Simba Sports Club Thread

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Pablo kufteka watatu Simba.
KIKOSI cha Simba hapo jana kiliwasili salama Bukoba Mkoani Kagera kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar, huku Kocha Mkuu, Pablo Franco akinoa panga kabla ya kufyeka vichwa vitatu ili kupisha majembe matatu ya maana yatue Msimbazi.
Simba itakuwa wageni wa Kagera Sugar keshokutwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na Pablo akitaka kuendeleza rekodi tamu tangu ajiunge na timu hiyo mwezi uliopita kuchukua nafasi ya Didier Gomes aliyetimuliwa baada ya Simba kung’olewa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Wakati kikosi kikiwa na mzuka baada ya juzi kuing’oa JKT Tanzania katika Kombe la Shirikisho (ASFC) kwa bao 1-0, Pablo amewasilisha ripoti kwa mabosi akiainisha wachezaji wanaotakiwa kutemwa na kuletwa majembe mapya matatu.
Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema aliwasilisha ripoti hiyo akiweka bayana alichokiona tangu alipotua, huku akitaja majina ya kufyekwa na vitu vinavyotakiwa kuboreshwa ikiwamo wachezaji wapya watatu ambao ni wakali kuliko waliopo kwa ajili ya michuano ya ndani na ya kimataifa.
Inaelezwa kuwa, huenda Simba ikaachana na wachezaji watatu wa kigeni wanaoweza kutolewa kwa mkopo ili nafasi zijazwe na majembe watatu wanaotakiwa, huku wanaotajwa kukalia kuti kavu ni pamoja na beki wa kati Pascal Wawa, Duncan Nyoni na Pape Ousmane Sakho.
Simba imetinga makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuing’oa Red Arrows ya Zambia na Kocha Pablo anataka kuhakikisha inafika mbali zaidi kuliko msimu uliopita katika Ligi ya Mabingwa Afrika ilipoishia ya robo fainali.
Taarifa zaidi zinasema Pablo katika usajili wa dirisha dogo lililofunguliwa jana ametaka kiungo mshambuliaji (namba 8) mwenye uwezo zaidi wa Sadio Kanoute anayecheza nafasi hiyo mara kwa mara.
Pia amependekeza washambuliaji wa kati watakaocheza pacha yaani namba 9 na 10 wenye uwezo mkubwa wa kutupia nyavuni kuliko Meddie Kagere, John Bocco na Chriss Mugalu.
Kwa mujibu wa chanzo ndani ya klabu hiyo, Pablo katika kuhakikisha analitumia vyema dirisha hili la usajili, amewaelekeza mabosi wake kuwa hakuna mchezaji mpya atakayesajiliwa bila kutoa maoni yake.
Inaelezwa mabosi wa Simba wameanza kushughulikia ripoti hiyo na taarifa zilizonaswa na Mwanaspoti nyota wawili toka Zambia wameanza kufuatiliwa.
Pablo aliwaelekeza mabosi wake anahitaji wachezaji wapya ambao watakuwa na ruhusa ya kucheza mashindano ya ndani na Kombe la Shirikisho Afrika ili kufanya vizuri na kufikia malengo ya timu kucheza nusu fainali ya michuano hiyo.
 

Attachments

  • pablo.PNG
    pablo.PNG
    496 KB · Somwa: 0
  • Like
Reactions: Brenda

tototundu

Kaka Mkubwa
Nov 26, 2021
23
25
6
#HABARI: Timu 15 kati 16 Ligi Kuu Tanzania Bara zakubali kuweka nembo ya GSM Tanzania Limited Mdhamini mwenza wa ligi kuu ya NBC. Simba pekee yagomea kuweka nembo hiyo. 10F3CCE4-BFB3-40D1-B652-D19EB20A2922.png
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

MWITIKIO UCHANGIAJI UJENZI WA UWANJA SIMBA WARIDHISHA​

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salum Abdallah 'Try Again" amesema zoezi la wanachama kuchangia fedha leo za ujenzi wa Uwanja wa klabu hiyo linaendelea vizuri.
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Abdallah amesema ndani ya muda mfupi tanhu kuzinduliwa kwa zoezi hilo Desemba 17, idadi kubwa ya wanachama imechangia fedha.
Mpango huu ni wazo la Mwanahisa mkuu Simba, Mohamed 'Mo' Dewji ambaye ameahidi kutoa Sh. Bilioni 2 ili wanachama wajazie klabu hiyo ijenge Uwanja wake kuepuka adha inazokutana nao kutumia Uwanja usio wake.
Kwa sasa Simba ina Uwanja wa mazoezi tu, Mo Simba Arena uliopo Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam na mechi zake za mashindano inatumia Uwanja wa Benjamin Mkapa.
 

Mkwavinyika

Administrator
Staff member
Dec 2, 2021
49
9
26
Dar es Salaam
Simba yatua mkoani Tabora kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC.

FHM7DglXMAITSEi


FHM7Dj3XMAkDkr1


FHM7DglXEAUpWu0


FHM7Dj1WQAEaT2c
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Pablo atikisa Simba, ataka majembe matatu​

1640167172756.png
KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco hataki utani, anataka timu hiyo ibebe ndoo ya tano mfululizo na ameainisha mengi kwenye ripoti yake ikiwamo kuimarisha benchi lake la ufundi na kuleta wachezaji mashine wapya watatu.
Pablo ameuomba uongozi wa klabu hiyo kumpa nafasi ya kuwaleta wasaidizi wake katika benchi la ufundi, hatua ambayo inaweza kufagia benchi lote la kina Selemani Matola na Thierry Hitimana, kama alivyotaka wakati akipewa dili hilo la kufundisha Msimbazi kwa mara ya kwanza.
Awali, uongozi wa Simba ulimuomba umpe muda wa kuwaangalia waliopo kwa miezi mitatu kabla ya kuongeza watu wapya.
Ni miezi miwili tu sasa tangu amefanya kazi na wasaidizi wake Hitimana na Matola, lakini Pablo anaona bado Simba inaweza kuboresha zaidi benchi hilo na kuifanya Simba iwe timu ya kutisha zaidi.
Pablo anataka kufanya kazi na benchi lake jipya na ikishindikana abaki japo na mmoja kati ya Matola au Hitimana,
Chanzo cha kuaminika ndani ya Simba kimelithibitishia gazeti hili kuwa Pablo anataka benchi lake liimarishwe.
“Kocha amesema anapenda kocha ambaye atamsaidia kwa vitendo na sio maneno, tangu ametua Simba amekuwa akisaidiwa kwa ukaribu zaidi na kocha wa viungo Daniel De Castro ambaye ni pendekezo lake mwenyewe ndani ya timu hiyo,” kilisema chanzo hicho ambacho hakikutaka jina lake liandikwe gazetini.
“Kocha anapenda kuchagua kikosi kwa njia ya michoro, anaamini makocha watakaokuja kuongeza nguvu watamsaidia sana katika hilo,” alisema.
Alisema katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili uongozi ukitumie pia kumtafutia wachezaji watakaoboresha timu.

MAJEMBE MATATU
Katika kuhakikisha malengo ya kutisha kwenye Kombe la Shirikisho na kubeba taji la tano mfululizo la Ligi Kuu Bara yanafanikiwa, mabosi wa Simba wapo katika mawindo makali kwenye nchi mbalimbali ndani na nje ya Afrika kwa ajili ya kufanyia kazi ripoti ya kocha wao mkuu, Pablo Franco aliyeeleza anataka majembe matatu mapya.
Mwanaspoti limejiridhisha katika majembe hayo matatu tayari mmoja ameshapatikana ni kiungo fundi kutoka RS Berkane ya Morocco, Mzambia Clatous Chama ambaye muda wowote atakuwa hapa nchini kujiunga na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara.
Wakati mabosi hao wa Simba wakiendelea kusaka mashine hizo nyingine mbili mpya, huenda wakafanya uamuzi mgumu wa kuachana na beki wake mkongwe, Erasto Nyoni ambaye hakuwepo katika orodha ya hapo awali.
Inaelezwa mabosi hao wa Simba wametoa ruhusa kwa timu ambayo itamtaka Nyoni Erasto kutuma maombi rasmi ya barua na wapo tayari kumuachia hata kwa mkopo kama ilivyo kwa nyota wengine wanne.
Nyota hao wengine wanne ambao huenda nao wakawa wamekalia kuti kavu na wakatolewa kwa mkopo ni Pape Ousmanne Sakho, Pascal Wawa,Abdulsamad Kassim na Duncan Nyoni.
Alipotafutwa Abdulsamad alisema alikuwa sehemu ya kikosi kilichokwenda Bukoba kwa ajili ya mchezo wa Kagera Sugar: “Bado sijapewa taarifa ya kwenda kwa mkopo katika timu nyingine.”
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

KIBU APIGA MBILI SIMBA SC YAITANDIKA KMC 4-1 TABORA​

1640450704243.png
MABINGWA watetezi, Simba SC wametoa onyo kali baada ya kuitandika KMC mabao 4-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Mabao ya Simba SC yamefungwa na mabeki, Mohamed Hussein ‘ Tshabalala’, dakika ya 10, Mkenya Joash Onyango dakika ya 12 na mshambuliaji Kibu Dennis mawili dakika ya 46 na 56, wakati la KMC limefungwa na Abdul Hillary dakika ya 41.
Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 21, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na vinara, Yanga SC baada ya timu zote kucheza mechi tisa.
KMC yenyewe inabaki na pointi zake 10 katika nafasi ya 11 baada ya kucheza mechi 10 sasa.
Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, wenyeji, Coastal Union wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ dakika ya 10 na la penalti dakika ya 90 na lingine Hajji Ugando dakika ya 45 na ushei, wakati ya Mbeya City yamefungwa na Juma Luizio dakika ya 33 na Richardson Ng’ondya kwa penalti dakika ya 72.
Coastal Union inafikisha pointi 17 na kupanda nafasi ya tatu ikiizidi pointi mbili Mbeya City inayoshukia nafasi ya sita baada ya timu zote kucheza mechi 10 sasa.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0
Kwa maslahi ya pande zote mbili, uongozi wa klabu umefikia makubaliano na mchezaji Ibrahim Ajibu kusitisha mkataba wake kuanzia leo Desemba 30, 2021. Tunamshukuru Ajibu kwa namna alivyojitoa kupambana kwa ajili ya Simba, na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake. #NguvuMoja
1640938433002.png
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Tulieni tunatoboa, mabosi Simba walitaja chama la Kisinda​

simba-pic.jpg


MABOSI wa Simba wamelichungulia Kundi D iliyopangwa timu yao katika mechi za michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika sambamba na ratiba ya mechi zao na fasta wakaifanyia tathmini haraka na kupata matumaini kuwa watapenya hadi robo fainali.

Sio hatua hiyo tu, kwa jinsi walivyopania msimu huu kimataifa wanaamini watafika mbali zaidi. Kundi hilo mbali na Simba, lina timu nyingine tatu - RS Berkane ya Morocco, Asec Mimosas (Ivory Coast) na US Gendarmerie Nationale (Niger).

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mulamu Nghambi aliliambia Mwanaspoti kwa namna kundi lao lilivyo na uzoefu walionao hawana presha yoyote na imani yao ni kufika mbali baada ya malengo katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu kutotimia.

“Berkane na Asec ni timu ambazo tunazifahamu vyema, ingawa kidogo hawa Gendarmerie hatuna taarifa zao za kutosha, ila kwa ukubwa na uzoefu wa Simba sidhani kama hilo ni tatizo sana naamini tuna nafasi kubwa ya kuingia hatua ya robo fainali,” alisema.

“Asec walikuwa tishio zamani lakini kwa sasa wachezaji wengi wazuri wa Afrika Magharibi wanakimbilia Ulaya, hivyo klabu zao hazina wachezaji bora kiasi hicho kulinganisha na kikosi cha Simba na Berkane sio tishio sana na tunaweza kupata matokeo mazuri dhidi yao.”

Nghambi alisema changamoto iliyopo mbele yao ni suala la usafiri na taratibu za kuingia katika nchi ambazo timu zilizopo kundi hilo zinatoka, lakini ana uhakika haiwezi kuwa shida kwao.

“Hizo nchi zote usafiri wa kwenda huko ni wa ndege za kuunganisha ambapo safari ya kwenda inaweza kuwa hata ya siku mbili au tatu. Hivyo kuna uwezekano mkubwa tukalazimika kutumia usafiri wa ndege ya kukodi kwani kuna muda mfupi kutoka nchi moja hadi nyingine.

“Ivory Coast tutakapoenda kucheza na Asec kwa mfano tumeshawahi kwenda. Ni nchi ambayo ina changamoto kubwa katika masuala ya utaratibu na hata Niger naamini iko hivyo, lakini kama ambavyo nimesema awali kuwa Simba ni timu kubwa na inafahamu hilo na haliwezi kutusumbua,” alisema Nghambi.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa baada ya droo ya juzi, Simba itaanzia nyumbani ikiivaa Asec Mimosas, Februari 13 mwakani na siku chache baadaye itaifuata Gendarmerie, mchezo utakaochezwa kati ya Februari 18-19. Februari 25 au 26 Simba itacheza tena ugenini dhidi ya RS Berkane watakaorudiana nao jijini Dar es Salaam kati ya Machi 11 na12 kisha itakwenda Abidjan kurudiana na Asec Mimosas kati ya Machi 18 na 19. Wekundu hao watakamilisha ratiba kati ya Aprili 1 na 2 nyumbani kucheza na US Gendarmerie.

Nghambi alisema wamepanga kuhakikisha Simba inapata ushindi katika mechi mbili za mwanzo, kwani ndizo zitawaweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya robo fainali.

“Siku zote mechi mbili za kwanza za makundi ndizo zinaamua kama unaenda robo fainali au hauendi. Hata msimu uliopita, mechi mbili za mwanzo ndizo zilichangia kutufanya tuongoze kundi.

“Kwa maana hiyo tukishinda nyumbani dhidi ya Asec na kisha ugenini dhidi ya Gendarmerie tutakuwa katika nafasi nzuri ukizingatia mechi mbili zitakazofuata zitakuwa dhidi ya Berkane nyumbani na ugenini,” alisema Nghambi. Ni mara ya kwanza kwa Simba kukutana na RS Berkane na Gendarmerie, lakini imekutana na Asec Mimosas katika makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2003 ambapo Simba ilishinda bao 1-0 nyumbani na ugenini ikapoteza 4-3.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Hitimana afichua siri za Mkude​

hitimana-pic-data.jpg


ALIYEKUWA kocha msaidizi wa Simba, Thierry Hitimana ameeleza namna alivyomsaidia kiungo wa timu hiyo Jonas Mkude kurejea kwenye makali.

Mkude anayetajwa kuwa kipenzi cha mashabiki wa klabu hiyo, alikuwa kwenye wakati mgumu kupata nafasi chini ya Kocha aliyetimuliwa klabuni hapo, Didier Gomes, ambaye alipenda kumtumia zaidi Mganda, Taddeo Lwanga kabla ya kupata jeraha la goti.

“Niliongea naye kwa muda mrefu na nilichokuwa namwambia atambue kuwa soka ni kazi ya muda mfupi, hivyo awekeze nguvu ndani ya uwanja,” alisema Hitimana na kuongeza:

“Alibadili fikra zake na akaanza kujituma na matunda yake yanaonekana, jambo ambalo najivunia kwake kumuona akifanikiwa.”

Kuonyesha kuwa kiungo huyo anazidi kuimarika aliweza kutoa pasi ya bao (asisti) aliyofunga beki wa kushoto wa timu hiyo Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwenye mchezo wao dhidi ya KMC waliifunga mabao 4-1 kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Ijumaa iliyopita.

Uongozi wa Simba uliachana na kocha huyo kutoka Rwanda baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja kandarasi baina ya pande mbili.

Hitimana alijiunga na Simba Septemba 11 kama kocha msaidizi kabla ya kumkaimisha ukocha Mkuu baada ya kumtema Didier Gomes, Oktoba 26.

Gomes aliyefutwa kazi baada ya kushindwa kuivusha timu hiyo kuingia hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha huyo mwenye uzoefu na soka la Tanzania amewahi kufundisha, Namungo aliyoachana nayo mwaka 2020 kisha kutua kwa muda Mtibwa Sugar, kabla ya kuchukuliwa na Simba.

Hitimana aliwahi pia kuwa kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Rwanda ya (U-23) mwaka 2012, kisha kuinoa Rayon Sports kabla ya kuiongoza Bugesera FC zote za nchini kwake.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA YAUNZA VYEMA 2022, YAIPIGA AZAM 2-1.​

1641101818460.png

MABINGWA watetezi, Simba SC wameuanza mwaka vyema mwaka 2022 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Baada ya dakika 45 kumalizika bila mabao huku kiungo Mzambia, Rally Bwalya akikosa penalti iliyopanguliwa na kipa Mzanzibari, Ahmed Ally Suleiman’Salula’ dakika ya 14 baada ya winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho kuchezewa rafu na kiungo Frank Raymond Domayo, milango ilifunguka kipindi cha pili.
Ni kiungo wa kimataifa wa Mali, Sadio Kanoute aliyefunga bao la kwanza la Simba dakika ya 68, kabla y Sakho kufunga la pili dakika ya 72 na Azam FC ikapata bao lake pekee kupitia kwa mshambuliaji Rodgers Kola dakika ya 80.
Simba SC inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 10, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na watani wao, Yanga ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 15 za mechi 11 sasa katika nafasi ya saba.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Ni kijana mchapakazi, mwenye uhusiano mzuri na watu wa aina zote, mtanashati na kubwa zaidi mapenzi yake kwa Simba hayapimiki. Ahmed Ally karibu kwenye klabu ya maisha yako kuwatumikia Wanasimba kama Afisa Habari na Mawasiliano. #NguvuMoja
1641194321768.png
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
Kiungo wa kati Sharaf Eldin Shiboub na MoukoroTenena wameanza majaribio ndani ya Simba Sc
Wachezaji hao watakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kitakachoriki Mapinduzi Cup.
1641280682544.png