Msheri aanza vizuri, Yanga ikiichapa Dodoma
MWANZO mzuri kwa kipa wa Yanga, Abuutwalib Mshery baada ya kumaliza dakika 90 za mchezo wake wa kwanza bila kuruhusu bao.
Mshery alikuwa langoni akiiongoza Yanga wakati wakiichapa Dodoma 4-0 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Mkapa.
Katika kipindi cha kwanza Yanga walianza kwa kushambulia na kuonyesha hawataki utani zaidi ya kupata
Dakika 19 Yanga ilitaka kupata bao kupitia kwa Fiston Mayele ambaye aliwazidi mbio mabeki wa Dodoma na kupiga shuti na kupanguliwa kisha kuwa kona isiyokuwa na faida.
Dakika 22 Jamal Mtegeta alionyeshewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Saido Ntibazonkiza na kuwa faulo isiyokuwa na madhara.
Dakika 30 Yanga ilitaka kupata bao baada ya Emmanuel Martin kumfanyia madhambi Ntibazonkiza ambaye alipiga faulo nje kidogo ya goli lakini kipa wa Dodoma Jiji, Hussein Masalanga aliucheza.
Yanga ilifanya shambulizi lingine dakika 32 baada ya mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele aliyefyatuka shuti kali na kupanguliwa na kipa Masalanga na kuwa kona isiyokuwa na faida.
Dakika 38 Masalanga alifanya sevu nyingine baada ya Mayele
Dakika 40 Dodoma Jiji na wao walifanya shambulizi kupitia krosi fupi iliyopigwa na Khamis Mcha na Anuary Jabir alionganisha lakini uliishia mikononi kwa kipa.
Yanga ilipata bao dakika 42 baada ya Yassin Mustapha kupiga krosi na Mayele aliunganisha na kwenda wavuni.
Dakika 43 Dodoma walijibu shambulizi kupitia kwa Jamal Mtegeta baada ya kucheza pasi za haraka na Jabir ndani ya boksi na kufyatuka shuti kali liliopanguliwa na Mshery kisha mabeki waliokoa hatari.
Dakika 45 Dodoma walifanya shambulizi lingine baada ya kiungo Cleofas Mkandala kumipigia pasi Khamis Mcha aliyefyatuka shuti pa chinichini na kuishia mikononi kwa kipa Mshery.
Kwenye kipindi cha pili Yanga waliendelea kufanyw mashambulizi na kuonyesha kuhitaji mabao zaidi kwenye mchezo huu.
Yanga ilitaka kupata bao dakika 48 baada ya Ntibazonkiza kupiga pasi kwa Feisal ambaye alimchungulia kipana kupiga mpira mfupi uliombaa ambaa karibu na gori.
Dodoma walifanya mabadiliko dakika 54 ya kuingia Waziri Junior, Erick Nkosi na Joram Mgeveke wakichukua nafasi za Khamis Mcha, Mbwana Bakari na Hassan Nassor.
Dakika 56 Yanga ilipata bao la pili kupitia kwa Jesus Moloko baada ya Yanick Bangala kupiga mpira mrefu na Moloko aliuwahi na kuingia ndani ya boksi kidogo na kuupiga kwa juu na kwenda wavuni.
Dakika 62 Dodoma walifanya mabadiliko mabadiliko ya kumtoa Jamal Mtegeta na kuingia Seif Karihe.
Mabadiliko ya Dodoma yalionekana kuhitaji kusogeza mashambulizi mbele zaidi licha ya kuwa nyuma kwa mabao mawili.
Dakika 70 Feisal aliipata Yanga bao la tatu baada ya kupiga krosi akiwa upande wa kulia na beki wa Dodoa Jiji, Justine Bilary akiwa kwenye harakati za kuokoa alijifunga.
Wakati huo Yanga walifanya mabadiliko ya kuingia Heritier Makambo na Mukoko Tonombe wakichukua nafasi ya Fiston Mayele na Feisal Salum huku upande wa Dodoma walimtoa Emmanuel Martin na kuingia Agustino Nsata.
Dakika 81 Yanga ilipata bao la nne baada ya kupigwa pasi za haraka haraka na kiungo Khalid Aucho aliupiga mpira na kwenda wavuni.
Baada ya bao hilo mabadilio ya Mayele, Ntibazonkiza na Aucho huku wakiingia Deus Kaseke, Farid Mussa na Salum Abubakari ‘Sure Boy’, mabadiliko hayo yalionekana kushangiliwa na mashabiki.
Dakika 89 Dodoma Jiji nusura wapate bao la kufutia machozi baada ya Waziri Junior kumtoka Dickson Job na kupiga pasi kwa Mkandala aliyefyatuka shuti na kupita nje kidogo ya goli.