Simba Sports Club Thread

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Chama Anatisha​

chama-1.jpg

UNAWEZA kusema Clatous Chota Chama anaendelea pale alipoishia kutokana na yale anayoyafanya ndani ya uwanja akiwa na jezi ya Simba SC yenye namba 17 mgongoni.
Kiungo huyo raia wa Zambia, amejiunga na Simba katika usajili wa dirisha dogo msimu huu uliofungwa Januari 15, mwaka huu akitokea RS Berkane ya Morocco.
Chama msimu uliopita, aliachana na Simba aliyoitumikia kwa misimu mitatu na kutimkia RS Berkane, lakini hakudumu sana, akarejea Msimbazi.
Tangu arudi Simba, nyota huyo amekuwa na kiwango bora kama ilivyokuwa awali ambapo juzi Ijumaa katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, aliendeleza makali yake kwa kufunga bao moja akiwatesa vibaya mabeki.
Bao hilo alilifunga dakika ya 18 akipokea pasi ya Pape Ousmane Sakho ambapo kabla ya kufunga, aliwapiga chenga mabeki wawili wa Biashara United, nahodha Abdulmajid Mangalo na Boniface Maganga, kisha akaukwamisha mpira kimiani uliowapita kipa James Ssetuba na beki wake, Fredy Sululu. Simba ilishinda 3-0.
Akizungumzia mateso aliyoyapata wakati anamkaba Chama asifunge bao hilo, Mangalo aliliambia Spoti Xtra kwamba: “Unajua kabla mpira haujamfikia Chama, sisi mabeki tulijua Sakho atafunga mwenyewe kutokana na nafasi aliyokuwepo, hivyo tulikuwa katika harakati za kumuwahi kwa nguvu.
“Sasa alipopiga pasi kwa Chama, ikatulazimu tubadilishe uelekeo, jambo ambalo lilikuwa gumu sana na kujikuta tunateleza na kuanguka.
“Kwa kuwa wajibu mkubwa wa beki ni kuzuia mpira usiingie nyavuni, basi niliamua kuubwaga mwili chini ili ikitokea amepiga mpira niuzuie, lakini tofauti na matarajio yangu, Chama alikuwa na utulivu mkubwa, akausogeza mpira pembeni zaidi na kufunga, nadhani anastahili kupongezwa kwa hilo.
“Kwa utulivu aliouonesha akiwa eneo lile na kufunga bao, inaonesha ni mchezaji tishio.”
Mara baada ya mchezo huo, Chama ambaye ana mabao mawili katika Ligi Kuu Bara msimu huu, alisema: “Ni ushindi mwingine muhimu leo (juzi), nina furaha kufunga tena.”
Chama tangu arejee Simba, amefanikiwa kufunga mabao sita na asisti tatu katika michuano yote, huku akiwa na hat trick moja aliyopiga katika Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) wakati Simba ikishinda 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa, Februari 16, 2022.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Simba vinara wa kukosa penalti​

penalti pic

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba ,imeingia katika takwimu ngumu wakiwa ndio timu inayoongoza kwa kukosa penalti.
Mpaka sasa Simba imekosa jumla ya penalti 5 huku tatu kati ya hizo wakikosa washambuliaji wao watatu.
Nahodha wa Simba John Bocco pamoja na wenzake Meddie Kagere, Chris Mugalu wameungana na kiungo Rally Bwalya huku beki Erasto Nyoni naye akiwemo.
Biashara wako nyuma ya Simba wao wakikosa penalti mbili kupitia wachezaji wao wawili tofauti Collins Opare na Baron Oketch.
Wachezaji waliokosa penalti mpaka sasa ni pamoja na Lusajo Mwaikenda (Azam FC), Oketch (Biashara United), Habib Kyombo (Mbeya Kwanza), Boban Zirintusa (Mtibwa Sugar).
Wengine ni Opare (Biashara United), Emmanuel Mvuyekule(KMC), Eliud Ambokile (Mbeya City), Raymond Masota (Geita Gold), Renatus Kisase (Ruvu Shooting), Kagere, Bocco, Bwalya, Mugalu na Nyoni (wote wa Simba).
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Simba: Ubingwa? subirini tu, hamtaamini​

ubingwa pic

KIKOSI cha Simba kinashuka uwanjani leo saa 1 usiku kuvaana na Dodoma Jiji katika mechi za mfululizo wa Ligi Kuu Bara, huku mabosi wake wakitamba hawana presha kabisa ya kutetea taji, kwani wanajua wataikamatia wapi Yanga inayoongoza msimamo.
Simba ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 34 ikizidiwa kwa pointi 11 na Yanga ambayo imecheza mechi moja zaidi, lakini Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema kwa namna walivyojipanga wala hawana presha ya ubingwa.
Licha ya Simba kumkosa beki Shomary Kapombe aliyeumia katika mchezo uliopita walioshinda 3-0 dhidi ya Biashara United, Try Again alisema wataishukia na Dodoma Jiji leo, kisha kuendelea na mipango yao ya mechi za kimataifa za michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa Kundi D itakapoialika RS Berkane ya Morocco katika mbio zao za kutinga robo fainali.
Try Again alisema kwa jinsi walivyojipanga kwao kila mchezo kwao ni kama fainali kwa nia ya kutaka kuvuna pointi tatu na kupunguza pengo baina yao na watani wao Yanga ambao jana walijimarisha kileleni kwa kuifunga Geita Gold 1-0 jijini Mwanza na kufikisha pointi 45.
“Sisi kama Simba tunaangalia kila mchezo tunaokutana nao kwa ukubwa bila ya kubagua wala kuangalia aina ya timu ambayo tutacheza nayo,” alisema.
Try Again alisisitiza malengo yao ni kuhakikisha wanatetea tena ubingwa kwa mara ya tano mfululizo, akisema nia, uwezo na sababu ya kufanya hivyo wanayo hata kama wameachwa nyuma kwa pointi kadhaa (11) na Yanga.
Alisema wanatambua ushindani mkubwa wa Ligi uliopo kwa kila timu, lakini watapigana kufa au kupona kuhakikisha michezo yao wanafanya vizuri.
“Tuna kikosi kizuri kila mchezaji anatamani kuiona Simba ikitetea ubingwa mara ya tano mfululizo kitendo ambacho kinaumiza timu nyingine, ndio mipango yetu hakuna namna na wala hatuna presha yoyote,” alisema Try Again.
Try Again aliwataka mashabiki wa Simba kuendelea kuwasapoti nyota wao wawapo katika majukumu yao kwa kuwa wao pia ni sehemu ya timu kupata matokeo.
“Mashabiki wetu tukawashukuru sana kwa kuwa pamoja na timu yao kila timu yao inapoenda waendelee hivyo hivyo ili tutimize malengo yetu kwa pamoja. Kuhusu Yanga kutuzidi pointi, ni kawaida yao karibu kila msimu wanaongoza, ila sisi ndio tunaobeba ubingwa na hilo hatuna wasiwasi kabisa,” alisema.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Simba: Tunaendelea tulipoishia​

tulipoishia pic

SIMBA inashuka tena uwanjani leo kuvaana na Dodoma Jiji saa 1:00 usiku, huku watetezi hao wakitamba wanaendelea walipoishia katika Ligi Kuu Bara.
Mechi hiyo ni ya nne kwa timu hizo kukutana katika Ligi Kuu, lakini ni moja kati ya mechi tatu zinazopigwa leo, nyingine ikiwa ni ya mapema saa 8 wakati Ruvu Shooting itakapoialika Biashara United na jioni KMC kuikaribisha Coastal Union.
Mashabiki wa Simba wameanza kutamba mtaani, baada ya kuishuhudia timu hiyo ikirejea kwa kishindo katika ligi ikitokea kwenye michuano ya kimataifa kwa kuifumua Biashara United kwa mabao 3-0, huku Dodoma iliyo chini ya kocha mpya, Masoud Djuma ikiwa na kumbukumbu ya satre ya 1-1 na Ruvu Shooting.
Rekodi zinaonyesha katika mechi tatu za awali baina ya timu hizo, Simba imeshinda, ikianza kwa kuikaribisha Dodoma katika Ligi Kuu msimu uliopita kwa kuipiga 2-1 kisha kuilaza tena 3-1 na msimu huu iliibwaga kwa bao 1-0 mjini Dodoma.
Aidha, katika mechi sita zilizopita za Simba kwenye ligi imepoteza mbili dhidi ya Mbeya City na Kagera Sugar na kutoka sare na Mtibwa Sugar na kushinda michezo mitatu dhidi ya Mbeya Kwanza, Tanzania Prisons na Biashara United.
Kwa upande wa wapinzani wao, Dodoma katika mechi kama hizo sita, haijashinda hata moja zaidi ya kupasuka mara nne dhidi ya KMC, Azam, Kagera Sugar na Yanga, kisha kutoka sare mbili na Geita Gold na Ruvu Shooting.
Matokeo hayo mabaya kwa Dodoma ndio yaliyomng’oa kocha Mbwana Makatta na kuletwa Djuma aliyeanza na sare akiwa jukwaani dhidi ya Ruvu na leo akiwa na kazi ya kukabiliana na waajiri wake wa zamani, yaani Simba aliyowahi kuinoa.
Uwepo wa Masoud kikosi cha Dodoma unaweza kuwa na faida mbili kila mchezaji atakayepata nafasi ya kucheza atakuwa na hamu ya kumuonyesha uwezo kocha mpya, anaifahamu timu hiyo aliwahi kuifundisha.
Hata hivyo, Dodoma itakuwa na kazi ya kuwazuia nyota wa Simba wakiongozwa na Clatous Chama, Ousmane Sakho, Meddie Kagere aliyewaliza mjini Dodoma na Bernard Morrison.
Kwa upande wa Dodoma nyota wanaweza kuipa misukosuko ngome ya Simba ni Cleophas Mkandala aliyewahi kuitungua mara mbili, Waziri Junior aliyefunga bao mchezo uliopita dhidi ya Ruvu, Anuary Jabir mwenye mabao matatu, Khamis Ncha ‘Vialli’ na Emmanuel Martin ambao ni wazoefu katika Ligi Kuu Bara.
Kocha wa Simba, Pablo Franco alisema licha ya kuwa mchezo huo kuwa mgumu, kutokana na Dodoma kuwa wachezaji wenye uwezo, lakini kiu yake kuendeleza moto walioanza nao baada ya kurejea kutoka mechi za CAF.
“Ukiangalia hata mechi ya mzunguko wa kwanza ilikuwa na ushindani wa kutosha ila dhamira yetu ni kupata ushindi na ninaamini itakuwa hivyo, hatukuwa na muda wa kutosha kufanya mazoezi ila tulioupata tuliutumia kwa kufanya vilivyo sahihi.”
Kocha Djuma wa Dodoma alisema kuna vitu alienda kuviangalia uwanjani wakati Sima ikishinda 3-0 dhidi ya Biashara.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0, CHAMA NA KAGERE​

AVvXsEjNG-Al7lJhyA5emPHTx3nGWjvKn2UQ9FUATLPOiti71V9F4m86NML8dNL7KHFK2vFkVE6niBV2hneN2a11cOu3U0vVy17cJ2KoTBuv_puHPsfIT0qDKQAT_AMMseaY2J7506nsHGLE1tszKqWkEBOqJ2N6-sRbGOhVS1LpuIYn71oMTzTuxbKmU0mX=w640-h422

MABINGWA watetezi, Simba SC wameilaza Dodoma Jiji FC mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba yamefungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chama dakika ya 56 kwa penalti na mshambuliaji Mnyarwanda, mzaliwa wa Uganda, Meddie Kagere dakika ya 74.
Kwa ushindi huo, timu ya kocha Mspaniola, Pablo Franco Martin inafikisha pointi 37, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi nane na jirani zao, Yanga SC baada ya wote kucheza mechi 17.
Katika mechi zilizotangulia leo, Ruvu Shooting imelazimishwa sare ya 0-0 na Biashara United Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, wakati Coastal Union imewachapa wenyeji, KMC 2-3 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Abdul Hamisi kwa penalti dakika ya 22, William Kisingi dakika ya 82 na Rashid Chambo dakika ya 90 na ushei, wakati ya KMC yamefungwa na Emmanuel Mvuyekure dakika ya 40 na Kenny Ally dakika ya 47.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Mastaa Simba Waongezewa Mzuka CAF​

SIMBA-2.jpg

KATIKA kuhakikisha timu yao inafuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, uongozi wa Simba SC umefanya kikao na wachezaji wote.
Simba ipo nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi D kunako michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, wakiwa na pointi nne, huku RS Berkane ya Morocco ikiwa na sita, ndiyo vinara. Timu hizo Jumapili hii, zinatarajiwa kucheza kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ukiwa ni mchezo wa nne kila mmoja katika Kundi D.
Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema juzi walifanya kikao na wachezaji, lengo likiwa ni kuwakumbusha majukumu yao ya uwanjani katika kuhakikisha wanachukua pointi zote sita kwenye Uwanja wa Mkapa.
Ally alisema hawataki kuona wanapoteza michezo hiyo miwili watakayocheza uwanja wa nyumbani dhidi ya RS Berkane na US Gendarmarie, huku wakihitaji sare ugenini dhidi ya ASEC Mimosas.
Aliongeza kuwa, wanaamini malengo yao yatatimia katika kufuzu robo fainali ya michuano hiyo inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
“Tunajivunia rekodi nzuri tuliyonayo katika miaka miaka miwili iliyopita tunapocheza uwanja wetu wa nyumbani.
“Rekodi hiyo tumepanga kuiendeleza msimu huu ambao licha ya ugumu, lakini tutahakikisha tunapambana kupata ushindi katika michezo miwili ijayo.
“Tumefanya kikao kizito kikihusisha viongozi na wachezaji ambacho kilikuwa na lengo la kuwaongezea morali na hali ya kujiamini wakiwa uwanjani, pia kuwakumbushia majukumu yao,” alisema Ally.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Simba Yatangaza Kishindo Kipya Kuwavaa Rs Berkane​

simba-5.jpg

Klabu ya Simba leo Machi 9, 2022 imeingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa makundi kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Rs Berkane ya Morroco kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa siku ya jumapili saa kumi kamili jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Meneja wa habari na mawasiliano hiyo, Ahmed Ally amesema wameingia mapema kambini kwa ajili ya kuonesha umuhimu wa mchezo huo huku nyota wawili pekee ambao watakosekana kwenye mchezo huo.
simba-4.jpg

“Taarifa ya awali kuhusu majeruhi ni kuwa Hassan Dilunga atakosekana kwenye mchezo na Clotas Chama anakosekana kutokana na kanuni za kimashindano ila Taddeo Lwanga, Kibu Denis, Chris Mugalu na Jonas Mkude wapo tayari kwa mchezo.
“Nawaomba mashabiki wetu tununue tiketi mapema. Wengi wetu tumekuwa na utaratibu wa kunua tiketi siku ya mchezo lakini ni jambo la kupendekeza siku ya mchezo kufika tukiwa na tiketi mkononi.”
“Kuna jambo lilijitokeza kwenye mchezo dhidi ya Asec la kuwaondoa mashabiki wao. Niwaombe kwenye mchezo huu tusifanye hivyo, tunaona siku ile baada ya mchezo waliondoka uwanjani kwa aibu.”
“Tanzania kwa sasa tupo nafasi ya 10 kwa kuwa na Ligi Kuu bora Afrika, hili halijaja pekee kwa michezo ya ndani bali kwa namna ambavyo tunafanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa ambayo tunashiriki.”
Berkane wamekuja wakati mbaya maana wametukuta tuko kamili.”- amesema Ahmed Ally.
Klabu ya Rs Berkane ambayo ni kinara wa kundi D inatarajiwa kuwasili kesho majira ya saa sita kamili mchana huku Simba ikikamata nafasi ya pili wakiwa na alama 4 sawa na timu ya US Gendermarie ya Niger huku Asec Mimosa ya Ivory Coast wakiwa wa mwisho na alama 3.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

KAPOMBE MCHEZAJI BORA WA SIMBA FEBRUARI​


BEKI wa kulia wa Simba SC, Shomari Kapombe akiwa ameshika Tuzo yake ya Mchezaji Bora wa mwezi Februari wa klabu hiyo baada ya kukabidhiwa na wadhamini, Emirate Aluminium.


Shomari Kapombe akikabidhiwa mfano wa Hundi wa Sh. Milioni 2 kama zawadi ya ushindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Simba mwezi Februari.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

WAZIRI WA ZANZIBAR MGENI RASMI SIMBA NA GENDARMERIE​

AVvXsEj50BiVrIoQzxTnjmdjIPqbPcLBcY-n3C1Y7A8-oQXYFwchccg92o3Qgsamt0ydHoeHtHjUxo-pfL1FXWBL-RxM55VSNzVIE5JG7PXMrCY1ztkT4UdGHZwrZ-HoM2erzDAc_ZF4kDiS5zMYnjGgPNyAl50KLAJjZ7M1OuCWl2DyaKY-fmGW88IzREGh=w534-h640

WAZIRI wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar, Omar Said Shaaban atakuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba SC dhidi ya RS Berkane ya Morocco.
Mchezo huo wa Kundi D utafanyika Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na kurushwa moja kwa moja na chaneli ya UTV ya Azam Tv kuanzia Saa 10:00 jioni.
Mechi ya kwanza wiki iliyopita Berkane ilishinda 2-0 mjini Berkane na sasa ndio inaongoza Kundi hilo kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Simba na US Gendamarie ya Niger zenye pointi nne kila moja, wakati ASEC ya Ivory Cost yenye pointi tatu inashika mkia baada ya mechi tatu za awali.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Pablo: Tutacheza Kibingwa Kwa Mkapa​

274301625_997489824214664_3028893231182487338_n.jpg

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameweka wazi kuwa kuelekea mchezo wao wa Jumapili dhidi ya RS Berkane, benchi la ufundi la timu hiyo linafanya maandalizi makubwa kuhakikisha si tu kwamba kikosi chao kinaibuka na ushindi dhidi ya Berkane, lakini pia kinatoa burudani ya kibingwa.
Simba wanatarajia kuvaana na Berkane keshokutwa Jumapili katika mchezo wao wa nne wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kukusanya pointi nne katika michezo yao mitatu ya awali wakishinda mchezo mmoja, sare mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara kwenye kundi lao D, wanakamata nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi zao nne, huku RS Berkane wao wakiwa ndio vinara wa msimamo na pointi zao sita walizokusanya katika michezo mitatu.
Akizungumza na Championi Ijumaa, kocha Pablo alisema: “Tunatarajia mchezo mgumu dhidi ya Berkane Jumapili, huu ni mchezo wa maamuzi mchezo ambao timu itakayoshinda itakuwa moja kwa moja inaongoza msimamo wa kundi hili, hivyo ni mchezo muhimu sana kwa kila mmoja.
“Lakini jambo zuri kwetu ni kuwa kwa sasa tupo katika kiwango kizuri na tutakuwa kwenye uwanja wa nyumbani, hivyo hatutacheza tu kwa ajili ya kutafuta matokeo lakini ni lazima tuonyeshe kiwango bora kama ambacho tulionyesha katika michezo yetu miwili iliyopita ya ligi kuu.”
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Pablo: Ushindi Uhakika Dhidi ya RS Berkane Leo​

SIMBA-3.jpg

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, amesema hakuna matokeo yoyote ambayo anayahitaji zaidi ya ushindi katika mchezo wa Kundi D dhidi ya RS Berkane.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa leo Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, kuanzia majira ya saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Akizungumza na Spoti Xtra, Pablo alisema wanatarajia kuwa na mchezo mzuri dhidi ya RS Berkane na kupata matokeo ya ushindi kwani ndio matokeo ambayo wanayahitaji kuliko jambo lolote licha ya kucheza na timu bora.


simba-berkane.jpg

“Tunacheza na timu nzuri ambayo ilipata matokeo mazuri dhidi yetu nyumbani kwao, kwa sasa tupo nyumbani, sehemu yenye matumaini makubwa kwetu.
“Tunahitaji kupata matokeo mazuri na naamini tutakuwa na mchezo mzuri utakaotupa ushindi kwa kuwa hakuna matokeo mazuri ambayo tunahitaji zaidi ya ushindi,” alisema kocha huyo.
Pablo aliongeza kwa kubainisha kwamba, amewataka mabeki wake wakiongozwa na Joash Onyango na Inong Baka kuacha kucheza faulo zisizo za lazima karibu na goli lao ili kutowaruhusu wapinzani kufunga mabao kwa mipira iliyokufa kama ilivyotokea katika mchezo wa kwanza kule Morocco wakati Simba ikifungwa 2-0.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA YAICHAPA BERKANE 1-0 NA KUONGOZA KUNDI​

AVvXsEgDyq2V_8hHxOlVAWESCxwmw4r76EU4AYNQW_9QXz2YnU9vDEIpeWDPy3gcdoBJApjKd89aaEjOYki4VWj1mfCDhdRjwX1i0TtiKGuEuUAmQiH7nfumIzMu8dTp3Z6nL_OjE-G5mCHSsOQPVVKmu_6vm9Wcl0R-Nc1pcUlLSoC1dLj6E9PCGKwuAURM=w640-h422

BAO la Pape Ousmane Sakho dakika ya 44 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya RS Berkane ya Morocco katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Winga huyo Msenegal alifunga bao hilo akimalizia pasi ya Mnyarwanda, Meddie Kagere na kwa ushindi huo, Simba inafikisha pointi saba na kupanda kileleni mwa kundi hilo, ikiizidi pointi moja Berkane.
Mechi nyingine ya Kundi hilo inafuatia Saa 1:00 usiku huu mjini Cotonou nchini Benin baina ya ASEC MIMOSAS ya Ivory Coast na US Gendamarie ya Niger kukamilisha mzunguko wa nne.
Kwa sasa Gendamarie ina pointi nne na ASEC pointi tatu baada ya mechi tatu.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Adebayor, Moses Phiri waiteka Simba​

SIMBA.jpg

HABARI njema kwa mashabiki wa Simba kwa sasa ni taarifa za rais wa heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji, kufungukia mipango ya usajili wa wachezaji wawili Moses Phiri na Adebayor kutua ndani ya timu hiyo katika dirisha kubwa la usajili huku wadau wakubwa wa Simba wakifurahishwa na taarifa hizo njema.

Moses Phiri, mwenye uraia wa Zambia, kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Zanaco, amekuwa akiwindwa pia na watani wa Simba, Klabu ya Yanga huku Victorien Adebayor mwenye uraia wa Niger, anayekipiga katika Klabu ya US Gendarmarie pia akiwa katika mazungumzo na uongozi wa Simba.

Akizungumza na Championi Jumatatu, kiungo mshambuliaji wa zamani wa Simba, Malota Soma ‘Ball Jagler’ yeye alisema kuwa utakuwa ni usajili mzuri kwa Simba kutokana na aina ya wachezaji hao kuwa bora na watawafaa katika michuano ya kimataifa kutokana na uwezo wao na mahitaji ya klabu hiyo.

“Ni wachezaji wazuri sana, Moses Phiri ukimtazama anaweza kucheza nafasi zote za mbele kuanzia winga ya kulia na kushoto lakini kama namba kumi au mshambuliaji wa kati, kote huko anafaa kucheza na anafanya vizuri sana, hivyo kama akisajiliwa basi ataiongezea kitu kikubwa sana Simba.

“Kwa upande wa Adebayor pia ni mchezaji mzuri, yeye nimemtazama katika mchezo mmoja pekee dhidi ya Simba ambapo alisumbua sana, kama ndio yupo hivyo siku zote basi atakuwa msaada mzuri kwa Simba maana inahitaji wachezaji wenye ubora mkubwa ili iweze kufanya vizuri katika michuno ya kimataifa,” alisema mchezaji huyo mstaafu.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

AISHI MANULA NA CLEEN SHEETS 118, KATIKA MECHI 200 SIMBA SC​

AVvXsEjZPiW-BBy4lsQaYih-mlRxo66Oljgnm0PINlNoH6qdWURhO8n-9yHQktq6ziYwCh2IIayNkJWtWoX_XBeRNopKJPd4sgSioNMfyVswYPjs98vYZwDfQC4W7TZBBH6rH-7DuQLTiQCD3oDHzw82Ztp76VEPRbmWOmR_CVpW1ULrDj89hiExnH92tJff=w640-h420

MABINGWA wa Tanzania, Simba SC Jumapili walipanda kileleni mwa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya RS Berkane ya Morocco, bao pekee la winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 44 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kwa matoke ohayo, Simba SC inafikisha pointi saba na kuongoza Kundi D, mbele ya RSB Berkane wenye pointi sita, sawa na ASEC Mimosas ya Ivory Coast, wakati US Gendamarie ya Niger inashka mkia ikiwa na pointi nne.
Matokeo haya yanaiweka Simba kwenye nafasi nzuri ya kwenda Robo Fainali ya michuano hiyo kuelekea mechi mbili za mwisho za kundi hilo, ugenini dhidi ya ASEC Machi 20 nchini Benin na nyumbani dhidi ya USGN nyumbani Aprili 3.
Sifa zimuendee kipa Aishi Salum Manula aliyekuwa langoni Jumapili na kumaliza dakika 90 bila kuruhusu bao, akiidakia Simba SC mechi ya 200 tangu ajiunge nayo kutoka Azam FC Juni mwaka 2017,

AVvXsEgyGmXl39_W5c3JZmJElHWNJ-n09bgRVqEnyjEj6CLgkOZM5I9kZwvOTPtgX_3BCq1_xqkM9sYtEzyWPZ-5IG6svd-j9xnilPkfQqLae_WIfoMmrYdlgqzkwHYh9LAV1SJKjX91xlP3XoQdYspXc4DfOt9TCT--oHs4Cx4ZRS2dIvYa1wLtOuHD7owi=w640-h392
AVvXsEi-wkC3s1baOpBLJVaO_2uktHU6266B8EhR8tVhHs76LxB5-tVqW-jIp5XG5jiFdmYR8MCKQwFb4sVDG3euijdyIUr5bF2oefD6GWB616CV9SlnEi8idraFjf9GUfb3Vkoxt0TcLp32zIBVxJH6SGl9bgrmpHXIeJ9_iw7iU1WNYjnkG2iQZGhTbbzt=w640-h418


Hapana shaka mechi 200 ndani ya miaka mitano ni kielelezo tosha cha namna Aishi, ambaye pia ni kipa bora zaidi kwa sasa nchini akiwa chachu ya mafanikio ya timu katika misimu hii mitano, akiiwezesha kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa mara mbili na kutwaa ubingwa wa Ligi Ku umara nne mfululizo.
Katika mechi zote 200 alizodaka hadi sasa, Aishi amesimama langoni mara 118 bila kuruhusu bao Simba SC na kwa ujumla amefungwa mabao 109, akiiongoza timu kushinda mechi 140, kufungwa 25 na sare 35.
Aishi mwenye umri wa miaka 26 tayari ameingia kwenye orodha ya makipa bora kuwahi kutokea siyo tu katika klabu yake, Simba bali hata na nchini kwa ujumla na sasa anawania kuweka rekodi zaidi ili kudhihirisha ubora wake.
Huyo ndiye kipa aliyeiwezesha Taifa Stars kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 nchini Misri ambaye Jumapili amedaka mechi ya 200 tangu ajiunge na Simba SC miaka mitano iliyopita.

AVvXsEiqFX2Lr_9l-UtO_54XpW4JQB2k2xyL9IGl-9RYoEBXdq1eQ7sVtDOctKsmOWMTz3Zq4UwZgGuBTGEGaxS3o-cpxTER7-LU6xcGhhw0tFJ5Udl7m4GTmWWDVbx7rwT8VfaPjHDNcPGopi9-_wBo6I5Stz3Ct5woz1LtFNpgjQJy5CbPQbo7Cd3Iv3pz=s1295
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

AISHI MANULA NA CLEEN SHEETS 118, KATIKA MECHI 200 SIMBA SC​

AVvXsEjZPiW-BBy4lsQaYih-mlRxo66Oljgnm0PINlNoH6qdWURhO8n-9yHQktq6ziYwCh2IIayNkJWtWoX_XBeRNopKJPd4sgSioNMfyVswYPjs98vYZwDfQC4W7TZBBH6rH-7DuQLTiQCD3oDHzw82Ztp76VEPRbmWOmR_CVpW1ULrDj89hiExnH92tJff=w640-h420

MABINGWA wa Tanzania, Simba SC Jumapili walipanda kileleni mwa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya RS Berkane ya Morocco, bao pekee la winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 44 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Kwa matoke ohayo, Simba SC inafikisha pointi saba na kuongoza Kundi D, mbele ya RSB Berkane wenye pointi sita, sawa na ASEC Mimosas ya Ivory Coast, wakati US Gendamarie ya Niger inashka mkia ikiwa na pointi nne.
Matokeo haya yanaiweka Simba kwenye nafasi nzuri ya kwenda Robo Fainali ya michuano hiyo kuelekea mechi mbili za mwisho za kundi hilo, ugenini dhidi ya ASEC Machi 20 nchini Benin na nyumbani dhidi ya USGN nyumbani Aprili 3.
Sifa zimuendee kipa Aishi Salum Manula aliyekuwa langoni Jumapili na kumaliza dakika 90 bila kuruhusu bao, akiidakia Simba SC mechi ya 200 tangu ajiunge nayo kutoka Azam FC Juni mwaka 2017,

AVvXsEgyGmXl39_W5c3JZmJElHWNJ-n09bgRVqEnyjEj6CLgkOZM5I9kZwvOTPtgX_3BCq1_xqkM9sYtEzyWPZ-5IG6svd-j9xnilPkfQqLae_WIfoMmrYdlgqzkwHYh9LAV1SJKjX91xlP3XoQdYspXc4DfOt9TCT--oHs4Cx4ZRS2dIvYa1wLtOuHD7owi=w640-h392
AVvXsEi-wkC3s1baOpBLJVaO_2uktHU6266B8EhR8tVhHs76LxB5-tVqW-jIp5XG5jiFdmYR8MCKQwFb4sVDG3euijdyIUr5bF2oefD6GWB616CV9SlnEi8idraFjf9GUfb3Vkoxt0TcLp32zIBVxJH6SGl9bgrmpHXIeJ9_iw7iU1WNYjnkG2iQZGhTbbzt=w640-h418


Hapana shaka mechi 200 ndani ya miaka mitano ni kielelezo tosha cha namna Aishi, ambaye pia ni kipa bora zaidi kwa sasa nchini akiwa chachu ya mafanikio ya timu katika misimu hii mitano, akiiwezesha kufika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa mara mbili na kutwaa ubingwa wa Ligi Ku umara nne mfululizo.
Katika mechi zote 200 alizodaka hadi sasa, Aishi amesimama langoni mara 118 bila kuruhusu bao Simba SC na kwa ujumla amefungwa mabao 109, akiiongoza timu kushinda mechi 140, kufungwa 25 na sare 35.
Aishi mwenye umri wa miaka 26 tayari ameingia kwenye orodha ya makipa bora kuwahi kutokea siyo tu katika klabu yake, Simba bali hata na nchini kwa ujumla na sasa anawania kuweka rekodi zaidi ili kudhihirisha ubora wake.
Huyo ndiye kipa aliyeiwezesha Taifa Stars kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 nchini Misri ambaye Jumapili amedaka mechi ya 200 tangu ajiunge na Simba SC miaka mitano iliyopita.

AVvXsEiqFX2Lr_9l-UtO_54XpW4JQB2k2xyL9IGl-9RYoEBXdq1eQ7sVtDOctKsmOWMTz3Zq4UwZgGuBTGEGaxS3o-cpxTER7-LU6xcGhhw0tFJ5Udl7m4GTmWWDVbx7rwT8VfaPjHDNcPGopi9-_wBo6I5Stz3Ct5woz1LtFNpgjQJy5CbPQbo7Cd3Iv3pz=s1295
REKODI YA AISHI MANULA SIMBA
1. Simba 1-0 Rayon Sport (Hakufungwa Kirafiki Simba Day Taifa)
2. Simba 0-0 Mlandege FC (Hakufungwa Kirafiki Amaan, Zbar)
3. Simba 0-0 (5-4 penalti) Yanga (Hakufungwa Ngao ya Jamii, Taifa Penalti)
4. Simba 7 – 0 Ruvu Shooting (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
5. Simba 0 – 0 Azam FC (Hakufungwa Ligi Kuu Chamazi)
6. Simba 3 – 0 Mwadui (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
7. Simba 2 – 2 Mbao FC (Alifungwa mbili Ligi Kuu Kirumba, Mwanza)
8. Simba 0-0 Milambo (Aliingia, hakufungwa Kirafiki A. Mwinyi, Tabora)
9. Simba 2-1 Stand United (Alifungwa moja Ligi Kuu Shinyanga)
10. Simba 1-1 Mtibwa Sugar (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
11. Simba 4-0 Njombe Mji (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
12. Simba 1-1 Yanga (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
13. Simba 1-0 Mbeya City (Hakufungwa Ligi Kuu Sokoine)
14. Simba 1-0 Tanzania Prisons (Hakufungwa Ligi Kuu Sokoine)
15. Simba 1-1 Lipuli FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
16. Simba 1-1 (Penalti 3-4) Green Warriors (Alifungwa moja na penalti nne Kombe la TFF Chamazi)
17. Simba 2-0 Ndanda FC (Hakufungwa Ligi Kuu Nangwanda)
18. Simba 4-0 Singida United (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
19. Simba 2-0 Kagera Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu Kaitaba)
20. Simba 4-0 Maji Maji FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
21. Simba 3-0 Ruvu Shooting FC (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
22. Simba 1-0 Azam FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
23. Simba 4-0 Gendarmerie Tnare (Hakufungwa, Kombe la Shirikiaho Kuu Taifa)
24. Simba 2-2 Mwadui FC (Alifungwa mbili Ligi Kuu Kambarage)
25. Simba 1-0 Gendarmerie Tnare (Hakufungwa – Kombe la Shirikisho Djibouti)
26. Simba 5-0 Mbao FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
27. Simba 3-3 Stand United (Alifungwa zote tatu Ligi Kuu Taifa)
28. Simba 2-2 Al Masry (Alifungwa mbili moja kwa penalti Kombe la Shirikisho Taifa)
29. Simba 0-0 Al Masry (Hakufungwa Kombe la Shirikisho Port Said)
30. Simba 2-0 Njombe Mji FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa Njombe)
31. Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
32. Simba 3-1 Mbeya City (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
33. Simba 2-0 Tanzania Prisons (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
34. Simba 1-1 Lipuli FC (Alifungwa moja, Ligi Kuu Samora)
35. Simba 1-0 Yanga SC (Hakufungwa, Ligi Kuu Taifa)
36. Simba 1-0 Ndanda FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
37. Simba 1-0 Singida United (Hakufungwa Ligi Kuu Namfua)
38. Simba 0-0 (3-2 Penalti) Kariobangi Sharks (Hakufungwa, akaokoa penalti moja SportPesa SuperCup Nakuru)
39. Simba SC 0-0 (Penalti 5-4i) Home Boys (Hakufungwa SportPesa Cup Nakuru)
40. Simba 0-2 Gor Mahia (Alifungwa mbili SportPesa SuperCup Nakuru)
41. Simba SC 1-1 F.C.E KSAIFA ya Palestina (Hakufungwa kirafiki ziara ya Uturuki)
42. Simba SC 3-1 MC Oujder ya Morocco (Hakufungwa Kirafiki ziara ya Uturuki)
43. Simba SC 1-1 Asante Kotoko ya Ghana (Alifungwa moja Simba Day Taifa)
44. Simba SC 2-1 Arusha United (Alifungwa moja Kirafiki S.A. Abeid, Arusha)
45. Simba SC 2-1 Mtibwa Sugar (Alifungwa moja Ngao ya Jamii Kirumba, Mwanza)
46. Simba SC 1-0 Tanzania Prisons (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
47. Simba SC 2-0 Mbeya City (Hakufungwa, Ligi Kuu alimpisha Abdul Salim dk53)
48. Simba SC 0-0 Ndanda FC (Hakufungwa Ligi Kuu Mtwara)
49. Simba SC 0-1 Mbao FC (Alifungwa moja kwa penalti Ligi Kuu Mwanza)
50. Simba SC 3-1 Mwadui FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Shinyanga)
51. Simba SC 0-0 Yanga SC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
52. Simba SC 2-1 African Lyon (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
53. Simba SC 3-0 Stand United (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
54. Simba SC 5-1 Alliance FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
55. Simba SC 5-0 Ruvu Shooting FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
56. Simba SC 2-0 JKT Tanzania (Hakufungwa Ligi Kuu Mkwakwani)
57. Simba SC 0-0 Lipuli FC (Hakufungwa Ligi Kuu Uwanja wa Taifa)
58. Simba SC 4-1 Mbabane Swallows (Alifungwa moja Ligi ya Mabingwa Taifa)
59. Simba SC 4-0 Mbabane Swallows (Hakufungwa Ligi ya Mabingwa Manzini)
60. Simba SC 1-2 Nkana FC (Alifungwa mbili Ligi ya Mabingwa Afrika Kitwe)
61. Simba SC 3-1 Nkana FC (Alifungwa moja Ligi ya Mabingwa Afrika Taifa)
62. Simba SC 3-0 Singida United (Hakufungwa Ligi Kuu Uwanja wa Taifa)
63. Simba SC 1-0 KMKM (Hakufungwa Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
64. Simba SC 3-0 JS Saoura (Hakufungwa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Taifa)
65. Simba SC 0-5 AS Vita (Alifungwa tano Kundi D Ligi ya Mabingwa Kinshasa)
66. Simba SC 2-1 AFC Leopards (Alifungwa moja SportPesa Super Cup Taifa)
67. Simba SC 1-2 Bandari FC (Alifungwa mbili SportPesa Super Cup Taifa)
68. Simba SC 0-5 Al Ahly (Alifungwa tano Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Cairo)
69. Simba SC 3-0 Mwadui FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
70. Simba SC 1-0 Al Ahly (Hakufungwa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Dar)
71. Simba SC 1-0 Simba SC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
72. Simba SC 3-0 African Lyon (Hakufungwa Ligi Kuu Sheikh Amri Abeid)
73. Simba SC 3-1 Azam FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
74. Simba SC 3-1 Lipuli FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Samora)
75. Simba SC 2-0 Stand United (Hakufungwa Ligi Kuu Kambarage)
76. Simba SC 0-2 JS Saoura (Alifungwa mbili Kundi D Ligi ya Mabingwa Bechar)
77. Simba SC 2-1 AS Vita (Alifungwa moja Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika Dar)
78. Simba SC 0-0 TP Mazembe (Hakufungwa Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Dar)
79. Simba SC 1-4 TP Mazembe (Alifungwa 4 Robo Fainali Ligi ya Mabingwa, DRC)
80. Simba SC 2-1 Coastal Union (Alifungwa moja Ligi Kuu Mkwakwani, Tanga)
81. Simba SC 1-2 Kagera Sugar (Alifungwa moja, Ligi Kuu Kaitaba, Bukoba)
82. Simba SC 2-0 Alliance FC (Hakufungwa Ligi Kuu Kirumba, Mwanza)
83. Simba SC 2-1 KMC (Alifungwa moja Ligi Kuu Kirumba, Mwanza)
84. Simba SC 1-0 Tanzania Prisons (Hakufungwa Ligi Kuu, Sokoine)
85. Simba SC 8-1 Coastal Union (Alifungwa moja Ligi Kuu, Uhuru)
86. Simba SC 0-1 Kagera Sugar (Alifungwa moja Ligi Kuu, Uhuru)
87. Simba SC 0-0 Azam FC (Hakufungwa Ligi Kuu, Uhuru)
88. Simba SC 3-0 Mtibwa Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu, Uhuru)
89. Simba SC 2-0 Ndanda FC (Hakufungwa Ligi Kuu, Uhuru)
90. Simba SC 4-5 Sevilla (Alifungwa moja akampisha Deo Munishi dk46, Taifa)
91. Simba SC 4-0 Orbit Tvet (Hakufungwa, alimpisha Benno Rusternburg)
92. Simba SC 1-1 UD Songo (Alifungwa moja Ligi ya Mabingwa Taifa)
93. Simba SC 3-1 JKT Tanzania (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
94. Simba SC 2-1 Mtibwa Sugar (Alifungwa moja Ligi Kuu Uhuru)
95. Simba SC 3-0 Kagera Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu Kaitaba)
96. Simba SC 2-0 Biashara United (Hakufungwa Ligi Kuu Musoma)
97. Simba SC 1-0 Mashujaa FC (Hakufungwa Kirafiki Kigoma)
98. Simba SC 1-0 Azam FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
99. Simba SC 1-0 Singida United (Hakufungwa Ligi Kuu Arusha)
100. Simba SC 0-1 Mwadui FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Shinyanga)
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania
REKODI YA AISHI MANULA SIMBA
101. Simba SC 4-0 Mbeya City (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
102. Simba SC 0-0 Tanzania Prisons (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
103. Simba SC 3-0 Ruvu Shooting (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
104. Simba SC 2-0 KMC (Hakufungwa Ligi Kuu Uhuru)
105. Simba SC 2-0 Ndanda FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
106. Simba SC 2-2 Yanga SC (Alifungwa mbili Ligi Kuu Taifa)
107. Simba SC 3-0 JKT Tanzania (Hakufungwa Ligi Kuu Jamhuri)
108. Simba SC 1-0 Lipuli FC (Hakufungwa Ligi Kuu Samora)
109. Simba SC 1-0 Kagera Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
110. Simba SC 3-1 Biashara Unted (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
111. Simba SC 2-0 KMC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
112. Simba SC 3-2 Azam FC (Alifungwa mbili Ligi Kuu Taifa)
113. Simba SC 0-1 Yanga SC (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
114. Simba SC 8-0 Singida United (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
115. Simba SC 3-1 KMC (Alifungwa moja Kirafiki Mo Simba Arena)
116. Simba SC 1-1 Ruvu Shooting (Alifungwa moja Ligi Kuu Taifa)
117. Simba SC 3-0 Mwadui FC (Hakufungwa Ligi Kuu Taifa)
118. Simba SC 2-0 Mbeya City (Hakufungwa Ligi Kuu Sokoine)
119. Simba SC 2-0 Mbeya City (Hakufungwa Ligi Kuu Sokoine)
120. Simba SC 2-0 Azam FC (Hakufungwa Kombe la TFF Taifa)
121. Simba SC 0-0 Ndanda SC (Hakufungwa Ligi Kuu Nangwanda Sijaona)
122. Simba SC 4-1 Yanga SC (Alifungwa moja Kombe la TFF Taifa)
123. Simba SC 2-1 Polisi Tanzania (Alifungwa moja Ligi Kuu Ushirika, Moshi)
124. Simba SC 2-1 Namungo FC (Alifungwa moja Kombe la TFF Sumbawanga)
125. Simba SC 6-0 Vital’O (Alimpisha Beno dk46, hakufungwa Kirafiki Simba Day)
126. Simba SC 3-1 KMC (Alifungwa moja kirafiki Uhuru asubuhi)
127. Simba SC 2-0 Namungo FC (Hakufungwa Ngao ya Jamii Arusha)
128. Simba SC 2-1 Ihefu SC (Alifungwa moja Ligi Kuu Sokoine)
129. Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar (Alifungwa moja Ligi Kuu Jamhuri)
130. Simba SC 4-0 Biashara United (Hakufungwa Ligi Kuu Mkapa)
131. Simba SC 3-0 Gwambina FC (Hakufungwa Ligi Kuu Mkapa)
132. Simba SC 4-0 JKT Tanzania (Hakufungwa Ligi Kuu Jamhuri)
133. Simba SC 3-1 Mlandege SC (Alifungwa moja Kirafiki Chamazi)
134. Simba SC 0-1 Tanzania Prisons (Alifungwa moja Ligi Kuu Sumbawanga)
135. Simba SC 1-1 Yanga SC (Alifungwa moja Ligi Kuu Mkapa)
136. Simba SC 7-0 Coastal Union (Hakufungwa Ligi Kuu Sheikh Amri Abeid)
137. Simba SC 1-0 Plateau United (Hakufungwa Ligi ya Mabingwa Jos, NIgeria)
138. Simba SC 0-0 Plateau United (Hakufungwa Ligi ya Mabingwa Mkapa)
139. Simba SC 2-0 Polisi Tanzania (Alifungwa moja Ligi Kuu Mkapa)
140. Simba SC 1-0 Mbeya City (Hakufungwa Ligi Kuu, Sokoine)
141. Simba SC 1-0 KMC (Hakufungwa alimpisha Beno dk46 Ligi Kuu, Mkapa)
142. Simba SC 0-1 FC Platinums (Alifungwa moja Ligi ya Mabingwa, Harare)
143. Simba SC 4-0 Ihefu SC (Hakufungwa Ligi Kuu, Mkapa)
144. Simba SC 4-0 Platinums FC (Hakufungwa Ligi ya Mabingwa, Mkapa)
145. Simba SC 2-1 Dodoma Jiji FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Dodoma)
146. Simba SC 2-2 Azam FC FC (Alifungwa mbili Ligi Kuu Mkapa)
147. Simba SC 1-0 AS Vita (Hakufungwa Ligi ya Mabingwa Afrika – Kinshasa)
148. Simba SC 1-0 Biashara United (Hakufungwa Ligi Kuu Musoma)
149. Simba SC 1-0 Al Ahly (Hakufungwa Ligi ya Mabingwa Afrika – Mkapa)
150. Simba SC 3-0 African Lyon (Hakufungwa Kombe la TFF – Mkapa)
151. Simba SC 3-0 JKT Tanzania (Hakufungwa alimpisha Beno dk70 Ligi Kuu)
152. Simba SC 1-1 Tanzania Prisons (Alifungwa moja Ligi Kuu – Mkapa)
153. Simba SC 3-0 El Merreikh (Hakufungwa Ligi ya Mabingwa– Mkapa)
154. Simba SC 0-1 Al Ahly (Alifungwa moja Ligi ya Mabingwa – Cairo)
155. Simba SC 5-0 Mtibwa Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu – Mkapa)
156. Simba SC 1-0 Mwadui FC (Hakufungwa Ligi Kuu – Kambarage)
157. Simba SC 2-0 Kagera Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu – Kaitaba)
158. Simba SC 1-0 Gwambina FC (Hakufungwa Ligi Kuu – Gwambina)
159. Simba SC 3-1 Dodoma Jiji FC (Alifungwa moja Ligi Kuu – Mkapa)
160. Simba SC 2-1 Kagera Sugar (Alifungwa moja Kombe la TFF – Mkapa)
161. Simba SC 0-4 Kaizer Chiefs (Alifungwa nne Ligi ya Mabingwa – Johannesburg)
162. Simba SC 3-0 Kaizer Chiefs (Hakufungwa Ligi ya Mabingwa – Mkapa)
163. Simba SC 3-0 Dodoma Jiji FC (Hakufungwa Kombe la TFF – Mkapa)
164. Simba SC 3-1 Namungo FC (Alifungwa moja Ligi Kuu – Majaliwa, Ruangwa)
165. Simba SC 3-0 Ruvu Shooting FC (Hakufungwa Ligi Kuu – Kirumba, Mwanza)
166. Simba SC 1-0 Polisi Tanzania (Hakufungwa Ligi Kuu – Kirumba, Mwanza)
167. Simba SC 1-0 Azam FC (Hakufungwa Kombe la TFF – Songea)
168. Yanga SC 1-0 Simba SC (Alifungwa moja Ligi Kuu Mkapa)
169. Simba SC 2-0 KMC (Hakufungwa Ligi Kuu – Mkapa)
170. Simba SC 4-0 Namungo FC (Hakufungwa Ligi Kuu – Mkapa –mabingwa tayari)
171. Simba SC 1-0 Yanga SC (Hakufungwa Fainali Kombe la TFF – Kigoma)
172. Simba SC 0-1 TP Mazembe (Alifungwa moja Kirafiki Simba Day Mkapa)
173. Simba SC 2-1 Aigle Noir (Alimpisha Beno, alifungwa moja kirafiki Arusha)
174. Simba SC 0-1 Yanga SC (Alifungwa moja Ngao ya Jamii Mkapa)
175. Simba SC 0-0 Biashara United (Hakufungwa Ligi Kuu Musoma)
176. Simba SC 1-0 Dodoma Jiji FC (Hakufungwa Ligi Kuu Jamhuri)
177. Simba SC 2-0 Jwaneng Galaxy (Hakufungwa Ligi ya Mabingwa Gaborone)
178. Simba SC 1-3 Jwaneng Galaxy (Alifungwa tatu Ligi ya Mabingwa Mkapa)
179. Simba SC 1-0 Polisi Tanzania (Hakufungwa Ligi Kuu Mkapa)
180. Simba SC 0-0 Coastal Union (Hakufungwa Ligi Kuu Mkapa)
181. Simba SC 1-0 Namungo FC (Hakufungwa Ligi Kuu Mkapa)
182. Simba SC 3-1 Ruvu Shooting (Alifungwa moja Ligi Kuu Kirumba)
183. Simba SC 3-0 Red Arrows (Hakufungwa Kombe la Shirikisho Mkapa)
184. Simba SC 2-1 Geita Gold (Alifungwa moja Ligi Kuu Mkapa)
185. Simba SC 1-2 Red Arrows (Alifungwa mbili Kombe la Shirikisho Lusaka)
186. Simba SC 0-0 Yanga SC (Hakufungwa Ligi Kuu Mkapa)
187. Simba SC 4-1 KMC (Alifungwa moja Ligi Kuu Mwinyi, Tabora)
188. Simba SC 2-1 Azam FC (Alifungwa moja Ligi Kuu Mkapa)
189. Simba SC 0-0 Mlandege FC (Hakufungwa Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
190. Simba SC 2-0 Namungo FC (Hakufungwa Nusu Fainali Mapinduzi, Zanzibar)
191. Simba SC 1-0 Azam FC (Hakufungwa Fainali Mapinduzi, Zanzibar)
192. Simba SC 0-1 Mbeya City (Alifungwa moja Ligi Kuu Sokoine)
193. Simba SC 0-0 Mtibwa Sugar (Hakufungwa Ligi Kuu Manungu)
194. Simba SC 0-1 Kagera Sugar (Alifungwa moja Ligi Kuu Bukoba)
195. Simba SC 1-0- Tanzania Prisons (Hakufungwa Ligi Kuu Mkapa)
196. Simba SC 3-1 ASEC (Alifungwa moja Kombe la Shirikisho, Mkapa)
197. Simba SC 7-0 Ruvu (Hakufungwa alimpisha Abdul Salum dk46 Kombe la TFF)
198. Simba SC 1-1 USGendarmerie (Alifungwa moja Kombe la Shirikisho, Niamey)
199. Simba SC 0-2 RSB Berkane (Alifungwa mbili Kombe la Shirikisho, Morocco)
200. Simba SC 1-0 RSB Berkane (Hakufungwa Kombe la Shirikisho, Mkapa)
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Pablo Aweka Mkakati Mzito Robo Fainali Caf​

pablo-1.jpg

KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco, ameweka wazi kuwa hesabu zao ni kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika michezo yao iliyosalia ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ili kumaliza kileleni mwa msimamo wa Kundi D, hali itakayowafanya wapate ahueni ya kukutana na ‘kibonde’ katika michezo ya robo fainali.

Pablo anataka kikosi chake kimalize kinara wa Kundi D, kwa kuwa kanuni za mashindano zinampa nafasi ya kinara wa kundi kukutana na timu iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi jingine, ambayo kwa kawaida inakuwa kibonde kulinganisha na zile zilizomaliza vinara kwenye makundi yao.

Simba jana Jumapili walikuwa na kibarua cha mchezo wao wa nne wa hatua ya makundi dhidi ya RS Berkane ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam, ambapo wamesaliwa na michezo miwili tu kutamatisha hatua hiyo, ule wa ugenini dhidi ya ASEC Mimosas na wa nyumbani dhidi ya USGN.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kocha, Pablo alisema: “Malengo yetu kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho msimu huu ni kuhakikisha tunacheza angalau nusu fainali, na katika kufanikisha hilo ni wazi tunapaswa kufanya kazi kubwa katika michezo yetu ya mwisho ili kuhakikisha tunapata matokeo.

“Tunataka kumaliza kama vinara wa kundi hili, ambapo hiyo itatusaidia kwa kiasi kikubwa kukutana na mpinzani ambaye atakuwa sio kiongozi wa kundi jingine katika hatua ya mtoano jambo litakalotupa ahueni zaidi.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA SC WAONGEZA NGUVU KUIVAA ASEC JUMAPILI BENIN​


KIUNGO wa Simba SC, Jonas Gerlard Mkude akifanya mazoezi Gym kujiandaa na mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, ASEC Mimosas Jumapili Uwanja wa De l'Amitié Jijini nchini Benin.


Mshambuliaji wa Simba SC, Kibu Dennis Prosper akifanya mazoezi Gym kujiandaa na mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, ASEC Mimosas mwishoni mwa wiki nchini Benin.


Wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi Gym kujiandaa na mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, ASEC Mimosas mwishoni mwa wiki nchini Benin.
Simba inaongoza Kundi D kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na
ASEC Mimosas yenye pointi sita sawa na RSB Berkane ya Morocco, wakati USGN ya Niger inashika mkia kwa pointi zake nne baada ya mechi za awali kuelekea mbili za mwisho.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Msuva atupia, Simba ikiifunga Cambiasso​

simba-msuva.jpg

KLABU ya Simba imeibuka na ushindi na 2-1 kwenye mchezo katika mechi ya kirafiki dhidi ya Cambiasso kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena, uliopo Bunju.
Mshambuliaji Simon Msuva ni kati ya wachezaji wa Cambiasso ambao wanacheza mechi hiyo na kufanikiwa kufunga bao.
Msuva yupo nje ya timu yake ya Wydad ya Morocco, huku sababu ikitajwa na kudai maslahi yake na kukaa kwake Cambiasso ni kulinda kiwango chake.
Katika mchezo huo hadi wanaenda mapuziko ubao ulikuwa unasoma Simba 1-1 Cambiasso kwa mabao ya Simon Msuva na Erasto Nyoni.
Kipindi cha pili kiungo wa Simba, Clatous Chama alikosa penalti dakika ya 68, ambapo shuti lake liliishia mikononi mwa kipa wa Cambiasso.
Penalti hiyo, ilitokana na Bernard Morrison kuwapangua mabeki wa Cambiasso, kisha akaangushwa ndani ya 18 akiwa katika harakati ya kufunga.
Chama alifunga bao la pili dakika ya 76, ilikuwa kazi ya Yusufu Mhilu ambaye akipambana na mabeki wa Cambiasso, akitokea pembeni ya uwanja kisha kutoa pasi kwa mfungaji.
Mechi hiyo, ilichezwa dakika 78 Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1, yakifungwa na Erasto Nyoni, Clatous Chama kwa Cambiasso alifunga Simon Msuva.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Duh! Bocco Hajafunga Mechi 14​

SIMBA-9.jpg

MSHAMBULIAJI wa Simba, John Bocco hajafunga bao ndani ya ligi kwa msimu wa 2021/22 katika mechi 14 ambazo amecheza.
Ikumbukwe kwamba Bocco ni mshambuliaji na ana kibarua cha kutetea kiatu bora ambacho alitwaa baada ya kufunga mabao 16 na asisti mbili msimu wa 2020/21.
Msimu huu mambo yamekuwa magumu kwa nyota huyo mzawa ambaye amecheza mechi 14 na kuyeyusha dakika 617 uwanjani.
Kinara wa utupiaji Simba kwenye mabao 21 ambayo wamefunga ni Meddie Kagere mwenye mabao 6 na pasi moja ya bao