Simba Sports Club Thread

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

SIMBA NA ASEC JUMAPILI KIINGILIO 5,000.​


KIINGILIO cha chini katika mchezo wa mchezo wa kwanza Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika baina ya wenyeji, Simba SC na ASEC Mimosas ya Ivory Coast Jumapili kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam ni Sh. 5,000 kwa mzunguko.
Viingilio vingine ni Sh. 20,000 VIP B na C na Sh. 40,000 VIP A, wakati tiketi za mashabiki maalum, maarufu kama Platinum zitauzwa kwa Sh. 150,000.

 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Ahmed Ally: GSM Amejitoa Sababu ya Simba.​

ahmed-ally.jpeg

KLABU ya Simba imesema aliyekuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League), GSM wamejitoa katika udhamini huo kutokana na Simba kutokubaliana na matakwa ya mkataba huo walioingia na Bodi ya Ligi.
Haya yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally; “Kwanza tuwapongeze TFF kwa kutuletea wadhamini maana ni jukumu la kila Klabu kutafuta mdhamini wake lakini sijui ni masoko yamekuwa magumu vilabu havipati hao wadhamini lakini isitumike kama fimbo ya kutuletea kila aina ya mdhamini.
“Kwa wakati ule hawakutuelewa lakini hatimaye jana wametuelewa na baada ya kutuelewa ndio tukasema “HAKI IMESHINDA sisi tulikuwa tunapigania haki na haki hiyo imeshinda.
“Simba hatukukubaliana na ule mkataba tangu mwanzo Kwasababu tuliona hauna viashiria bora kwenye maslahi ya mpira wetu na tulijaribu kupambana lakini bahati mbaya wenzetu hawakutuelewa kwa maana ya vilabu na hii ndio shida kubwa ya mpira wetu.
“Vilabu kama tunashindwa kusimama na tukapigania haki yetu kwa pamoja tataendelea kuburuzwa, tulijaribu kuonyesha njia, wenzetu waliplay part yao sijui niite ni uoga, lakini Simba tulionyesha ujasiri wetu na uelewa wetu wa masuala ya kimkataba.
“Mwezi wa 1, 2 na 3 imepita hela haijawekwa na klabu hailalamiki bodi ya Ligi hailalamiki, Bodi ya Ligi iko pale kwa maslahi ya Vilabu, Bodi ilipaswa kumwambia TFF mbona huyo mtu haleti hela. ‘Basi Mimi nabandua logo kwenye jezi za vilabu vyangu na mabango siweki uwanjani mapaka hela iingie’ hilo halijafanyika tunakuja kusikia jana baada ya Mguto kusema.
“Tuwatoe Yanga wanaonufaika moja kwa moja na huo mkataba hivi vilabau 14 vilishindwa kujipanga vikamwambia mwenyekiti wa bodi ya Ligi kuwa hatuweki mabango hatuvai wadhamini mapaka hela iingie.
“Katika sababu nane walizotoa za kuvunja mkataba ya nane ilikuwa ni Simba, inamaana hawa watu walitaka kuidhamini Simba, Tafsiri yake ni kwamba wamedhamini vilabu 15 wakiweka mabango 4 kwenye viwanja 15 ni sawa na mabango 60. Inamaana hayo hayawatoshi mpaka wavunje mkataba kwa sababu ya Simba Sports,” amesema Ahmed.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Simba Hatuna Mashabiki Lialia – Ahmed.​

ahmedd.png

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally klabu ya Simba kwa sasa haina washabiki lialia kwa sababu simba hawaliilii lakini wana mashabiki wa kufurahia, ‘lialia timu nyingine hizo zenye maisha magumu’.
Akizungumzia GSM kujitoa kudhamini Ligi Kuu Tanzania Bara, Ahgmed amesema; “Tufike mahali tuvalue thamani ya Ligi yetu, thamani ya timu zetu, unakwenda kuipa timu ya Ligi Kuu milioni 3 kwa mwezi ? Kuna wakati mwingine inakulazimu uonyeshe thamani yako.
“Milioni tatu haitoshi hata maandalizi ya machezo mmoja, achilia mbali mwezi mmoja na kama Prison huyo anayelia hana milioni tatu ni Timu ya Kushuka daraja, hatuwezi kuwa na Timu ambayo haiwezi kuwa hata na milioni tatu tutakuwa tunashindana nini sasa?
“Tumeshafahamu tulikosea wapi, zile moods za mechi tatu tumeshamalizana nazo, tumejipanga tumejua makosa yalikuwa wapi, tumejifunza kutokana na hayo makosa sasa tunaelekea mbele.
“Kwenye mechi hizi za Shirikisho huwezi kucheza kwenye uwanja kama Manungu, unacheza na watu wenye mentality, hizi ni mechi za kikubwa tunacheza kikubwa, mnaenjoy,”
Ahmed Ally.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Kapombe: Mechi ngumu, tumejipanga.​

kapombe pic

Wachezaji wa Asec Mimosas ya Ivory Coast wakiwa katika picha ya pamoja katika mazoezi ya timu hiyo wanaojiandaa kucheza na Simba Jumapili Februari 13 katika uwanja wa Mkapa.
BEKI wa Simba, Shomari Kapombe amesema wanatambua ugumu wa mechi ya Jumapili dhidi ya Asec Mimosas, mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).
Kapombe amesema wanajiandaa vilivyo kuhakikisha wanapata ushindi mnono, utakaowapa nguvu katika mechi ya ugenini.
"Tunajua utakuwa mchezo mgumu, lakini tumejipanga kuhakikisha mashabiki wetu wanaondoka na kicheko kitakachotokana na ushindani tutakaotoa" amesema Kapombe na kuongeza;
"Tunahitaji kusonga mbele zaidi, kwani Simba ndio timu pekee inayoliwakilisha taifa kimataifa."
Simba imefanya mazoezi leo Februari 8 jioni katika uwanja wa Mo Simba Arena, uliopo Bunju jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo sio kikosi kizima kilichomfanya mazoezi leo, kutokana program aliyoiweka kocha wa timu hiyo, Pablo Franco.
Wachezaji ambao wamefanya mazoezi katika uwanja huo ni wale walioingia katika mchezo uliopita wa ligi dhidi ya Mbeya Kwanza na ambao hawakucheza kabisa.
Mastaa hao ni Beno Kakolanya, Ally Shomari, Pascal Wawa,Erasto Nyoni, Kennedy Juma, Joash Onyango, Mzamiru Yassin, Israel Mwenda, Gadiel Michael, Peter Banda, Clatous Chama na Hassan Dilunga ambaye ameumia na kutolewa nje.
Mastaa ambao hawakuwepo, walipangiwa programu ya gym.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Wawa aitahadharisha Asec Mimosas.​

wawa pic

BEKI wa Simba, Pascal Wawa amesema wamejiandaa vizuri katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast.
Simba inakutana na Mimosas katika mchezo wa kwanza hatua ya makundi utakaopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
"Tumejiandaa vizuri kwa sababu tunatambua ubora wa wapinzani wetu, ni mchezo mgumu ila tutahakikisha tunapata ushindi." amesema Wawa na kuongeza;
"Ni muda mrefu nimecheza huko, kipindi hicho na sasa ni tofauti na wachezaji wanabadilika mara kwa mara, hivyo jambo la msingi ni kujiandaa vizuri."
Wawa raia wa Ivory Coast amewahi kucheza Asec Mimosas kwa miaka saba kuanzia mwaka 2013-2010, kabla ya kujiunga rasmi na Simba Mwaka 2017.
Simba imepangwa kundi D katika michuano hiyo ikiwa na timu za Asec Mimosas (Ivory Coast), RS Berkane (Morocco) na Gendarmerie Nationale ya Nigeria.
Wawa amesema jukumu lao kama wachezaji nikuhamasishana kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kuwapa kicheko mashabiki wao.
"Tutapambana kwa kadri tunavyoweza,tunatamani kusonga mbele zaidi kwenye michuano hiyo," amesema.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Simba, ASEC kazi imeisha.​

ASEC PIC

SIMBA inacheza mechi yake ya kwanza ya makundi ya Shirikisho Jumapili ijayo dhidi ya Asec ya Ivory Coast Jijini Dar es Salaam.
Simba imesisitiza kwamba wameshamaliza mambo mengi ya ndani ya nje ya Uwanja kwenye mchezo huo na kwa asilimia kubwa wanategemea kuanza kwa kishindo.
Mulamu Ng’ambi ambaye ni mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Simba, ameliambia Mwanaspoti kwamba wao kama viongozi wameshafanya yanayowahusu kuhusu wachezaji na mipango mingine ya nje ya uwanja.
Lakini ndani ya uwanja, Kocha Msaidizi, Selemani Matola alisema baada ya mechi ya Mbeya Kwanza kuna vitu wameviona vya kiufundi na wanavifanyia kazi.
Matola alisema miongoni mwa mambo hayo hasa ni mastraika kupoteza nafasi nyingi za kufunga jambo ambalo limekuwa na shida muda mrefu lakini kama Benchi la Ufundi hawatachoka kulifanyia kazi katika mazoezi.
Alisema mastraika wao wanapitia wakati mgumu kipindi hiki na kwamba hatua hiyo inaweza kumtokea mchezaji yoyote kwenye maisha ya soka hivyo wanalifanyia kazi ili kuwa na mabadiliko na kufanya vizuri mchezo wao na Asec Mimosas.
“Benchi la Ufundi tutakuwa tumewafuatilia na tunazo taarifa za kutosha dhidi ya wapinzani wetu kuna mambo ya kiufundi tunayo na tunaendelea kuyafanyia kazi kabla ya kukutana nao,” alisema Matola na kuongeza;
“Lazima tuwaangalie katika maeneo mbalimbali vile ambavyo wanashambulia wapo imara maeneo gani wanashida wapi kisha nasi tutakuwa na silaha zetu za kwenda kukabiliana nao ili tufanye vizuri,”alisema.
“Watakuwa na maeneo yenye wachezaji wazuri, kulingana na malengo tuliyojiwekea katika mashindano haya tunakwenda kupambana na kuanza vizuri mchezo wa nyumbani kwa kupata ushindi.
“Mazoezi tutaendelea nayo wakati huu ni kulingana na mahitaji ya mechi yalivyo na yale ya kiufundi tutakayokwenda kuyatumia kama silaha zetu kwenye mchezo huo.”
Matola alisema malengo ya Simba ni kufanya vizuri kwenye mashindano hayo na mara zote wanatakiwa kuwa na mwanzo mzuri na faida nyingine ya kucheza uwanja wa nyumbani.
Kwenye Ligi Kuu ya Ivory Coast iliyopo mzunguko wa nane, Asec Mimosa ndio vinara katika msimamo wakiongoza kwa pointi 21 huku wakiwa wamecheza mechi saba, wameshinda zote hawajatoka sare wala kufungwa.
Mimosa kwenye ligi wamefunga mabao 13 na kufungwa matatu, kutokana na data hizo inaonyesha timu hiyo ni nzuri kushambulia ndio maana wamefunga idadi hiyo ya mabao lakini wana wastani wa kufunga mabao mawili kila mchezo mmoja na wana safu ngumu ya ulinzi ndio maana wamefungwa mabao matatu.
Kwenye kikosi chao kuna wachezaji wa safu tofauti ambao Simba wanatakiwa kuwachunga kutokana na uwezo wao tofauti ambao ni Konate, Diakite, Singone, Serge Pokou na Aubin Kramo.
Simba imepania kufanya vizuri kwenye mashindano hayo na kutinga hatua ya nusu fainali na zaidi msimu huu ambao ndiyo wa kwanza wanashiriki kwani walizoea Ligi ya Mabingwa.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Kwa utamu huu Bocco anabaki juu.​

bocco pic

BOCCO apewe ulinzi.” Ndivyo unavyoweza kuitafsiri kauli ya makocha na wachezaji baada ya nahodha wa Simba, John Bocco kushindwa kucheka na nyavu katika mechi 14 ambazo timu yake imecheza kwenye Ligi Kuu Bara.
Kauli hiyo ya kutaka apewe ulinzi ni kutokana na supastaa huyo wa kizazi hiki anayeongoza kwa mabao 142 aliyofunga ndani ya misimu 14, huku anayeshikilia rekodi ya mabao mengi ni Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ mwenye mabao 153 ndani ya misimu 13.
Ukame anaoupitia mchezaji huyo msimu huu umeelezwa siyo mara ya kwanza, kwani wamezoea kumuona anaanza kwa udhaifu na anapomaliza humaliza kishujaa.
Ukiachana na rekodi hiyo Bocco ndiye aliyekuwa kinara wa Ligi Kuu akiwa na mabao 16 msimu uliopita jambo linalowafanya wadau hao wakinzane na maneno ya baadhi ya mashabiki wanaoona ameishiwa na kumshauri akasomee ukocha.
Straika wa Kagera Sugar, Hamis Kiiza ni kati ya wanaomtetea Bocco kwa kumlindia heshima yake kwamba ni mchezaji mzawa anayeongoza kwa mabao mengi.
“Kuna nyakati washambuliaji tunapitia ukame. Haumaanishi kwamba tumeishiwa. Inanishangaza wanaosema Bocco akasomee ukocha. Bado ni hatari akianza moto wake hauzimiki,” anasema Kiiza.
“Watanzania wajaribu kulinda heshima yake, siyo tu msaada kwa Simba bali kwa timu ya Taifa Stars.”
Wakati wa mahojiano hayo Mbaraka Yusuf, straika mwingine wa Kagera Sugar anasema ana uzoefu na Bocco na kwamba siyo mara ya kwanza kuanza akichechemea na akamaliza kishujaa.
“Heshima yake itunzwe. Mashabiki wasimshushe kirahisi Bocco bado ana mpira wake mguuni. Naamini atafanya maajabu. Nampa muda atawanyamazisha wengi,” anasema.
Naye kocha wa timu hiyo, Francis Baraza anasema Bocco ni straika hatari, lakini ni upepo mbaya tu anapitia, ila anaamini atafanya mengi na makubwa.
“Kuna wakati wachezaji wanapitia mengi. Naamini (Bocco) atabadilisha upepo kila mtu atamuona ni fundi,” anasema.
Straika wa zamani wa Yanga, Mohammed Hussein ‘Mmachinga’ anasema kitendo cha Bocco kutofunga hadi sasa hakimaanishi kwamba amefulia, lakini anaamini ni nyakati tu za mpito anazopitia na kwamba atarejea kwenye kiwango chake.
“Bocco ni mzawa, lazima nitamuunga mkono. Naamini ipo siku atarudisha ubora wake na kila mmoja atamzungumzia kishujaa,” anasema.

REKODI ZAKE
2008-2009 (bao 1), 2009-2010 (14), 2010-2011 (15), 2011-2012 (19), 2012-2013 (7), 2013-2014 (7) na katika msimu huu ndipo alipotwaa taji lake la kwanza la Ligi Kuu akiwa na Azam.
Mabao yake mengine ni ya msimu wa 2014-2015 (3), 2015-2016 (12), 2016-2017 (10) uliokuwa wa mwisho kuwa na Azam kabla ya kuhamia Simba 2017-2018 (mabao 14), 2018-2019 (15), 2019/20 (9) na 2020/21 (16).
Aliondoka Azam FC akiwa ameacha alama ya mabao 88 na akiwa Simba amekwishafunga mabao 54 akiwa amecheza misimu minne na msimu huu ni wa tano.
Ndani ya Azam FC msimu ambao alifunga mabao mengi zaidi 19 ukiwa ni ule wa 2011/12 na kwa Simba ni mabao 16 msimu wa 2020/21 na ambao alifunga bao moja ni 2008/9.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Matano kumng'oa Morrison Simba.​

Morrison PIC

KIWANGO cha Simba msimu huu sio cha kuridhisha kwenye Ligi Kuu Bara kutokana na aina ya matokeo wanayopata pamoja na kile wanachoonyesha wachezaji wa kikosi hicho katika kila mechi.

Kuna baadhi ya wachezaji walitegemewa kufanya makubwa mwanzoni mwa msimu huu kama Bernard Morrison aliyeshindwa kufanya hivyo kutokana na kile anachokionyesha Msimbazi.

Kwenye msimu huu, Morrison mechi aliyocheza katika kiwango cha juu ni ile ya mzunguko wa kwanza hatua ya mtoano Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows ya Zambia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Ukiachana na mechi hiyo, Morrison amekuwa mchezaji wa kawaida ndani ya Simba na hata kukosa baadhi ya mechi muhimu na sio kwa bahati mbaya, bali kiwango chake hakiriridhishi benchi la ufundi.

Uongozi wa Simba haujaweka wazi kinachoondelea kati yao, ukiachana na sakata lake la kusimamishwa, lakini Morrison ila kuna mambo ambayo amekuwa akifanya yanayoweza kumuondoa katika kikosi hicho mwisho wa msimu huu baada ya mkataba wake kumalizika.

Makala haya inakuletea mambo yanayoweza kumuondoa Morrison Simba mwisho wa msimu licha ya kusajiliwa kwa mbwembwe nyingi na miamba hiyo ya soka nchini akitokea Yanga misimu miwili iliyopita.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mo Dewji: Kuwekeza Simba ni hasara.​

MO PIC

Mdhamini wa Simba, Mohammed Dewji amesema kilicho mpeleka kambini leo ni mapenzi yake kwa Simba na amekutana na viongozi wachezaji kwa ajili ya kuwapa hamasa kuelekeachezo dhidi ya ASEC.
Mo Dewji amesema wakati huu wapo katika kombe la Shirikisho Afrika lazima wajipange kwa sababu ni mashindano ya kweli ila bado wanakazi ngumu kwenye ligi na lazima kuwa na malengo makubwa.

"Ukweli kwanza kuwekeza ndani ya Simba ni hasara bado tunapambana sana kuifikisha Simba katika bajeti kubwa ya kujiendesha yenyewe, katika miaka minne nilikuwa kiongozi ila sasa hivi sina mamlaka yoyote," alisema Mo Dewji na kuongeza;

"Nipo pamoja sana na Mwenyekiti, Salim Abdalla 'Try Again', Bodi ya wakurugenzi pamoja na mashabiki kuendelea kuisaidia timu ili kuwa na bajeti kubwa kushindana na klabu kama Al Ahly,"

Mo Dewji alisema sawa wanahuzunika kwa nini Simba imekuwa kwenye klabu kumi bora Afrika kwa sababu wanashindana katika Ligi ya mabingwa ila bahati mbaya mwaka huu wametolewa.

"Unajua Simba ni klabu kubwa Afrika na tunatakiwa kuwa na muendelezo wa kucheza robo, nusu fainali mara kwa mara ya mashindano ya kimataifa lakini la pili Super Cup sina taarifa nalo ila viongozi wakubwa wa Simba walienda Misri katika mkutano na bado hawajanipa feedback yoyote.

"Naamini kwamba mafanikio ya Simba ni mashabiki na wiki hii tuna mechi ngumu na wakijitokeza watu 3,5000, Mungu atujalie hizo pointi tatu tutapata na nitakuwepo uwanjani, kwani bila ya mashabiki hakuna Simba wala Mo Dewji," alisema Mo Dewji.

Katika hatua nyingine Mo Dewji alisema amewapa motisha wachezaji na la pili waone ya Simba katika miaka minne wamefika hatua ya makundi na robo fainali.

"Kitu ambacho tunataka awamu hii ni kuvuka katika hatua ya robo fainali na kuweka historia kwani wachezaji nao wataingia kwenye historia ya Tanzania na ya Simba kitu ambacho tunataka tusonge mbele zaidi kwani hapo siku na watasema wameitumikia Simba tushinde ubingwa wa Afrika na kombe la Shirikisho Afrika," alisema Mo Dewji.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Simba Kuwakosa Watano Mechi ya ASEC.​

SIMBA-3.jpg

Kocha wa Kikosi cha Simba, Pablo Franco Martín amesema kuwa Katika mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) dhidi ya ASEC Mimosas 🇨🇮 watawakosa nyota wao watano kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo majeruhi.
Wachezaji hao ni mshambuliaji Chris Mugalu 🇨🇩 ambaye amevunjika mkono hivyo hatahusika katika mchezo huo, Kibu Denis 🇹🇿 ambaye anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi leo, Clatous Chama 🇿🇲 Hatashiriki kabisa michuano hiyo kutokana na kanuni za (CAF), Thadeo Lwanga majeruhi na Bernard Morrison 🇬🇭 aliye simamishwa kutokana na utovu wa nidhamu.
Simba, Februari 13, 2022 saa 10:00 jioni watashuka Katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kumenyana na ASEC Mimosas ya Ivory Coast 🇨🇮 katika mchezo wa Kombe la Shirikisho AFRIKA.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Mo Dewji: Kuwekeza Simba kwa Sasa ni Hasara.​

mo-dewji.jpg

MWEKEZAJI katika Klabu ya Simba, Mohammed Dewji amesema kilicho mpeleka kambini leo ni mapenzi yake kwa Simba na amekutana na viongozi wachezaji kwa ajili ya kuwapa hamasa kuelekeachezo dhidi ya ASEC.
Mo Dewji amesema wakati huu wapo katika kombe la Shirikisho Afrika lazima wajipange kwa sababu ni mashindano ya kweli ila bado wanakazi ngumu kwenye ligi na lazima kuwa na malengo makubwa.
“Ukweli kwanza kuwekeza ndani ya Simba ni hasara bado tunapambana sana kuifikisha Simba katika bajeti kubwa ya kujiendesha yenyewe, katika miaka minne nilikuwa kiongozi ila sasa hivi sina mamlaka yoyote,” alisema Mo Dewji na kuongeza;
“Nipo pamoja sana na Mwenyekiti, Salim Abdalla ‘Try Again’, Bodi ya wakurugenzi pamoja na mashabiki kuendelea kuisaidia timu ili kuwa na bajeti kubwa kushindana na klabu kama Al Ahly,”
Mo Dewji alisema sawa wanahuzunika kwa nini Simba imekuwa kwenye klabu kumi bora Afrika kwa sababu wanashindana katika Ligi ya mabingwa ila bahati mbaya mwaka huu wametolewa.
“Unajua Simba ni klabu kubwa Afrika na tunatakiwa kuwa na muendelezo wa kucheza robo, nusu fainali mara kwa mara ya mashindano ya kimataifa lakini la pili Super Cup sina taarifa nalo ila viongozi wakubwa wa Simba walienda Misri katika mkutano na bado hawajanipa feedback yoyote.
“Naamini kwamba mafanikio ya Simba ni mashabiki na wiki hii tuna mechi ngumu na wakijitokeza watu 3,5000, Mungu atujalie hizo pointi tatu tutapata na nitakuwepo uwanjani, kwani bila ya mashabiki hakuna Simba wala Mo Dewji,” alisema Mo Dewji.
Katika hatua nyingine Mo Dewji alisema amewapa motisha wachezaji na la pili waone ya Simba katika miaka minne wamefika hatua ya makundi na robo fainali.
“Kitu ambacho tunataka awamu hii ni kuvuka katika hatua ya robo fainali na kuweka historia kwani wachezaji nao wataingia kwenye historia ya Tanzania na ya Simba kitu ambacho tunataka tusonge mbele zaidi kwani hapo siku na watasema wameitumikia Simba tushinde ubingwa wa Afrika na kombe la Shirikisho Afrika,” alisema Mo Dewji.




 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Simba Yawaita Yanga Kuwasapoti CAF.​

273175120_151972573854602_4461920906590845852_n1.jpg

UONGOZI wa Simba umewakaribisha mashabiki wa timu mbalimbali ikiwemo Yanga kuwaunga mkono katika
mchezo wao wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas kutoka Ivory Coast, unaotarajiwa kufanyika Februari 13, katika Uwanja wa Mkapa, Dar.
Simba inatarajiwa kucheza mchezo huo ambao ni wa kwanza wa Kundi D ambapo timu nyingine ambazo zipo katika kundi hilo ni RS Berkane ya Morocco na Union Sportive Gerndamarie ya nchini Niger.
Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba,AhmedAlly, alisema: “Nawakaribisha mashabiki wa timu zote kuja kutushangilia, sio tu mashabiki wa Simba japo naamini kuwa Simba tuna mashabiki wengi sana ambao wangetosha kuja lakini hata wale wengine pia mnakaribishwa kuja kutushangilia.
“Kwetu michuano ya kimataifa si jambo geni na tumezoea kushiriki, safari hii tunahitaji kuona tunafika mbali katika michuano hii, hivyo tumejipanga kupambana katika mchezo huo kuhakikisha kuwa tunafikia malengo yetu katika michuano hii mikubwa baraniAfrika.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Simba Yamchimba Mkwara Bernard Morisson.​

272780500_1348468638916041_5936348269823492964_n.webp.jpg

UNAAMBIWA KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morisson, mpaka Feb 8, 2022 hakuwa ameandika barua ya maelezo baada ya kutakiwa kuandika kujibu makosa ya kinidhamu yanayomkabili huku uongozi ukimchimba mkwara kama akiendelea kuchelewa atapelekwa kamati ya nidhamu.
Kiungo huyo ambaye alitimka nchini kwenda kwao Ghana ikiwa ni muda mfupi baada ya kusimamishwa alitua
nchini usiku wa kuamkia jana Jumanne na uongozi wa Simba umemkumbusha kuwa anatakiwa kuandika barua
hiyo la sivyo hatocheza mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Asec Mimosas Jumapili hii.
Morrison ambaye mpaka sasa hayupo kambini baada ya kusimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na kile kilicholezwa kuwa mtovu wa nidhamu, kwa siku za karibuni amekuwa akihusishwa kurudi
kuichezea Yanga.
Hivi karibuni, wakati Simba ikitangaza kumsimamisha nyota huyo raia wa Ghana, taarifa yao ilibainisha kwamba
lazima aandike barua ya maelezo kwenda kwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalez.
Lakini inaelezwa kuwa, kiungo huyo yupo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba wa
miaka miwili ya kuichezea Yanga wenye thamani ya Sh 230Mil.
Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja Habari wa timu hiyo, Ahmed Ally Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, amesema: “Kwanza kabisa ijulikane kuwa Morrison ni mchezaji halali wa Simba mwenye mkataba, yeye amerejea nchini leo (jana) usiku akitokea kwao Ghana.
“Mpaka leo (jana) asubuhi, Morrison bado hajatuma barua ya aina yoyote ile ya kujieleza makosa yake kwa uongozi
labda hapo baadaye huenda akatuma barua hiyo.
“Kama hataweza kutuma haraka barua hiyo na kamati kuamua hukumu yake, basi ataukosa mchezo wetu ujao dhidi ya Asec Mimosas,” alisema Ahmed na kuongeza kuwa: “Suala lake limefikia katika hatua hiyo kwa hivi sasa,
lakini kama akiendelea kugoma kuandika barua basi litapelekwa katika kamati ya nidhamu ya timu Simba
kwa ajili ya kumjadili kabla ya maamuzi mengine kuchukuliwa.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Simba Yashtukia Janja Ya Asec, Yatangaza Vita.​

asec-768x512-1.jpg

LICHA yawapinzani waSimba, Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast kuficha kuhusu ujio wao hapa nchini
kwenye mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, wawakilishi hao wamesema
wala hawatishiki kwani kichapo kipo palepale.
Timu hizo zinatarajiwa kuvaana katika mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambao
utapigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
273175120_151972573854602_4461920906590845852_n1.jpg

Simba ipo Kundi D, ikiwa imepangwa pamoja na US Gendarmerie ya Niger na RS Berkane ya nchini Morocco
ambayo anaichezea Tuisila Kisinda.
Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa maandalizi ya kikosi chao yamekamilika, ambacho jana jioni kiliingia kambini sambamba na kuanza mazoezi ya pamoja kuelekea mchezo huo.
Ally alisema kuwa, hadi hivi sasa bado wapinzani wao hawajawapa taarifa za siku za kutua nchini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo mgumu ambao ni muhimu wapate ushindi nyumbani.
Aliongeza kuwa licha ya wao kutopata taarifa ya siku ya kutua nchini, wanaendelea na maandalizi ya nguvu kuhakikisha wanafanikisha malengo yao ya kushinda michezo yote ya nyumbani.
“Sisi kwa upande wetu Simba, tupo katika maandalizi mazuri ya mchezo wetu huu dhidi ya Asec na kikubwa tunazitaka pointi tatu za kila mchezo tutakaoucheza hapa nyumbani.
“Tunafahamu siyo rahisi lakini tutapambana kufanikisha malengo yetu, uzuri timu imeingia kambini leo (jana) sambamba na kuanza mazoezi kabisa.
“Hivyo tumejipanga vema katika hilo, wapinzani wetu hadi kufikia leo (jana) hawajatupa taarifa za ujio
wao, hatujui sababu ni ipi,” alisema Ally.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Simba wavunja ukimya mkataba wa GSM.​

gsm pic

SAKATA la Kampuni ya GSM kujiondoa katika udhamini mwenza wa Ligi Kuu Bara limechukua sura mpya baada ya klabu ya Simba ambayo inatajwa kuhusika kuweka msimamo huku wanasheria nchini wakieleza kwa maelezo ya GSM inaonyesha kuna udhaifu kwa upande wa Shirikisho la Soka nchini (TFF).
Juzi, Ofisa Biashara wa GSM, Allan Chonjo alisema wamejiondoa kwenye udhamini huo wa ligi baada ya TFF na Bodi ya Ligi kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopo kwenye mkataba walioingia Novemba mwaka jana.
Mwanaspoti limedokezwa, fedha za udhamini zilipaswa kuanza kutolewa Januari mwaka huu lakini baada ya kuonekana kuna vipengele vya kimkataba vinakiukwa, GSM walisimamisha zoezi hilo kabla ya kutangaza kujiondoa juzi huku klabu ya Simba ikitajwa kuhusika.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mulamu Nghambi alisema licha ya wao kutajwa kuhusika katika barua iliyotolewa, lakini kama viongozi wataendelea kusimamia msimamo ambao ulilenga kutaka uwazi juu ya makubaliano yaliyopo baina ya GSM na TFF.
“Kujitoa kwao hatuwezi kusema sisi tuko sahihi au laah! lakini itoshe kusema hilo liko juu yao nasi tutabaki na msimamo wetu kwenye jambo lolote, maana hatuwezi kuingia mikataba ambayo hatujui klabu yetu itanufaika na nini hasa,” alisema Mulamu
Wakizungumzia sakata hilo zikiwa zimepita siku 76 tangu mkataba huo wa miaka miwili wenye thamani ya Sh2.1 bilioni uliposainiwa Novemba mwaka jana, baadhi ya wanasheria nchini walisema kila mkataba una njia ya kuingia na kutoka na ndivyo ulikuwa huo wa GSM.
Wakili Frank Chacha alisema kwa namna moja au nyingine kumeonekana na udhaifu upande wa TFF kutokana na maelezo ya barua ya GSM.
“Hatufahamu kiini cha mkataba, lakini kwa barua ya GSM kama ni kweli, basi inaonyesha kuna udhaifu upande wa TFF na Bodi ya Ligi,” alisema.
Ingawa TFF na Bodi ya Ligi jana walipotafutwa walikataa kuzungumzia sakata hilo, Chacha alisema Simba ilikataa kutii matakwa ya mkataba huo kwa kuvaa nembo ya mdhamini mwenza na TFF ilishindwa kuibana klabu hiyo.
“Mdhamini mwenza ni kama hakupewa mazingira rafiki na nembo zake kushindwa kuheshimiwa na baadhi ya klabu, pia kwa nini TFF ilidhamini mkataba bila mdhamini kuweka kianzio?” alihoji.
Alisema kingine kinacholeta ukakasi ni klabu nyingine 15 ambazo zilitimiza masharti ya mkataba, wametekeleza na hawajapata haki.
Awali klabu nyingi za Ligi Kuu zilifichua kwamba katika mkataba wa GSM na TFF bado hawajapata pesa yoyote, ingawa habari zaidi zinadai zipo klabu ambazo zimepata, lakini TFF wala Bodi ya Ligi hawakutaka kuweka wazi juu ya hilo.
“TFF kama mwakilishi wao kwenye mkataba huo anapaswa kuzilipa klabu kwa kile walichotangaza kipindi chote tangu mkataba kusainiwa kwa kuwa zinapaswa kunufaika tangu mkataba uliposainiwa,” alisema.
Wakili mwingine wa kujitegemea, Kasanda Mitungo alisema japo mkataba ulikuwa ni wa Bodi, TFF na GSM, lakini klabu kama wadau wa mkataba ule zilipaswa kuufahamu.
“Ilizuia mtu yoyote kuhoji, lakini klabu zilipaswa kufahamu na sintofahamu ilianzia kwa Simba kukataa kuvaa nembo ya mdhamini mwenza huyo kwa madai kwamba hawakushirikishwa.
“Kwa maelezo ya barua ya GSM, inaonyesha TFF na Bodi ya Ligi ndiyo wamevunja mkataba huo kwa kutotimiza makubaliano na GSM yenyewe imeusitisha.
“Kisheria ni sahihi, japo hatujui kitu gani ambacho TFF na Bodi hawakuvitimiza kwa kuwa mkataba huo hatujauona na ni sahihi TFF kutuonyesha, lakini klabu zote 16 zilipaswa kuufahamu,” alisema Mitungo.
Alisema sheria ya mkataba inatoa nafuu kwa mtu aliyeumizwa na upande mwingine katika masuala ya kimkataba na kubainisha kwamba kipimo cha mkataba ni utekelezaji na uwajibikaji.
“Kama kile ambacho GSM anakisema ni kweli basi ni haki yao kusitisha na kwenye hilo waliovunja mkataba ni wale walioshindwa kutimiza majukumu na sheria inaruhusu kudai fidia kutegemea na mkataba wao unasema vipi, kama hausemi, basi wanaweza kufungua shauri la kudai fidia,” alisema.




 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

SIMBA SC YAKABIDHIWA JEZI ZA KUTANGAZA UTALII CAF.​

AVvXsEiNWTyKX47ygtOnAbvBPBnIxSRCB933wbY_t-_xhOBMTf83Vdo8fn6MbQSVN4pViwjzCRBY0DoYAZgyE1D9GDU_YN_VMRsW8Ts932Ayqt_RhP7_UYsK88hxQ11TVNSJ2IS67wiG8K8Aw8qzK0vBKvuzSVtlWCGz1ipOIYxrPxd85KpvBJyQmuGo3PmN=w640-h426

MWENYEKITI wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (kulia) akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez jezi yenye ujumbe wa kuitangaza nchi leo hoteli y Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
AVvXsEjX2GZsp9QBvlZrC5y6iadPW4iqBeIVcxdqAAtOCj1eQ44YrJs6CODw_uF2UjsvJmUS2DBT90mYBUGb6TTnnPuWu_H-BENrpdAfOc7uLdXTAGl1SU53CmWvRiUgluU82-IdAAwf-DZ9DkELoiLF3xjXKfW9aeWylz5UfumUZkejADyUmNal7rVAI1FJ=w640-h426

Simba watatumia JEZI hizo kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kuanzia Jumapili kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa Kundi D dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast Saa 10:00 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Kibu Denis, Dilunga Majanga Simba.​

simba-2-2.jpg

MENEJA Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amefungukia maendeleo ya wachezaji wao Kibu
Denis na Hassan Dilunga ambao kwa sasa ni majeruhi.
Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi dhidi ya Asec Mimosas utakaochezwa Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Akizungumza na Spoti Xtra, Ally amesema: “Leo (jana) asubuhi Dilunga ameenda kuangaliwa tatizo
lake na kujua ni kwa muda gani atakaa nje ya uwanja.
“Kwa upande wa Kibu, yeye bado hali yake siyo nzuri, ila Taddeo Lwanga amesharejea na kuanza
mazoezi na timu na huenda mwalimu akamtumia katika mchezo wa Jumapili.”
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Kilichomkuta Chama Simba.​

chama pic

CLATOUS Chama amerejea Simba lakini si kwa kiwango kile alichoondoka nacho kwenda RS Berkane, na anahitaji muda zaidi ili awe kwenye ubora wake huku Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola akiweka wazi sababu kuwa ni kiungo huyo kutopata muda mwingi wa kucheza kule Morocco.
Akizungumza na Mwanaspoti, Matola alisema kuwa nyota huyo hajawa fiti kwa kiwango kikubwa hivyo itamchukua muda kurejesha makali yake yaliyozoeleka.
“Hakuna asiyejua ubora wa Chama awapo uwanjani na isitoshe hakupata muda mwingi wa kucheza kule, lakini kadri anavyozidi kupata muda inazidi kumjengea hali ya kujiamini na kufanya vizuri zaidi,” alisema Matola na kuongeza;
“Uwepo wake kwenye kikosi chetu umetuongezea wigo mpana wa wachezaji wabunifu hususani eneo la kiungo ambalo husaidia kuunganisha safu ya ushambuliaji licha ya kutofanya vyema michezo ya hivi karibuni changamoto ambayo kwa sasa tunaifanyia kazi,” alisema Matola.
Awali alipojiunga na Simba, Septemba 15, 2019, Chama, raia wa Zambia alikuwa muhimili mkubwa ndani ya kikosi hicho kabla ya kuondoka msimu uliopita kisha kurejea kwenye dirisha dogo lililopita.
Kiungo mchezeshaji huyo alifanya makubwa akiisaidia Simba kutisha kwenye michuano ya ndani na ile ya kimataifa, wakibeba mataji ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) huku akiwa miongoni mwa nyota walioipigania timu hiyo kufika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kurejea kwake ni faida kwa timu hiyo kutokana na mchango wake wa kufunga na kupika mabao na hilo alilionyesha msimu uliopita kabla ya kuondoka kwani katika mabao 78 ambayo Simba ilifunga alihusika kwenye mabao 23, akifunga mabao nane na kutoa asisti 15.
Msimu wa 2021/22 amerejea tena wakati wa dirisha dogo la usajili la Januari na kucheza michezo minne ya Ligi Kuu Bara ambapo alianza dhidi ya Mtibwa Sugar walipotoka suluhu, walipolala 1-0 dhidi ya Kagera Sugar na ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya Kwanza Februari waliyoshinda pia 1-0, bao alilofunga yeye.
Chama pia ana dakika 540 za kuisaidia timu yake kupata matokeo chanya katika michezo ya Kombe la Shirikisho Afrika inayotarajiwa kupigwa mwezi huu wakianza na Asec Mimosas ya Ivory Coast itakayochezwa Februari 13 kwenye Uwanja wa Mkapa huku wakicheza mechi nyingine ya hatua ya 16 ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Ruvu Shooting.
Baada ya hapo Simba itaenda ugenini kucheza na Gendarmerie Nationale (Nigeria) Februari 20, RS Berkane ya Morocco Februari 27 kisha itarejea nyumbani kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United Machi 3 na kurudiana na RS Berkane Machi 13 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Morrison aomba radhi, Simba wakausha.​

bm pic

STAA wa Simba, Bernard Morrison ametuma ujumbe kwenye kundi la WhatsApp la wachezaji wa timu hiyo na kufowadi vilevile kwa viongozi akiomba radhi kwa kilichotokea.
“Naomba mnisamehe jamani. Nimekosa,” alisema Morrison kwa lugha ya Kiswahili. Siku moja kabla ya kucheza mechi na Mbeya Kwanza, Morrison aliwatumia ujumbe huo wa sauti, uliokuwa ukiomba msamaha kwa kosa alilolifanya usiku wa Jumatatu wiki iliyopita.
Morrison alitoroka kambini usiku wa kuamkia Jumanne wiki iliyopita na benchi la ufundi, wachezaji na viongozi walimshtukia na wakampa adhabu ya kumsimamisha muda usiojulikana.
Katika grupu hilo Morrison alisema; “Naomba radhi kwa wachezaji, kocha, meneja, kapteni na wachezaji wazoefu na kila mmoja aliyepo humu. “Naomba radhi sana kwa yale yote yanayoendelea na yaliyotokea kwani naamini nimefanya jambo la kutowaheshimu kila mmoja wenu, najua nimeikosea klabu na sikulenga kufanya hivyo,” alisema staa huyo ambaye habari zinasema kwamba amefanya mazungumzo ya awali na timu kadhaa ikiwemo Yanga na huenda akatimka Simba muda wowote baada ya sakata hilo.
“Lakini kwa jambo lililotokea haina maana kwangu kujielezea binafsi naomba msamaha kutoka kwenu wote, naomba msamaha kwenu, John Bocco, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Joash Onyango, Clatous Chama siwezi kuwataja wote hapa, ila naomba kwenu wote mnisaidie kuomba radhi kwa kocha na Bodi ya Wakurugenzi.
“Nina imani baada ya hapo nakwenda kufanya vitu vilivyokuwa bora natamani amani iwepo pamoja na upendo kwa mara nyingine tena kwenu kwa yale yote yaliyotokea kambini. Naomba mnisamehe jamani. Nimekosa.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Bosi Simba Apiga Mkwara Mzito CAF.​

2e795122f854fa0d35c62e3d6abab521.jpg

MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu, ametamba kuwa, malengo waliyojiwekea msimu huu
ni kufika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, hivyo kwa kuanza wataanza kuchukua pointi tatu mbele
ya ASEC Mimosas, kisha RS Berkane.
Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Saalaam, Simba itapambana na ASEC Mimosas, ukiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya michuano hiyo inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambapo
timu hizo zipo Kundi D.
Msimu uliopita, Simba iliishia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku malengo yakiwa ni kufika
nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa Afrika kwa ngazi ya klabu.
Akizungumza na Spoti Xtra, Mangungu alisema kikubwa walichopanga msimu huu ni kuvuna pointi tatu katika
kila mchezo watakaocheza nyumbani kwenye Uwanja wa
Mkapa.
Aliongeza kuwa, hakuna kitakachoshindikana kwao kutokana na maandalizi makubwa waliyoyafanya chini ya Kocha Mkuu, Pablo Franco raia wa Hispania.
“Niwaombe mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi Jumapili hii katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi
ya ASEC Mimosas utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.
“Uwepo wa mashabijki uwanjani ndiyo chachu ya ushindi katika mchezo huo ambao muhimu kupata pointi tatu katika uwanja wetu wa nyumbani.
“Simba imekuwa na historia ya kipee katika michuano ya kimataifa tangu miaka ya 1970, kama uongozi
tumeshakamilisha maandalizi yote ya mchezo huo,” alisema Mangungu.