Ligi Kuu Thread

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

GSM, TFF warudi upya mezani​

New Content Item (1)




KAMA ulikuwa unadhani dili la udhamini wa Kampuni ya GSM katika Ligi Kuu Bara limekufa, pole yako kwani kampuni hiyo na Shirikisho la Soka nchini (TFF) wamerudi mezani kuujadili upya mkataba huo ili GSM iendelee kuidhamini ligi.
GSM ilitangaza kujitoa kama mdhamini mwenza wa Ligi, Februari 7 kwa madai ya kutotimizwa kwa makubaliano ya mkataba baina yao, TFF na Bodi ya Ligi (TPLB).
Uamuzi huo ulikuja zikiwa zimepita siku 76 tu, tangu waliposaini mkataba wa Sh2.1 bilioni Novemba 23, mwaka jana huku mkataba huo uliopingwa na Simba kueleza kutoutambua na kugomea kuvaa logo za udhamini huo.
Hata hivyo, juzi mmoja wa viongozi wa juu wa TFF aliyeombwa kuhifadhiwa jina lake, alilidokeza Mwanaspoti kuwa, tayari wameanza mazungumzo ya kuona ni namna gani GSM atarejea kuendelea kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu.
“Kinachofayika sasa ni kuona ni namna gani changamoto zilizojitokeza zinawekwa sawa na mazungumzo yanakwenda vizuri na kuna matumaini kwa kiasi fulani wa kupata muafaka wa jambo hili ili GSM arudi Ligi Kuu,” alisema kigogo huyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mnguto alipoulizwa kuhusu mpango huo alisema suala hilo liko chini ya Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao na Mkuu wa Idara ya Habari na Masoko, Boniface Wambura.
“Kitengo cha Habari na Masoko ndicho kinasimamia mchakato wote kuona ni namna gani jambo hilo linakwisha, ndio maana hata mabango ya GSM bado hayajatolewa tukitarajia kufikia muafaka na kuendelea na udhamini huo,” alidokeza kigogo huyo wa TFF.
Mkuu wa Idara ya Habari na Masoko wa TFF, Boniface Wambura alipotafutwa kwa siku tatu mfululizo ili kutoa ufafanuzi wa taarifa hizo, simu yake iliita bila kupokewa.
Hata hivyo, taarifa ya GSM kutaka kurudi ilipokelewa kwa shangwe na baadhi ya klabu za Ligi Kuu zikieleza kufurahishwa na mkakati huo kama utafanikiwa na kusisitiza kwamba zinahitaji udhamini kwa sasa kuliko kitu chochote.
“Maisha ya klabu yetu ni magumu mno, hivyo tunapopata udhamini kutoka sehemu tofauti tofauti inatusaidia kwa kiasi kikubwa,” alisema mwenyekiti wa moja ya klabu hizo.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Wanne wawekwa pembeni, City ikijiwinda na Prisons, Lule acharuka​

MBEYA PIC

Mbeya. Baada ya kuambulia kipigo katika mchezo uliopita, leo Alhamisi kikosi cha Mbeya City kimeendelea na mazoezi yake kujiandaa dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo utakaopigwa Jumapili katika uwanja wa Sokoine jijini hapa, huku wachezaji wanne wakipewa programu maalumu.
Katika mchezo uliopita City ilichezea kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Namungo, ambapo Jumapili hii watakuwa tena uwanjani kuwavaa ndugu zao, Prisons walio mkiani kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa alama 11.
Hata hivyo mchezo huo unatarajia kuwa wa visasi na heshima kwani City watahitaji kuendeleza rekodi ya ushindi, huku Wajelajela wakisaka alama tatu ili kufuta uteja na kujikwamua mkiani na kufanya timu hizo kuwa na maandalizi ya ukweli ili kufikia malengo.
Prisons chini ya Kocha wake, Patrick Odhiambo haijapata ushindi wala sare katika mechi nne za Ligi Kuu wakicheza vichapo tu, hivyo kufanya mpambano huo kuwa wa kufa na kupona kusaka ushindi wa kwanza ili kurejesha matumaini kwa mashabiki na mabosi lakini zaidi kulinda kibarua chake.
Katika mazoezi ya leo kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Iyunga, timu hiyo ilionekana kuelekeza nguvu kwenye pumzi, pasi na kufunga mabao, huku Kocha wa timu hiyo, Mathias Lule akiwafokea nyota wake walioonekana kutofuata maelekezo yake.
Pia Lule aliwatenga wachezaji wanne, mabeki David Mwasa aliyerejea baada ya kukaa nje muda mrefu akiuguza majeraha, Hamad Waziri na Seleman Boban pamoja na Straika Juma Luizio ambao walikuwa na programu yao maalumu walijikita kukimbia kuuzunguka uwanja.
Akizungumza wakati wa mazoezi hayo, Lule amesema anafahamu mchezo huo kuwa na ushindani lakini matarajio yao ni kusahihisha makosa yao na kupata alama tatu na kurudi nafasi yao ya nne huku akifafanua kuwa anaamini vijana wake watafanya vizuri.
"Kipigo cha juzi dhidi ya Namungo kimetuamsha, tunaendelea na maandalizi kuhakikisha mchezo ujao na Prisons tunapata matokeo mazuri, tulifanya makosa ambayo yalitugharimu hivyo hatutarajii kuyarudia" amesema Lule.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Djuma aanza na pumzi​

djuma pic

Kocha mpya wa timu ya Dodoma Jiji Masoud Jumaa ameanza rasmi kibarua cha kukinoa kikosi cha timu hiyo leo katika uwanja wa Jamhuri jijini hapa.
Masoud anachukua nafasi ya Mbwana Makata ambaye hivi karibuni amefungashiwa virago na uongozi wa timu hiyo sababu zikitajwa ni kutoridhishwa na matokeo ya timu hiyo.
Katika mazoezi ya Leo yaliyoanza majira ya saa 10 jioni Kocha huyo alianza kwa kutambulishwa kwa wachezaji na uongozi wa timu hiyo na kisha kuanza mazoezi ya mbio.
Akiwa na kocha Msaidizi Mohammed Muya,Jumaa alionekana kusisitizia mazoezi ya kutafuta pumzi ambapo muda wote alikuwa akibadilisha Koni na wachezaji wakikimbia katika koni hizo.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Kifo cha Sonso chaitesa Ruvu​

Sonso pic

KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Boniface Mkwasa ‘Master’ amesema msiba wa beki wao, Ally Mtoni ‘Sonso’ bado unawatesa nyota wa kikosi cha timu hiyo na kama kocha ameamua kukomalia kuwajenga kisaikolojia ili wakae sawa.
Nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, alisema licha ya ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Tanzania Prisons bado amewaona wachezaji wake hawako vizuri kutokana na kuondokewa na mchezaji mwenzao.
“Itawachukua muda kidogo kurudi katika hali yao ya kawaida ukizingatia hata mchezaji aliyekuwa akilala naye chumba kimoja bado hajawa sawa kisaikolojia, hivyo naendelea kuwajenga li kurejea kwenye hali zao za kawaida,” alisema Mkwasa na kuongeza;
“Tunaendelea na maandalizi ya michezo yetu inayofuata, kama unavyojua hatupo katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi, hivyo tunahitaji kupambana ili tuweze kujinasua kwenye nafasi za chini.”
Sonso aliyewahi kuzichezea Lipuli, Yanga, Kagera Sugar na pia timu ya taifa, Taifa Stars alifariki dunia Februari 11, 2022, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na matatizo ya mguu.
Ruvu kwa sasa ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 15 baada ya kushuka uwanjani katika mechi 15, ikishinda nne, sare tatu na kupoteza nane.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

GEITA, NAMUNGO ZAFUNGUA MZUNGUKO WA PILI KWA SARE​

AVvXsEiz7bYdRGiaEvVqmUHJCnsyfMKwxf2W6isbaCOZNuIra1qeKmDVZdj5kL6eCDKXw1mYxGBJvy2bIxpAcUy3H-mskoKQaB5QpRm-K24FDc-cPnCwmIvznq_2L1EI2LqRiMuYGZdO7oF4I5K__6I4IhEgaSU9JDym_f4cgsLKO8WMePgTgEsfZz85Shm0=w640-h480

WENYEJI, Geita Gold wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC katika mchezo wa kwanza kabisa wa duru la pili Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
Geita Gold walitangulia kwa bao la George Mpole dakika ya 73, hilo likiwa bao lake la nane la msimu, kabla ya Iddi Farjala kuisawazishia Namungo FC dakika ya 84.
Kwa sare hiyo, Namungo FC inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 16, ikizidiwa wastani wa mabao tu na Azam FC zikifuatana nafasi ya tatu na ya nne, wakati Geita Gold inafikisha pointi 21 mechi 16 nafasi ya sita.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MBEYA CITY YAICHOMOLEA PRISONS JIONI KABISA, 1-1​

AVvXsEgwztlKVj2UubrsDTSfEqxyekSNJrVbOIhTNwj1Z0VhTj4-3SrtL-SiOzLouoh9hYeWm3s4aR8XCn-A2FEZgclqQpb9-A_xo-WwoubJ2kw0SMP1P9j36ayalXKyO7UyxfvqP2VAm9vfTwpKEoDrPbcRzYt-TsvlXYGHk1m5QNaNSPMQZtdkMMtLXGOd=w640-h456

TIMU za Tanzania Prisons na Mbeya City zimegawana pointi baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Adili Buha alianza kuifungia Prisons dakika ya saba, kabla ya Ssemuju Joseph kuisawazishia Mbeya City dakika ya 86.
Kwa sare hiyo, Mbeya City inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 16, ingawa inabaki nafasi ya tano, ikizidiwa tu wastani wa mabao na Azam FC ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Hali ni mbaya kwa Tanzania Prisons ambayo baada ya sare ya leo inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 16 na kuendelea kuzibeba timu nyingine 15 kwenye Ligi Kuu.
Mechi iliyotangulia mchana wa leo, wenyeji, Ruvu Shooting wamelazimishwa sare ya 1-1 pia na Dodoma Jiji FC Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
Waziri Junior alianza kuifungia Dodoma Jiji dakika ya 11, kabla ya Abrahman Mussa kuisawazishia Ruvu Shooting dakika ya 58.
Ruvu Shooting inafikisha pointi 16 katika mchezo wa 16 na kurejea nafasi ya 12, wakati Dodoma Jiji wanafikisha pointi 18 katika mchezo wa 16 na kusogea nafasi ya 10.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Mechi za leo za Ligi Kuu ya NBC
🇹🇿

Mbeya Kwanza vs. Mtibwa Sugar
🏟
Sokoine
Kmc Fc vs. Polisi Tanzania
🏟
Azam Complex
#NbcPremierLeague
🇹🇿

MTIBWA SUGAR YAICHAPA MBEYA KWANZA 2-1 SOKOINE​



TIMU ya Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Mayanja Mululi dakika ya 38 na Omary Sultan dakika ya 75, wakati la Mbeya Kwanza limefungwa na Habib Kyombo kwa penalti dakika ya 41.
Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya 13, wakati Mbeya Kwanza inabaki na pointi zake 13, ikishukia nafasi ya 15 katika ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MTIBWA SUGAR YAICHAPA MBEYA KWANZA 2-1 SOKOINE​



TIMU ya Mtibwa Sugar imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Mbeya Kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Mayanja Mululi dakika ya 38 na Omary Sultan dakika ya 75, wakati la Mbeya Kwanza limefungwa na Habib Kyombo kwa penalti dakika ya 41.
Kwa ushindi huo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya 13, wakati Mbeya Kwanza inabaki na pointi zake 13, ikishukia nafasi ya 15 katika ligi ya timu 16, ambayo mwisho wa msimu mbili zitashuka na mbili zitakwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kubaki Ligi Kuu.
Mechi za leo za Ligi Kuu ya NBC
🇹🇿

Mbeya Kwanza vs. Mtibwa Sugar
🏟
Sokoine
Kmc Fc vs. Polisi Tanzania
🏟
Azam Complex
#NbcPremierLeague
🇹🇿

KMC YAIMIMINI​


A POLISI TZ 3-1 CHAMAZI​

WENYEJI, KMC imeibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya KMC yamefungwa na Iddi Kipagwile dakika ya 15, Emmanuel Mvuyekure dakika ya 73 na Sadallah Lipangile dakika ya 88.
Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 22 katika nafasi ya sita, wakati Polisi Tanzania inabaki na pointi zake 19 katika nafasi ya tisa baada ya wote kucheza mechi 16.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MJUAJI: Rais alitaka Simba, Yanga jengo moja​

Simba, Yanga PIC

UTAJUA haujui. Wanasiasa huwa na mambo yao! Mara nyingi huja na mipango ambayo wakati mwingine haiwezekani kutekelezeka.
Sijui ingekuwaje leo hii kutokana na uhasama uliopo kati ya Simba na Yanga, maana zimeshatoka kwenye utani wa jadi na kuwa na uadui mkubwa. Jambo hili lilitakiwa litokeee mwaka 1970.
Simba na Yanga zilitakiwa ziishi kwenye jengo moja ambalo lingejengwa kutokana na pesa za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Hadi leo hii haijulikani jengo hilo lingejengwa maeneo gani, Kama ni Jangwani au Msimbazi. Wakati huo Simba ikiwa na maskani yake katika Mitaa ya Mchikichi na Congo, Kariakoo jijini Dar es Salaam ilikataa mpango huo.
Chini ya uongozi wa Rais ya Simba, Ramadhani Kilundu na makamu wake, Juma Mzee, klabu hiyo iligomea mpango huo wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania na Rais wa Zanzibar Abeid Amaan Karume.
Rais Karume aliwafuata viongozi hao na kuwaambia kwa kuwa wote ni wanamichezo na ni ndugu moja, walipaswa kuwa pamoja na kuendeleza udugu kwa kuishi kwenye jengo moja.
Ikumbukwe awali, Simba na Yanga zilikuwa timu moja zikiundwa na wakazi wa Dar es Salaam na wote walishiriki katika kupigania Uhuru wa Tanzania. Mbali na wanasiasa wengine walikuwapo kina Rashid Kawawa na Abdul Sykes ambao walikuwa mashabiki wa Simba ile kindakindaki.
Viongozi wa Simba ambayo awali ilikuwa ikiitwa Sunderland walikataa mpango huo, huku wakifahamu kuwa Rais Karume alikuwa akiishabikia Yanga na wao hawakutaka kuishi pamoja na watani wao. Baada ya Simba kugomea, Rais Karume aliwapa kiasi kidogo cha pesa na kingine kikubwa zaidi alikipeleka kwenda kujenga jengo la Yanga pale katika mitaa ya Twiga na Jangwani jijini Dar es Salaam.
Kiasi kidogo walichopewa Simba waliongeza na michango ya wanachama wao, huku baadhi yao wakijitolea na kununua na kufyatua matofali na kufanikiwa kujenga jengo lililopo Mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Simba ndio ilikuwa ya kwanza kumaliza jengo lao na kufuatiwa na Yanga na yote yalifunguliwa na Rais wa Zanzibar, Karume mwaka 1971. Mara nyingi viongozi wetu huwa wanakuja na mipango migumu kutekelezwa na kuwaacha watu midomo wazi na mipango mingi huwa inafeli.
Mfano Rais wa Kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta aliwahi kutaka Mashemeji Dabi ichezwe kila wikiendi kutokana na fedha nyingi ambazo zilikuwa zinaingizwa na timu za Gor Mahia na AFC Leopards. Mpango huo ulifeli. Ni kama ulivyofeli mpango mwingine wa Rais wa Kenya aliyemfuata Kenyatta, Daniel Moi. Yeye alinogewa na mafanikio ya Timu ya Taifa ya Kenya, Harambee Stars miaka ya 90.
Moi alitaka Harambee Stars ikiwa katika ubora wake iwe timu ya kudumu, yaani wachezaji wa timu hiyo wasizitumikie timu nyingine isipokuwa Harambe Stars tu!
Moi alikuwa tayari kuwapa nyumba za kuishi wachezaji wa Harambe Stars maeneo ya Kasarani karibu kabisa na ulipo uwanja mkubwa wa taifa hilo uliojengwa katika utawala wake wa Moi Kasarani.
Jambo hilo nalo lilishindikana, nyumba zilizojengwa zikapewa jeshi la Polisi la nchi hiyo! Juzi tu katika Afcon kule Cameroon, Rais wa Guinea, Mamady Doumbouya aliwataka wachezaji wa nchi hiyo kubeba taji hilo la sivyo warudishe gharama zote walizotumia. Hayati Rais John Magufuli aliwahi kutamani kuwachukua wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kutoka jeshini. Kikubwa alichokuwa akikitaka Magufuli ni wachezaji kucheza kwa uzalendo ili kuisaidia timu ifanye vizuri zaidi kimataifa.
Kali zaidi Rais wa Ivory Coast, Félix Houphouët-Boigny
aliwahi kuipeleka timu ya taifa ya nchi yake jeshini na kwenda kuwapigasha kwata mbele ya bendera ya taifa ili kuwafundisha uzalendo. Kitendo hicho kilizaa matunda kwani mwaka 1992, Ivory Coast ilitwaa ubingwa wa Afcon kwa kuifunga Ghana kwa penalti 11-10.

Simba, Yanga zikae jengo moja? Tupe maoni yako;
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Bao La Mayele Lampa Ugonjwa Kifaru​

122768385_200237015002006_326846353485678896_n.jpg

BAO alilofunga mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, limesababisha msemaji timu hiyo, Thobias Kifaru apate homa ya ghafla iliyomfanya akae kimya kwa muda kupambania afya yake.
Yanga na Mtibwa zilikutana hivi karibuni katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa mkoani Morogoro ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Saido Ntibazonkiza na Fiston Mayele.
Ikumbukwe siku chache kabla ya mchezo huo, msemaji huyo aliweka wazi mikakati yao ya kuhakikisha wanaifunga Yanga ikiwemo kumzuia mshambuliaji wao hatari Fiston Mayele kwa kumpa kazi kumkaba beki wao Ibrahim Ame lakini haikuweza kusaidia wasifungwe na mshambuliaji huyo.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Kifaru alisema kuwa amekuwa kimya kwa muda baada ya mchezo dhidi ya Yanga kwa kuwa alikuwa akiumwa baada ya kupata homa iliyotokana na maumivu ya kufungwa na Yanga.
“Tumeanza kukaa sawa kwa sababu tumefanikiwa kushinda mchezo wetu wa kwanza wa mzunguko wa pili dhidi ya Mbeya Kwanza lakini nilikuwa kimya kwa sababu niliumwa baada ya mchezo wetu na Yanga hivyo nikawa napambania afya yangu kwa kuamua kukaa kimya.
“Kiukweli sikupendezwa na matokeo yale hasa safu ya ulinzi ilikuwa hovyo kabisa, sikutaka kusema kama nilikuwa naumwa ila yale matokeo yalinipa maumivu makali sana kutokana na historia ya hii timu jinsi ambavyo tuliianzisha mwaka 1983 lakini inaoneka vijana hawajui maumivu tunayopata,” alisema Kifaru.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Yanga waiteta Simba kambini​

Mayele PIC

VIGOGO wa Yanga wakiongozwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk. Mshindo Msolla juzi walitimba kambi ya kikosi hicho na kufanya kikao kizito na wachezaji, kubwa ni kupeana michongo mizima ya kuhakikisha msimu huu wanabeba ndoo ya Bara.
Yanga kwa misimu minne mfululizo imekuwa ikitoka kapa kwenye Ligi Kuu Bara, lakini safari hii mabosi wa klabu hiyo wamegoma kuwaachia watani wao Simba kubeba tena ndoo ya msimu huu na ndipo juzi wakaamua kutinga kambini na kuteta na wachezaji wao wakipeanda mikakati ya kulirejesha taji Jangwani.
Ipo hivi. Dk Msolla akiambatana na wengine wakiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano, Rogers Gumbo na Mwenyekiti wa kamati ya ufundi, Dominic Albinus kufanya kikao kizito na wachezaji wao.
Mabosi hao wa Yanga walitinga ilipo kambi ya Yanga, Avic Town Kigamboni na kufanya kikao kizito na wachezaji, benchi la ufundi kilichozungumzwa mambo muhimu matano ndani yake.
Inaelezwa kuwa, Dk. Msolla ndiye alikuwa akizungumza na jambo la kwanza aliwapongeza wachezaji na benchi la ufundi kwa kazi kubwa waliyoifanya mpaka mzunguko wa kwanza unamalizika wakiwa vinara wa ligi.
Baada ya pongezi hizo Msolla aliwakumbusha wachezaji na benchi la ufundi kuwa msimu uliopita mpaka duru la kwanza linaisha walikuwa vinara wa ligi lakini duru la pili walishindwa kumaliza vyema na kushindwa kutwaa ubingwa.
Jambo la pili, mwenyekiti huyo aliwaambia duru la kwanza wamepoteza pointi sita ili kufikisha zile 45 kama wangeshinda michezo yote, hivyo duru hili la lala salama wachezaji na benchi la ufundi wanatakiwa kupambana vya kutosha na kama watapoteza pointi zisiwe zaidi ya sita.
Pia aliwaambia kwenye duru la pili kila mechi itakuwa ngumu zaidi na ushindani wa kutosha kutokana na wapinzani wao hawatakubali kufungwa mara mbili, pia wanahitaji pesa za udhamini wa ligi na kila moja inapambana kumaliza vizuri.
Baada ya hapo kila mchezaji aliambiwa anapaswa kupambana kadri ambavyo anaweza kulingana na majukumu ya nafasi yake na kuhisi Yanga msimu huu inahitaji mafanikio.
Mwisho Dk. Msolla aliwaeleza uongozi upo nao bega kwa bega katika kila jambo kuhakikisha msimu huu wanatwaa ubingwa wa ligi waliyoukosa misimu minne pamoja na kutwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho (ASFC).
Msimu uliopita Yanga ilimaliza duru la kwanza ikikusanya pointi 37, ikiitangulia Simba kwa tofauti na pointi mbili, lakini mwishoni mwa msimu ikajikuta ikimaliza ya pili na pointi 74 na Simba ikibeba ubingwa mwa msimu wa nne mfululilo ikikusanya alama 83. Kwa msimu huu Yanga imemalizia duru la kwanza na pointi 39 baada ya mechi 15, huku Simba ikiifuata na pointi 31.

WASIKIE SASA
Mshambuliaji Heritier Makambo alisema mara nyingi wanapotembelewa na viongozi, huwapa morali na hali ya kushindana zaidi katika kila mechi iliyokuwa mbele yao.
“Jambo kubwa kwetu hilo wamelifanya kwani tunaamini tupo pamoja na viongozi na wanatambua kile ambacho tunakifanya uwanjani,” alisema, Makambo huku Meneja Hafidh Saleh alisema jambo hilo la kawaida kwa viongozi kuwapa maneno yenye ujumbe mkubwa ndani yake ni kama Baba kwenye familia anapomueleza mwanae akasome vizuri.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mastaa KMC waachiwa msala​

KMC PIC

TANGU kocha Mnyarwanda Thierry Hitimana amechukua mikoba ya kuinoa KMC, kutoka kwa Habib Kondo timu hiyo imeonekana kuimarika siku hadi siku na sasa kazi kubwa imebaki kwa wachezaji.
Hitimana aliyejiunga na Wanakinondoni hao Januari 6, mwaka huu baada ya kumalizana na Simba, hadi sasa ameiongoza timu hiyo kwenye mechi tano za ligi na kushinda tatu na kutoa sare mbili huku akivuna pointi 11 na kupanda hadi nafasi ya sita kwenye msimamo alama ambazo ni sawa na ilizovuna kwenye mechi 11 za mwanzo.
Akizungumza na Mwanaspoti, kocha msaidizi wa timu hiyo Hamadi Ally ameeleza kuwa kuna mabadiliko makubwa kwenye timu tangu kuja kwa Hitimana na sasa wanaamini kufanya vizuri kama wachezaji watatenda kwa ufasaha kile wanachoelekezwa.
“Nawapongeza vijana kwa kazi waliyofanya, kwa hivi karibuni wameweza kufanya kile tunachowaelekeza kwa asilimia kubwa ndio maana tunapata matokeo haya,” alisema Hamad na kuongeza;
“Pia nampongeza bosi Hitimana kwa kazi kubwa anayofanya, naamini kabisa kama vijana watafuata kile tunachowaelekeza na kujituma kwa nguvu zao zote basi tutafika malengo yetu na kufanya vizuri zaidi.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

AZAM FC YALAZIMISHWA SARE 0-0 NA COASTAL CHAMAZI​

AVvXsEhlZCfKF1j-9yRp_846xFv04vYNzS9fq08iurQ8TXNPECx99JhcKc_u5qddLSb0cjgroma5r_MzIORYtKMtWIl3lp3_jRfUGOWnFiKNp1LKa1F8EdLKoFZQ3ph6P3qhHpsG1ey98I8gwnqUSv3VUXRA2QXswK0cjPszgW0gl9rrGkf-k9WYcqHOcCt0=w640-h516


WENYEJI, Azam FC wamelazimishwa sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kwa sare hiyo, Azam FC inafikisha pointi 25 katika mchezo wa 16 na kuendelea kushika nafasi ya tatu, ikizidiwa pointi sita na mabingwa watetezi, Simba yenye mechi moja mkononi, ikiwa nyuma ya Yanga yenye pointi 42 za mechi 16 pia.
Coastal Union kwa upande wao wanafikisha pointi 18 katika mchezo wa 16 pia sasa wakiwa nafasi ya 10.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAMA MKAPA AKUTANA NA MABOSI TFF, BODI YA LIGI​

AVvXsEg_bHIn6qz2jYvxqfdCfpxFfmJhchifj_CZf2EP-LYzBeJhaEcPboyQ-09ZBYxAatijiO8zJFf9j-uAb8wKzbdQrNzDLi3k28XopuRe4ZOCJ6Ct05RD0iPd0AY-_tnqjG5gStuXgiYvklPLQxV_3zy2uMeNqUB2mfJ3lL242EZHJR-bfHzRAZv3Uj7o=w640-h426

MWENYEKITI wa mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa leo ametembelea Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu, Kidao Wilfred (wa pili kutoka kulia).
Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Mashindano TFF Salum Madadi (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa EOTF, Stephen Emanuel (wa pili kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Almasi Kasongo (wa kwanza kulia).
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Biashara kamili yaifuata Simba​




biashara pic

KIKOSI cha Biashara United kitawasili Dar es Salaam kwa michezo miwili ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba na Ruvu Shooting.
Akizungumza na Mwanaspoti, kocha mkuu wa timu hiyo, Mrundi Vivier Bahati alisema kuwa wamekuja kutafuta alama sita katika mechi hizo mbili ili kujikwamua kutoka nafasi za chini kwenye msimamo.
Hadi sasa Biashara ina pointi 15 ikishika nafasi ya 13 kwenye msimamo na inakutana na Simba yenye pointi 31 na ipo nafasi ya pili keshokutwa Alhamisi na baadaye itacheza na Ruvu Shooting inayoshika nafasi ya 12 kwa pointi 16.
“Tunahitaji alama tatu kwenye kila mchezo, tumekuja na wachezaji wote, na wanatambua umuhimu wa mechi hizo hivyo wapo tayari kwa kupambana,” alisema Vivier na kuongeza;
“Simba ni timu bora, tunaiheshimu lakini soka ni mchezo wa uwanjani, tunahitaji kushinda ndani ili kuongeza morali kwa wachezaji na kujikwamua huku chini tulipo.”
Biashara itaanza kucheza na Simba kwenye Uwanja wa Mkapa timu ambayo mzunguko wa kwanza wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Karume walitoka suluhu.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Kiiza: Huyu Mayele Atafunga Sana Yanga​

274235279_261437032807508_4171306007109705528_n.jpg

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba ambaye hivi sasa anacheza Kagera Sugar, Mganda, Hamis Kiiza
‘Diego’amemuangalia straika waYanga, Mkongomani, Fiston Mayele na kutamka kuwa jamaa anajua huku akimtabiria makubwa katika timu hiyo.
Kiiza aliyewahi kuichezeaYanga kabla ya kwenda Simba, alitoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati yaYanga dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa wikiendi iliyopita kwenye Uwanja
wa Mkapa, Dar es Salaam.
Mchezo huo ulimalizika kwaYanga kushinda mabao 3-0 yakifungwa na Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’na Mayele aliyepachika mawili.
Akizungumza na Championi Jumatano, Kiiza ambaye aliwafunga Simba katika mchezo wa ligi, alisema kuwa kwa aina ya uchezaji na mfumo ambao wanautumiaYanga, mshambuliaji huyo atafunga mabao mengi
msimu huu.
Kiiza alisema kuwaYanga mashambulizi yao wanayafanya kutokea pembeni wakiwatumia mabeki wa pembeni na mawinga kupiga krosi ambazo ndiyo zinamrahisishia Mayele kufunga mabao.
Aliongeza kuwa uzuri wachezaji wote wa Yanga wanamjua vizuri Mayele, hivyo wanatumia mipira ya krosi katika kumpa mipira hiyo ambayo inazaa mabao.
“Kwa aina ya uchezaji na kimbinu wanayotumia wachezaji wenzake kumchezesha Mayele, basi namtabiria kufanya mengi mazuri katika msimu huu ikiwemo kutwaa ufungaji bora.
“Yanga mashambulizi yao wanayatumia kupitia pembeni kwa maana ya kupiga krosi ambazo zote wanampigia Mayele, ni kitu ambacho wanaonekana kukifanyia kazi mazoezi.
“Mabao yote aliyotufunga Mayele yametokea pembeni moja la krosi na lingine la faulo iliyotokea pembeni ambayo yote yakifungwa kwa kichwa,” alisema Kiiza.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

PRISONS YATOA SARE 0-0 NA MTIBWA SOKOINE​

AVvXsEhzSEFm7Auc1x87pIZLp8hCGmJpnUS8_ReIr2JeLh4rbUt71jruptQpLIjoojffWz8tt4sXKHcNhCHcPYdekTzphLF3SZ8s0IX97AzdYygrSYJh4nwz1j4gu0OfPEJGKubQDog3SO40XrcX1yUqHQA6ngjT_pb5pZO5zQBC-ptL__b1AAJwvwO4P0CK=w640-h418

WENYEJI, Tanzania Prisons wamelazimishwa sare ya bila mabao na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Kwa sare hiyo ambayo inaiongezea kila timu pointi moja, Tanzania Prisons inafikisha 13 katika mchezo wa 17 ikiendelea kushik mkia, wakati Mtibwa Sugar inafikisha 16 katika mchezo wa 17 pia nafasi ya 12.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Masoud Djuma Arudisha Matumani Dodoma Jiji​

dodoma-1.jpg

UONGOZI wa Dodoma Jiji, umeibuka na kusema una imani timu hiyo itafanya vizuri na kufanikisha malengo yake ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Masoud Djuma.
Februari 24, mwaka huu, kocha huyo raia wa Burundi ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Simba, alitambulishwa rasmi kikosini hapo akichukua mikoba ya Mbwana Makata.

dodoma-2.jpg


Akizungumza na Spoti Xtra, Katibu Mkuu wa Dodoma Jiji, Fourtnatus Johnson, alisema: “Tuna imani na Kocha Masoud Juma, mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting ambao tulifanikiwa kupata pointi moja ulikuwa mchezo wake wa kwanza tangu ajiunge na sisi japokuwa hakukaa kwenye benchi la ufundi kwa sababu bado hatujamaliza mchakato wa vibali vyake, lakini tutegemee kumuona hivi karibuni.
“Tunatarajia kuweka kambi nje ya Dodoma kuelekea maandalizi yetu dhidi ya Azam Machi 4, dhumuni kuu la kuweka kambi hiyo ni kwa ajili ya kumpa kocha nafasi ya kukaa na wachezaji wake na kufanya tathmini ambayo itamsaidia kuweka mipango ya ushindi.”