Ligi Kuu Thread

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Masau Bwire Ataja Sababu Kufungwa 7.​

Masau-Kuliga-Bwire-1-1.jpg

MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Simba, amesema kuwa ni mambo matatu yamesababisha timu hiyo kuondolewa kwenye Kombe la Shirikisho baada ya ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Ruvu Shooting 0-7 Simba.
Juzi Simba ilitinga robo fainali ya michuano hiyo maarufu kama Kombe la FA, huku mabao yakifungwa na Clatous Chama aliyetupia matatu, John Bocco mawili na Michael Mainda alijifunga pamoja na Jimmyson Mwanuke.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Bwire alisema kuwa kufungwa mabao 7 sio tatizo kwa kuwa tayari wameshatolewa na hata Brazil ilishawahi kufungwa lakini kilichowaponza ni wachezaji kukumbwa na
mambo matatu.
“Kwanza ninaweza kusema ni majonzi, ikumbukwe kwamba tumetoka kwenye majonzi ya kuondokewa na mchezaji wetu muhimu na tumepiga picha kwa pamoja kumuombea hivyo wachezaji walikuwa wanacheza wakiwa kwenye majonzi.
“Pili ninaweza kusema ni dharau, wachezaji wetu waliwadharau Simba na kuona ni timu ya kawaida haina madhara, ndio maana tulikuwa hatuzuii bali tunashambulia.
“Tatu niseme kwamba kuna suala la majira, wakati na ukombozi, kwa waliopita kwenye maandiko wanaweza wakajua lile tukio la Yusuph familia yake ilitaka kumuangamiza lakini akatokea mmoja akasema kwamba tusimuangamize, Yusuph akapelekwa utumwani na mwisho akawa ni mkombozi kile kipindi cha njaa,” alisema Bwire.
Mchezaji ambaye ametangulia mbele za haki hivi karibuni ni beki kiraka, Ally Mtoni ‘Sonso’ aliyekuwa akiichezea Ruvu Shooting.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

REFA KOMBA KUCHEZESHA AMAZULU NA SETIF AFRIKA KUSINI.​

AVvXsEhHb8Ig0Gu4F76QWOKOqJMfNQNn19MXp2ohLco56VU9x6m5N-YozlQdJAOZ8rPNYmNGsPbGCI8kfjJClhatxiZrhW-brQmK_RW4rMIy1XwrFXDYL9HgYyjRek5Q0cokiZdZatpAoufQFyJGszpBQsJNpkKVobeZFJ54LUF8KLYwxOnuia-5n_n5nhnN=w640-h522

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemteua refa wa Tanzania, Frank Komba kuwa miongoni mwa Waamuzi watakaochezesha mchezo wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya wenyeji, Amazulu na ES Sètif ya Algeria) Februari 25, mwaka huu Uwanja wa Mosses Mabhida, Durban nchini Afrika Kusini.


Aidha, CAF pia imewateua marefa wa kike wa Tanzania, Florentina Zablon, Janeth Balama, Glory Tesha na Tatu Malogo kuchezesha mchezo wa Kufuzu Kombe la Dunia kwa Wanawake U20 baina ya Ethiopia na Ghana Machi 13, mwaka huu Uwanja wa Abebe Bekila, Jijini Addis Ababa, Ethiopia.


CAF pia imemteua Meneja wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB), Jonathan Kasano kuwa Mratibu wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya ndugu, Al Merrikh na Al Hilal Februari 25, mwaka huu Jijini Khartoum nchini Sudan.
Naye Meneja Mashindano wa TFF, Baraka Kizuguto ameteuliwa na CAF kuwa Mratibu wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya ndugu pia, GD Sagrada Esperança na Petro Atlético Februari 26 nchini Angola.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Deo Kanda Ruksa Kuivaa Yanga​

269949212_1115045569039559_6237248116241113519_n.jpg

MTIBWA Sugar imethibitisha kuwa muda wowote kuanzia sasa, itaanza kumtumia winga wao raia wa DR Congo, Deo Kanda baada ya kila kitu kukamilika.
Msemaji wa klabu hiyo, Thobias Kifaru, amesema kuwa walikuwa wanashindwa kumtumia nyota huyo kwa sababu kuna vitu kuhusu uhamisho wake vilikuwa havijakamilika ila kwa sasa kila kitu kipo sawa.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kifaru alisema: “Tunatarajia kuanza kumtumia Deo Kanda hivi karibuni changamoto ilikuwa upande wa wenzetu kushindwa kutuma kibali chake.
“Deo Kanda tulimsajili sisi wakati wa dirisha dogo ila hakuwa anaonekana uwanjani kwa sababu ya kibali chake lakini mawasiliano yamefanyika tayari na wenzetu.
“Na tutakipata hivi karibuni, yeye mwenyewe anatamani kuitumikia Mtibwa Sukari. Kama itakuwa sawa huenda akacheza dhidi ya Yanga.”
Kanda aliibuliwa na Motema Pemba ya DR Congo, kisha akajiunga na TP Mazembe, Vita Club, Raja Raja Casablanca, Simba na nyingine.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

GEITA GOLD YAICHAPA COASTAL 2-0, POLISI 0-0 KAGERA.​

AVvXsEhFilSwPSI2WKhsp-q4AO385czlJb-pGno6TV2pCJNIRPHguOD2SMtebUyFtPkzkzPNuTr6PgbyDlYK0rSqotwncAZVS_ndMFCv_tzxuiv1g_nidnUBQCK5xg9NGCG4N-iSMQmHMzMP5cPZAygZchmZTDCITq3KyxtkVAriHHpL_gOIRCOfSlR9wTMe=w640-h444

WENYEJI, Geita Gold wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
Mabao ya Geita Gold yamefungwa na George Mpole kwa penalti dakika ya 38 na Danny Lyanga dakika ya 41 na kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 15 na kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi katika nafasi ya nne.
Coastal Union, mabingwa wa Ligi Kuu mwaka 1988, wanakamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi wakiwa na pointi 17 katika nafasi ya tisa.
Mechi nyingine wa Ligi Kuu leo, wenyeji, Polisi Tanzania wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Kagera Sugar Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kagera Sugar inafikisha pointi 20 na kushuka kwa nafasi moja hadi ya saba, wakati Polisi inafikisha pointi 19 katika nafasi ya nane baada ya timu zote kukamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

KMC YAICHAPA DODOMA JIJI 2-0 DAR​

AVvXsEg6pw28YDlh6TgHAWvQcMOXoFfcELrcEu-Znqj8SdUKlp6JYhUjdfizoNvgoilXR63kfxItP_xIdFN7Vam8G_roKmUz5xhaQXKuWiuj4xTJFpawDhwoR3fO_kXSWuvqwAXwYiiM1OMnA_3sfnNt6DkujJbKXPFnKqE2nS2ZwImi_2C_jePmO-1TK7aB=w640-h532

MABAO ya Awesu Awesu dakika ya 68 na Salum Kabunda dakika ya 90 na ushei yameipa KMC ushindi wa 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi 19 katika mchezo wa 15 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 17 za mechi 15 katika nafasi ya 11.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

RUVU SHOOTING YAIPIGA PRISONS 1-0 SOKOINE​

AVvXsEh3UJWBQJbauFHZ0liBk8wz5objOhSqUTpixZgb3-g9Jfpp1IURVrSmjg8M9_1ptFiD_-I7XgQRI1FKdPFnpsrruRnfW6-Sbu8fG_GVpgmXbYG1TB7XQeXwmSGXNRZepCGBm409JDe1d-dJyprvz93MKg9rwytFQwrtlP4VTcheE0jWXAvQMiW2OKtI=w640-h428

BAO pekee la Hamadi Majimengi dakika ya 44 limeipa Ruvu Shooting ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
Ruvu Shooting inafikisha pointi 15 mchezo wa 15 na kusogea nafasi ya 12, wakati Prisons inayobaki na pointi zake 11 za mechi 15 sasa inaendelea kushika mkia.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mtibwa Yaahidi Kuitibulia Yanga​

273849620_676194817073020_7348114598058763460_n.webp.jpg

UONGOZI wa Mtibwa Sugar, umebainisha kuwa, kikosi chao kipo tayari kuvunja rekodi ya Yanga ya kutopoteza mchezo hata mmoja kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Februari 23, mwaka huu ambapo Mtibwa watakuwa wenyeji wa Yanga kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro.
Ikumbukwe kuwa, Mtibwa Sugar wanaingia kwenye mechi hii wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo kwa mabao 3-1 pamoja na kutolewa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Coastal Union kwa kipigo cha 2-0 mbele ya Coastal Union.
Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, alisema wanafahamu kwamba mchezo dhidi ya Yanga utakuwa wa mwisho kumaliza mzunguko wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara, hivyo kutokana na nafasi mbaya waliyopo kwenye msimamo, lazima wahakikishe wanapata ushindi.
“Kikosi kinaendelea kunolewa na Kocha Mkuu Salum Mayanga, nafahamu kuwa Kocha Mayanga ana kazi kubwa sana ya kufanya mazoezini kuelekea mchezo huu kutokana na kupoteza michezo miwili iliyopita.
“Licha ya hivyo, lakini morali ya wachezaji ni kubwa, wanafahamu umuhimu wa mchezo huu, hivyo najua watafuata maelekezo muhimu ya mwalimu na watafanikiwa kuyatimiza.
“Mechi hii itakuwa moja ya mechi kubwa ya mzunguko wa kwanza kwenye ligi kwa sababu Yanga watahitaji kuendeleza rekodi ya ya kutopoteza, wakati Mtibwa tukihitaji alama tatu kujinasua kwenye nafasi mbaya tuliyopo.
“Tunafahamu Yanga haijafanikiwa kupoteza mchezo wowote wa ligi kuu tangu kuanza kwa msimu huu, lakini hilo halitutishi, tutahakikisha tunawaonjesha utamu wa pilipili uwanjani, tutawaonesha maana halishi ya ushindani, nawaambia tukutane Februari 23,” alisema Kifaru.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

NAMUNGO FC YAICHAPA MBEYA CITY 2-0 ILULU​

AVvXsEh7R06acLT2J-doCPVMTsdSv3iXljGh3XQ7Um-OqbHHMgz5u47XK_gz4kzUgzSci1rkyqoEITxpoFvv2pdsLXWgF8rJ3jsGT0AugcimN19ubjVdSvhCj1-tcIRk_-EUdVzr14Vb88TMHwQUx8te0jRX4GkN1M9q-Vh9keV8gAslrMssggY8VfJcLe_9=w590-h640

WENYEJI, Namungo FC jana wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Lucas Kikoti dakika ya 40 na Relliant Lusajo dakika ya 48 na kwa huo wanafikisha pointi 23 na kumaliza mechi ya 15 za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu katika nafasi ya nne, wakiziwa moja tu na Azam FC inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na mechi moja mkononi pia.
Mbeya City inabaki na pointi zake 23 za mechi 15 pia nafasi ya tano.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Banda: Yanga haitegemei mtu, tutawakwamisha​

yanga pic

BEKI wa Mtibwa Sugar, Abdi Banda amesema licha ya kucheza na Yanga isiyotegemea mchezaji mmoja kupata matokeo, ila Februari 23 wapinzani wao hao wajue wataziacha pointi tatu Uwanja wa Manungu.
Banda alikiri namna Yanga ilivyosukwa kucheza kitimu kuanzia kwa kipa hadi mshambuliaji, huku akiiona safu yake ya kiungo ndio injini inayopika mabao, pamoja na hilo haliwatishi kukabiliana nao katika mchezo huo.
“Yanga imeanza vyema msimu ikiwa kileleni mwa msimamo, hilo sio jambo dogo, inakuja kucheza nasi tunaojikwamua kutokana nafasi 14 ambayo siyo alama nzuri kwetu, huo mchezo utakuwa mgumu sana.” alisema na kuongeza; “Tayari tumejua maeneo ya kuwadhibiti, mfano kiungo inayowafanya washambuliaji wawe bora.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Vivier: Tunahitaji ushindi kurejesha imani na kutoka kwenye hatari​

biashara pic

KOCHA Mkuu wa Biashara United, Vivier Bahati amesema wanahitaji kushinda mchezo wa kesho dhidi ya Azam FC ili kurejesha imani ya mashabiki na kiwango chao walichokuwa nacho msimu uliopita wakimaliza kwenye nafasi ya nne.
Bahati amesema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Mwanza juu ya maadalizi ya mchezo huo utakaopigwa kesho Jumanne Februari 22, mwaka huu katika uwanja wa CCM Kirumba.
Mchezo huo ulipaswa kupigwa uwanja wa Karume mkoani Mara lakini ukahamishiwa jijini Mwanza kutokana na uwanja huo kuwa kwenye marekebisho.
Amesema baada ya kuondolewa kwenye michuano ya kombe la shirikisho na Yanga wamejipanga kikamilifu kupata ushindi kwenye mechi zao la Ligi Kuu wakianza na Azam kesho huku akikiri kiwango chao cha sasa hakilingani na walichokuwa nacho msimu uliopita na kuwaomba mashabiki kuendeleza uvumilivu.
Kocha huyo Mrundi amesema kwa sasa anaridhishwa na mabadiliko ndani ya kikosi hicho tangu alipokabidhiwa majukumu mapema mwaka huu ambapo kikosi kinacheza kwa maelewano, kujiamini, kutengeneza nafasi na kufunga mabao huku akisema bado kuna kazi kubwa ya kufanya kukiboresha zaidi.
"Tuko vizuri baada ya kupoteza FA tumejipanga mechi ya nyumbani tufanye vizuri, ni kweli hali ya timu kimatokeo siyo nzuri na tunahitaji kutafuta alama tuwe pazuri na kuifanya Biashara iwe sehemu nzuri, kiukweli ukitazama biashara ya msimu uliopita na sasa ni tofauti,"
"Tunaingia uwanjani kutafuta ushindi ili kuleta furaha hadi sasa naridhishwa na mabadiliko ya timu nahitaji tutafute nafasi na tufunge mabao, mabadiliko ya uwanja hayana athari kwetu Kirumba ni uwanja mzuri na ni kama nyumbani kwahiyo wachezaji wamejiandaa," amesema Kocha Bahati.
Nahodha wa timu hiyo, Abdulmajid Mangalo amesema awali kikosi kilikuwa kinakabiliwa na changamoto ya kutumia nafasi za mabao zilizokuwa zinatengenezwa huku akitamba kuwa wamejiandaa kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
"Sisi wachezaji tumejiandaa vizuri tunatambua umuhimu wake kwa sababu utakuwa mchezo muhimu tumejiandaa kupambana tupate ushindi, hatuko vibaya sana tumekuwa tunatengeneza nafasi nyingi lakini hatupati bahati ya kufunga kwahiyo naamini mwalimu amekuwa akilifanyia kazi na bila shaka kuanzia mchezo huu tutaanza kuonyesha mabadiliko," amesema Mangalo.
Katibu Msaidizi wa chama cha soka mkoa wa Mwanza, Khalid Bitebo amesema mashabiki watapata fursa ya kupata huduma ya chanjo ya Uviko-19 ambapo mashabiki 50 wa kwanza watakaochanja wataingia uwanjani bure kuushuhudia mchezo huo.
Viingilio vya mchezo huo ni Sh 5,000 jukwaani na 2,000 kwa mzunguko ambapo utakuwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu kupigwa uwanjani hapo kwa mwaka 2022.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Simba, Yanga zilivyoiga utamaduni wa Ghana​

mjuaji pic

WAKATI naanza kuandika makala haya namkumbuka rafiki yangu kocha aliyewahi kufundisha timu kadhaa za taifa na klabu ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. Kocha huyu aliwahi kuniambia ni Tanzania pekee timu ya kigeni inapofungwa na mwenyeji wanaochukia na kuumia zaidi ni mashabiki wa Simba au Yanga kuliko hata timu zenyewe za kigeni.

Kisa kilianzia wapi?
Mwaka 1974, Simba iliwakilisha Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika (zamani Klabu Bingwa Afrika). Ilicheza dhidi ya Accra Hearts of Oak ya Ghana.
Mchezo wa kwanza wa robo fainali ulichezwa ugenini. Simba ilifika hatua hiyo baada ya kuitoa Linare ya Maseru, Lesotho. Kabla ya mchezo dhidi ya Accra Hearts of Oak, mchezaji Willy Mwaijibe alikuwa amesimamishwa. Wachezaji wa Simba wakauomba uongozi arudishwe kutokana na umuhimu wa mchezo huo.
Uongozi ukakubali na jukumu hilo akapewa mchezaji Omary Gumbo kumfuata. Timu ikamaliza mazoezi Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam na kuondoka nchini.

Asante Kotoko chanzo cha yote
Timu mbili za Ghana, Asante Kotoko na Accra Hearts of Oak zilikuwa na upinzani mkali mithili ya utani wa jadi wa Simba na Yanga. Simba ilipofika nchini humo, ikapokewa na Asante Kotoko na kuonyeshwa njia zote.
Lakini kwa bahati mbaya ikiwa katika maandalizi ya mchezo Mwaijibe akaumia mazoezini kiasi cha kutoweza kucheza.
Maandalizi yaliendelea viongozi wa Asante Kotoko wakawapa Simba mchongo mzima wa ndani na nje ya uwanja dhidi ya Accra Hearts of Oak. Simba waliambiwa wakati timu zinatoka vyumbani na kuingia uwanjani kuna mtoto mdogo atakatiza mbele ya msafara huo laiti kama wataweza kumdhibiti asikatize basi watashinda, vinginevyo watapokea kichapo.
Siku ya mechi viongozi wa Simba wakati wanatafakari na kujiuliza jinsi ya kulifanyia kazi ndipo Mwaijibe akawaambia yuko tayari kuifanya kazi ya kumdhibiti.

Mtoto adhibitiwa
Timu zikiwa zinatoka uwanjani Mwaijibe alimuona mtoto akitaka kupita mbele ya msafara.Alitoka kwa kasi na kumdhibiti. Yule mtoto alifurukuta kujiondoa maungoni mwa mchezaji huyo lakini hakufanikiwa. Mwaijibe alimwachia baada ya msafara wote kuingia uwanjani.
Kitendo hicho kilimfanya Mwaijibe asumbuliwe na polisi na mashabiki wa Accra Hearts of Oak wakiamini amewaharibia mipango yao ya nje ya uwanja.
Hadi mwisho Simba ilishinda 2-1 ugenini kwa mabao ya Abdallah ‘King’ Kibadeni na Adam Sabu. Mchezo wa marudiano Dar es Salaam uliisha kwa sare tasa na kufanikiwa kucheza nusu fainali dhidi ya Mehalla El Kubra ya Misri.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

BIASHARA UNITED YAICHAPA AZAM FC 2-0 KIRUMBA​


MABAO ya Collins Opare dakika ya 49 na James Shagara dakika ya 90 na ushei yameipa Biashara United ushindi wa 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Kwa ushindi huo, Biashara inafikisha pointi 15 na kumaliza mechi 15 za mzunguko wa kwanza katika nafasi ya 12, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 24 za mechi 15 pia katika nafasi ya tatu.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Mkwasa: Bado hatupo sawa kisaikolojia​

picmkwasa.jpg

LICHA ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Prisons, Kocha Mkuu Ruvu Shooting, Charles Mkwasa, amefunguka kuwa bado wachezaji wake hawajakaa sawa kisaikolojia kutokana na msiba wa aliyekuwa beki wa timu hiyo, Ally Mtoni maarufu Sonso.
Ruvu Shooting ilipoteza kwa mabao 7-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa raundi ya tano ya Kombe la Shirikisho la Azam uliopigwa Jumatano iliyopita, kabla ya juzi Jumapili kuibuka na ushindi dhidi ya Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Dimba la Sokoine, Mbeya.
Februari 11, mwaka huu, Ruvu Shooting ilipata pigo baada ya Sonso aliyekuwa akicheza beki wa kati kikosini hapo, kufariki kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya mguu.
Akizungumza na Spoti Xtra, Mkwasa alifunguka kwamba: “Tumepata matokeo chanya ambayo tulikuwa tunayatarajia, ni jambo jema lakini bado vijana wangu hawapo sawa kisaikolojia kutokana na msiba mzito uliotukuta wa kumpoteza mchezaji wetu Sonso. “Itawachukua muda kidogo kurudi kwenye hali ya kawaida ukizingatia hata mchezaji ambaye alikuwa analala naye chumba kimoja bado hajawa sawa kisaikolojia na hajaungana na wenzake.
“Tunarudi nyumbani kuendelea na maandalizi kwa ajili ya michezo yetu inayofuata, hatupo kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi, hivyo tunahitaji kupambana ili tuweze kujinasua kwenye nafasi za chini.” Ruvu Shooting inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 15 baada ya kushuka dimbani katika mechi 15 wakishinda nne, sare tatu na kupoteza nane.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Dodoma Jiji Yavunja Mkataba na Kocha Wao Makata​

makata-pic.jpg

TAARIFA rasmi kutoka kwenye klabu ya Dodoma Jiji, imethibitisha kumfungashia virago, aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mbwana Makata kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo.
Ndani ya michezo mitano iliyopita, Makata alijikuta akiongoza Dodoma Jiji kuambulia pointi moja tu dhidi ya Geita Gold na kukumbana na vipigo vinne, ikiwemo vitatu mfululizo ambavyo ni kama vilikoleza kuota nyasi kwa kibarua chake makao makuu ya nchi.
Taarifa rasmi iliyotolewa leo, Jumatano imeeleza kuwa,”Hatua hizi zimechukuliwa kutokana na mwenendo mbaya wa matokeo ya timu katika mashindano mbalimbali ya msimu huu wa 2021/22.”
274640813_690358438652403_4217034105660073528_n.jpg
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

YANGA SC YAWAPIGA MTIBWA 2-0 MANUNGU​

AVvXsEjSuR8Sy-JPOwLYPQRHTSUVoXu1FMhwrJw6GLAmUV93rgUewRkRbPIzJwjAe0LrlJQbsX__E528ZTVqeONlAhIObQ42EH1mKJMOt1bU_6ycLjSjUgegH7i8z89_pNV6PdGlGOX4uIa34_cNBo2Hd5rwvWwQ8bJmOCUmFP86eB76h-gNmCaQeCVQ2KYx=w640-h614


VIGOGO, Yanga SC wamekamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzonkiza dakika ya 45 na ushei na mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 66.
Kwa ushindi huo, Yanga inakamilisha mechi 15 za mzunguko wa kwanza wa ligi na pointi 39, nane zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao pia wamecheza mechi 15.
Mtibwa Sugar baada ya kipigo cha kwanza nyumbani, Manungu msimu huu wanabaki na pointi zao 12 za mechi 15 nafasi ya 15 Ligi ya timu 16, ambayo mwishowe mbili zitateremka moja kwa moja na mbili kwenda kumenyana na timu za Championship kuwania kusalia Ligi Kuu.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

HAWA NDIO MAWAKALA WANAOTAMBULIWA TANZANIA​

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa orodha ya mawakala nane tu wanaotambuliwa kufanya shughuli za kuwakilisha wachezaji nchini.
AVvXsEgKDVwT1xRbO9VOMfuSKb8XjdKrrwhXlgys7RFuxY_aFS7nAyK2hj0Cs8XY__hPiJ8MaGQ0KOoz543_ntQbo12xUQQQ8UhY2vOgBd-0ykfcjQaVhZT2daHMrL0sqkhj_oinosWrrl6kP5unIEBrmE9q3Nlv-J3U0KDqsEs9_LyFdtRTNrl8PI6AFWhp=w594-h640
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

LUSAJO AMFUNIKA MAYELE KWA MABAO LIGI KUU​

AVvXsEhqRq7XJmQbpJSMtT2LBAxOXOSPF4LseyRAOZEH1BysphF___mEUnxMCNePXUniotkYzBGSaBEH9dLeK9bOJBjwuKk-vv1RX8MIQMQw6y_buKWJsgYF4m82FXkEeRMlF6ziEeBpA-jvcWqmOWmP4Hvn6sTysEqHU38uLtzxU_EYOJDbnJfVRfqmPLKI=w640-h640

MSHAMBULIAJI wa Namungo FC, Relliant Lusajo amemaliza mzunguko wa kwanza anaongoza kwa mabao Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kufumania nyavu mara 10, mara tatu zaidi ya Mkongo wa Yanga, Fiston Kalala Mayele.