufuku Tochi za miale ya kijani, ambazo zimekua zikitumiwa na Mashabiki kuwamulika wachezaji wanapokua kwenye makujumu yao Uwanjani.
Simba SC imepiga marufuku Tochi hizo, kuelekea mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho dhidi ya Orlando Pirates utakaopigwa Jumapili (April 17), Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es salaam.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema Mashabiki wa Simba SC wanapaswa kuacha mpango wa kuingia na Tochi hizo, ili kuinusuru klabu yao kutozwa faini na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.
“Mchezo wetu uliopita dhidi ya USGN, baadhi ya Mashabiki waliingia Uwanjani na hizi Tochi licha ya kupiga marufuku, Simba kama taasisi na kama klabu hatupendezwi na utamaduni huu, ambao sio utamaduni wetu,”
“Simba SC ina utamaduni wake, sio huu ambao baadhi ya wenzetu waliuchagua katika mchezo uliopita, tunawaomba sana Wanasimba wote huu mpango wa kuja na Tochi uachwe mara moja, ili kuinusuru klabu yetu kuingia kwenye kadhia ya kutozwa faini na Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’. Amesema Ahmed Ally alipozungumza na Waandishi wa Habari leo Jumatatu (April 11).
Simba SC ilitinga Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika ‘CAF’ kwa kishindo, kufuatia kisago kilichoishukia USGN ya Niger cha 4-0 Jumapili (April 03), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.
Simba SC ilimaliza nafasi ya pili kwenye Kundi D ikiwa na alama 10 sawa na RS Berkane ya Morocco, huku ASEC Mimosas ya Ivory Coast na USGN ya Niger zikitupwa nje ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

HIVI NDIVYO MORRISON ALIVYOIPATIA SIMBA PENALTI YA USHINDI​


BEKI wa Orlando Pirates, Fortune Makaringe akimuangusha winga Mghana wa Simba, Bernard Morrison kwenye boksi jana katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.


Refa Mtunisia, Haythem Guirat aliamuru mkwaju wa penalti ambao uliwekwa nyavuni na beki kimataifa wa Tanzania, Shimari Salum Kapombe kuipatia bao pekee Simba katika mchezo huo.
Timu hizo zitarudiana Jumapili ijayo Uwanja wa Orlando Pirates Jijini Johannesburg na mshindi wa jumla atakwenda Nusu Fainali.

 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA YAJIBU TUHUMA ZA ORLANDO PIRATES NA KUFICHUA MENGI​



KLABU ya Simba SC imejibu tuhuma zilizotolewa na wapinzani wao, Orlando Pirates ya Afrika Kusini baada ya mchezo wa kwanza wa Robo Fainali Kombe la Shirikisho Afrika Jumapili.



 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA SC YAFA KIUME, YATOLEWA KWA MATUTA SAUZI​


KWA mara nyingine tena, safari ya Simba katika michuano ya Afrika imeishia kwenye Robo Fainali baada ya kutolewa na Orlando Pirates katika Kombe la Shirikisho leo kwa penalti 4-3.
Orlando Pirates walimaliza dakika 90 wakishinda 1-0 Uwanja wa Orlando Jijini Johannesburg, Afrika Kusini, bao la Peprah Kwame dakika ya 60 kwa kichwa, hivyo kufanya sare ya jumla ya 1-1 baada ya Simba kushinda 1-0 kwenye mechi ya kwanza ya Robo Fainali wiki iliyopita Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kwenye mikwaju ya penalti Jonás Mkude na Hennock Inonga Baka walikosa upande tea Simba, huku Shomari Kapombe, Meddie Kagere na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ wakifunga.
Waliofunga penalti za Orlando Piratas ni Deon Hotto, Hellings ‘Gabadinho’ Mhango, Tshegofatso Mabasa na kipa Richard Ofori , huku ya Kabelo Dlamini ikiokolewa na kipa Aishi Manula.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

KAPTENI BOCCO AREJEA KUIVAA YANGA JUMAMOSI​


NAHODHA wa Simba SC, John Raphael Bocco amerejea mazoezini kuelekea mechi dhidi ya watani, Yanga Jumamosi baada ya kuwa nje kwa zaidi ya mwezi .
Simba watakuwa wageni wa Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mchezo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya mechi ya kwanza miamba hiyo kutoa sare.
Na Bocco, mshambuliaji tegmeo la kocha Mspaniola, Pablo Franco Martin ameanza mazoezi baada ya kukosekana kikosini kwa muda.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

SIMBA SC YAITANDIKA RUVU SHOOTING 4-1 DAR​


MABINGWA watetezi, Simba SC wameibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba yamefungwa na Kibu Dennis dakika ya 39, Rally Bwalya dakika ya 66, Nahodha John Bocco dakika ya 81 na beki Inonga Baka ‘Varane’ dakika ya 85, wakati la Ruvu Shooting limefungwa na Haroun Athumani Chanongo akiiadhibu timu yake ya zamani dakika ya 83.
Simba inafikisha pointi 46, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi 10 na watani, Yanga baada ya wote kucheza mechi 22 kuelekea mechi nane za kukamilisha msimu.
Hali ni mbaya kwa Ruvu Shooting baada ya kupoteza mechi ya leo 22, wakilingana kila kitu na Tanzania Prisons hadi mechi za kucheza, 22 na wastani wa mabao, wote wamefungwa mabao 11 zaidi ya waliyofunga na wanashika nafasi za 14 na 15, wakiizidi pointi moja tu Mbeya Kwanza inayoshika mkia.