Yanga Thread

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Timu ya Wananchi leo Jumatano tutashuka Dimbani kwenye mchezo wetu wa kwanza Kombe la Mapinduzi, Zanzibar dhidi ya Taifa Jang’ombe ndani ya Dimba la Amaan. Wananchi burudani imevuka maji sasa inapatikana kwenye visiwa vya marashi ya karafuu.
1641373540336.png
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

YANGA YAINGIA MKATABA NA MAKAMPUNI MAWILI KWA MPIGO.​

1641457367972.png
MAKAMU Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, Mtendaji mkuu wa klabu, Senzo Mazingiza pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa Kilinet Mohammed Saleh na Mkuu wa bidhaa ya N-Card Khalifa Mwinyi wakisaini mkataba wa
makubaliano na Kampuni za KILINET na N-Cards kwa ajili ya kutengeneza kadi za kidigitali zitazokuwa zinatumiwa na wanachama, ikiwa ni sehemu ya hatua za awali za mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu. Kadi moja itauzwa kwa Sh. 29,000.
Yanga imeingia mkataba na kampuni za Kili- Net na N-Card kwa masuala tofauti - Kili Net – wakipewa jukumu la kusimamia na kuendesha mfumo Kidigitali, yaani kushughulikia Digital Plaoform za Yanga, usjaili wa wanachama na Social Media za klabu, wakati N-Card watafanya jukumu la kutengeneza kadi za uanachama ambazo zitawawezesha wanachama kununulia za Kielektroniki pia.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

KIPA WA YANGA, DJIGUI DIARRA AENDA MAKKA KUFANYA UMRAH.​

1641547254744.png
KIPA namba moja wa Yanga SC, Djigui Diarra amekwenda Makka kufanya ibada ya Hija ndogo, ijulikanayo kama Umrah kabla ya kwenda na timu yake ya taifa, Mali kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Cameroon.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Afisa Habari wa klabu ya Yanga Sc Hassan Bumbuli amethibitisha kuwa wachezaji wao waliokuwa Mapumzikoni na wengine waliokuwa kwenye majukumu ya timu zao za Taifa watajiunga na kikosi cha timu hiyo kilichopo Zanzibar Jumapili hii tayari kwa mechi zilizosalia za Mapinduzi Cup
Wachezaji hao ni:
✅
Fiston Mayele
🇨🇩

✅
Saido Ntibanzokinza
🇧🇮

✅
Djuma Shabani
🇨🇩

✅
Yannick Bangala
🇨🇩

✅
Mukoko Tonombe
🇨🇩

✅
Khalid Aucho
🇺🇬

Pamoja na kocha Mkuu Nasreddine Nabi
🇹🇳

1641633828767.png
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Mapema leo timu ya #wananchi tulipata fursa ya kwenda kutembelea Kituo cha Watoto Yatima Mzizini, Zanzibar. Huu umekuwa ni utamaduni wetu katika kurudisha kwa jamii na kuweza kufanya kilicho bora ili kuleta furaha kwenye maisha yetu.
1641634581242.png
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Kaze: Mabadiliko yametugharimu.​

1642057635024.png
Zanzibar. Yanga imetema taji la Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti 9-8, wakati dakika 90 za mchezo wa nusu fainali ukimalizika kwa suluhu.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, kocha msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze alisema vijana wake walichoshwa na kucheza mechi mfululizo huku akitumia vijana wengi waliokuwa wakikosa nafasi katika mechi nyingi za Ligi Kuu msimu huu.

Kaze alisema alilazimika pia kutumia wachezaji ambao walitoka mapumziko na kushindwa kuwa na utimamu wa mwili wa kutosha kwa ajili ya mchezo mgumu kama huo.
“Tulianza mashindano haya na vijana ambao walikosa nafasi mara nyingi katika mechi zetu za kimashindano lakini tukashindwa kuwa na wale wote wa kikosi cha kwanza ambao walikuwa mapumzikoni.
“Lakini mchezo umemalizika na tunawapongeza wapinzani, kwani hiyo si sababu ya kutosha kwa kupoteza mchezo, mwisho wa siku mshindi amepatikana na tutajipanga kwa mechi zetu zijazo za mashindano mengine,” alisema Kaze.
Kwa matokeo hayo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, jana, Azam FC sasa itakutana na mshindi kati ya Simba na Namungo, mchezo ambao ulichezwa saa 2 usiku, jana.
Mkwaju wa penalti ya beki wa kushoto wa Yanga, Yassin Mustaph ulimpa nafasi kiungo wa Azam FC, Mudathir Yahya kushinda mkwaju wake wa ushindi na kuipa timu yake nafasi ya kutinga fainali ya saba ya Kombe la Mapinduzi.
Yanga haikuonekana kuwa katika ubora wake uliozoeleka tangu kipinddi cha kwanza na kuwa na hatari chache katika lango la Azam, huku ikikosa mashuti yaliyolenga lango.
Yanga ilimwanzisha Herritier Makambo mwenye mabao mawili ya mashindano hayo, ambaye hata hivyo hakuwa na nafasi mbele ya mabeki wa Azam walioongozwa na Aggrey Morris na Daniel Amoah.
Kocha wa Yanga, Kaze alikibadilisha kikosi chake kilichoanza katika mechi mbili zilizopita, akiwarudisha kikosini Yannick Bangala na Fiston Mayele, ambaye aliingia kipindi cha pili.
Lakini pigo kwa Yanga ni kumpoteza kiungo wake mshambuliaji, Feisal Salum, ambaye alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kukaa chini mara mbili akilalamikia misuli ya paja.
Kwa upande wa Yanga, nyota wa zamani wa Simba, Ibrahim Ajibu alikuwa akiitumikia miamba hiyo katika mchezo wake wa tatu msimu huu, lakini bado hajafanikiwa kufanya makubwa.

Fainali ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuchezwa Januari 13, kwenye Uwanja wa Amaan
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mukoko aigomea Yanga, GSM aingilia kati.​

Mukoko PI

DILI la kiungo na nahodha msaidizi wa Yanga, Mukoko Tonombe kwenda TP Mazembe ya DR Congo, limekufa baada ya nyota huyo kugoma kutolewa kwa mkopo katika klabu hiyo, huku bilionea wa klabu hiyo Ghalib Mohamed ‘GSM’ akiingilia kati.
Mabosi wa Yanga walishakubaliana na mchezaji huyo kwenda Mazembe baada ya kuona hapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha Nasreddine Nabi, pia ili kupishana na Chico Ushindi ambaye jana alitambulishwa Tanga akitokea Mazembe.
Katika dili la Yanga kumtaka Ushindi walitaka kumpeleka Mukoko na makubaliano mengine ili kumpata winga huyo mwenye spidi na uwezo wa kuitumikia vizuri nafasi hiyo na tayari Mukoko alifanyiwa taratibu zote za kusafiri kwenda DR Congo pamoja na mambo mengine ya msingi ikiwemo kutumiwa tiketi ya ndege saa 9:00 alfajiri ya Jumamosi kwenda Lubumbashi kujiunga na kikosi hicho.
Hata hivyo, Mukoko aligomea safari hiyo na kwenda kuzungumza na mdhamini wa klabu ya Yanga, bilionea Ghalib Said Mohammed ‘GSM’ juu ya yote anayopitia.
Inaelezwa hatma ya katika kikao hicho kizito kati ya Mukoko na GSM, ilikuwa ni mchezaji huyo kutokwenda tena DR Congo kujiunga na Mazembe na badala yake kukatiwa tiketi ya kwenda Arusha kuisubiri Yanga iliyokuwa Tanga ikicheza na Coastal Union katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu jana Uwanja wa Mkwakwani.
Mukoko alisema mbali ya kufanya taratibu zote alishindwa kusafiri kutokana na kushindwa kufahamu hatma yake kwamba anaenda TP Mazembe kama mchezaji wa mkopo au anauzwa moja kwa moja na kumfanya amuone GSM.
“Bosi ameniambia nisiende kokote nitabaki hapa Yanga mpaka mwisho wa msimu utakapomalizika na baada ya hapo ndio kutakuwa na mazungumzo mengine kati yetu,” alisema Mukoko na kuongeza;
“Nimeambiwa keshokutwa nitapewa tiketi ya ndege kwenda kujiunga na timu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

YANGA SC WATUA ARUSHA KUMENYANA NA MBUNI​

AVvXsEhLZ7I60LMzvC9egXyuVqrpWa5WYCqZk22WVw83cAR8cpITZ12G6PPAiNyQ9KcackCHAV0UoIUhTbn6KMsLt_Q4mmIOy3iNB56dLp212ltRX8Uy2n7dcbF2CLonkRbQ2XJjk9F0uY_3af2vbXKBvLSWc9nd6ixIPFqGaWmKGj55GITBTtc-myAePQEc=w640-h640


VINARA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara tayari wapo Jijini Arusha kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya jeshi, Mbuni FC ya Monduli kesho kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MUKOKO AFUNGA PENALTI MBILI, YANGA YASHINDA 2-0 ARUSHA​

AVvXsEiH7VKtIEfiaiTmWggr-Vxp-EzE9Q9kS4HInJa_zzvjChRUZ9MO-o1DA76DtfiZdv8KPrMxfzAnxV_Yd_dF1ZyWo6wyTolGCEx-cOtJ1fVN6kH0mpcdjUgjgthH5ZBq2f1NfRG7uo01nD6tHI_7EMSUI_5ocnWVutF1GXT8PccHQ123CJfbr7Z2vord=w640-h544


VINARA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Mbuni FC ya Monduli katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Mabao yote ya Yanga yamefungwa na kiungo wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mukoko Tonombe aliyekuwa anacheza kama sentahafu leo.
Tonombe amefunga mabao yote hayo kwa penalti kipindi cha pili, la kwanza baada ya beki wa Mbuni kuunawa mpira kwenye boksi dakika ya 56 na la pili baada ya Mkongo mwenzake, Chico Ushindi kuangushwa kwenye boksi dakika ya 82.
AVvXsEjKJs_apY_HkzUjgzxJuoapFkQKpWiZKSfDruQ6R9Pfz675MpyUobsS79JkiZYwqP59k5tye7kzfds64bYCe3vfNVMHNlpfSIBQEHLwwjpUx0eeBdQN0weHYQ4Lig5U6zpQoLaXbWn3l090eJTgFIZG-HaCbrXlMzieeEW8-BpT-zSQUZ1Dq9a3JMni=w640-h612


Ushindi amecheza mechi ya kwanza Yanga leo baada ya kusajiliwa mwishoni mwa wiki kutoka TP Mazembe ya kwao, Kinshasa.
Yanga imeutumia mchezo huu kama sehemu ya maandalizi ya mechi yake ijayo ya Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Polisi Tanzania Jumapili Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Yanga Waishtukia Simba Kwa Bangala​

bangala-1.jpg

YANGA ni kama wameshtukia kitu vile, ni baada ya mabosi wa timu hiyo kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja kiraka wake Mkongomani, Yannick Bangala na kufikisha miaka miwili ya kuendelea kukipiga hapo.
Hiyo ikiwa ni siku chache tangu tetesi zienee za kiungo mkabaji wa timu hiyo, Mkongomani Mukoko Tonombe kugomea kuuzwa TP Mazembe ya nchini DR Congo.
Bangala alijiunga na Yanga katika msimu huu akitokea FAR Rabat ya nchini Morocco baada ya kuvunja mkataba wa kuendelea kukipiga huko kabla ya kutua Jangwani.
Mmoja wa mabosi wa timu hiyo, ameliambia Championi Jumatano kuwa, kiungo huyo wiki mbili zilizopita mabosi wa timu hiyo walimuongezea mkataba wa mwaka mmoja na kufikisha miwili baada ya ule wa awali
kubakisha miezi sita.
Bosi huyo alisema kuwa viongozi wa timu hiyo walishtukia kiraka huyo kuwepo katika mazungumzo na klabu yake ya zamani ya FAR Rabat aliyokuwa anaichezea.
Aliongeza kuwa pia uongozi wa timu hiyo ulishtukia kuzidiwa ujanja na watani wao Simba na haraka kumuongezea mkataba wa kuendelea kubakia kukipiga hapo kwa misimu miwili.
“Yanga ipo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji wake ambao mikataba yao imebakisha miezi sita na kati ya hao yupo Bangala ambaye tayari wamemuongezea mkataba wa mwaka mmoja.
“Bangala alisaini mkataba wa mwaka mmoja baadaya viongozi kuhofia kiwango chake, lakini baada ya kujiridhisha haraka wakamuongezea mkataba mwingine wa mwaka mmoja na kufikisha miwili.
“Kikubwa viongozi walihofia kutokea kile kilichotokea kama cha Morrison (Bernard) ambaye walimpa mkataba wa miezi sita wakati inaelekea kumalizika haraka Simba wakamuwahi na kumsajili,” alisema bosi huyo.
Alipotafutwa Ofisa Habari wa timu hiyo, Hassani Bumbuli kuzungumzia hilo simu yake ya mkononi
iliita bila ya mafanikio ya kupokelewa.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Kocha Yanga Amtaja Mshery.​

Aboutwalib-Hamidu-Mshery-1.jpg

KOCHA mpya wa makipa wa Yanga, Mbrazili, Milton Nienov amefunguka kuwa usajili wa kipa, Aboutwalib Mshery ni usajili bora kufanywa na klabu hiyo kutokana na ubora wake, Kocha huyo ameweka wazi kuwa ameanza na suala la kuhakikisha makipa wa timu hiyo wanahimili presha ya michezo mikubwa.
Milton alitambulishwa rasmi na Yanga Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ambapo alikuwa sehemu ya mashuhuda wa mchezo kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga huku Yanga wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Kabla ya kujiunga na Yanga, Milton alikuwa akihudumu kama kocha wa makipa wa Simba kabla ya kuachana nao Oktoba 26, mwaka jana muda mfupi baada ya Simba kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kuhusu kiwango cha makipa wa timu hiyo, Milton amesema:-“Siwezi kuzungumza mengi kuhusiana na uwezo wa makipa wetu kwa sasa, kwa kuwa ndiyo kwanza nimefika hapa lakini katika vipindi vichache vya mazoezi ambavyo nimekuwa pamoja nao naweza kusema tuna makipa bora sana.
“Huyu Mshery ni kijana mdogo na mwenye uwezo mkubwa sana, naamini ulikuwa usajili bora kwetu, niliona alikuwa na presha kidogo kwenye mchezo dhidi ya Coastal na nimepanga kuhakikisha nalifanyia kazi hilo kwa kuwa ni muhimu kwa kipa kuhimili presha ya michezo mikubwa ili kutofanya makosa,”.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Yanga: Tunazidi Kuimarika.​

YANGA-HATARI.jpeg

CEDRICK Kaze, Kocha Msaidizi wa Yanga ameweka wazi kwamba kikosi hicho kinazidi kuimarika taratibu kutokana na mechi ambazo wanacheza.
Mpaka sasa ndani ya Ligi Kuu Bara, Yanga haijapoteza mchezo kwenye ligi na inaongoza ligiikiwa na pointi 32.
Jana Januari 18, Yanga ilikuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni FC ambapo iliweza kushinda mabao 2-0 na mtupiaji alikuwa ni Tonombe Mukoko aliyefunga mabao hayo kwa penalti.
Kaze amesema:”Tunazidi kuimarika taratibu na kila mchezaji anajua kwamba kuna jambo ambalo tunahitaji kulifanya na tunazidi kupambana.
“Ushindi mbele ya Mbuni kwetu ni jambo kubwa hasa kuendelea kuwa kwenye hali ya kujiamini zaidi bado kazi inaendelea na tutazidi kupambana ili kupata matokeo zaidi,”.
Miongoni mwa nyota ambao walianza jana ni pamoja na Heritier Makambo huku Chico Ushindi yeye akianzia benhi na aliweza kupata muda wa kucheza pamoja na Crispiin Ngushi ambaye ni ingizo jipya pia kutoka Mbeya Kwanza.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Bacca Aaanza Kazi Yanga Kwa Mkwara.​

bacca.jpg

BEKI mpya wa Yanga, Ibrahim Abdallah ‘Bacca’ amesema licha ya kutua kwenye timu hiyo huku ikiwa na nyota kadhaa wa nafasi anayocheza, lakini bado anaamini kwa kipaji alichonacho atapambana na uamuzi wa mwisho utakuwa kwa kocha wao.
Akizungumza hivi karibuni Bacca alisema anaifahamu Yanga na hajakurupuka kumwaga wino, ila ameona nafasi yake ya kucheza nddio maana akajiunga timu hiyo huku akiweka wazi kuwa anawaheshimu wachezaji wote wa timu hiyo.
“Yanga ni timu ya presha kubwa kutokana na kuwa na mashabiki wengi ambao wanahitaji matokeo mazuri, hilo nalifahamu ila sitafanya makosa nawaomba wanipokee na kunipa ushirikiano ili niweze kuwa miongoni mwa wachezaji ambao watafanikisha malengo ya klabu,” alisema Bacca na kuongeza;
“Naheshimu uwezo wa Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na kaka yangu Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kila mmoja ana namna yake ya uchezaji na umuhimu wake kikosini kocha ndiye atakayeamua amtumie na amuache nani kwani hatuwezi kucheza wote.”
Beki huyo kutoka KMKM na aliyeng’ara katika michuano ya Mapinduzi alisema ametumia muda mwingi kuwafuatilia mastaa wanaocheza nafasi yake kwa kuangalia ubora wao na mapungufu yao ili aweze kuwa na vitu vya tofauti vitakavyompa ushawishi kocha kumpa nafasi anaamini hivyo ndio vitampa namba.
“Kucheza timu kama Yanga inahitaji ubunifu kila mchezaji anatamani kupata nafasi kama niliyoipata kwa kusajiliwa kinachofuata ni kujituma na kufanya vitu tofauti na waliokutangulia najiona nikiwa bora na kufanya tofauti,” alisema Bacca.