Ligi Kuu Thread

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Sheikh Amri Abeid kufumuliwa upya​

Sheik PIC

ARUSHA. CHAMA Cha Mapinduzi ambao ndio wamiliki wa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kimesema kinatarajia kutumia muda wa miezi mitatu kuufunga uwanja wao kwa ajili ya kufumua na kuotesha nyasi mpya za kisasa ili kubadili mwonekano wa uwanja huo eneo la kuchezea.
Akizungumzia hilo ofisini kwake, Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Gerald Munisi alisema wameona umuhimu wa kufanya hivyo baada ya nyasi hizo kuonekana kuzeeka hali inayochelewesha kurudisha ukijani wake hata ukimwagiwa maji baada ya kutumika.
“Tathimini kuwa tutatumia shilingi ngapi bado hatujafanya, kikubwa bado tunamalizana na mhusika wa kufumua nyasi hizo na baadae tutakuwa na vibarua wa kuotesha nyasi mpya tunazoamini zitapendezesha uwanja na kuwa mpya tena, maana nyasi hizi za miaka ya sabini kiukweli zimechoka,” alisema na kuongeza pia wanatarajia kurekebisha miundombinu yote kwa jumla.
“Huu uwanja una jina kubwa sana Tanzania na nje ya Tanzania lakini bila marekebisho na maboresho ya mara kwa mara utapoteza sifa zote, sisi kama chama tawala na wamiliki wake hatutaki hilo litukute hivyo niwaombe wadau watuelewe kwa hili.”
“Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wametupa dhamana ya kuwa wenyeji wa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la AFSC hivyo tunashukuru kwa sifa hiyo na hii inaonekana wana imani kubwa na uwanja wetu, na sisi hatutaki kupoteza heshima hii, ili tupate michezo mingine mikubwa ya ndani na ile ya kimataifa,” alisema
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Masau Bwire: Simu 9, Magrupu 286 ya WhatsApp​

masau pic

KATIKA watu wenye mbwembwe kwenye soka la Tanzania kwa sasa ni Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire. Ni miongoni mwa watu wenye vitu adhimu ambavyo vimetokea kuwakosha mashabiki wengi nje ya uwanja na hata kunogesha ushindani wa Ligi Kuu hasa kwa mechi zinazohusisha timu yake.

Mwanaspoti limefanya naye mahojiano maalumu na kueleza mambo mengi kuhusiana na yeye, timu yake pamoja na Ligi Kuu msimu huu. Hivi unajua ana simu ngapi?

Msemaji huyo anasema kumiliki kwake simu tisa kumetokana na waandishi wa habari, hivyo aliona achukue uamuzi huo ili iwe rahisi kwao kufanya naye mawasiliano.

“Ujue kuna muda wanahabari walikuwa wakinipigia simu na kuuliza swali sasa wakati nafafanua unakuta simu yake inakatika kiasi cha kushindwa kumaliza mazungumzo yetu. Nililichukua hilo na kuona ufumbuzi wake ni kuwa na kila laini ya mtandao.

“Nina laini tisa za mitandao tofauti, sasa mwanahabari akiwa mtandao fulani nampa namba inayoendana na yeye ili tumzungumze mpaka atakapotosheka,” anasema.

Licha ya kumiliki simu tisa, Bwire anasema ni ngumu kuishiwa bando kwenye simu hizo na amekuwa akiweka la kutosha, “siwezi kukueleza natumia bei gani kwa sababu kila mtandao una vifurushi vya gharama tofauti labda nianze kupiga hesabu.”

Hivi karibuni, Bwire anasema amepoteza simu karibu tatu kwenye mazingira tofauti.
“Bahati nzuri namba huwa nahifadhi kwenye google, hivyo nikiibiwa nanunua nyingine na mawasiliano yanaendelea bila tatizo lolote. Kuna moja niliibiwa barabarani kibaka alikwapua, nyingine uwanjani kwenye msongamano na mashabiki ambao walinizonga mpaka nikafikia kuwatishia.”



MAGRUPU WHATSAPP

Kati ya simu tisa za Bwire zipo nne ambazo ni za kisasa na moja kati ya hizo ipo yenye magrupu 286 ya Whatsapp.

“Huwa sizimi data, muda wote simu zangu huwa na chaji ni mara chache kukuta zimezima na zikizima zinazima zote kwa pamoja,” anasema.

“Nimekuwa nikijitahidi kupitia meseji na kujibu kila ambayo inahitaji ufafanuzi wangu japo muda mwingine huwa changamoto kutoka na wingi wake. Mara nyingi usiku nikiwa kitandani ndio napata muda wa kuzitazama meseji katika hayo magrupu na hata jambo langu tulivu nalifanya usiku mnene.”



NAFASI YAO KWENYE LIGI

Akizungumzia timu yake kwenye msimamo wa Ligi Kuu, Bwire anasema: “Kama sisi ni upepo mbaya tu tunaupitia, lakini timu yetu ni nzuri sana na ukishinda mechi moja unapanda juu, hivyo mpaka sasa hakuna ambaye ana uhakika wa ubingwa. Mechi bado nyingi sana.

Bwire anasema Ruvu Shooting ina uwezo wa kumaliza nafasi tano za juu na kushiriki kimataifa kwa kuwa uwezo huo inao.

Anasema yeye sio muumini wa mapro wengi katika timu za Ligi Kuu kwa kuwa hasara kubwa inakuja katika nchi.

“Ukiangalia wachezaji ambao wanaitwa Taifa Stars asilimia kubwa ni wale wa Simba, Yanga na Azam ambazo ndizo timu zenye mapro kibao, sasa shida inakuja timu ya Taifa tunakosa wachezaji kwa kuwa hata hao wazawa wa hizo timu wengi hawapati nafasi,” anasema Bwire.

Anasema Ruvu Shooting wana imani ipo siku watapata uwakilishi wa michuano ya kimataifa na wataiwakilisha vyema nchi wakiwa na nyota wazawa.



UBAGUZI WACHEZAJI

“Timu za Taifa zikiitwa unajiuliza wanatumia vigezo gani kuwaita? Maana wachezaji wakiwa timu ndogo hawaonekani, lakini huku wanakuwa bora ila wakienda Simba na Yanga tu siku hiyo hiyo wanaitwa Stars nashindwa kupata jibu,” anasema.

“Mfano halisi Oscar Joshua alitokea kwetu kwenda Yanga, lakini alivyotua tu Jangwani akaanza kuitwa timu ya Taifa na Hassan Dilunga naye alikuwa kwetu alipoenda Yanga sasa Simba akaanza kuitwa. Sasa najiuliza wanaochagua wachezaji wanatazama mechi za Simba na Yanga pekee au inakuwaje?”



GSM KUJITOA LIGI KUU

Hivi karibuni Bilionea Gharib Said ‘GSM’ alijiondoa kudhamini ligi licha ya timu kuanza kuvaa nembo yake katika mabega ya jezi zao isi-pokuwa Simba pekee ambayo iligomea udhamini huo.

“Nakumbuka siku sio nyingi kuna timu zilikuwa zinashindwa hadi kusafiri, kulipa mishahara na hata nyingine zilisafiri na ubwabwa kupunguza gharama za vyakula. Sasa anapojitokeza mtu kama huyu halafu tukampoteza ni majonzi makubwa,” anasema Bwire.Anasema wao Ruvu Shooting huo muda wote ambao walikuwa wakivaa jezi zenye nembo ya GSM na kuitangaza hawakuwahi kupata pesa na bado wataendelea kuvaa kwa kuwa jezi zao ni gharama mpaka kuagiza mpya haiwezi kuwa leo.

“Sisi jezi hatununui Kariakoo tunaagiza nje, sasa kitendo kilichotokea ni hasara kubwa kwa klabu wanatakiwa kutuangalia sisi timu za chini wanatusaidiaje hususan katika suala la jezi maana hauwezi kubandua logo begani, hapana, tunaendelea kumtangaza tu bila faida jambo ambalo sio sawa.”



SIMBA, YANGA MABATINI

Simba na Yanga wamecheza kwenye viwanja vidogo kama Manungu kule Morogoro hivyo hata Ruvu Shooting na wao wanataka mechi zao na vigogo hivyo vya soka nchini zipigwe kwao Mabatini, Pwani.

Bwire anasema anaamini hakuna kinachoshindikana kufanyika michezo hiyo Mabatini kwa kuwa kamati za ulinzi na usalama zina uwezo wa kulinda amani na mchezo ukachezwa vilivyo bila kuwa na shida yoyote.

“Tutaandika barua (TFF) ili msimu ujao tena tutumie uwanja wetu wa Mabatini ambao una sifa zaidi hata ya Manungu na sisi watu wetu wa Mlandizi wapate nafasi ya kuwaona nyota wao wakizichakaza Simba na Yanga,” anasema.



VIGOGO WANAMTAKA

Bwire anasema timu zote kubwa hapa nchini Simba, Yanga na Azam kwa nyakati tofauti zimehitaji nafasi ya yeye kuwa msemaji wao.

‘’Nakumbuka kipindi hicho nilikuwa Corefa (Chama cha Soka Pwani), Simba walinipigia (simu) nikawaambia siwezi. Ndipo nilipomsikia Haji Manara ametangazwa, niliamua kumpigia simu na kumpongeza na alifanya vizuri sana kazi hiyo,” anasema Bwire.

Baadaye Yanga wao walimtumia mwandishi mkubwa wa habari ili azungumze naye, lakini hakuwa tayari sawa na Azam FC ambao mtendaji mkuu wa zamani, Saad Kawemba alimfuata mwenyewe nako aliwagomea.

‘’Huyo mwandishi walidhani niko karibu naye, alinipigia simu na kuniambia unatakiwa kusema ndio ili leoleo utangazwe kuwa msemaji wa Yanga, nikamwambia waambie siko tayari. Siku nyingine nilikutana na Mkwasa (Charles) akiwa katibu (mkuu) wa Yanga akaniambia tena nikamwambia hapana.

‘’Nilijaribu kuwauliza waandishi wenzangu Jesse John na hayati Alex Kashasha wakanitania nenda kachukue mpunga wewe, mimi hapo akili yangu inajua inataka nini,” anaongeza Massau akisisitiza kwamba alikataa nafasi hizo kutokana na kuelewa umuhimu wake ndani ya Ruvu Shooting na alikotoka na timu hiyo ambayo ni zaidi ya fedha za harakaharaka kwa timu za Kariakoo.



JEZI/BARAKOA YA SIMBA

Bwire anasema siyo dhambi kuvaa vitu hivyo kwa kuwa mpira sio uhasama, bali ni burudani.

“Mimi nilipewa jezi ya Simba kutoka kwa Vunjabei mwenyewe, alinipatia zawadi sasa naikataaje hata Yanga wakinipa zawadi ya jezi yao nachukua tu siwezi kuikataa, halafu utasikia…sijui navaa barakoa ya Simba sasa kama kuna sehemu nimeenda inatakiwa kuvaa barakoa na ikawepo hata ya kampuni nyingine nikivaa ni kosa?

‘’Napenda sana timu ikiwa ina majukumu ya kuwakilisha nchi mimi naisapoti. Hata hao Yanga walikuwa wanacheza na moja ya timu kutoka Ethiopia nilihamasisha watu waisapoti niliandika kwa kirefu sana, nakumbuka ilikuwa mwaka 2017,” anasema Bwire.

Anasema kitendo cha mtu kupiga picha na watu fulani ikaonekana kuwa uko na watu hao sio vizuri kwa kuwa kuna maisha nje ya mpira ambayo kila mtu anayaishi.

“Nakumbuka barakoa ya Simba nilienda kwenye msiba wa Simba, kufika pale unatakiwa kuvaa barakoa na mimi sikuwa nayo ilinilazimu nivae hiyo ya Simba ambayo nilipewa msibani na nisingeweza kuikataa,” anasema.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Biashara Utd yapiga mkwara​

Biashara PIC

WACHEZAJI wa Biashara United wamekiri kuwa mechi yao ya kesho IJumaa dhidi ya Simba ni ngumu, lakini watafanya kama walichoifanyia Azam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kwani gari lao ndio limewaka hivyo.
Biashara ilikuja kuzindukia kwa Azam kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika Februari 22 baada ya timu hiyo kukaa siku 117 bila ushindi.
Tangu ilipopata ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Prisons, Oktoba 27 mwaka jana, Biashara haikushinda tena hadi iliposhinda kwa Azam lakini sasa wametamba kuwa gari ndio limewaka Simba ijipange.
Nahodha wa Biashara, Abdulmajid Mangalo alisema wamejiandaa kikamilifu kukabiliana na Simba na wana uhakika wa kufanya vizuri licha ya kwamba mechi itakuwa ngumu.
Naye mshambuliaji Atupele Green alisema wanaendelea na maandalizi ili kuhakikisha wanatoka na ushindi kujiweka salama kwenye msimamo wa ligi.
Katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu msimu huu timu hizo zilitoka suluhu mjini Musoma.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Malale akipigwa tu anatimuliwa Polisi​

Malale PIC

WAKIPIGWA tu, jamaa wanamtimua. Hivyo ndivyo ilivyo kwa Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini baada ya mabosi wake kumtega kwa kumpa mechi moja tu dhidi ya Azam itakayopigwa Jumapili ambapo kama timu hiyo itapoteza tena, basi kibarua chake kitaota nyasi.

Mechi hiyo ya Jumapili inatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam na inaelezwa matokeo mabovu inayopata timu hiyo imewafanya mabosi wote wa maafande hao kukutana Jumapili wakati chama lao likishuka dimbani kusikilizia matokeo yatakavyokuwa.

“Kutakuwa na kikao cha viongozi wote Jumapili na mchezo wa wa siku hiyo unaweza kutoa mustakabali wa kocha kujadiliwa kama tutapoteza lakini tukipata ushindi nadhani hiyo haitakuwa ajenda yetu.

“Moja ya lengo letu msimu huu ni kumaliza nafasi tano za juu lakini matokeo yanayoendelea sasa yanatufanya kujiuliza mara mbili tatizo lililopo ndani yetu,” alisema mmoja wa viongozi wa timu hiyo ambaye jina lake limehifadhiwa.

Hata hivyo, Malale alisema amefanyia kazi makosa aliyoyaona mchezo uliopita na anatarajia ushindani dhidi ya Azam FC huku akisisitiza matokeo mabaya wanayoyapata sasa ni upepo mbaya tu kikosi chao kipo imara. “Pamoja na matokeo mabaya yaliyopo ndani ya timu bado tuna nafasi ya kufikia lengo tulilojipangia kuanzia mwanzo wa msimu kwa kuhakikisha tunamaliza nafasi tano za juu kwa tulipo sasa tukishinda mechi mbili mfululizo tunapanda hadi nafasi ya tatu,” alisema.

“Ligi ni ngumu sana ni timu mbili tu ambazo zimekusanya pointi nyingi na kujihakikishia nafasi za juu lakini ukiangalia kuanzia nafasi ya tatu kushuka chini hakuna mwenye uhakika anayeshinda anapanda na mwingine anashuka.” Mara ya mwisho Polisi ilipata ushindi kwenye ligi Desemba 4, mwaka jana ilipoichapa Tanzania Prisons bao 1-0 mchezo uliopigw Uwanja wa Ushirika, Moshi.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Dodoma Jiji yaiwahi Simba mapemaaa​

Dom PIC

TIMU ya Dodoma Jiji bado haijakaa vyema licha ya kupata kocha mpya, Djuma Masoud, aliyechukua nafasi ya Mbwana Makatta na katika kulitambua hilo mabosi wa timu hiyo wameamua kujipanga mapema ili kuhakikisha inavuna pointi kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Simba na tayari wameweka kambi nje ya Jiji la Dar es Salaam.

Simba na Dodoma zitacheza Jumatatu ijayo kwenye pambano la Ligi Kuu Bara litakalopigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam mchezo unaotarajiwa kuanza saa 1 usiku.

Dodoma iliyolazimishwa sare ya bao 1-1 na Ruvu Shooting Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani mara baada ya mchezo huo iliamua kuweka kambi hukohuko Pwani ili kuliandaa jeshi kabla ya kuvaana na Simba iliyowafunga kwa bao 1-0 kwenye mechi yao ya duru la kwanza.

Habari ambazo Mwanaspoti limezipata kambi hiyo imewekwa ili wachezaji wasijichanganye mjini bali akili zao zijikite katika maandalizi ya mchezo ujao.

Mwanaspoti lilimtafuta Katibu mkuu wa timu hiyo, Johnson Fortunatus aliyekiri kuwa timu hiyo imebaki Pwani kwa lengo la kupata utulivu na wapo kwenye kambi nzuri. “Mchezo wa mwisho tumecheza na Ruvu. Tulifikia Kibaha (Camp) na ni sehemu nzuri tumeona itawapa wachezaji utulivu wa kutosha wakiwa wanajiandaa na mchezo huu,” alisema.

“Tunaendelea kuwajenga kisaikolojia ili watambue umuhimu wa kuhitaji pointi kwa kila mchezo.”
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

#TBT ZILITRENDI: Mahakama yamtimua kazi Mwakalebela​

Zengwe PIC

TAREHE kama ya leo yaani Machi 3, ila ndani ya mwaka 2008 iliripotiwa stori ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka (TFF), Fredrick Mwakalebela ni kama hana kazi baada ya mahakama ya kazi kumrejesha katibu mkuu wa zamani wa shirikisho hilo, Ashery Gassabile.
Uamuzi huo ulifikiwa baada ya mahakama hiyo kuridhika kwamba Gassabile aliondolewa TFF kimakosa.
Gassabile aliondolewa kazini mwaka 2006 akiwa katika muda wake wa (probation) wa miezi sita jambo ambalo lilimfanya asiajiriwe hivyo akaamua kukimbilia mahakamani.
Kamati ya Utendaji ya TFF haikuridhika na utendaji kazi wake Gassabile na kuamua kusitisha ajira yake na badala yake akaajiriwa Mwakalebela ambaye siku hiyo ya Machi 3, alikuwa mkoani Manyara kutatua mgogoro wa soka huko.
Habari zilizopatikana siku hiyo zilizema Gassabile ataanza kazi Jumatatu kama Katibu Mkuu wa TFF, lakini shirikisho hilo litakata rufani kupinga uamuzi huo.
Hata hivyo TFF ilisema Mwakalebela ataendelea na kazi zake zote kwa sababu Jumatatu yake wataenda kukata rufaa.
Kwa sasa Mwakalebela ni Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga baada ya kuchaguliwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Mei 4, 2019.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Simba: Fiston Mayele Akitufunga Tunampa Mbuzi​


274480447_373713300869546_3870057394497176153_n-1.jpg

MJUMBE wa Kamati ya Wazee ya Klabu ya Simba, Said Muchacho, amemuahidi kumpatia zawadi ya mbuzi mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele kama atafanikiwa kuifunga Simba katika michezo inayofuata ambayo watakutana.
Ahadi hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya shabiki mmoja wa Yanga kutoka Morogoro kumpa Mayele ng’ombe baada ya kufunga bao dhidi ya Mtibwa Sugar.
Tayari Simba na Yanga msimu huu zimekutana mara mbili, awali ilikuwa katika Ngao ya Jamii, Yanga ilishinda 1-0 kwa bao la Mayele, kisha suluhu ukiwa mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Timu hizo zinaweza kukutana tena katika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam endapo zote zitashinda mechi zao za robo fainali, huku pia zikiwa bado hazijacheza mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara inayotarajiwa kuchezwa Aprili, mwaka huu.
Ahadi hiyo ya Mzee Muchacho ameitoa pindi alipokutana na Mayele katika mazishi ya Baba wa Mmiliki wa Kampuni ya GSM, Ghalib Said Mohamed, Mzee Said Mohamed yaliyofanyika Machi Mosi, mwaka huu kwenye Makaburi ya Kisutu, Dar.
Akizungumza na Spoti Xtra, mzee Muchacho alisema: “Tayari nimeongea na Mayele, nimemuahidi kumpatia zawadi ya mbuzi kama atafanikiwa kutufunga Simba katika michezo ijayo ya Ligi Kuu na Kombe la FA, ningeweza kumuagizia hata ngamia kutoka nje ya nchi, lakini naamini zawadi ya mbuzi ni nzuri kwake.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mbeya Kwanza, City hakuna mbabe Songea​

mbeya pic

Licha ya kuhamia mjini Songea kwenye uwanja wa Majimaji, Mbeya Kwanza imeshindwa kutamba dhidi ya ndugu zao, Mbeya City kwa kulazimisha suluhu ya bila kufungana.

Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo ngeni Ligi Kuu kufikisha alama 14, huku City wakifikisha alama 25 baada ya timu zote kucheza mechi 17

Katika mchezo huo uliopigwa leo Jumamosi mkoani Ruvuma, wenyeji Mbeya Kwanza ndio walionekana zaidi kuwa na uchu wa alama tatu kutokana na mashambulizi waliyoyafanya haswa kipindi cha kwanza lakini mabeki wa City chini ya Hamad Waziri na Kipa wao, Deogratias Munish 'Dida' walikuwa katiri kuzuia hatari zote.

Straika na kinara wa mabao kwa Mbeya Kwanza, Habibu Kyombo mwenye mabao manne alipambana kulazimisha bao lakini mashuti yake yalipaa huku mengine yakizuiwa vyema na kufanya dakika 45 za awali kumalizika kwa suluhu.

Kipindi cha pili timu zote ziliingia na mipango zikifanya mabadiliko ambapo City waliwapumzisha Peter Mapunda, Paul Nonga na Frank Ikobela na kuingia, Joseph Ssemuju, Richardson Ng'ondya na Siraji Juma.

Kwa upande wa Mbeya Kwanza waliwatoa
Eliuta Mpepo, James Mwasote aliyeumia na kuwapa nafasi Waliam Edgar na Brown Mwankemwa japokuwa timu zote hazikuwa na wala hasara kwa mabadiliko hayo kutokana na kutoleta kitu kwenye matokeo.

Mbeya City walipambana zaidi kipindi cha pili kupitia kwa Ssemuju na Luizio lakini mipira yao haikuwa na macho kuliona lango na kufanya mpambano huo kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Matokeo hayo yanazifanya timu hizo za jijini Mbeya kutotambiana msimu huu ikiwa mechi ya raundi ya kwanza wakitoshana nguvu ya sare ya mabao 2-2 na leo ikiishia suluhu ya bila kufungana.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

NTIBA MCHEZAJI BORA, NABI KOCHA BORA FEBRUARI LIGI KUU​

AVvXsEhIm1P5F1hJGFeu2euDBv1fYZ3oQM9kz8m4EFDVrm_V5FuElNhADx8WeMfJroQ8kpXyYynmwS8-n8sPYXlaxoaJWzkus9yQ2OkcuKr5B4ioRMqjubk81-wzY-o8cRa0wzPZoVOoj36eTGtIRfS1wq7ui6oJyMnDEVZCttfW0KynKkabRx2Ol9p2r2Lw=w640-h504

KIUNGO Mrundi, Saido Ntibanzokiza ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mwezi Februari baada ya kuwapiku mchezaji mwenzake wa Yanga, mshambuliaji Mkongo Fiston Kalala Mayele na Relliant Lusajo wa Namungo FC.
AVvXsEithHz7suhyW5adBtE1tAu0YuSQlkEuB-RYU1WubOM9mGeJDHxDahisw3ZgsVoFoCCWvemjLAbYpg9LKrjVUg0XqC33QLEfzEXkK91LLvmGSh3ZjCTikTCH2vG29iD2QuIoVsE4gHXkZsnjDlTwWm5CxtOljHgAoPzpZH_YMMV-bV1n9to4JHds3hby=w640-h630

Kwa upande wake, kocha Mtunisia Nasredine Mohamed Nabi ameshinda tuzo ya Kocha Bora wa Februari dhidi ya Freddy Felix Minziro wa Geita Gold na Thierry Hitimana wa KMC.
AVvXsEhv-HBv3ZCxhJpmcuF_G7h7gBKmu23TsGT0Jk4KE3ACmD59ndheEkCuGJBWEg53wA8EE30GhVzeC8tWdhfoU6cArw1vpt18yFanxn2IVVIRmXqCDrVtC1zCziLRbRRlyzN-IHTTvvPWOkj7VTdSqpsSIxVBQBmIOR5XUaP0OeoSyPJ6IjEU-rY-ZN0U=w518-h640
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

City Gold, Mbinga United ni vita kali RCL Songea​

Mbeya. Matokeo ya kufungwa mabao 2-1 Mbinga United dhidi ya Stand FC kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa wa Mikoa (RCL) yameipunguza kasi timu hiyo ya mkoani Ruvuma, huku ikiipisha nafasi ya kwanza, City Gold kwenye kundi lao A.

Hadi sasa ikiwa inaingia raundi ya nne kwa timu hizo, City Gold ndio vinara kwenye kundi hilo ikiwa haijapoteza mchezo wowote kwenye michuano hiyo kwa kuwa na pointi tisa na kesho Jumanne itakuwa kazini kuwakabili Mbinga United ambao ni wenyeji kwenye kitu hicho.
Ikumbukwe timu mbili kutoka kila kundi zitaungana kucheza nane bora kupata timu mbili za kwenda moja kwa moja First League msimu ujao huku zile zitakazoshika nafasi ya tatu na nne zikicheza mtoano 'play off' ya kupanda dhidi ya zile za First League.
city pic 1

Katika mechi zilizochezwa jana jioni na leo mapema, Mbinga United walikubali kipondo cha mabao 2-1 dhidi ya Stand FC ya mkoani Mtwara ikiwa ni kipigo cha kwanza wa wenyeji hao kutoka wilayani Mbinga mkoani Ruvuma baada ya kucheza mechi tatu bila kupoteza ikiwa ni sare moja na kushinda mbili.
Kwa upande wa City Gold ya wilayani Chunya mkoani Mbeya, imeendeleza ubabe baada ya kushinda mchezo wake wa tatu na kupaa hadi kileleni kwa alama tisa na kuwashusha wenyeji wao.
Ushindi wa leo wa mabao 3-1 dhidi ya Mtama Boys ya mkoani Lindi umeifanya kujitanua na kuongeza matumaini ya kufuzu hatua ya nane bora ya michuano hiyo kusaka tiketi ya kupanda First League msimu ujao.
Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Mjaimaji mjini Songea, mabao ya washindi yaliwekwa wavuni na James Moradi dakika ya 23, Teddy Fredi dakika ya 39 na Arsu Mwasengu dakika ya 68.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Serikali Inatambua Mchango wa Chuo Cha IAA Kuendeleza Michezo​

01-scaled.jpg

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akiwa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Dkt. Cairo Mwaitete Machi 7, 2022 ambapo wamekutana na kufanya mazungumzo katika ofisi za wizara
hiyo zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Serikali inatambua na kuthamini mchango unaotolewa na Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) katika kuendeleza na kuimarisha sekta ya michezo nchini hatua inayosaidia kutoa ajira kwa vijana na kukuza pato la mtu mmoja mmoja na uchumi wa taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu alipokutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Cairo Mwaitete Machi 7, 2022 katika ofisi za wizara hiyo zilizopo
katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
“Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) ni mdau muhimu katika kulea vipaji kwenye sekta ya michezo nchini, wamekuwa na ushirikiano mzuri na Serikali kwenye michezo hatua inayosaidia kutoa mchango wao kuendeleza vipaji vya wanafunzi katika michezo mbalimbali” amesema Naibu Katibu Mkuu Bw. Yakubu.
Aidha, Bw. Yakubu ameongeza kuwa zaidi ya michezo, chuo hicho kimebobea pia kufundisha lugha mbalimbali ikiwemo Kiswahili na Kichina na kuwaelekeza washirikiane na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ili weweze kuwaandaa wataalamu wa lugha ya
Kiswahili kwa wageni ikizingatiwa jiji la Arusha ni kitovu cha wageni wengi wanaokuja nchini kwa kazi mbalimbali ikiwemo utalii.
“Hivi karibuni kutakuwa na kongamano la pili la kimataifa la idhaa zinazotangaza kwa lugha ya Kiswahili duniani ambapo mada mbalimbali zitatolewa na wabobezi wa Kiswahili, tumieni fursa hiyo muweze kuitangaza vizuri lugha yetu kimataifa” amesema
Naibu Katibu Mkuu Bw. Yakubu.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Dkt. Cairo Mwaitete amesema chuo hicho kinatoa ufadhili kwa kuwalipia ada ya chuo wanafunzi wenye vipaji vya michezo chuoni hapo ambapo hadi sasa zaidi ya wanafunzi 26 wamenufaika
na ufadhili huo.
“Chuo chetu kina idadi kubwa ya vijana wanaopenda michezo, tutaibua vipaji vingi katika taifa ili vijana waweze kujiajiri katika michezo kwa kuwa tunatambua usimamizi wa biashara kama biashara ikiwemo michezo” Dkt. Mwaitete.
Fauka ya hayo, Dkt. Mwaitete ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wanaoendelea kupa pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) ambapo wanandelea kujenga miundombinu ya michezo chuoni hapo ili chuo hicho kiweze kuwa kituo bora
cha michezo nchini na chuo hicho kinamatawi katika mikoa ya Manyara (Babati), Dodoma, Dar es salaam na Ruvuma (Songea).
Michezo inayofundishwa chuoni hapo ni pamoja na mpira wa miguu, mpira wa wavu, mpira wa kikapu, mpira wa netiboli pamoja na kutoa huduma za hosteli kwa timu za vijana za taifa zinapokuwa kwenye maandalizi mbalimbali ya michezo ya kimataifa.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Metacha atajwa kipigo cha Azam​

METACHA.png

KOCHA mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini ameweka wazi kuwa sababu kubwa ya ushindi wao wa juzi Jumamosi dhidi ya Azam ni ubora mkubwa aliokuwa nao kipa wao, Metacha Mnata katika kuokoa hatari zilizoelekezwa golini kwao. Juzi Jumamosi Polisi
Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, ushindi huo umeifanya Polisi Tanzania kufikisha pointi 22 zinazowaweka katika nafasi ya saba ya msimamo (kabla ya mchezo wa Geita Gold vs Yanga, jana Jumapili).
Kwenye mchezo huo, Metacha alionyesha kiwango bora na kufanikiwa kutoruhusu bao yaani ‘Clean sheet’, ambapo hii inakuwa Clean Sheet yake ya sita ndani ya Polisi Tanzania msimu huu.
Akizungumza na Championi Jumatatu, kocha Malale alisema: “Ulikuwa mchezo mzuri na mgumu kwetu hususan kwa kuwa tulikuwa na wachezaji wengi ambao walikuwa majeruhi, lakini jambo la muhimu ni kuwa tumefanikiwa kupata pointi tatu muhimu.
“Pia napenda kumpongeza kipa wangu Metacha Mnata ambaye ni wazi alikuwa kwenye kiwango bora Jumamosi, na naweza kusema bila yeye ingekuwa vigumu kupata ushindi.”
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

SIO ZENGWE: Si vyema Karia, wachambuzi kucharurana​

TFF PIC

WIKI iliyopita iliisha vibaya baada ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia kurusha kombora kwa wachambuzi wa soka ambao hivi sasa wamekuwa wengi, wakisifiwa na kupondwa.
Katika moja ya hafla, Karia alisema wachambuzi wanatakiwa kwenda kusoma kwanza kabla ya kurudi kufanya kazi hiyo ya uchambuzi “wa kila kitu” kuanzia mechi hadi masuala mengine ya maendeleo ya michezo.
Kauli hiyo imesababisha wachambuzi wahamaki na kutoa maneno makali kumjibu Karia, ambaye pia alizungumzia masuala mengine mengi, ikiwemo michuano ya mitaani, maarufu kwa jina la Ndondo ambayo kiutamaduni ilikuwa ikifanyika wakati msimu umeisha ili kuwapa nafasi wachezaji nyota wa klabu kubwa kurudi nyumbani kuungana na vijana wa mitaani kwao katika timu ambazo hazijasajiliwa.
Nimefuatilia mjadala na malumbano hayo, nikaona yanaelekea sehemu ambayo haiwezi kusaidia mpira wetu zaidi ya kupata mshindi katika malumbano. Na ushindi wake si muhimu kwa maendeleo ya mpira na badala yanaweza kutujengea imani potofu itakayochangia zaidi kuuporomosha.
Namuelewa Karia kwa kuwa alikuwa kiongozi wangu. Naelewa jinsi anavyozungumza na jinsi ambavyo anaweza kutoka nje ya mstari wakati anataka kueleza jambo muhimu sana.
Nakumbuka kule Arusha kwenye Mkutano Mkuu aliwahi kutamka neno ambalo lilitafsiriwa kuingiza siasa katika soka alipokuwa akiponda wapinzani. Nia yake ilikuwa kutaka kuzungumzia madhara ya upinzani usio na maana au usio muhimu, lakini akajikuta anataja majina ya wanasiasa.
Na nahisi katika hili la wachambuzi alitaka kumaanisha kusomea mifumo, falsafa na mambo muhimu katika mchezo, uongozi, biashara na mambo mengine ya soka.
Pengine anadhani wachambuzi wanahitaji ufahamu zaidi wa masuala yanayozunguka soka ili waweze kufanya kazi yao bila ya kuegemea upande mmoja au kuweka mbele maslahi binafsi.
Wenzetu hutumia watu waliowahi kucheza mpira kuchambua mechi kwa sababu hawa wanakuwa wamepitia chini ya walimu tofauti wenye ujuzi tofauti na pia mambo yanayozunguka maandalizi ya mchezo na hali ya mchezo yenyewe.
Hivyo, hawa si kwamba wamesomea kuwa wachambuzi bali wana ufahamu wa kutosha kuhusu mchezo na mechi zenyewe.
Hali kadhalika kwa viongozi au au waliojikita katika masuala ya uongozi huitwa kutoa maoni yao kuhusu masuala ya uongozi pale matatizo yanapotokea au mazuri yanapotokea. Vivyo hivyo kwa waamuzi na watu wa fani nyingine. Baadhi huwa wamesomea eneo wanalotoa maoni na wengine huwa na uzoefu na masuala yanayohusu eneo hilo.
Na wote hawa hawaajajiriwa kwa kutoa maoni au kuchambua, bali pengine hulipwa posho ya kulipia muda waliotumia kukaa studio au mafuta waliyotumia kwenda eneo la kuhojiwa.
Nitamani iwe na pengine ndicho alichomaanisha Karia ambacho kimetafsiriwa kama dongo kwa wachambuzi.
Kama nilivyowahi kuandika huko nyuma, uchambuzi ni muhimu katika uendeshaji mpira kama zilivyo sehemu nyingine kwa kuwa unasaidia viongozi, wachezaji, mashabiki na wadau wengine kuwa na ufahamu mpana wa kile wanachokifanya au kukipenda.
Na sio hilo tu, muda wanaotumia kujadili soka, unatangaza zaidi mchezo huo na hivyo umuhimu wao hauwezi kupuuzwa au kudhihakiwa.
Ndio! Kumekuwa na lawama nyingi kwa wachambuzi pengine kutokana na masihara wanayofanya wanapochambua, misimamo wanayoiweka badala ya kuhifadhi maneno. Mfano mtu anasema anaamini; “Hakuna mchezaji wa timu fulani mwenye uwezo wa kuchezea timu nyingine.” Hii ni dhahiri kuwa utaudhi mashabiki wa timu hiyo.
Mingine ni mijadala isiyo na kichwa wala miguu ya kulingankisha makocha au wachezaji, baadhi wakiapa kuwa fulani ndio bora hata kwa nini.
Hivyo, kama Karia anaungana na fikra hizo, alifikirie TFF ifanye nini kuboresha uchambuzi wao na kupata mafunzo mafupi ili kuwawezesha kupata ufahamu mkubwa wa uendeshaji mpira ili wachambue kwa usahihi zaidi na kuusaidia mchezo badala ya kutafuta majukwaa ya kucharurana.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MZEE WA UPUPU: Wamekumbwa na nini?​

dube pic

Ligi Kuu Bara iko katika mzunguko wa pili na timu zote zimeshacheza mechi 17. Ukweli mchungu kuhusu hilo ni kwamba hadi sasa wafungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, wana hali mbaya sana.
Ni wachezaji sita tu msimu uliopita ambao walifikisha tarakimu mbili kwenye idadi ya mabao yao, yaani walifunga mabao zaidi ya tisa...kuanzia kumi.
Wachezaji hao ni John Bocco (Simba) - mabao 16, Chris Mugalu (Simba) - mabao 15, Prince Dube (Azam) - mabao 14,
Maddie Kagere (Simba) - mabao 13, Idd Nado (Azam) - mabao 10 na Danny Lyanga (JKT TZ) - mabao 10,
Hao ndio wachezaji pekee msimu uliopita waliofunga mabao ya idadi ya tarakimu mbili na walitarajiwa msimu huu kuanzia walipoishia, lakini wapi.

JOHN BOCCO
Mfungaji bora mara mbili wa Ligi Kuu Bara 2011/12 na 2020/21. Tanzania inamtambua Bocco kama mmoja washambuliaji hatari katika kizazi chake.
Tangu ajiunge na Simba katika msimu wa 2017/18 akitokea Azam FC, Bocco amekuwa akifunga mabao zaidi ya 10 kila msimu, kasoro msimu mmoja tu - 2019/20 ambao alifunga mabao tisa.
Kwa ujumla huu ni msimu wa 14 kwake tangu aanze kucheza ligi kuu 2008/09 na ameshafunga mabao 142. Msimu wake wa kwanza, 2008/09, alifunga bao moja tu, na hii ni kutokana na uchanga wake wakati huo na wapinzani wake wa namba kikosini.
Yahya Tumbo, Nsa Job na Philip Alando walikuwa wachezaji wakubwa waliomzidi kila kitu. Hakupata namba mbele yao. Kukosa namba kukamfanya aonekane mzigo kikosini na alipendekezwa kukatwa mwisho wa msimu na mmoja wa makocha wake wazawa, lakini Mungu akamsimamia.
Msimu mwingine mgumu kwake ulikuwa 2014/15 ambao alifunga mabao matatu tu. Hata hivyo alitumia sehemu kubwa ya msimu huo akiuguza majeraha aliyoyapata Rwanda kwenye Kombe la Kagame alikoumizwa na Pascal Wawa (huyuhuyu) wa El Merreikh kwenye robo fainali.
Ukiacha misimu hiyo ambayo sababu zake zinaeleweka, Bocco hakuwahi kuwa na msimu mbaya kama huu. Hadi ligi inafika mchezo wa 17 hajafunga hata bao moja na amecheza asilimia kubwa ya mechi hizo.

CHRIS MUGALU
Alitokea Lusaka Power Dynamos ya Zambia akitajwa kama mmoja wa washambuliaji hatari wanapokuwa timamu kimwili. Na kweli, huko kuwa timamu kimwili hakukutajwa burebure au kwa bahati mbaya.
Maisha ya Mugalu ndani ya Simba yamekuwa ya kuumia umia sana. Sehemu kubwa ya maisha yake klabuni hapo ameitumia akiwa hospitali kutokana na majeraha. Mabao yake 15 msimu uliopita yalikaribia kumpa kiatu cha dhahabu cha ufungaji bora kama siyo penalti ya dakika za mwisho iliyopigwa na kufungwa na Bocco.
Hadi sasa Mugalu hajafunga hata bao moja kutokana na kukosekana uwanjani kwa muda mrefu.

PRINCE DUBE
Alikuwa na msimu mzuri 2020/21. Alifunga mabao ya kuunganisha kwenye mstari na alifunga mabao ya mbali. Alifunga kwa mguu wa kulia na akafunga kwa mguu wa kushoto. Alifunga kwa kichwa na alifunga tumbo. Alifunga kwelikweli.
Lakini, majeraha yaliyoanzia kwenye mchezo dhidi ya KMC pale Chamazi yalikuja kumgharimu baadaye na kumuweka nje msimu wote uliobaki na mwanzoni mwa msimu huu.
Tukiwa kwenye mechi za 17, Dube hajafunga hata bao moja la ligi.,Majeraha yake na mbinu sahihi za timu pinzani kumdhibiti vimempa wakati mgumu na kumfanya hadi sasa aonekane mchezaji wa kawaida.
Ujio wa Mzambia Rodgers Kola pia ni tatizo kwake kwani kocha Abdihamid Moallin anamtumia zaidi Mzambia kama mshambuliaji kinara huku Dube akitumika zaidi kama winga au msaidizi wa Kola.

MEDDIE KAGERE
Mfungaji bora katika misimu miwili mfululizo ya kabla ya msimu huu; 2018/19 na 2019/20. Msimu uliopita hakuonekana sana uwanjani kutokana misimamo ya kocha wake raia wa Ubelgiji, Van de Broeck.
Lakini, hata hivyo alijitutumua na angalau kufikisha mabao 13. Msimu huu ameshafunga mabao matano na kumfanya angalau kuwa na afadhali mbele ya wenzake. Lakini, hata hivyo ukiyachambua mabao yenyewe utaona kwamba naye ni walewale tu.
Mabao matatu kati ya hayo matano ameyafunga kwa penalti zenye utata. Mabao mengine mawili amefunga dhidi ya wapinzani walipopungua baada ya mchezaji mmoja kuony eshwa kadi nyek undu. Kwa hiyo hata yeye haone kani kama ni hatari kiasi hicho.

IDD NADO
M moja wa wachezaji waliokuwa na kiwango bora msimu uliopita. Alihusika katika mabao 18 ya Azam FC; akifunga mabao 10 na kutoa pasi nane zilizozaa mabao. Msimu huu hadi sasa amefunga bao moja tu.
Na hii inatokana na majeraha makubwa aliyoyapata Novemba 30, 2021 ambayo yanamuweka nje kwa miezi tisa. Lakini hata kabla hajaumia Nado alikuwa tayari ameshacheza mechi saba na kufunga bao moja pekee, ikiwa ni dalili za kuanza vibaya msimu.

DANNY LYANGA
Katika vinara wa mabao wa msimu uliopita, Danny Lyanga ndiye mchezaji anaichezea timu ambayo hakuwa nayo msimu uliopita. Alifunga mabao 10 akiwa na JKT Tanzania na sasa yuko Geita Gold ambayo ameshaifungia mabao manne.
Angalau yeye unaweza kumpa faida ya mashaka kwamba amefanya vizuri hadi sasa. Amefunga mabao safi kabisa bila utata wala tata. Ukizingatia yuko katika timu mpya na ambayo ni ngeni kwenye ligi unaweza kumpa heshima kwamba angalau kafanya vizuri.

SIMBA SC
Unapozungumzia vinara wa mabao siyo tu wachezaji, lakini hata timu pia zinahusika. Kwa misimu yote minne ambayo Simba SC wamekuwa mabingwa wa Tanzania wao ndio walikuwa vinara wa kupachika mabao. Lakini, msimu huu tukiwa katika mchezo wa 17 Simba hawajafikisha hata mabao 20.
Msimu uliopita katika mechi 17 walikuwa wameshafikisha mabao 40. Kuondoka kwa mashine zao mbili, Luis Miquisone na Clatous Chama kulipunguza uhatari katika safu ya ushambuliaji. Ukichanganya na tatizo lao kuu msimu huu la kukosa penalti, Simba wamekuwa wa kawaida sana mbele ya lango la mpinzani.

HITIMISHO
Bado kuna michezo 13 mbele na chochote kinaweza kutokea maana mpira wa miguu una maajabu yake. Lakini, hadi sasa kitu pekee ambacho unaweza kusema ni kwamba huu sio msimu bora kabisa kwa vinara wa mabao wa msimu uliopita.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mbeya City waipeleka Kagera Sugar ilipofia Simba​

mbeya pic

Mbeya. Baada ya kutumia zaidi ya masaa matatu kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Kagera Sugar, Mbeya City imefichua kilichowaangusha katika mechi zake tatu za nyuma, huku Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mathias Lule akisema amepata dawa.
City ilikuwa na matokeo mazuri ikiwamo kuzisimamisha timu kubwa, Simba, Yanga na Azam kwa kuvuna jumla ya pointi tano kwa miamba hao wa soka nchini lakini kwa sasa kasi yao imeonekana kupungua haswa kufululiza sare nyingi.

Timu hiyo ya jijini hapa mara ya mwisho kushinda mechi yake ilikuwa Januari 20 ilipoinyuka Ruvu Shooting bao 1-0 kwenye uwanja wa Sokoine na tangu hapo imekuwa ni sare na kupoteza.

Katika mechi nne za mwisho, timu hiyo imepoteza mchezo mmoja dhidi ya Namungo mabao 2-0 kisha suluhu dhidi ya Yanga sawa na Mbeya Kwanza na sare ya bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons.

Katika mechi hizo, timu hiyo ilikuwa ikijifua kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Iyunga,huku matokeo ya ushindi ikiwamo Simba walipoichakaza bao 1-0 walikuwa wameweka kambi viwanja vya Isyesye ambapo sasa wamerudi tena kujiwinda dhidi ya Kagera Sugar.

Akizungumza baada ya mazoezi ya leo Jumatano yaliyofanyika kwenye uwanja wa Isyesye, Lule amesema kukosa ushindi kwenye mechi zilizopita ni kutokana na uwanja waliokuwa wanatumia wa Shule ya Sekondari Iyunga na kwamba kwa sasa wamerejea Isyesye, hivyo mchezo na Kagera Sugar watashinda.

Pia amesema anafahamu mchezo huo utakuwa mgumu lakini kutokana na ukame waliopitia hawatakuwa na mzaha katika kupata alama tatu na kurudi kwenye nafasi nzuri.

"Tumeamua kurudi hapa uwanja wa Isyesye kuhakikisha mchezo ujao dhidi ya Kagera Sugar tunashinda, tulipokuwa hali haikuwa nzuri tunataka ushindi Jumamosi na kukaa nafasi nzuri, vijana wako fiti kila mmoja ana ari na morari kubwa," amesema Lule.

Timu hizo zinakutana ikiwa Mbeya City wamekusanya pointi 25 nafasi ya tano, huku Kagera Sugar wakiwa na alama 21 nafasi ya tisa baada ya pande zote kucheza mechi 17.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

YANGA NA KMC YASOGEZWA, KUCHEZWA NA SOMALIA JUMAMOSI​

AVvXsEiqiyXVxHU5iOm3IK_sUu5G9yAJ0HrR6ChCd6a0w_coROkqGtMM3Em8hIHq5q8LkT0YYUCbQGm_Wj-qtpo4jLH148dRC1AASqKQqB_bcgbBQAk_JX7d9vGXQA7WzkIEENJ5t2BcCaKHLrZvVFQ3lBB40LZBEQwBsM5J5rDYJTX63t72IYqe_wn3Kqoc=w640-h442

MECHI ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya wenyeji, Yanga SC dhidi ya KMC iliyopangwa kufanyika Machi 16, mwaka huu umesogezwa mbele hadi Machi 19 hapo hapo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
AVvXsEgPni0gKPzQi23xR481mrYX66Z4iAKPWq5CU3_1P2HaWyFh5ORQcQXRP9SfoL5zUZiNqXVzd1luvcsh59mC4DJ0ywiALDRrvyzdz7pFy3Z8wTlrDfgoYHKftfjR50gG4sJ94T3DRaDe1CVDAGF9X72o_YRMdWxpBJY8hk1mQtCYt93gFo4pMvM0CZuD=w556-h640
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Namungo Wadai Ubingwa Msimu Huu ni Wao​

NAMUNGO.png

KOCHA Msaidizi wa Namungo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amesema wao ndio watakaokuwa mabingwa mwisho wa msimu hata kama watu hawawapi nafasi.
Julio amesema, kila mechi ambayo wanakwenda kuicheza kwa sasa itakuwa ni kama fainali, kwa sababu wanahitaji kupata alama tatu ambazo zitawafanya wawe mabingwa mwisho wa msimu.
Namungo wanakamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, wakiwa na pointi 25, ambazo ni 20 nyuma ya vinara Yanga wenye pointi 45.
Akizungumza na Championi Ijumaa Julio aliweka bayana mipango yao ya kutaka ubingwa kwa kuwa wamekuwa na mipango madhubuti ya kuona hilo lengo lao linatimia kwa kuwa uwezo wa kufanya hivyo na nia wanayo.
“Namungo tunautaka ubingwa na tutaupata msimu huu, nimekuwa nikiwaambia watu kuhusu hiki mara kwa mara. Uwezo wa kufanya hivyo tunao kwa sababu ndiyo malengo tuliyojiwekea tangu tuchukue timu hii,” alisema Julio.