Yanga Thread

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Yanga bado Ushindi tu!​

Ushindi PIC

YANGA ya msimu huu sio ya mchezo, kwani timu pinzani zikiamua kumkomalia nyota mmoja, basi wengine hasa wa kigeni wanawaadhibu na rekodi zinaonyesha kwa kikosi cha sasa ni Chico Ushindi tu na kipa Djigui Diarra ndio hawajatupia.
Katika msimu huu Yanga ina maproo 11, kati ya hao tisa tayari wameshafunga mabao kwenye mechi za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), isipokuwa Ushindi aliyesajiliwa dirisha dogo na Diarra.
Mabao 23 ya Yanga katika Ligi Kuu, 17 yamefungwa na wageni huku sita yakifungwa na wazawa wakiongozwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’. Straika Fiston Mayele anaongoza akifunga sita, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ (4), Shaban Djuma (1), Tonombe Mukoko (1), Khalid Aucho (2) na Jesus Moloko (3). Nje na mabao ya ligi katika michuano ya ASFC straika wa timu hiyo, Heritier Makambo ana mabao matatu, huku Mayele akitupia mawili, ilhali kiungo Yannick Bangala juzi dhidi ya Biashara United alifunga bao moja.
Kwa upande wa wazawa waliofunga ni Fei Toto (4), Dickson Ambundo (1) na bao moja alijifunga Justine Bilary (Dodoma Jiji).
Akizungumza na Mwanaspoti, mchambuzi wa soka George Ambangile alisema ndio maana halisi ya kikosi kipana kila mmoja anategemewa na wachezaji wenyewe wanatambua nini wanakifanya.
“Wanajenga kitu kimoja hawataki kugombea fito na ndio maana kila mmoja anapambana na akipata nafasi anafanya kile timu inatakiwa ifanye.Hamuwezi kuwa na matokeo mazuri kama kila mmoja anacheza ili aonekane yeye,” alisema.
Mchambuzi wa soka, Tigana Lukinja alisema kitu alichokitengeneza kocha Nasriddine Nabi ndani ya kikosi chake ndicho kimekuwa chachu ya mafanikio kwa wachezaji na sasa wanambeba.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Yanga Yazindua Kadi za Kielektroniki Bungeni.​

274070653_380393280463660_4142786943783440360_n.jpg

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson akikabidhi kadi ya Uanachama ya Kielektroniki kwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Yanga, Kapteni Mstaafu, George Huruma Mkuchika na Waheshimiwa Wabunge katika hafla ya uzinduzi wa kadi mpya za uanachama za Yanga leo Bungeni Jijini Dodoma.




Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson akikabidhi kadi ya Uanachama ya Kielektroniki kwa Wabunge katika hafla ya uzinduzi wa kadi mpya za uanachama za Yanga leo Dodoma.

 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Nabi Ampa Mayele Kazi Maalum​

yangasc_272929964_899875410699999_6070729047343910339_n.jpg

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ametoa majukumu mazito kwa wachezaji wa timu hiyo, akiwemo kinara wa mabao, Fiston Mayele kwa kuhakikisha wanatupia mabao ya kutosha katika mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar kwa lengo la kuendelea kuongoza ligi.
Nabi ametoa kauli hiyo baada ya kurejea kwa ligi kufuatia kumaliza mechi za Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) huku wakiwa na kumbukumbu za matokeo ya suluhu katika mchezo wa mwisho dhidi ya Mbeya City kabla ya ligi kusimama kupisha Shirikisho.
Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 14, ikishinda 11 huku ikiwa imetoka sare tatu. Ni timu pekee ambayo haijapoteza mechi hadi sasa kwenye ligi huku ikitarajiwa kuivaa Mtibwa Sugar Jumatano
ijayo, Manungu.

YANGA-9-1.jpg


Akizungumza na Championi Ijumaa, Nabi alisema kuwa wanarejea kwenye ligi wakiwa na lengo moja la kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi katika mchezo wao ujao dhidi ya Mtibwa ili kuendelea kuongoza ligi hiyo, hivyo
amewataka kupambania matokeo ya uhakika katika mchezo huo.
“Tunarejea kwenye ligi baada ya mapumziko ya kucheza Kombe la FA, tunaelekea kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo mgumu wa ugenini ambao ni wazi tunahitaji kupata matokeo mazuri kwa hali yoyote ili kuendelea kubakia juu kuongoza ligi, kwa matarajio yetu msimu huu ni ubingwa ila presha ya ushindani imekuwa juu kutokana na wapinzani wetu kujipanga vizuri.
“Kila mchezaji kwa sasa anajua jukumu lake kuelekea kwenye mchezo huu mkubwa ambao matokeo kwetu ni jambo
la lazima, ukiangalia safu ya ushambuliaji tumekuwa na maongezi ya mara kwa mara kuhakikisha tunafikia
malengo ya kushinda katika kila mchezo, ingawa siyo kazi nyepesi,” alisema Nabi.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

YANGA YAWAASA MASHABIKI WAKE KULINDA AMANI.​

AVvXsEiuJfFJcHxdXPuH227QyS59tMobZtZM5Hh1WWL58y13FyBamJLagNWS6QR8AomBrBzD75JWmua0Qs3-E3NNdceS95LQuATanS3dhQTMBLQ2ZHK9NXJ_6BaXSdpyhon2nONdrkA_lyyDuZ_hVEocRJWxoveQQrNG8X-NleYcoljmAu76Twn-3QX56usr=w640-h640

KLABU ya Yanga imewaasa mashabiki wake kuwa mstari wa mbele kulinda amani kwa kuepuka kuwa chanzo cha vurugu popote kwenye mechi za timu hiyo.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Chico, Moloko Wamvurugia Nabi.​

CHIKO..JESUS_.png

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema kuwa kukosekana kwa wachezaji wake zaidi ya saba katika kikosi chake, kunamvurugia mipango ya ushindi kuelekea michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC).
Hiyo ni baada ya kuongezeka kwa majeruhi katika kikosi chake ambao ni Mkongomani, Jesus Moloko aliyeshindwa kumalizia mchezo wa FA dhidi ya Biashara United uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Yanga katika mchezo huo iliwakosa wachezaji saba, kati ya hao ni kutokana na majeraha ambao ni Yacouba Songne, Kibwana Shomari, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Chico Ushindi, Denis Nkane, Chrispin Ngushi na Dickson Job anayetumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Nabi alisema kuwa katika timu wanapokosekana wachezaji zaidi ya saba kunaharibu mipango ya kiufundi ya kocha katika kupata ushindi.
Nabi alisema kuwa kikosi chake kinakabiliwa na wachezaji wengi majeruhi, hadi unafikia wakati analazimika kuwatumia majeruhi kama ilivyokuwa kwa Moloko ambaye alimtumia akiwa ana majeraha katika mchezo.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Yanga Ina Presha ya Ubingwa
273265682_337236161610068_6204935112247286040_n.jpg

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga, amesema kuna presha kubwa katika kusaka ushindi uwanjani ambao utawapa ubingwa kutokana na kila timu kupiga hesabu za kuifunga Yanga.
Yanga ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 36 kibindoni baada ya kucheza mechi 14, ndani ya ligi hiyo hawajapoteza mchezo msimu huu, huku Jumatano ijayo wakitarajiwa kupambana na Mtibwa Sugar.
Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi alisema: “Presha inakuwa kubwa hasa timu inaposaka ushindi, ukizingatia kwamba ili uwe bingwa ni lazima ushinde mechi zako, hivyo hakuna tatizo katika hilo, tunalifanyia kazi.
“Kwa timu ambazo tunakutana nazo ninaona kwamba zinataka kuifunga Yanga, hapo inafanya kila mechi kwetu kuwa ngumu. Lakini inatakiwa kuwa hivyo kwa kuwa unapokuwa unashindana na mpinzani lazima awe ana malengo ya kushinda kama ambavyo sisi tunahitaji kushinda.”
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Yanga wana jambo, Msikie Senzo​

Yanga pic

YANGA imebakiza dakika 90 dhidi ya Mtibwa kumaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ambazo wamepania kumaliza kwa kishindo.
Kocha wa Yanga, Nesreddine Nabi ameangalia rekodi zao na Mtibwa akabadilisha ghafla programu za mazoezi ambapo sasa zimefanana na zile za maandalizi ya mechi ya watani kuanzia ndani na nje ya uwanja.
Amewasisitiza mastaa wake kila mmoja akilala akiamka kila muda aufikirie mchezo huo kwani una umuhimu mkubwa kwao.
Hata kwenye kambi yao iliyopo Kigamboni, makocha wamekuwa wakikaa na mchezaji mmojammoja kila mara kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusiana na mchezo huo ambao Simba walilazimishwa suluhu hivi karibuni na kuyumba mechi zilizofuata.
Nabi amepania kukwepa mtego wa suluhu, lakini kuongeza tofauti yao na Simba ambao ni mabingwa watetezi wanaotamba kwamba Yanga imewashikia nafasi yao pale kileleni.
Mechi hiyo itakayopigwa Manungu - Morogoro ina rekodi ambazo zimewashtua Yanga na kulazimika kubadili staili ya mazoezi kuanzia jana watawahi zaidi kufika Morogoro.
Kirekodi Yanga walipokutana na Mtibwa ugenini ndani ya misimu 10 wameshinda mechi mbili pekee huku wenyeji wao wakishinda nne na sare nne.
Rekodi hizo zikawashtua mabosi wa timu hiyo, lakini pia Nabi kisha wakaanza kuchora ramani wakikumbuka kwamba watani wao - Simba waliangusha pointi mbili katika uwanja huo msimu huu.

RAMANI YA NABI
Nabi ambaye uongozi umemhakikishia mkataba mpya wa miaka miwili baadaye mwaka huu, ameanza maandalizi magumu kuanzia juzi akiwarudisha tena wachezaji wake gym wanapojifua kwa saa tatu na nusu. Programu hiyo hufanyika pakiwa na mechi ngumu ya watani.
Jana waliingia katika ratiba ya uwanjani wakianzia asubuhi katika mazoezi makali ya kujaza zaidi ufiti wa mwili kisha jioni wakarudi tena kwa ratiba ya mbinu.
Nabi ameliambia Mwanaspoti kuwa wataingia katika mchezo huo wanaoutazama kama fainali nyingine kutokana na rekodi, lakini ugumu wa wapinzani wao na mapema wanatakiwa kuwa na maandalizi mazuri.
Alisema kwa sasa mbali ya mambo ambayo wameendelea kupambana nayo katika stamina pia wanataka kuhakikisha wanakuwa na ubora mkubwa wa kutumia nafasi ambazo wanatengeneza kazi ambayo itafanyika katika siku tatu kabla ya safari yao ya kuwafuata Mtibwa.
“Tunaiheshimu kila timu. Unajua Yanga kila mechi imekuwa ni kama fainali hatujawahi kuwa na mchezo rahisi. Nimeona hizo rekodi hatuna matokeo mazuri sana ingawa msimu uliopita tulishinda mechi mbili zote,” alisema Nabi akizungumzia mechi hiyo ya Jumatano.
“Ingawa tunakabiliwa na idadi kubwa ya wachezaji majeruhi lakini wapo ambao wanaweza kurejea tutaangalia hizi siku mbili, nimewaambia wachezaji kitu pekee ambacho kitatubeba katika mechi hizi ngumu ni ubora wetu wa kutumia nafasi ambazo tunatengeneza.
“Angalia jinsi tulivyocheza mechi iliyopita niliwapongeza wachezaji wangu kwa jinsi walivyopambana kwa kuwa na kasi kubwa ya kusaka mabao lakini sasa tunatakiwa kuhamia katika kutulia na kuzitumia.”

MSIKIE SENZO
Viongozi nao wamekuwa na hesabu zao na haraka wameshaanza kuufuatilia Uwanja wa Manungu ambao wanakwenda kuutumia kujua mastaa wao watakumbana na changamoto gani wakati wa mchezo.
Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa ameliambia Mwanaspoti kuwa uongozi wao uko makini kufuatilia maandalizi ya mechi hiyo na kwamba watahakikisha wanakuwa na morali kubwa kwa wachezaji wao kuelekea mechi hiyo.
“Kazi yetu kama uongozi ni kuhakikisha timu inaandaliwa vizuri na hilo linafanyika kule kambini lakini pia tutahakikisha wachezaji wanakuwa katika morali nzuri hili litafanyika, tunajua kwamba mpaka sasa mechi inaonekana itacheza Manungu lakini tuna taraifa kwamba hali ya uwanja ni nzuri labda itokee mabadiliko ya hali ya hewa,” alisema Senzo.

Nini maoni yako kuhusiana na mchezo huu;
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Nabi: Simba? Thubutuuu​

nabi pic

YANGA ipo kambini ikiendelea na maandalizi ya mchezo ujao dhidi ya Mtibwa Sugar, huku kocha Nasreddine Nabi akisisitiza hataki kusikia chochote msimu huu, zaidi ya kubeba ndoo, lakini akiipika safu yake ya ushambuliaji.
Katika tizi la juzi kambini Avic, Kigambini kocha Nabi alikomaa na washambuliaji wake ili kuongeza umakini wa kufunga na habari njema ni kwamba staa wao Fiston Mayele jamaa anauwasha moto hadi mazoezini.
Mayele katika mazoezi hayo ya alikuwa mwiba akifunga mabao matano tofauti, lakini Nabi alipomaliza mazoezi hayo aliwabakisha washambuliaji wake wengine wawili, Yusuf Athuman na Heritier Makambo.
Kubaki kwao hapo pia Nabi akawabakiza mabeki wawili wa kati Ibrahim Bacca na beki mmoja wa kutoka timu ya vijana kisha kila mmoja kumtaka kupambana kufunga.
Washambuliaji hao walikuwa wakipewa mipira tofauti na viungo wa pembeni Dickson Ambundo na Denis Nkane kisha kutaka Makambo na Yusuf kufunga, huku langoni kukiwa na makipa wawili tofauti kwa kila goli Eric Johora na chipukiz Geofrey Magaigwa.
Mazoezi hayo yalikuwa maalum kwa washambuliaji hao, Nabi akitaka kuona wanakuwa bora katika kufunga na Yusuf alifanya vizuri kuliko Makambo.
Yusuf anayepambana kurejea katika ubora akitokea majeruhi alifunga mara tatu, huku Makambo akifunga mara moja kabla ya kuumia kwa kugongana na Bacca.

MATIZI YA FEI TOTO
Naye kiungo Feisal Salum alikuwa na moto akionyesha ubora wa kufunga mazoezi ya pamoja na wenzake akifunga mara nne.
Kiungo huyo alipigishwa tizi la maana na kuonyesha kama wapinzani wa Yanga wakikaa kizembe wataumia kwa jinsi alivyoonyesha kuiva zaidi hasa kwa pasi mbali na kufunga.
Hadi sasa katika Ligi Kuu, Fei Toto amefunga mabao manne akilingana na Saido Ntibazonkiza wakiwa nyuma ya kinara Fiston Mayele.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Moloko, Bryson kuikosa Mtibwa, Sure Boy arejea​

yanga safari pic

KIKOSI cha Yanga kimeondoka jana Februari 21 tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar Februari 23 Mwaka huu kwenye Uwanja wa Manungu Morogoro.
Mhamasishaji wa klabu hiyo, Haji Manara anasema timu inaondoka mchana wa leo huku ikitarajia kuwakosa baadhi ya mastaa wao wanaokabiriwa na majeraha.
Anasema kwenye mchezo huo wanatarajia kumkosa Jesus Moloko, Abdallah Shaibu na David Bryson huku akimtaja Aboubakal Salum ‘Sure Boy’ na Yassin Mustafa kurudi baada ya kukaa nje kwa muda.
“Maandalizi kwa upande wa timu yanakwenda vizuri na tunakwenda Manungu tukiachana na histori zilizopita tunafuata pointi tatu muhimu ili kuendeleza mpango kutwaa taji,”
“Mtibwa Sugar ilishawahi kuwa bingwa mara mbili mfululizo ni timu ya kuheshimiwa wanauzoefu mkubwa wana misimu 25 kwenye Ligi ukitoa Simba na Yanga hakuna timu iliyocheza mfululizo ligi bila kushuka,” anasema.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

"Asikwambie Mtu, Yanga Tamuu"​

yanga tamu pic

BAADA ya kuhama Yanga akitaja kuwa ni timu inayomuumiza kutokana na kukosa mataji msanii wa muziki wa kizazi kipya Marioo amerudi tena Yanga kwa kuachia wimbo wenye maudhui ya kuisifia.
Marioo alihama Yanga msimu uliopita na kujiunga na Simba ambayo ilitwaa mataji mara nne na kuiwakilisha nchi kimataifa.
Mkali huyo wa mashairi ya mapenzi amefanya remix ya wimbo wa Bia tamu na kuwa Yanga tamu ukiambatana na video inayoonyesha matukio mbalimbali ya wachezaji wa Yanga wakiwa uwanjani.
“Nimerudi nyumbani namepata nafasi hadi ya kutoa nyimbo kwaajili ya mashabiki ni zawadi yangu kwao waitumie kila timu inapopata matokeo,” anasema.
“Naamini nimefanya uamuzi sahihi aliyeniamisha Yanga kanirudisha tena nawapenda wanayanga naomba mfurahie wimbo huu maalum kwaajili yenu,” anasema.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Nabi awatega mastaa Yanga​


nabi pic

YANGA ipo kwenye maandalizi ya mwisho kabla ya kuifuata Mtibwa Sugar kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Manungu, lakini kocha Nesreddine Nabi amewashusha presha mashabiki wa timu hiyo.
Kocha huyo mwenye uraia wa Ubelgiji na Tunisia, ambaye mkataba wake unamalizika, alifichua kuna uwezekano mkubwa akasalia kikosini, lakini akaweka wazi sifa za mastaa wake wapya wa msimu ujao, hivyo hata wale watakaosalia ndani ya timu hiyo lazima wajipange.
Akizungumza na Mwanaspoti juzi kwenye kambi ya mazoezi ya timu hiyo iliyopo Avic, Kigamboni pembezoni mwa Jiji la Dar es Salaam, Kocha Nabi alisema kama kikosi chake kitachukua ubingwa kisha akasajili watu wapya wanatakiwa kuwa na sifa tatu kuu kulingana na ubora wa wachezaji mbalimbali wanaopatikana nchini.
Nabi alisema msimu ujao anataka kuwa na kikosi kitakachokuwa na wachezaji wenye sifa tatu ambapo akazitaja ya kwanza kuwa ni uelewa mkubwa utakaoambatana na uthubutu awapo uwanjani.
Alisema watakaporejea katika michuano mikubwa ya Afrika ubora wa namna hiyo ni kitu muhimu ambacho kitamsaidia mchezaji kufanya makubwa uwanjani.
“Lazima uwe na mchezaji mwenye uelewa mkubwa lakini pia aliye na uthubutu wa kutamani na ari ya kufanya uamuzi mzito awapo uwanjani. Kwa sasa tunao katika kikosi chetu lakini tunawahitaji wengi zaidi ambao watasaidia hata usindani wa ndani ya kikosi,” alisema Nabi.
Akitaja sifa ya pili, Nabi alisema ni mchezaji mwenye haiba anapokuwa katika umati wa mashabiki wengi aweze kuwa na ujasiri wa kufanya kitu bila wasiwasi.
“Tuna wachezaji hapa tumewaleta baadhi bado hawajafanya kile tulichotarajia ingawa hatujakata tamaa, tukiwa mazoezini wamekuwa na ujasiri mkubwa wa kufanya mambo ambayo utafurahia lakini wakiingia katika mechi sijajua wanaogopa mashabiki wanacheza chini sana,” alisema Nabi na kuongeza;
“Mchezaji anatakiwa kuanza kufanya makubwa katika eneo la mazoezi na akija kwenye mechi atafanya kama kile cha mazoezini au zaidi yake lakini hapa kuna baadhi hiyo hali wamekuwa wakikumbana nayo.
“Mchezaji anatakiwa kuwa na ari kubwa anapocheza mbele ya mashabiki wake anatakiwa kuonyesha thamani yake kwanini yupo hapa Yanga lakini sio unawaogopa mashabiki wako na jambo zuri hapa Tanzania kila unapokwenda unakutana na mashabiki wengi wa timu yetu.”
Alisema sifa ya mwisho lakini ya umuhimu mkubwa ni ubora wa mchezaji mwenyewe kwa wakati husika na kwamba ana rekodi gani za ubora kwa msimu uliopita na mitatu nyuma.
“Tutazingatia sana ubora, bahati mbaya mimi sio muumini wa wachezaji wa kuletewa nafikiri hiki kimetusaidia sana sisi makocha na viongozi wa klabu, tulikuwa tunakaa pamoja na kuamua kwa kuangalia ubora wa wachezaji,” alisema na kuongeza:
“Kuna wakati lazima tuseme kilichosahihi, moja ya sifa bora hapa Yanga ni kuanzia kiongozi wa juu mpaka chini kuheshimu nafasi ya makocha kuamua mambo mbalimbali ya ufundi hii imetupa wachezaji bora sana.”
Aidha, kocha huyo alisisitiza kurejea kwa beki Djuma Shaban katika kikosi kutoka kutumikia adhabu ya kufungiwa iliyotokana na kumpiga kiwiko mchezaji wa Polisi Tanzania, kumeongeza mzuka kwa timu hiyo kabla ya kuwakabili Mtibwa katika mechi aliyokiri ni ngumu.
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Aucho, Bangala waundiwa tume​

Nabi PI

VIUNGO wa Yanga, Khalid Aucho na Yanick Bangala wameundiwa tume mapema na Mtibwa Sugar kuhakikisha hawaendi kusumbua kwa kutumia uzoefu wao kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu.
Mtibwa na Yanga zitakutana keshokutwa katika pambano litakalopigwa kwenye Uwanja wa Manungu litakaloanza saa 10:00 jioni, huku Yanga ikiwa kileleni mwa msimamo kwa pointi 36 baada ya mwechi 14, ikifunga mabao 23 hadi sasa.
Akizungumza na Mwanaspoti, kiungo wa Mtibwa Sugar, Baraka Majogoro alisema mbinu kubwa ya kukabiliana na wachezaji hao wameambiwa kucheza nao kwa nidhamu ya hali ya juu.
Majogoro alisema wachezaji hao wana uzoefu mkubwa hivyo mwalimu wao mara kwa mara amekuwa akiwaambia wawaheshimu wapinzani na kucheza kwa nidhamu kubwa uwanjani.
“Kwanza mimi binafsi nawaheshimu wapinzani hao kwa sababu wapo kwenye timu kubwa, kikubwa tumesisitizwa kuwaheshimu na sisi tucheze mpira wetu kwa utulivu ndani ya uwanja,” alisema Majogoro.
Majogoro kwenye eneo la kiungo huwa anacheza sambamba na Said Ndemla kwenye kikosi cha Mtibwa.
Rekodi zinaonyesha Yanga hutaabika sana mbele ya Mtibwa katika mechi zinazopigwa mjini Morogoro kwani katika mechi 10 zilizopita mjini humo Yanga imeshinda mara mbili tu huku nyingine zikiwa ni vipigo ama sare.
Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana Manungu baada ya uwanja huo kuzuiwa na mamlaka za soka na mechi za nyumbani za Mtibwa kuhamia Jamhuri Morogoro, kabla ya safari hii kurudishwa tena Manungu.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Mayele: Hao Mtibwa Sugar Waje​

273265682_337236161610068_6204935112247286040_n.jpg

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele, ameapa kuipambania Yanga katika mchezo unaofuata wa ligi kuu
dhidi ya Mtibwa Sugar kwa kuhakikisha timu hiyo inaibuka na ushindi wakiwa ugenini.
Yanga katika mchezo huo, wanatarajiwa kuwa ugenini kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro, utakaochezwa leo.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Mayele alisema kuwa licha ya kufahamu kuwa mchezo huo utakuwa mgumu
lakini watapambana kama timu kuhakikisha wanaibuka na ushindi muhimu katika mchezo huo kutokana na kufahamu umuhimu wa mchezo wenyewe.
“Tunafahamu ukubwa wa mchezo huu, ni mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi, hivyo tunatakiwa kuumaliza kwa ushindi, naona utakuwa mchezo mgumu kwa kuwa tutakuwa ugenini lakini hatuhofii
hilo.
“Sisi tupo tayari kwa ajili ya mapambano na tutapambana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha tunaondoka na
ushindi, kila mchezo kwetu unahitaji ushindi, na hiyo ni kutokana na kuhitaji kutimiza malengo yetu msimu huu,” alisema Mayele.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Fei Toto apewa kazi maalum Yanga SC​

FEI-TOTO.jpg

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amepanga kumtumia kiungo wake, Feisal Salum ‘Fei Toto’, kama njia rahisi ya kupata ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar, kesho Jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Manungu, Morogoro.
Mchezo huo ni wa kumaliza mzunguko wa kwanza ambapo Yanga ipo kileleni na alama zake 36, huku Mtibwa ikishika
nafasi ya 15, ikikusanya alama 12, zote zikicheza mechi 14. Chanzo chetu kutoka Yanga, kimeliambia Spoti Xtra kwamba, katika mazoezi ya kuelekea kwenye mchezo huo, Nabi ameamua kumuongezea mbinu za ufungaji Fei Toto, lengo likiwa ni kumfanya afunge wakati wapinzani wakimkaba mshambuliaji wao hatari, Fiston Mayele.
“Kocha wetu hana shaka kabisa na taarifa za ubovu wa Uwanja wa Manungu, zaidi yeye yuko bize kuhakikisha anamnoa Fei Toto katika suala la kufumania nyavu kwani mazoezi mengi ameonekana akimtaka kutumia kila nafasi kufunga.
“Hiyo ni katika kuhakikisha timu inapata ushindi kwa sababu tunafahamu kwamba wapinzani watakuwa bize kumkaba Mayele, jambo ambalo litatoa mwanya kwa wengine kufunga na kupata ushindi tunaouhitaji,” kilisema chanzo hicho.
Msimu huu katika Ligi Kuu Bara, Mayele amekuwa chachu kubwa ya ushindi kwa Yanga akiwa amefunga mabao sita, ndiye kinara wa mabao kikosini hapo, huku Fei Toto akiwa nayo manne.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Yanga SC: Manungu Sio Tatizo Kwetu​

274491263_646055986724431_8847295988061661253_n.jpg

HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari waYanga,amesema kuwa Uwanjawa Manungu ambaounatarajiwa kutumika leo kwa
mchezo wao wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar kwao sio tatizo.
Yanga ambao ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 36, wanatarajia kukutana na Mtibwa Sugar iliyokusanya pointi 12 na zote zimecheza mechi 14.
Akizungumza na Championi Jumatano, Bumbuli alisema kila mechi wanazocheza kwao ni muhimu bila kujali wanacheza wapi kwa kuwa kikubwa ni pointi tatu.
“Mkulima mzuri yeye hachagui jembe kikubwa ambacho anaangalia ni namna gani anaweza kulitumia hivyo iwe ni Uwanja wa Manungu ama uwanja mwingine kwetu hakuna tatizo.
“Ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu na wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu kwani malengo yetu ni kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zetu zote,” alisema Bumbuli.
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Nabi Awabadilishia Mbinu Mtibwa Manungu​

YG.jpg

MECHI ya kisasi! Ndivyo utakavyosema katika kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaozikutanisha Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga utakaopigwa leo saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Timu hizo zitavaana katika mchezo wa kwanza wa ligi, lakini Mtibwa wataingia uwanjani wakitaka kulipa kisasi cha kufungwa katikamchezo wa mwisho msimu uliopita bao 1-0 lililofungwa na kiungo mshambuliaji raia wa Angola, Fernandos Carinhos.
Wakati Mtibwa wakiingia kutaka kulipa kisasi, Yanga wenyewe wanahitaji pointi tatu ili waendelee kukaa kileleni kwa kuwaacha watani wake kwa gepu kubwa la pointi katika msimamo wa ligi.

FMRFPzAXIAEEKS5.jpg

Yanga inaongoza katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 36 ikifuatiwa na watani wao Simba wenye 31 huku
Mtibwa 12 wakiwa katika nafasi ya 14.
Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia Nasreddine Nabi alisema kuwa anafahamu
anakwenda kucheza mchezo mgumu dhidi ya Mtibwa huku akiwa amekiandaa kikosi chake kukabiliana na changamoto zote watakazokutana nazo.
Nabi alisema kuwa moja ya changamoto anayokwenda kukutana nayo ni ubovu wa uwanja, ambao kwake
hataki iwe sababu ya kupoteza mchezo huo muhimu kwao kupata matokeo mazuri.
Alisema kuwa siku tatu alizotumia kukiandaa kikosi chake kambini Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam,
zimetosha vijana wake kupata matokeo mazuri, licha ya changamoto ya uwanja watakayokutana
nayo.
“Nimeki– andaa kikosi changu kutokana na aina ya uwanja nitakaokwenda kuutumia dhidi ya Mtibwa, siufahamu lakini nimepata taarifa za uwanja huo.
“Mimi ninakiandaa kikosi changu katika mazingira yote, kwani uzuri nafahamu changamoto iliyopo hapa nchini ya viwanja,uzuri vijana wangu wanafahamu vizuri hivyo sina hofu, tumejiandaa kwa ajili ya kupata matokeo mazuri, licha ya kukabiliwa na majeraha kikosini kwangu,”alisema Nabi.
Kwa upande wa Kocha Msaidizi wa Mtibwa, Awadh Juma, alisema: “Maandalizi yapo vizuri na wachezaji wana morali kubwa ya kupata matokeo mazuri.
“Tunashukuru namba ya wachezaji waliokuwa wana majeraha imepungua, tunaamini kwetu yatakuwa mazingira rafiki kutokana na kutumia uwanja wa nyumbani.
“Morali ipo juu kwa wachezaji wetu wote, hivi sasa tunawatengeneza kisaikolojia tu kutokana na ukubwa
wa mchezo huu, kwani mazoezi ni yaleyale wanay– ofanya kila siku,” alisema Juma.
 

vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5
𝗙𝗨𝗟𝗟 𝗧𝗜𝗠𝗘⏱

Mtibwa Sugar 0-2 Yanga Sc (Ntibazonkiza 45+ | Mayele 67’ )

Tutaelewana tu msimu huu🤫


Image
 

mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

Huyo Fei Toto kumbe alijitabiria mapemaa​

Fei PIC

UMAARUFU alionao kiungo fundi wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’ haujaja kwa bahati mbaya bali ni jambo alilojitabiria tangu akiwa na umri mdogo mbele ya marafiki wake.
Beki wa Namungo, Abdulaziz Makame ‘Bui’ ni kati ya mashuhuda wa maneno ya Fei aliyosema miaka mingi iliyopita kuwa, atakuja kuwa na jina kubwa ndani na nje.
Bui alisema Fei Toto alikuwa na kipaji tangu akiwa mtoto, kipindi hicho wakicheza mtaani watu wengi walikuwa wanakusanyika kumtazama anavyocheza.
“Kama kuna neno nalikumbuka ambalo Fei aliongea kipindi tukiwa wadogo, ingawa mimi ni mkubwa kidogo kwake, alisema nitakuja kuwa staa mkubwa sana, tukawa tunacheka, tukijua ni maneno ya kitoto.” alisema Makame na kuongeza;
“Kauli yake imetimia jina lake limekuwa kubwa, naamini akiamua kwenda kucheza nje basi atakamilisha ndoto zake ambazo alikuwa anasema atakuwa staa ndani na nje.”
Alibainisha kipaji cha Fei kilikuwa kinavutia tangu akicheza mtaani, kutokana na namna wachezaji wenzake walivyokuwa wanapenda aanzishwe kwenye kila mechi.
Alisema baada ya Fei kusajiliwa Yanga, alifurahia na kuona anakwenda kuishi ndoto zake.
“Nje na soka kitu ambacho Fei alikuwa ananichekesha alikuwa anapenda kulakula sana, ukishika kitu anakwambia kaka naomba, kiukweli tumetoka mbali nikikumbuka huwa nacheka sana.”
 

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mayele Amkosesha Usingizi Beki Simba​

yangasc_272929964_899875410699999_6070729047343910339_n.jpg

BEKI wa kati wa Simba anayekipiga kwa mkopo Mtibwa Sugar, Ibrahim Ame, amesema mshambuliaji wa Yanga, Mkongomani, Fiston Mayele ameshindikana huku akisisitiza amemkosesha usingizi.
Kauli ya beki huyo imekuja baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kumalizika kwa Yanga kuwafunga Mtibwa mabao 2-0 juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Ame alisajiliwa na Simba msimu uliopita akitokea Coastal Union ya Tanga ambaye msimu huu alitolewa kwa mkopo Mtibwa pamoja na Said Ndemla na Jeremiah Kisubi.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Ame alisema kuwa kabla ya mchezo huo, alipewa jukumu la kumkaba Mayele kwa lengo la kutofunga, lakini imeshindikana baada ya kumruhusu mshambuliaji huyo kufunga bao. Ame alisema kuwa bao hilo alilofunga Mayele, limemfanya akose furaha na amani huku akishindwa kupata usingizi.
Ame ambaye alishindwa kuendelea na mchezo baada ya bao hilo kutokana na maumivu, alionekana akiwa chini nje ya uwanja akisononeka. “Mayele ni mshambuliaji hatari na wa kuchungwa akiwa uwanjani kutokana na kiwango chake bora.
“Nakumbuka kabla ya mchezo wetu huo, nilipewa jukumu la kutembea na Mayele kila sehemu kwa lengo la kutofunga, lakini ikashindikana na kupata upenyo akafunga.
“Kiukweli nilifanya jitihada nyingi za kutosha za kuhakikisha Mayele hafungi lakini nimeshindwa, alitumia nafasi moja aliyoipata kufunga, kiukweli siku yangu imeharibika baada ya bao hilo, sitaweza kupata usingizi,” alisema Ame.