Ligi Kuu Thread

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

UBISHI WA MZEE WA KALIUA: Kiiza 'Diego' niliyemuona Taifa zamani na Kaitaba juzi.​

kiiza pic

TAKRIBANI miaka 11 iliyopita, nilikuwa juu ya kiti katikati ya mashabiki wastaarabu wa jukwaa kuu Uwanja wa Taifa (sasa Uwanja wa Mkapa) nikitazama mechi ya kirafiki kati ya Yanga na URA ya Uganda.
Licha ya kwamba ulikuwa ni mchezo wa kirafiki, mchezaji aliyeongoza safu ya ushambuliaji ya URA hakuwa na urafiki na mtu yoyote.
Baada ya kumtazama kwa muda mrefu, baadae nilifanikiwa kulifahamu jina lake kupitia kwa mwandishi mmoja wa Uganda.
Aliniambia anaitwa Hamis Kiiza ‘Diego’.
Kiiza alimkosha kila mtu aliyekuwa ameketi jukwaa kuu siku ile. Alikuwa na maarifa mengi na kasi ya ajabu. Angeweza kwenda winga ya kushoto kuchukua mpira kisha angemtambuka beki na kulikimbilia sanduku la Yanga kama hana akili timamu.
Angetisha kama anatoa pasi kisha angepiga shuti kali, alikuwa hatari kuliko hatari yenyewe. Baada ya dakika kama 70 uwanjani, kocha wa URA alimpumzisha na kumuingiza mchezaji mwingine.
Huo ulikuwa mwanzo wa macho yangu kumshuhudia Kiiza na kumkubali ndani ya dakika sabini tu nilizomshuhudia akiiteketeza Yanga.
Dirisha la usajili lililofuata sikushangaa kuwaona Yanga wakimalizana na klabu yake na kumshusha jangwani.
Hawakuhitaji kujiuliza juu ya uwezo wake wakizingatia mateso aliyowapa mabeki wao zile dakika sabini jioni ile pale kwa Mkapa. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kumshuhudia Nadir Haroub akimkimbia mshambuliaji.
Yanga hawakukosea kwa Hamis Kiiza. Yale makali alioyaonyesha dhidi yao pale Lupaso aliyahamishia kwa timu zingine za ligi kuu. Kiiza aliiiongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga kwa miaka minne. Alikuwa mshambuliaji hatari aliyewahakikishia mabao kila msimu.
Haikunishtua nilipoona ‘wikipedia’ wakisema Kiiza amefunga mabao 56 katika mechi 80 alizovaa uzi wa Yanga. Ni wastani wa bao moja kwa kila mechi mbili.
Kiiza wa miaka ile asingeshindwa kufanya hivyo.
Baadae Yanga walimsajili Amis Tambwe aliyetemwa na Simba. Yanga wakaamua kulichinja jina la Hamis Kiiza siku ya kufunga dirisha la usajili kwa kigezo cha utovu wa nidhamu. Inadaiwa Kiiza hakuwa anapatana na Kocha Mbrazil, Marcio Maximo. Kiiza akarudi nyumbani Uganda kupumzika. Simba hawakupoteza muda, walienda Uganda na kumrudisha Kiiza nchini.
Simba walimsajili Kiiza kwa sababu mbili, kwanza walikosea kumwacha Tambwe na hawakuwa na mshambuliaji wa kati anayewapa mabao ya uhakika. Pili ni kwa sababu kipindi akiwa Yanga Kiiza alikuwa anawafunga sana.
Hii sababu ya pili ilimpa nguvu zaidi, Kiiza hakuikuta Simba imara sana lakini bado alifanikiwa kupiga mabao mengi kama alivyokuwa Yanga. Kwa mujibu wa Wikipedia tena wanadai Kiiza alifunga mabao 24 katika mechi 30 za Simba.
Kwa uwezo aliokuwa nao Kiiza miaka ile sina shaka na takwimu hizo. Kiiza aliondoka nchini na kuzurura klabu kadhaa kabla ya kurejea tena majuzi.
Mechi yake ya pili tu aliwalaza waajiri wake wa zamani na viatu.
Simba wakaondoka Kaitaba vichwa chini kwa bao la Kiiza, Kilichonishtua ni kumwona Kiiza anacheza kwa ubora mkubwa sawa na vijana wadogo baada ya miaka mingi kupita.
Kwa mujibu wa Wikipedia, Kiiza ana miaka 31, nilipoona takwimu za mabao ya Kiiza sikubisha lakini kwenye umri nilipata wasiwasi kidogo. Kama Kiiza hatari sana nilimwona miaka 11 iliyopita, ina maana miaka ile alikuwa na miaka 20 tu. Ni kweli Kiiza alikuwa na ukomavu ule akiwa na miaka 20 tu? Hapana! Lazima ni mwendelezo wa maisha ya wachezaji wa kiafrika na umri. Licha ya hivyo bado tunaweza kumuona Kiiza akicheza kwa ubora mkubwa kama tulivomwona katika mechi zake mbili za kwanza kwa sababu ya ushindani wa ligi yetu.
Tunapaswa kuumia moyo kuona mchezaji ambaye umri umekwenda anatisha katika ligi yetu. Wachezaji wazee wanapaswa kukimbia kwasababu ya ushindani mkali wanaokutana nao na si kuja kwasababu wanaona hapa ndipo wanaweza kupumzika katika umri wao wa uzee.
Pia tunapaswa kumpongeza Kiiza. Katika umri wake tunaotilia shaka bado anaweza kucheza kwa ubora mkubwa katika ligi aliyotisha miaka 10 iliyopita.
Si wachezaji wote wanafanikiwa kujitunza kama yeye, kwani wapo wapi wachezaji vijana wa Kitanzania waliopaswa kucheza katika nafasi yake?
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Kaseja alivyouzwa Simba SC kimafia kutoka Moro United.​

JANA kipa Juma Kaseja alianza kuzungumzia mambo mbalimbali yanayomhusu ikiwemo ubora ambao ameendelea nao katika soka, leo staa huyo anaendelea kushusha vitu kuhusu maisha yake ya soka. Endelea naye.. Kaseja anasema baada ya kuonyesha kiwango bora aliingia kwenye mtego wa usajili na kukutana na ofa tatu mezani kutoka Mtibwa Sugar, Simba na Yanga na hatimaye alitua Msimbazi.
Anasema kutua Simba ulikuwa ni usajili wa aina yake baada ya Yanga kumtaka, huku ofa yao ikiwa ni kubwa zaidi lakini kigogo mmoja wa Moro United, Merrey Bahlabou alimpeleka Msimbazi akijazia pesa iliyopungua kwenye ofa ya Simba.
Kaseja anasema licha ya Yanga kuwahi kutoa ofa na Simba kuja baadaye, lakini ilikuwa ngumu kumpata japo-kuwa nafasi ku-bwa alikuwa akiwapa Mtibwa Sugar. “Yanga walinifuata kupitia kwa jamaa mmoja anaitwa Godson Karigo nikawaambia Sh4 milioni ambayo walitaka kupunguziwa wakati watani wao Simba walitaja Sh2.5 milioni kupitia kwa Athuman Kambi. Nakumbuka na (Crescentius) Magori alikuja pia lakini Merrey aliamua kujazia iliyopelea ili nikacheze Simba na ndivyo Yanga walivyonikosa,” anasema.
“Nilipewa pesa niliyotaka na gari, hiyo ndio sababu kubwa iliyonifanya nikaachana na Yanga na Mtibwa na kuamua kukipiga Simba.”

MSHAHARA WAKE SIMBA
Baada ya kupokea pesa yake ndefu ya usajili akiwa Simba, Kaseja anaweka wazi kuwa awali alianza kulipwa mshahara wa Sh50,000 akiwa Moro United hata alipokwenda Simba mshahara ulikuwa Sh80,000 kisha Kassim Dewji akaupandisha hadi Sh120,000.
“Nakumbuka huo mshahara wa Sh50,000 Moro United tulikuwa tunapewa Sh10,000 wiki ya kwanza ya pili na ya tatu, huku ya nne wakimaliza Sh20,000 lakini kwa wakati huo ilikuwa na thamani kubwa tofauti na sasa hivi mchezaji anachukua hadi Sh20 milioni,” anasema Kaseja.

MSIMU MMOJA YANGA
Kaseja baada ya kutumika Simba ndani ya miaka 12 alifanyiwa umafia na viongozi na Yanga ambao walitumia mkwanja wa maana kumnasa kwa mkataba wa mwaka mmoja msimu wa 2014/15.
Anasema Yanga waliwatumia watu kadhaa ili kufanikisha kuipata saini yake na ndipo alipoamua kuichezea timu hiyo baada ya kutangaziwa ofa kubwa ambayo vigogo wa Simba walikiri kutoiweza huku wakimtaka akasaini kandarasi fupi ya mwaka mmoja.
“Nakumbuka Beka ndugu yake Iman Madega wa Yanga alinipigia simu na kuniambia juu ya Yanga. Nilimsikiliza na kufanikisha, lakini viongozi wa Simba kina Adam Mgoi walijua na hawakuwa na namna ya kunizuia,” anasema.
“Mimi nina misimamo sana na sikutaka kutetereka maana niliwekewa dau kubwa ambalo hata nilivyowashirikisha viongozi wa Simba walikubali niondoke nikacheze timu hiyo kwa msimu mmoja.”

KAKIPIGA DENMARK
Kasema ni Tanzania One, lakini hajapata nafasi ya kutoka kwenda kuiwakilisha nchi katika soka la kulipwa nje ya nchi, lakini mwenyewe anafunguka sababu kuwa ni suala la fursa kwani kipindi anaonyesha ubora wa juu, hakukuwa na fursa nyingi za kutoka.
Anasema hakwenda nje kutokana na teknolojia kuwa chini tofauti na sasa na anakiri kuwa angekuwa na umri mdogo na kiwango bora kama alichokuwa nacho miaka ya nyuma asingeweza kuendelea kubaki Tanzania.
“Hata kujiuza nje ilikuwa sio kama sasa, na mimi kila kitu najisimamia mwenyewe kwa sababu nina akili timamu na najua nini nakifanya. Haikuwezekana kucheza nje ndio hivyo, lakini kama kipindi hicho mitandao ingekuwa kama sasa basi ningekuwa Ulaya siku nyingi.
“Niliwahi kwenda nje mwaka 2002 Sweden na Denmark katika mashindano ya Tivon Cup mwaka uliofuata nilitoroka nikiwa timu ya Taifa na kwenda kwenye hayo mashindano tena ambayo yalinisababishia kufungiwa kucheza timu ya taifa,” anasema Kaseja ambaye ameweka wazi kuwa alirudishwa tena Stars baada ya miezi mitatu na Mshindo Msolla aliyekuwa kocha wa timu hiyo.
 
YUPO YUPO SANA
Wakati wadau wengi wakiamini kipa huyo ambaye amethibitisha kuvutiwa na namna makipa chipukizi wanavyopambana kuwa ana muda mfupi wa kuendelea kucheza, mwenyewe amefunguka kuwa bado ataendelea kucheza.
Anasema maisha yake ni soka na hana kazi nyingine zaidi, hivyo katika muda wa kutafuta bado ataendelea kucheza na endapo atafikia kikomo kuitumikia milingoti mitatu mpango wake ni kuwafundisha makipa.
“Unajua watu wananijaji sana kuhusu umri, naomba niwaambie tu bado nina nafasi ya kucheza na wala sina mpango wa kustaafu hivi karibuni. Muda ukifika nitafanya hivyo lakini sio sasa na siwezi kufanya hivyo eti kwa sababu fulani kafanya na kuna wengine nalinganishwa nao lakini niliwakuta,” anasema.
“Watu wanatamani niache kucheza mpira sasa, nikiacha nitakula nini, waniache ni kazi yangu na ndio maana naifanya na timu nyingi tu zinahitaji huduma yangu kama mchezaji.
“Nina malengo mengi sana na ndio maana nimesomea hadi ukocha. Nina leseni B mpaka sasa na pia nina Advanced ya makipa namshukuru sana Mungu kwa hiki kidogo alichonipatia ambacho wengine hawana.”
Lakini, anasema endapo atakuwa kocha timu yake itanyooka kwani hatapenda longolongo kwa kuwa katika maisha yake ya mpira hajawahi kuwa msumbufu hata siku moja.
“Siwezi nikawa kocha au kiongozi halafu mchezaji unipande kichwani, hapana. Kusema kweli nitakuwa mkali sana naumia kuona mchezaji analipwa mshahara na timu fulani halafu kila siku huyohuyo ndiye msumbufu, aisee mimi siwezi kukubali,” anasisitiza.

SIMBA, YANGA, KMC
Kaseja ambaye amecheza kwa mafanikio makubwa Simba na Yanga anakiri kuwa timu hizo zina presha kubwa kutokana na wingi wa mashabiki, hivyo wachezaji hucheza kwa kuzipambania huku wakiwa na hofu kwa mashabiki kutokana na matokeo yatakayopatikana tofauti na KMC japo pia anakiri kucheza kwa presha kutokana na kuwa kiongozi wa timu (nahodha).
“Simba na Yanga kuna presha ya benchi la ufundi, viongozi na mashabiki, lakini hapa KMC mashabiki ni wachache nguvu kubwa ni benchi la ufundi, japo tunaweza tukafungwa na kukalishwa namna ya kujipanga na mechi ijayo, mimi nakuwa na maumivu mara mbili kwani ni nahodha wa timu na nafahamu madhara ya kufungwa kutokana na namna nilivyojengewa nikiwa timu kubwa,” anasema.
“Wingi wa mashabiki katika hizo unaweza kukufanya hata mchezaji ukatoka mchezoni kama hauna malengo na kuamini kile ambacho unatakiwa kukifanya, maana ukikosea kidogo unazomewa, ukifanya vizuri kila mmoja rafiki yako.”

KISA LUNYAMILA ALALA NJAA
Kaseja anasema Edibilly Lunyamila ni staa aliyekuwa akimchanganya akili yake wakati huo akimsikia akitangazwa katika redio kutokana na uwezo wake.
Ilipotokea akamuona uso kwa uso hakuamini macho yake na kuamua kumfukuzia njia nzima na kwa bahati mbaya alishindwa kupata nafasi hiyo.
“Sina kumbukumbu ilikuwa ni mwaka gani Lunyamila alikuwa Kigoma kulikuwa na mashindano yeye hakuniona, ila mimi nilimuona nikaanza kumfuatilia kwa nyuma baada ya mechi kuisha. Sikupata bahati ya kuonana naye na kuzungumza kwani alipanda gari ndogo na kuondoka ndipo nilipoamua kurudi nyumbani.
“Baada ya kukosa bahati hiyo niliamua kurudi nilipotoka na kukuta gari lililokuwa limetubeba wachezaji kwenda kwenye mechi aliyokuwepo Lunyamila siku hiyo limeondoka. Nikaanza kutembea kwa miguu mpaka nyumbani kufika mida ya saa 3 usiku ndio nilifika nyumbani na kukuta nimefungiwa mlango wameshalala. Hapo ili kufunguliwa mpaka uchapwe kwanza fimbo na ndio ulale hakuna kula tena hapo,” anasema na kuongeza alijikuta akiumia nafsi bora hata angeongea na Lunyamila.

MSOMALI AMTOA MCHEZONI
Katika maisha yake ya mpira anasema yapo mambo mengi mengine atakuja kuyaweka wazi pale atakapoacha kucheza mpira, lakini kwa kuwa mpaka sasa anacheza anabaki nayo moyoni.
Licha ya wingi huo wa matukio, anasema kubwa akiwa Mtibwa Sugar walienda kucheza mechi na Kagera Sugar wakafungwa na waliporejea kocha wake Mohamed Msomali alitoa kauli nzito kuwa, “tumepoteza lakini makipa wangu hakuna kitu. Basi niliumizwa sana na hiyo kauli na wakati tunapoteza nilipambana sana lakini bahati haikuwa yetu ila ni jambo ambalo linaniumiza mpaka sasa.”
 
KUTOKA NJIWA HADI MAKOMBE
Maisha yanaenda kasi sana, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya Kaseja kuweka wazi kuwa kabla hajaanza kucheza gozi la ng’ombe alianza kucheza mpira wa maka-ratasi (chandimu) ambao ndio walikuwa wanagombania njiwa.
“Nimepambana sana. Nakumbuka kipindi hicho tunagombea njiwa na sio kwamba ni timu mbili, hapana. Inakuwa ligi kabisa timu nyingi kwa kukutanisha timu za mitaa,” anasema.
Kaseja anasema timu yake ilikuwa Usagara ndio mtaa waliokuwa wanaishi Kigoma, hivyo mipango ilifanyika mitaa ikapangana na kuanzisha mashindano ambayo bingwa alikuwa anapata njiwa akisema hakikuwa kitu kidogo kipindi hicho.
“Wakati huo njiwa anauzwa Sh250 na ushindi Sh50 lakini ilikuwa na raha sana tunafurahia. Kwa sasa unakaona kadogo ila kipindi kile alikuwa mkubwa na tulikuwa tunapigana kabisa,” anasema akieleza tofauti hiyo na ambavyo amecheza kwa kiwango cha juu akishinda mataji mbalimbali.

NENO KWA WATU WA MPIRA
Akizungumzia mpira wa miguu kwa ujumla wake, Kaseja anasema: “Nawaomba waache tabia za kuwafikiria watu visivyo na kuwatungia mambo ambayo sio sawa, kwani naamini kupitia wao mpira wetu utazidi kupiga hatua zaidi endapo wataacha mambo hayo.”
Kaseja anasema watu wa mpira wanaweza kukuamulia na kukuzushia jambo kwa mapenzi yao wenyewe kitendo ambacho kinamuumiza katika maisha yake, hivyo ni wakati kwao wa kubadilika.
“Kama mchezaji hujajifunga mkanda na kukomaa kwa kile unachokiamini, basi unapotea maana hao watu wanaweza kukutoa mchezoni kabisa,” anasema.

KUTOKATA TAMAA
Wakati wachezaji wengi hasa chipukizi wakihofia kusajiliwa na timu aliyopo kwa kuhofia kupata namba ya kucheza, Kaseja anafunguka kuwa woga wao ndio umaskini wao kwani hawana wanachoweza kupoteza chini yake na zaidi watafurahia kujifunza.
Anasema hakuzaliwa kwa ajili ya kuziba riziki za watu wengine alipopata nafasi ya kucheza amewapisha wengi na walipata nafasi ya kucheza, hivyo anaamini katika kutoa nafasi kwa wengine.
“Wakisikiliza maneno ya watu sijui unaenda hiyo timu yupo Kaseja hauchezi watapotea, kwani mimi mbona siku nyingine nakaa ben-chi na ha-ta siwezi kuhoji wala kulalamika kwa kuwa najua na naelewa hamuwezi kuanza wote kikosi cha kwanza,” anasema Kaseja.
Anasema wachezaji ambao wametangulia wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa kwa chipukizi ili wajifunze vitu vingi kutoka kwao.
“Wanatakiwa kukomaa na kuamini katika malengo na mipango yao kwenye mpira, kwani naamini wakifuata hiyo misingi wataweza kufika mbali kama sisi tulivyo.”

MECHI BORA STARS
Akiizungumzia Taifa Stars, Kaseja anasema mechi ya kwanza kudaka akiwa na timu ya Taifa ni dhidi ya Kenya, kipa akiwa yeye na Peter Manyika na hapo ndipo alipata nafasi ya kucheza wakati huo Manyika alitoka timu iliyovunjwa baada ya mchezo wa kwanza Tanzania kufungwa 5-0 na Kenya.
Anasema anakumbuka kabla ya mchezo aliitwa na Manyika na kumuandaa kisaikolojia kuwa ataanza kwenye mchezo na hakuamini hilo hadi alipocheza.
“Manyika alianza kunijenga kabla ya kupangwa na hapo ndipo hofu ilipozidi baada ya kuona senior (mkongwe) kakaa benchi mimi napangwa sio kwamba kachoka, hapana,” anasema.
Kipa huyo anasema alipagawa na huo mchezo, lakini baada ya mechi walishinda 1-0 na kocha wa Kenya alimzungumzia zaidi kutokana na uwezo aliouonyesha na kuweka wazi kuwa wamekubali matokeo na juhudi za kipa ndizo ziliibeba Tanzania.

KASEJA, MATOLA
Wakati wadau wengi wakiamini kuwa Matola na Kaseja wamecheza pamoja mwenyewe anafunguka kuwa hilo halipingiki ni kweli ilikuwa hivyo lakini yeye alikuwa timu ya vijana wakati Matola anacheza timu ya wakubwa.
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

MAREFA WALIOIAMULIA YANGA DHIDI YA MBEYA CITY WAFUNGIWA.​

REFA Hussein Athumani kutoka Katavi na Msaidizi wake namba mbili, Godfrey Msakila wa Geita wamefungiwa mechi tatu baada ya kuvurunda katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya wenyeji, Yanga na Mbeya City Februari 5, Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Waamuzi hao walimhukumu kinyume cha sheria mshambuliaji Mkongo wa Yanga, Fiston Kalala Mayele kuotea akiwa kwenye nafasi ya kufunga katika mchezo ambao timu hizo zilitoka sare ya 0-0.

REFA ALIYEWABEBA SIMBA DHIDI YA MBEYA KWANZA AFUNGIWA​

REFA Ahmada Simba wa Kagera amefungiwa mechi tatu kwa kosa kukubali bao la kuotea la kiungo Mzambia, Clatous Chama katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mbeya Kwanza, Simba SC ikiibuka na ushindi wa 1-0 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Februari 3, mwaka huu.

AVvXsEgASOEX1UMxChKPOweIzHJ18UfWN4d_dqyHH-02mAHyNN4bw4Ka0XICCIF1q-AOwpK5QDh3D7iMhEvIVDmGLh6-u_gr_dZdohEIT_txfg1actv6v2r0kM-dD8v6jKVcP--H6FnoXixGoimXmEU6BeV3DB6qLhCQ9ZMWBC0b4yfk6gt4Fe9h3SEQWLxS=w512-h640
AVvXsEhzCf0iQwFNeKxyNo7dt1R19hS3XaivRloUOUpKRuhuNxKcYh3CaOjcBU8_UKKmNHygx-qtitmAg8DeFWBCGDN9dQb7JNvzhBPtc1VGbDg0UrpHVhqI2E-_2JYS2Z1v6440tMO74KlgEdFDzLZ8GanT78Bv__52sap1GkxulgEuPHGo8c-wIfexsiOu=w512-h640

AVvXsEgt9wMSaBZrG5HxZ-7JbUwJv5DJzDnrPEAz7lqZD8nzt54Kc638Vc4d8g9DBn4DRR2G9VN8IjIVKgfwBu1isRfFvimXjjZyS1ThQqAzebRnViCM339tKbldN24zeLRcBDGUtmytHy0uP15hc2Tke0KycFeC37c59Ld-Vc4byoY1UdrDxp_RX93R8Nlk=w512-h640

AVvXsEg5lufKexm3zURiHjorqRvVwDDaoDJnuERt6ZGxl6jSo-ewacoucos1uc3Xfr1Wr2349yPzgVVcjnspbX3X3fZ0M7rX7cIcKNmDL9hIWjpSg3716Bhz_mPnz-6kXxb3CZMIi7CKXWwE_kDnt_9JJcNnEzUhAXm6PTPZ5BDUKJNctX520vq0y-tSmIhb=w512-h640
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

DICKSON JOB AFUNGIWA MECHI TATU FAINI 500,000.​

AVvXsEi7Do1Sl48_21OD0A7wIXaR7NuM_sF3ICvyUTrIJ_7Xv9D9IaFYM_QXu5g8ieQtnnkEdEyVTW3sw7bEG1xoqJLBxGrW5Gwlmc3dMEp16x5yrzRH_Lx_e9uUVjyP42mhtaLtDbUA7Bly62l9K8-t4m8Uu6Q9JEyUqCLMEq5nwb2Rfs2_v1jCmVnyDiF3=w640-h568

BEKI wa Yanga, Dickson Job amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Sh. 500,000 kwa kosa la kumkanyaga mchezaji wa Mbeya City, Richardson Ng’ondya kwenye mchezo baina ya timu hizo Februari 5, mwaka huu.
AVvXsEgX3vVVQl6A7f2krRTroWaxeo4OdImiaKhmEwlqUpajF-ETxAIIJo9pqm9ZjIAdPcewzbuOxtpglwAEfUNLGA1RHSljJFVc-ZpsVOQIdpYGRD8Ke_n0y4uppvXZ9l7N44F4WJkeAOQRbOH0gbse6rgHGNhO4COk0k7WEduMqpq4fDXmCUJ6U12vg_YO=s1351
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

IHEFU YAZIDI KUJISOGEZA ANGA ZA LIGI KUU.​

AVvXsEiZIZW2pC3BzQhX5uLK_x5UcE9vLsNYHC1pdiqxCSYIyHTd3KGtG6m8q6GWWuynXNZtNR3auAZPoXOk25UlmvUoIjTfrHOECJTuW2CIVo3Y-8gJuTaFPxmGreXZNe7DHStv-YDIM3aMQrWtqTRc5vvINnABAZ8LE-glZ9AK4GSW2b_FpUoZbmz4xWew=w640-h570

TIMU ya Ihefu SC ya Mbarali mkoani Mbeya imezidi kuweka hai matumaini ya kurejea Ligi Kuu baada ya ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Pamba FC Uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza.
Kwa ushindi huo, Ihefu inafikisha pointi 41 katika mchezo wa 17, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na DTB ambayo pia ina mechi moja mkononi na leo itamenyana na Green Warriors.

MATOKEO YOTE CHAMPIONSHIP JANA
Transit Camp 1-0 African Lyon
Kengold 2-1 Gwambina FC
Pamba FC 0-1 Ihefu SC
JKT Tanzania 4-0 Fountain Gate
Ndanda FC 1-1 Mashujaa FC
AVvXsEgdX6ByiEtfxelT3Q65eyyq4rWOR6_DYdsJv-pJ37ZukGWOtAM_JbfbifNmoD56p-9bF005rBFCAT-gZCs9hKLVDXs9FPtt04FtXnOEPkzTsqZAoFCEhZdWsjzHETdZ4iqbwzOJBkzE64WDKXZ5OWnExUtnc96_Tu8iRaC0ZfWevndNhag9xnqRlElg=w640-h640
 
vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Biashara Kufa na Kupona kwa Yanga.​

biasharautd_241182653_2985254285074728_9199527890377565480_n.jpg

KOCHA Mkuu wa Biashara United ya Mara, Vibier Bahati ameweka wazi kuwa watacheza kwa kufa na kupona kwenye mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga kwa ajili ya kupata matokeo.
Biashara watakuwa ugenini kwenye mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar Februari 15.
“Tangu msimu huu wa ligi uanze Yanga wamekuwa na timu bora yenye wachezaji wazuri, lakini sisi hatutaangalia hilo na badala yake tutapigana kufa na kupona ili tupate matokeo katika mchezo huo.
“Bado malengo yetu ni kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa kwa hivyo dhamira yetu ni kutwaa ubingwa wa kombe hili ili hapo baadae tuwakilishe nchi kimataifa baada ya kufanya hivyo msimu huu japokuwa hatukuwa mabingwa wa mashindano haya.
“Tutautumia mchezo huo kujijenga uwanjani lakini pia kuangalia makosa ambayo tumeyarekebisha kama tumefanikiwa, tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi kutuunga mkono,” alimaliza Bahati.
 
vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Lusajo: Nitampoteza Mayele.​

mayele-yanga.jpg

KINARA wa wafungaji kwenye Ligi Kuu Bara mpaka sasa, Reliants Lusajo, amemtangazia vita mpinzani wake mkubwa katika vita ya ufungaji bora msimu huu, Fiston Mayele akisema amejipanga kuendelea kutupia mabao kwa kila nafasi atakayoipata.
Lusajo ambaye ni nahodha wa Namungo, mpaka sasa amefanikiwa kuifungia timu hiyo mabao tisa akifuatiwa na Mayele wa Yanga mwenye mabao sita.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Lusajo alisema: “Nafurahia kiwango ambacho nimekuwa nacho kwa sasa, kama mchezaji hususani ambaye ninahudumu kwenye unahodha ni jambo muhimu kuhakikisha ninaipambania timu yangu ili iweze kupata matokeo mazuri.
“Kuhusu vita ya ufungaji bora ni kweli hiyo ni sehemu ya malengo ambayo nimejiwekea msimu huu, najua ushindani ni mkubwa kutokana na ubora wa washambuliaji wengine kama vile Fiston Mayele, lakini nimejipanga kutumia kila nafasi ambayo nitaipata kuhakikisha ninafunga mabao mengi zaidi.”
 
mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Kagere, Mayele mbona kazi ipo.​

kagere pic

LIGI Kuu Bara imesimama kwa muda na inatarajiwa kurejea wikiendi ijayo kwa michezo miwili itakayozikutanisha Polisi Tanzania dhidi ya Kagera Sugar na ule wa Geita Gold watakaoikaribisha Coastal Union mjini Geita.
Lakini sasa ligi hiyo ikirejea ili kukamilisha mechi za raundi ya 15 za kufungia duru la kwanza, kuna vita kubwa ya ufungaji wa kati ya wachezaji wazawa na wageni, pia mapro wa kigeni wakiwa na vita yao wenyewe kwa wenyewe.
Ndio, kwa sasa kwenye orodha wa wafungaji, Reliants Lusajo wa Namungo FC anaongoza kwa mabao tisa, akifuatiwa kwa mbali Fiston Mayele wa Yanga, George Mpole wa Geita na Vitalis Mayanga wa Polisi ambao kila mmoja ana mabao sita.
Nyuma ya kina Mayele kuna Meddie Kagere wa Simba mwenye mabao matano sawa na Jeremiah Juma wa Tanzania Prisons kuonyesha msimu huu kwenye vita ya mabao kazi ipo kwelikweli.
Ukiachana na vita ya wazawa na wageni, huku Lusajo akiongoza jahazi kuna vita nyingine ya mapro wa kigeni wakiongozwa na Mayele ambao anapambana kuzima ufalme wa Kagere aliyouweka kwa misimu mitatu mfululizo iliyopita katika ligi.
Kagere ndiye mchezaji wa kigeni mwenye mabao mengi katika ligi kwa miaka ya karibuni akiwa ametumia misimu minne mfululizo kufunga 63, lakini msimu huu ana kazi ya kuchuana na Mayele aliyesajiliwa msimu huu kutoka DR Congo.
Kwa misimu miwili ya 2018-2019 na 2019-2020, Kagere ndiye aliyekuwa Mfungaji Bora kabla ya msimu uliopita wa 2020-2021 kuporwa ufalme na John Bocco ambaye ameanza simu na ukame wa aina yake katika ligi hiyo.
Bocco aliyefunga mabao 16 msimu uliopita na kuwapiku Chris Mugalu na Kagere wote akicheza nao Simba, hajafunga bao katika Ligi tangu Julai 18 mwaka jana alipotupia kambani mkwaju wa penalti wakati Simba ikiishindilia Namungo 4-0.
Ukihesabu tangu Julai 18, 2021 hadi leo ikiwa Februari 13 ni miezi sita na wiki tatu na siku tano au sawa na jumla ya siku 210 au saa 5,040.
Achana na Bocco, turejee kwa Mayele na Kagere, nyota hao ambao timu zao zinachuana pia katika mbio za ubingwa, wanachuana kuweka heshima zao mbali na kutaka kuwabeba wenzao wa kigeni kwenye vita ya kuwania tuzo ya ufungaji.
Kama hujui ni kwamba hadi sasa ligi ikiwa imesimama zimechezwa jumla ya mechi 113, huku yakifungwa mabao 218, yakiwamo 10 ya kujifunga na mengine 154 yakifungwa na wazawa 81, huku wageni 28 wametupia 54 hadi sasa.
Katika mabao hayo 54, Mayele ndiye kinara kwa wageni akifuatiwa na Kagere huku Saido Ntibazonkiza wa Yanga na Rogders Kola wa Azam wakiwa nyuma yao na mabao manne kila mmoja.
Orodha ya wafungaji wa kigeni inawagusa pia Jesus Moloko na Khalid Aucho wote wa Yanga wenye mabao matatu kila moja kama Charles Zulu na Idris Mbombo wa Azam, huku Bigirimana Blaise na Obrey Chirwa wote wa Namungo, Ambrose Awio na Collins Opare wote wa Biashara Utd kila mmoja ametupia mabao mawili.

WASIKIE WADAU
Kocha wa Vijana wa Azam, Mohamed Badru alisema uwepo wa nyota wa kigeni umechangia kumfanya Lusajo awe bora, lakini lazima akaze buti amalize mbabe.
“Uwepo wa Mayele, Kagere, Mbombo na wengine umefanya wazawa waongeze bidii ya kufanya vizuri zaidi,” alisema Badru aliyewahi kuinoa Gwambina, huku nyota wa zamani wa Simba na Bandari Kenya, David Naftar alisema kitendo cha nyota wa kigeni wenye ubora kama Kagere, Mayele, Kola na wengine inachangia wazawa kutokaa kizembe, huku akitamani kuona msimu huu mzawa akibeba tena tuzo kama ilivyokuwa kwa msimu uliopita.
 
mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Biashara tatizo viwanja.​

biashara pic

BIASHARA United tayari ipo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya pambano lao la ASFC dhidi ya Yanga, huku kocha mkuu wake, Bahati Vivier akilia kukutana na changamoto ya viwanja vya kupigia tizi kwa timu hiyo.
Yanga na Biashara zitaumana Jumanne katika mechi ya 16 Bora ya Kombe la ASFC itakayopigwa kuanzia saa 1:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa na Vivier alisema wamekutana na ugumu wa upata viwanja vya mazoezi kwa uharaka licha ya kuandaa programu zao mapema.
“Una plani mazoezi, lakini inafika mpaka saa tisa jioni haujajua unafanya wapi mazoezi hii inakuwa inasumbua, tunaelewa ni mazingira ya hapa, tukipata uwanja hata kwa kukawia inabidi tuutumie vizuri, ila inanipa mawazo kwenye mipango yangu,” alisema kocha msaidizi huyo wa zamani wa Azam raia wa Burundi.
Mwanaspoti liliwashuhudia wakifanya mazoezi yao katika uwanja wa Uhuru wenye nyasi bandia huku mchezo wao na Yanga ukipigwa kwenye Uwanja wa Mkapa.
Vivier alisema suala la kikosi chake kufanya mazoezi kwenye uwanja wa bandia halisumbui na hakuna shida yoyote ile unapoenda kucheza kwenye nyasi za asili.
“Hakuna tabu kama ukifanya mazoezi kwenye nyasi bandia ukacheza mechi kwenye nyasi hasili, anayejua anajua tu na hatuwezi kulazimisha kupata uwanja mwingine, tumepata Uhuru hapa ndio maana tunautumia,” alisema Vivier na kuongeza; “Tunaenda kucheza mechi moja ambayo mmoja anatakiwa atoke, tunazungumza timu nzima kuhakikisha kila idara inakuwa vizuri ili tuweze kupata ushindi.
 
mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

TFF yamlilia Kondo.​

tff pic

SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limepokea kwa mshtuko kifo cha aliyekuwa katibu wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), Msanifu Kondo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF Rais wake Wallace Karia amepokea kwa masikitiko makubwa msiba huo mkubwa katika tasnia ya soka.
Karia ametuma Salam za rambirambi kwa Mwenyekiti wa DRFA Lameck Nyambaya kutokana na msiba huo mzito pamoja na familia ndugu jamaa na marafiki na wanafamilia wa mpira kwa ujumla.
Aidha Karia amewaomba familia, ndugu, jamaa, marafiki na wanafamilia wa mpira wa miguu na wote walioguswa na msiba huo kuwa na Subira wakati huu ambao wamepoteza mpendwa wao.
"Mpaka mauti yanamkutaalikuwa akihudumu kwenye nafasi ya katibu wa DRFA na msimamizi wa kituo Cha Dar es Salaam, Mungu ailaze roho ya marehemu Msanifu Kondo mahala pema peponi amen, "
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SERIKALI YAAGIZA TFF IWAKUTANISHE MAREFA NA TAKUKURU.​

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa jana ametoa maelekezo mazito kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) yanayolenga kuboresha mchezo wa mpira wa miguu nchini.
Maelekezo hayo ameyatoa katika mkutano wa Waandishi wa Habari aliofanya katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baada ya kufanya kikao na Viongozi wa TFF, BMT na watendaji wa Wizara.
Amefafanua kuwa Serikali ipo katika mikakati kabambe ya kuboresha miundombinu ya michezo katika shule 56 nchini ikiwa ni pamoja na kufunga mashine za kisasa za kufuatilia michezo (VAR) kwenye viwanja vitano kwa kuanzia pamoja na kujenga vituo vikubwa vya michezo.

Akitoa maelekezo ya Serikali, Mhe. Mchengerwa amesema BMT ikutane na TFF mara moja kujadili namna ya kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa Sheria na taratibu za mchezo huo pendwa nchini ambapo pia amesisitiza kuwa Kamati inayohusika na Waamuzi ijitafakari kwa kuwa hadi sasa kwenye msimu huu wa ligi tayari imeshawaondoa waamuzi 13 kwa makosa ya upendeleo na rushwa.
Mhe.Mchengerwa amesema, TFF ikutane na waamuzi wote ili kupata uvumbuzi wa changamoto na sintofahamu zinazoendelea kujitokeza katika mchezo huo kinyume na sheria ambapo ameagiza TAKUKURU washirikishwe ili waweze kutoa elimu ya rushwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
Amefafanua kuwa, iwapo vitendo vya rushwa havitadhibitiwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu, mchezo huo hautakuwa na maendeleo.
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

JICHO LA MWEWE: Sonso ameacha maandishi ukutani, tujitafakari.​

sonso pic

IJUMAA iliyopita amefariki dunia beki wa Ruvu Shooting, Ally Mtoni ‘Sonso’ na alizikwa Jumamosi. Sonso enzi za uhai wake aliwahi pia kuzicheza Lipuli, Yanga na Kagera Sugar. Zaidi ya hapo amewahi kuipigania jezi ya timu ya taifa.
Ni mara chache kwa taifa letu kutokea kifo cha mchezaji wa Ligi Kuu ambaye anaendelea kucheza soka. Tumewahi kushuhudia wachezaji wengi wa zamani walioacha soka wakifariki lakini sio kwa wachezaji ambao wanaendelea kucheza.
Jina lake lipo katika ofisi za TFF kama mchezaji wa Ligi Kuu na ni Novemba mwaka jana tu Sonso alikuwa amecheza pambano lake la mwisho la Ligi Kuu. Ni Novemba mwaka jana tu tunaambiwa kwamba Sonso alishapangwa katika kikosi ambacho kingecheza na Simba, lakini mguu ukaanza kumpa maumivu.
Huu ulikuwa mwanzo wa safari yake ya mwisho. Kinachosemwa ni kwamba baada ya hapo alipelekwa hospitali ya Muhimbili lakini yeye na familia yake wakamtoa hospitali na kuamua kumpeleka kusikojulikana kwa ajili ya matibabu zaidi.
Hili ni fumbo. Kusikojulikana ni wapi? Hatuwezi kufichana kuhusu matibabu. Sonso alikwenda kupata matibabu ya kienyeji. Inadaiwa kulikuwa na hisia kwamba huenda alikuwa amefanyiwa mambo ya kishirikina. Sio jambo jema.
Kumekuwa na wimbi la wachezaji ambao wanaamua kuifuata njia hii. Hatuelewi kwanini, lakini kikubwa zaidi ni elimu miongoni mwa wachezaji wetu. Wachezaji wetu wanapaswa kufundishwa kuamini katika magonjwa halisi yaliyopo na yanayoweza kutibika kitalaamu.
Staa mmoja wa Yanga aliwahi kupata hisia hizi. Akagomea matibabu ya hospitali. Alikwenda kusikojulikana kwa ajili ya kupata matibabu, lakini hali ikaendelea kuwa mbaya. Baadaye Yanga wakamkimbiza Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu zaidi. Alirudi akiwa ametengemaa na maisha yake ya soka yanaendelea. Alitibiwa kitaalamu zaidi kwa mujibu wa ugonjwa wake na hali ikawa sawa.
Imewahi pia kutokea hapo zamani kwa staa wa zamani wa Simba na timu ya taifa. Aliwahi kupata majeraha ya kawaida, lakini akagoma kutibiwa katika njia za kawaida za kitabibu. Bahati mbaya alikuwa anaelekea katika siku zakeza mwisho za maisha yake ya soka. Sijui kama alienda hospitalini au vinginevyo. Namuona akicheza mechi za mitaani.
Hili ni fundisho kwa soka letu na tunahitaji kujitafakari. Tunahitaji elimu kwa wachezaji wetu. Elimu ya saikolojia na elimu ya kawaida kabisa. Itasaidia kwa wachezaji kujua kwamba mwanadamu, hasa mwanamichezo anaweza kuumia kama Cristiano Ronaldo huwa anaumia.
Unajaribu kujiuliza kwa Sonso. Ni kwanini ilifikirika hivyo? Timu kama Ruvu Shooting ina riziki gani ya kuweza kuwahangaisha wachezaji wawafanyie wachezaji wenzao mambo mabaya? Kama haikuwa hivyo Yanga vipi itokee kwa Ruvu Shooting?
Kitu kingine ambacho kinaweza kuwahangaisha wachezaji wetu ni bima ya Afya. Wachezaji wetu wana bima za Afya? Tufanye kwamba Sonso angeamua kukaa hospitalini na matibabu yake yakachukua muda mrefu. Je ni kweli alikuwa na bima ya afya?
Wachezaji wengi wa Ligi Kuu hawana bima za Afya. Sio kwa wao tu, bali pia kwa familia zao. Mchezo wa soka unaonekana kama sehemu ya kuzugia tu na sio kazi kamili. Ni kosa kubwa kwa mwanamichezo kukosa bima ya Afya hasa ukizingatia pia kazi zao zinawafanya wawe katika hatari kubwa ya kuumia.
Wengine wanaweza wasiumie kazini, lakini mtazame mchezaji kama Gerald Mdamu wa Polisi Tanzania ambaye aliumia katika ajali ya gari akiwa na timu. Baadaye ilibainika kwamba Mdamu hakuwa na bima ya Afya. Hata kama angeumia ndani ya uwanja bado angepata wakati mgumu.
Wachezaji wa Yanga, Simba na Azam wana bahati ya kwenda kutibiwa nchi za nje. Wapo wanaokwenda zaidi Afrika Kusini lakini Yanga pia wameanzisha utaratibu kwa kuwapeleka wachezaji wao Tunisia. Sio kila timu inaweza kufanya hivi. Tusisitize wachezaji kuwa na bima. Mchezaji anayefikia hadhi ya kucheza daraja la pili, la kwanza na Ligi Kuu lazima awe na bima.
Tukirudi kwa Sonso, ndani ya uwanja nitafafanua mambo mawili. Kwanza kabisa tumempoteza mchezaji ambaye alikuwa na umbo refu kabla ya kila kitu. Baada ya maumbo ya kina Bakari Malima kuondoka nchini kwa sasa tumebakiwa na wachezaji wachache warefu hasa katika maeneo ya ulinzi. Sonso alikuwa mmoja wao.
Lakini vile vile tumempoteza mchezaji aliyeweza kucheza nafasi nyingi tofauti uwanjani. Angeweza kucheza kama beki wa kushoto, pia kama beki wa kati na pia alimudu kiungo cha ukabaji yaani namba 6. Hii pengine ilitokana na matumizi sahihi ya mguu wake wa kushoto.
Hatuna wachezaji wengi wanaoweza kufanya hivi katika zama za kisasa. Wengi wanaweza kucheza nafasi moja uwanjani. Kitu ambacho kwa sasa Dickson Job au Kibwana Shomari wamekuwa wakiifanyia Yanga ni kitu adimu kwa soka letu.
Zamani tulikuwa na wachezaji wengi ambao wangeweza kucheza katika nafasi tofauti kutokana na upungufu wa baadhi ya wachezaji uwanjani. Marehemu Saidi Mwamba Kizota alikuwa mmojawao. Angeweza kucheza nafasi tatu uwanjani. Angeweza kucheza kama beki wa kati, kiungo na pia mshambuliaji. Mungu amrehemu.
Pamoja na yote haya, lakini kifo cha Sonso kimetukumbusha umoja wetu katika soka. Inawezekana Sonso hakuwa maarufu sana kama Mbwana Samatta, lakini jamii ya wanamichezo imewakumbusha watu wa fani nyingine jinsi mchezo wa soka ulivyo na nguvu.
Msiba wa Sonso ulitufanya tuwe wamoja na kuungana katika majonzi yetu. Ambao wapo katika fani nyingine na hawakumfahamu Sonso walijikuta wakimfahamu na kutaka kujua mengi yanayomuhusu. Ni heshima pia kwa familia yake.
Mungu amlaze mahala pema peponi.
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIO ZENGWE: Tukerwe, tusizoee ubora wa waamuzi.​

zengwe pic

KUNA video mbili zinazotembea hivi sasa kuhalalisha makosa ya waamuzi wa Ligi Kuu. Mpya ni ile inayoonyesha refa wa mechi baina ya Simba na Prisons akitoa uamuzi wa adhabu ya penati kwa tukio ambalo alikuwa mbali karibu hatua 18.
Video ya pili ni ile iliyoibuliwa baada ya tukio hilo la katikati ya wiki. Video hiyo inamuonyesha refa aliyetoa adhabu ya penati kwa Yanga kwa tukio ambalo linaonekana kuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele aliunawa mpira wakati akijaribu kufunga kwa pigo la mkasi.
Na baada ya mechi ya Jumamosi baina ya Yanga na Mbeya City, video nyingi Zaidi za makosa ya waamuzi zitaibuka, hasa wakati huu ambao Ligi Kuu ya soka ya Bara inaingia katika duru la mwisho.
Ni matukio ambayo hayajaanza leo. Kila mara refa anapokosea katika mechi ya Yanga, basi itatafutwa video ya makosa kama hayo katika mechi ya Simba na baada ya hapo mchezo unakuwa umekwisha.
Ni kama tunajifunza kuzoea makosa ya waamuzi na kuyaona kwamba si kitu kikubwa kwa sababu yapo. Na hilo lilidhihirika baada ya kiongozi mmoja wa juu kueleza kuwa maneno mengi husemwa inapotokea makosa ya waamuzi katika mechi za vigogo hao, akithibitisha kuwa kuna makosa mengi Zaidi katika mechi zisizohusu klabu hizo mbili.
Maana yake ni kwamba tuzoee hayo makosa na wala tusiingie kulaumu kwa sababu yapo!
Ajabu sana. Na pengine kwa kauli kama hiyo, Kamati ya Waamuzi nayo inabidi ikae kimya, Isifikirie njia za kupunguza makosa hayo ambayo kuna uwezekano mkubwa hugharimu klabu kiuchumi kwa kuwa si rahisi wadhamini waendelee kuwa na Imani na timu ambazo hazipati ushindi kwa sababu ambazo hazielezeki.
Kwa hiyo chombo pekee kinachoshughulika na waamuzi ni ile Kamati ya Masaa 72, ambayo kazi yake kuu ni kuwaadhibu waamuzi wanaonekana kuvurunda. Watajirekebisha vipi si jukumu lao.
Tatizo ni kwamba hao wanaoadhibu wanatumia picha za marudio za video kuona kosa, wakati pale uwanjani refa hana hiyo fursa ya kuangalia tukio kwa mara ya pili. Wapo vijana wadogo waliofungiwa mwaka mmoja kwa kufanya makosa kwenye ligi ambayo hawakutakiwa hata wachezeshe. Watajifunza wapi baada ya kukosea, si jukumu la Kamati ya Masaa 72!
Wakati fulani mwenyekiti wa zamani wa waamuzi, Nampunde alikuwa na mpango wa kuanzisha kundi la marefa wa ubora wa juu (elite group of referees) kwa ajili ya kuwa na waamuzi wachache, wanaowezekana kuwamudu kwa mafunzo na marekebisho kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu.
Yaani kwa ligi ambayo ina timu 16, unahitaji marefa angalau 12 wa kati na wengine 20 wasaidizi kwa ajili ya Ligi Kuu na pengine mechi muhimu za Kombe la Shirikisho.
Kwa Uingereza, Select Groiup 1 lina waamuzi 22 wa kati ambao huteuliwa na Professional Game Match Officials Limited (PGMOL). Pia PGMOL ina waamuzi wasaidizi na jumla yao ni zaidi ya 70. Miongoni mwao wamo wa kulipwa na wale wa dei waka.
Lakini PGMOL ina jukumu la kuboresha viwango vya waamuzi hao, pia kila mechi huchambuliwa na mwamuzi wa zamani, ambaye huangalia kwa makini kila uamuzi kwa kutumia video za mchezo huo na taarifa za matukio kupima kiwango cha mwamzi. Wachezaji wateule wa zamani (Match Delegates) pia hupima kiwango cha usahihi wa uamuzi na jinsi waamuzi walivyomudu mechi.
Kabla ya kuteuliwa kuingia kwenye Select Group, waamuzi hufuatiliwa uchezeshaji wao na baadaye kuingia kambi ya siku mbili ambayo huhusisha mazoezi ya kimwili na kiufundi na baadaye kuchambua video za mechi na wanaofaulu ndio wanaingia kundi hilo.
 
mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Kondo aacha pengo soka la Bongo.​

kondo pic

KATIBU mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Wilfred Kidao amesema kifo cha aliyekuwa katibu wa chama cha mpira wa miguu Dar es Salaam (DRFA), Msanifu Kondo ni pigo kwenye soka la Tanzania.
Kondo alifariki Februari 14 asubuhi wakati akiwa njiani kuelekea hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Kidao amesema Msanifu alikuwa anafanya kazi kwa weledi mkubwa kwenye upande wa chama chake kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.
“Mkoa wa Dar es Salaam ndio unachezwa mechi nyingi kwa siku lakini yeye aliweza kusimamia kwa nguvu zote na kila kitu kikaenda sawa,” amesema na kuongeza;
“Nje ya ukatibu huyu alikuwa mchezaji mzuri lakini pia ni wakili msomi mzuri ambaye kesi zingine yeye alikuwa anazimaliza kwa kutumia sheria.”
Naye mhasibu wa DRFA, Issa Masoud amesema mara kwa mara viongozi kwa pamoja walikuwa wanawasiliana na familia ya marehemu na hata kazi inapohitajika kufanywa na yeye walikuwa wanamfuata mpaka nyumbani kwake.
Issa amesema marehemu alikuwa na wepesi wa kuamua kesi kwenye soka kwa sababu alikuwa ni wakili kutoka Mahakama kuu.
“Upande wa kuzungumza nae mara ya mwisho alinitumia meseji asubuhi na nilipoijibu hakutuma tena, tukapanga kama viongozi tuje kumuona,” amesema na kuongeza;
“Jana Jumatatu ndio ilitakiwa tuje kuonana nae na kwenda kupatiwa matibabu zaidi lakini akiwa anaenda hospitali alifariki akiwa njiani.”
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mguto amesema ;”Hili ni pigo kubwa kwetu sisi kwa sababu alikuwa mjumbe pia wa masaa 72, pengo lake litazibika lakini sio kama ambavyo alikuwa anafanya Msanifu.
 
mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Dauda Afungiwa Miaka Mitano Kujihusisha Na Soka.​

shaffihdauda_273048835_232774755721111_8468649412253525356_n.webp-1.jpg

Kamati ya maadili ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, imemfungia kwa miaka mitano kujihusisha na shughuli za mpira ndani na nje ya nchi Mjumbe wa Mkutano mkuu wa TFF Shafii Dauda na pamoja na kumtoza faini ya Sh. mil 6.
Dauda amefungiwa kwa kwenda kinyume na maadili na kanuni za utii za TFF kwa kutoa taarifa za uwongo na kuchochea umma kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram.
FLuXu7OXEAMNYNR.jpeg
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Masau Bwire Atoa Visingizio Kipigo cha Simba.
masau.jpg

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya klabu ya Ruvu Shooting Masau Bwire amekiri kuwa mnyonge, kufuatia timu yao kukubali kichapo cha mabao 7-0, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Hatua ya 16 Bora dhidi ya Mabingwa watetezi Simba SC.
Ruvu Shooting ilikua mwenyeji wa Mchezo huo jana Jumatano (Februari 16), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam na kukubali kipigo hicho cha aibu tangu msimu huu 2021/22 ulipoanza.
Masau Bwire amesema matokeo hayo sio rafiki kwa afya, kwa yoyote anayehusika na Ruvu Shooting, kwani yameumiza nyoyo zao na kuwatia majonzi makubwa.
Amesema hawakutarajia kukutana na matokeo ya namna hiyo, kutokana na kikosi chao kilivyojiandaliwa kwa zaidi ya juma moja, lakini kilichotokea jana Jumatano (Februari 16) hawana budi kukubaliana nacho kwa sababu ndio matokeo ya mchezo wa soka.
“Imenitia simanzi sana mimi, naamini hata kwa wengine wanaohusiska na timu hii wana uchungu wa kupoteza mchezo huu kwa kiasi kikubwa cha mabao, tunapaswa kukubaliana na matokeo haya, lakini yanaumiza sana,” amesema Masau Bwire
Hata hivyo Masau Bwire kuna sababu ambazo anaamini zilimepeleka kupoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 7-0 na Simba SC ambayo imeanza kuamka kutoka usingizini.
Jambo la kwanza ambalo Masau amelitaja ni Majonzi ya kufiwa na mchezaji wao Ally Mtoni Sonso, ambaye alifariki dunia mwishoni mwa juma lililopita jijini Dar es salaam.
Lingine ni Dharau ambayo anaamini iliwavaa Wachezaji wao ambao walihisi wangeimudu Simba SC kwa urahisi, hasa baada ya kuona madhaifu yao katika michezo kadhaa iliyopita, hivyo walijitoa na kucheza soka la kufunguka na ambalo lilitoa nafasi kwa wapinzani kupata ushindi mkubwa.
Kwa matokeo hayo Simba SC imetinga hatua ya Robo Fainali ya Michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ikiungana na Pamba FC, Young Africans, Coastal Union, Azam FC, Polisi Tanzania, Kagera Sugar na Geita Gold FC.
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

BAADA YA SEMINA YA MAREFA, TUTARAJIE MABADILIKO?​

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace John Karia jana amefunga Semina ya siku tatu ya Waamuzi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Je, tutarajie mabadiliko juu ya uchezeshaji wa marefa katika sehemu iliyobaki ya msimu?
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mtibwa Waitaka Yanga Manungu.​

273849620_676194817073020_7348114598058763460_n.webp.jpg

UONGOZI wa Klabu ya Mtibwa Sugar, umeweka wazi kuwa, mchezo wao dhidi ya Yanga utafanyika Uwanja wa Manungu uliopo mkoani Morogoro na wala hawatauhamisha kwenda popote.
Februari 23, mwaka huu, Mtibwa watakuwa wenyeji wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, alisema: “Watu wanazusha kuwa mechi sijui itafanyika Tabora, lakini nataka niwaambie kuwa mechi ipo palepale katika uwanja wetu wa Manungu.
“Sisi tunaitaka Yanga ije hapa Manungu, tumejipanga vizuri kuwakabili. “Kwa namna yoyote ile tutapata ushindi, huko nyuma tumepoteza mechi, lakini kwa Yanga tutapambana kushinda.”