Yanga Thread

Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Senzo: Yanga chini ya Rais inakuja​

senzo pic

Senzo Mazingisa, mtendaji mkuu wa Yanga anasema kwa ukubwa wa timu kama Yanga hauwezi ukaanza msimu wakiwa hawana malengo ya kumaliza nayo wakina na taji lolote.

Katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti, Senzo anasema baada ya kupoteza Kombe la Mapinduzi wamejiwekea lengo kuchukua Ligi Kuu Bara na lile la Shirikisho la Azam huku wakiweka mkazo katika kila mechi.

“Mapinduzi ilishapita na sasa tunaendelea kusonga mbele zaidi. Tunafanya kazi kubwa sio tu kwa wachezaji, bali kila mtu katika timu hii na lengo likiwa ni kuchukua mataji,” anasema.

Akizungumzia usajili anasema waliufanya kwa umakini wakihakikisha wachezaji wanaisaidia Yanga kutimiza malengo iliyonayo.

ISHU YA MABADILIKO

Senzo anasema wapo kwenye hatua nzuri kuhusu mabadiliko ya uendeshaji wa klabu baada ya kuruhusiwa na mamlaka husika juu ya katiba mpya.
“Yanga haipo tu kwa BMT bali ipo pia kwa TFF na baada ya katiba yetu kukamilika tuliipeleka kwao na wao wametupa sisi miezi sita na wametuambia kila kitu kilichopo kwenye katiba kikamilike ndani ya miezi hiyo.” Senzo anasema jambo la kubwa ni mashabiki wa timu hiyo kubadilika na kuwa wanachama na hawana muda wa kupoteza kwani tayari mchakato huo unaendelea vizuri.
“Tumeanza kusajili wanachama wetu na namba zinaenda vizuri. Mpaka sasa tunaona mabadiliko yanaenda vizuri na kutakuwa na mabadiliko ya kimuundo kwenye uongozi wa Yanga na lengo likiwa ni kupata muundo wa timu,” anasema.

THAMANI YA KLABU

Senzo anasema baada ya kukamilika kwa usajili wa wanachama watageukia upande wa thamani halisi ya klabu ili wawekezaji wapate picha kamili ya Yanga kabla ya kuweka pesa zao.

“Tutaweka thamani halisi ya Yanga na tutaita watu ambao watakuja kutusaidia kwenye kuweka sawa. Katika mchakato huu moja kwa moja kutakuwa na mabadiliko makubwa kwenye upande wa uongozi.”

Senzo anasema hakutakuwa na mwenyekiti wala makamu tena, badala yake kutakuwa na rais wa timu na hakutakuwa na cheo hicho bila kuwapo kwa uchaguzi huru ndani ya klabu.

“Kupitia matawi tutakuwa na viongozi wa matawi ambao watatoka kwa ajili ya kwenda kwenye uchaguzi huu na hili linatakiwa lifanyike ndani ya miezi sita kuanzia sasa. Jambo la kushukuru ni mabadiliko yanaendelea vizuri na lengo kuifanya timu kuwa kwenye levo nyingine,” anasema Senzo.

“Hauwezi kuwa mwanachama wa timu kama haupo kwenye tawi. Ukiwa nje ya nchi unatakiwa kuhakikisha unajisajili kwenye tawi na ukiwa huko utapokea meseji ambayo inakupa taarifa na hii imetokana na kuwekeza kwenye upande wa dijitali.”

Mtendaji huyo anafunguka zaidi na kusema mambo yote ya mabadiliko yatazidi kwenda vizuri kupitia matokeo ya uwanjani yakiwa mazuri kwa sababu vitu hivyo vinakwenda pamoja.

MFIKIRWA AWEKA SAWA

Mkurugenzi wa Fedha na Utawala Yanga, Haji Mfikirwa ambaye aliyeambatana na Senzo katika mahojiano haya anasema muundo wa kidijitali kwa wanachama ni mzuri kwa sababu unasaidia kujua wana wanachama wangapi tofauti na ilivyo sasa.

“Hata huko nyuma klabu ilikuwa na wanachama lakini mfumo huu unakuja kuipa faida kwa kujua tuna wanachama kiasi gani wakati wowote. Kwenye mabadiliko yetu kuna kipengele cha uhusiano mzuri na wanachama,” anasema Mfikirwa.

“Kipindi cha nyuma tukiwa na La Liga (Ligi Kuu ya Hispania) na klabu ya Sevila tuliulizwa tuna wanachama kiasi gani, lakini hatukuwa na jibu kamili. Kila mtu alikuwa na jibu lake, sasa kitendo tunachofanya ni kuwa na kumbukumbu ya wanachama ambao wataweka kila kitu chao kwenye fomu.”

Mfikirwa anasema faida ambayo wanachama wataipata ni kununua bidhaa zao moja kwa moja kutoka Yanga kwa sababu rekodi zao zitakuwapo.

“Matawi zaidi ya 500 yamejisajili mpaka sasa na kwenye kila tawi kunatakiwa kuwe na wanachama 100 na kwa upande wa juu ni wanachama 500. Mwitikio ni mkubwa na tunafanya hili kwa nguvu kubwa na mwisho wa siku tuje kupata viongozi,” anasema.

“Katiba inasema sio wanachama wote wanakuja kwenye uchaguzi, lakini kupitia matawi wao ndio watachagua watu wa kwenda katika uchaguzi mkubwa na mwezi wa saba tunatakiwa tuwe na viongozi wapya kwa mujibu wa katiba.”

BILA ADA INAKULA KWAKO

Zamani ilikuwa ni kawaida kwa mwanachama wa Yanga kutolipia kadi yake mpaka muda wa uchaguzi mkuu ndio wengi hulipa, lakini kupitia mabadiliko suala hilo limeondolewa.

Mfikirwa anasema katiba mpya inasema mwanachama hai ni yule ambaye analipia kadi na kupitia matawi ndio itasaidia kujua uhai wa wanachama.

“Haya matawi tunataka yawe hai muda wote. Tunataka kuona uhai wa mwanachama na usipolipa ada kwa muda wa miezi sita sifa yako inaondoka. Fomu ya mwanachama kujaza gharama yake ni Sh2,000 na pesa hiyo inabaki katika tawi ili kusaidia hapohapo,” anasema Mfikirwa. ”Wanachama ambao wapo kwenye matawi watakuwa na bei punguzo ya kununua vitu halisi kutoka Yanga kwa sababu watakuwa wanapata moja kwa moja kutoka kwenye klabu. Hii itakuwa rahisi kupitia matawi kwa sababu tutakuwa tunawasiliana.”

Upande wake Senzo anasema kitendo cha kuweka rekodi ya wanachama ni sehemu ya Yanga kupata pesa kwa sababu hata wakienda kwa wafadhili wakitaja wingi wa wanachama watawapata wengi na thamani halisi ya klabu itajulikana.

“Kama Haji alivyosema wanachama watakuwa hawapati tena jezi feki kwa sababu watakuwa wanaweka oda ya mapema kwenye jezi moja kwa moja Yanga na hii itasaidia kupata pesa,” anasema.

CHANGAMOTO

Mfikirwa anasema changamoto ambayo timu nyingi za Tanzania zinakutana nazo ni kutomiliki viwanja na hiyo inawanyima uhuru wa kufanya mambo mengi kwani duniani kwenda uwanjani ni kama vile unatoka ‘out’ na familia yako.

“Kama vile ambavyo tunafanya Siku ya Wananchi ilitakiwa iwe kila siku kwenye mechi watu waje na familia zao kufurahia timu yao, lakini haijatukatisha tamaa tuna imani kubwa kupitia hii kujua wanachama wetu tutafanikiwa,” anasema.

Anasema wana mawazo mengi mazuri na kwa kuanzia kwenye kusajili wanachama kutafungua mipango mingi mizuri ambayo mwanzoni ilishindwa kutimia.

“Miradi inakuwa ngumu kufanyika mara nyingi ukiwa hauna namba ya wanachama, lakini kwa sasa tuna imani kubwa tutafanikiwa kwa sababu tuna watu ambao wana mapenzi makubwa na klabu yao.”

KAUNDA NA KIGAMBONI

Yanga ilianzisha miradi ya ujenzi viwanja viwili eneo la Kaunda na Kigamboni, lakini imeonekana kutokuwa na mwendelezo kama ambavyo ilitambulishwa awali.

senzo pic 1

Mfikirwa anasema miradi hiyo ilikuwa ngumu kufanyika kutokana na kutokuwa na kumbukumbu halisi ya wanachama wake kiasi cha kuwafanya washindwe kupata pesa za mikopo.

“Bila fedha utabaki kuwa na ndoto huku hujui lini utaikamilisha. Tuna miradi mingi na yote inahitaji fedha. Huwezi kwenda kwenye benki halafu ukasema una mashabiki ukiwa unataka mkopo hivyo ni ngumu kufanyika. Tulijaribu kwa siku nyuma kutembeza bakuli, lakini hatukufanikiwa kwa kiwango kikubwa na ndio maana tumekuja na mfumo mpya,” anasema Mfikirwa.

“Tunaona mwanga mzuri mbele tunapoenda na imani yetu tutakuwa miongoni mwa timu kubwa barani Afrika.”

ZAHERA ATAJWA

Uongozi wa Yanga umemrejesha aliyekuwa kocha wao, Mwinyi Zahera, lakini alirejea kama mkurugenzi wa ufundi na maendeleo ya soka la vijana katika timu hiyo.

Senzo anasema lengo kubwa la uwepo wa Zahera ni kuwa na muundo mzuri wa ukuaji wa wachezaji kuanzia katika upande wa soka la vijana kwenye ngazi za chini za miaka 15, 17 na 20.

“Lazima uwe na mipango ya ukuaji wa vijana kwenye timu. Kwenye miaka minne nyuma hatukuwa bora katika hilo na ndio maana tumeweka nguvu huko na kupitia wafadhili wetu wametusaidia katika hilo,” anasema.

Senzo anasema nguvu nyingine ipo kwenye upande wa timu ya wakubwa kuhakikisha inafanya vizuri kisha ndipo wanageukia katika upande mwingine.

“Hatujaisahau timu ya wanawake lakini lazima uwe na mpangilio kwenye uendeshaji. Ndio maana tumeanzia huku na kila kitu kikisimama tutageukia huko na hautakiwi kumaliza tatizo kwa malengo mafupi bali kutumia malengo marefu,” anasema Senzo.

Hata hivyo, Mfikirwa anakazia akisema: “Kuna muda tulikuwa na wachezaji lakini baada ya miaka miwili wanaondoka na ndio maana tumekuja na mpango mwingine. Hauwezi kuwa na timu kila siku mpya ni ngumu mno kuendeleza utamaduni wetu na ndio maana kwenye usajili wapo wachezaji wa kucheza sasa na wengine kwa ajili ya miaka ijayo ili wazoee tamaduni zetu na ndio maana tunataka kutoka kwenye usajili wa muda mfupi.”
 
SUBIRA KWA MASHABIKI

Mfikirwa anasema mambo mazuri hayataki haraka, hivyo mashabiki wawe na subira wakati viongozi wanapambana kuitengeneza timu iwe na muundo mzuri na kupata matokeo bora.

“Waswahili wanasema ukiona vinaelea ujue vimeundwa na kwenye miradi hii kuna siku tutashuka na siku tutapanda kama barabara ndefu itakuwa na kona na milima,” anasema.

“(Wanachama) waendelee kuisapoti timu na viongozi. Tumekaa muda mrefu bila mataji lakini tukiwa pamoja na kila mtu akitimiza wajibu wake tutafikia malengo yetu.”

Senzo anatia msisitizo akisema, “kitu kikubwa ni kupata ushindi na pointi tatu. Nawaomba mashabiki waisapoti timu kwa kuja viwanjani na kuwapa nguvu wachezaji, unajua hata wachezaji wataona wanasapotiwa vizuri. Wakati huohuo waendelee kujisajili.”
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mayele Limemkuta Jambo Yanga.​

yangasc_272929964_899875410699999_6070729047343910339_n.jpg

BAADA ya kuona mabeki wa timu pinzani wakimkamia kila wanapokuwa uwanjani, Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, amemtaka straika wake, Fiston Mayele kuhakikisha hakai na mpira mguuni kwa muda mrefu ili kujiepusha na kupata majeraha yatakayoigharimu timu.
Mayele ndiye straika tegemeo kwenye kikosi cha Yanga akiwa kinara wa mabao akifunga sita ndani ya Ligi Kuu Bara, huku wikiendi iliyopita akifunga bao pekee kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbao FC na kufuzu 16 bora ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.
Kocha Nabi ambaye aliungana na Yanga Machi 2021, msimu huu amepania kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara ambapo hadi sasa ameiongoza timu hiyo kukaa kileleni mwa msimamo kwa kukusanya pointi 35 kwenye mechi 13 akishinda 11, sare mbili, hajapoteza.
Chanzo kutoka Yanga, kimeliambia Spoti Xtra kwamba, kufuatia mwenendo mzuri wa Mayele katika safu ya ushambuliaji, Nabi amemtaka kuwa makini na wapinzani ambao akifanya mzaha, watamuumiza na kuigharimu timu.
“Kocha amemtaka Mayele kuwa makini zaidi awapo uwanjani ili kuepuka kupata majeraha ambayo yataigharimu
timu.
“Ukiangalia hivi sasa wapinzani wanawakamia sana wachezaji wetu, hivyo amemtaka kutokaa sana na mpira mguuni
na badala yake awe anaachia haraka akipewa pasi au afunge akiona kuna nafasi ya kufanya hivyo.
“Mbinu hiyo itamfanya hata yule mwenye nia ya kutaka kumuumiza kushindwa kufanikisha jambo lake,” kilisema chanzo hicho.
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mastaa Yanga Wazuiwa Kula Burger, Pizza.​

yangasc_272956522_621035745676948_9039599249652413405_n.jpg

KATIKA kuhakikisha wachezaji wake wanaepukana na majeraha ya mara kwa mara, Daktari wa Viungo waYanga,
MtunisiaYoussefAmmar amewapiga stop mastaa wa timu hiyo kutumia vyakula aina ya Burger na Pizza.
Hiyo ni katika kuhakikisha wanapunguza ongezeko la wachezaji wenye majeraha katika kikosi chao hicho ambacho kimepiga kambi hukoAvic Town, Kigamboni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Daktari huyo hivi sasa anawapambania nyota wake watatu warejee uwanjani ambao aliwapeleka nchini Tunisia kwa ajili yakufanyiwa upasuaji hivi karibuni kutokana na kuwa matatizo ya goti.
Wachezaji hao waliofanyiwa upasuaji ni Kibwana Shomari, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Mburkinabe,Yacouba
Songne.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ammar alisema kuwa vyakula vya aina hiyo ya Burger na Pizza chanzo cha
wachezaji kupata majeraha yasiyotegemewa katika timu.
Ammar alisema kuwa tayari amewataarifu wachezaji kula vyakula vinavyohitajika ikiwemo ‘sea food’ili kuzuia majeraha yanayoepukika katika timu.
“Hili la ubovu wa viwanja lipo wazi kabisa, ndiyo chanzo cha wachezaji kupata majeraha kama vile magoti na enka ambalo kuepukika ni ngumu kutokana na miundombinu ya viwanja vya hapa nchini.
“Lakini lipo hili la vyakula, linaweza kuepukika kabisa kwa wachezaji kufahamu madhara watakayopata kutokana na vyakula ambavyo wanavyotakiwa kula katika maisha yao binafsi ya nyumbani tofauti na kambini ambako ni ngumu
kupikwa.
“Hivyo wachezaji hawatakiwi kula vyakula vya aina ya Burger na Pizza kwa faida yao na timu, kwani wanapokosekana katika mechi kutokana na tatizo la majeraha wanaidhohofisha timu,” alisemaAmmar
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Wauza Jezi Feki za Yanga Wanaswa Dar.​

jeszi-fekii.jpg

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limewakamata watu 17 kwa tuhuma za kuuza jezi bandia za timu ya Yanga Afrika 1,208 zinazotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya GSM.
Kazi hiyo ilifanyika katika maeneo mbali mbali ya Jiji Dar es salaam, lakini pia kwa kushirikiana na baadhi ya mikoa nchini kwa kipindi cha kuanzia tarehe Januari 2 hadi Januari 28, 2022.
Kamanda wa Polisi Kanda Malalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema katika Jiji la Dar es salaam Jeshi la Polisi limewakamata watuhumiwa watano, akiwemo Zahiri Hassan (17) aliyekutwa Uwanja Benjamin William Mkapa akiwa na Jezi bandia za timu ya Yanga seti 52.
Wengine ni Majiba Ndahya (50) ambaye alikamatwa maeneo ya Kariakoo mtaa wa Agrey akiwa na Jezi seti 124, Mohamed Ramadhani alikutwa na Jezi seti 86, John Staslaus alikamatwa na Jezi seti 39 na Emmanuel Kinasa alikutwa na Jezi seti 60.
“Watuhumiwa hao waliwataja wenzao wa Zanzibar, ambapo Uwanja wa Amani watuhumiwa watatu walikutwa na Jezi bandia seti 36, Jezi zingine bandia 134 zilipatikana kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa Tanga na Mwanza ambapo watuhumiwa tisa walikutwa na Jezi seti 811.
Aidha Kamanda Muliro amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawatahadharisha wananchi wote wanaojihusisha na vitendo vya kutengeneza, kuuza na kusambaza, bidhaa kwa kuiga au kufananisha nembo za biashara au huduma za watu wengine iliyosajiliwa kisheria, kufanya hivyo ni kosa na kinyume na sheria za nchi.
“Jeshi la Polisi litashirikiana na mamlaka nyingine za kisheria ili kuona watuhumiwa wamechukuliwa hatua kali za kisheria,” amesema Kamanda Muliro.
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mwamnyeto, Job Wapo Sana Yanga.​

bakarmwamnyeto_03_272915894_667288207761776_6865980531395398495_n.jpg

UONGOZI wa Yanga, umezima tetesi za kuondokewa na baadhi ya wachezaji wake ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu kwa kusema hao wanaowahitaji wanajisumbua na badala yake mastaa hao wataendelea kukipiga Jangwani.
Baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu ni nahodha Bakari Mwamnyeto anayetajwa kuwaniwa na Simba.
Wengine ni Dickson Job, Kibwana Shomari, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’, Yacouba Songne, Deus Kaseke na Abdallah
Shaibu ‘Ninja’ ambaye hivi karibuni alipelekwa nchini Tunisia kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa goti.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, kutoka kwa mmoja wa mabosi wenye ushawishi ndani ya timu hiyo, alisema wachezaji hao wameshamaliza mazungumzo ya awali kwa ajili ya kuongeza mikataba kuendelea kukipiga Yanga.
Bosi huyo alisema kabla ya kuanza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, baadhi ya wachezaji hao watakuwa wamesaini mkataba baada ya kukamilishiwa mahitaji yao muhimu ikiwemo mshahara.
Aliongeza kuwa, ni ngumu kwa uongozi wa timu hiyo kukubali kuwaachia kirahisi wachezaji hao akiwemo
Mwamnyeto, Job, Kibwana na Saido ambao wapo kikosi cha kwanza.
“Mashabiki waondoe hofu juu ya wachezaji wetu hao kwenda Simba, kati ya hao wanaotajwa wote wameonesha nia na kukubali kuendelea kubaki Yanga.
“Hivyo Mwamnyeto hatakwenda popote, waacheni waendelee kujidanganya hao wanaotangaza kutaka kumsajili,” alisema bosi huyo.
Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said, aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa: “Hizo zinazoendelea ni tetesi tu, achana nazo hakuna mchezaji yeyote tunayemuhitaji tutakayekubali kumuachia akiwemo Shomari na Mwamnyeto.”
Naye Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela, alisema: “Hao wanaotangaza kumsajili Mwamnyeto wameshakata tamaa ya ubingwa wa ligi, hivi sasa wamehamia katika propaganda. Hakuna mchezaji tunayemuhitaji tukamuachia akaondoka.”
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mayele: Huu mwaka wa Yanga.​

mayele pic

‘HUU ni mwaka wa Yanga’ hiyo ni kauli ya straika wa timu hiyo Fiston Mayele, akiwaambia mashabiki wa timu hiyo, licha ya kukutana na changamoto ya baadhi ya viwanja vya mkoani, hawataacha kitu.
Akizungumza na Mwanaspoti, Mayele alisema kuna wakati wakicheza mikoani, wanakumbana na changamoto ya kushindwa kucheza kwa ushindani wa mbinu kutokana na viwanja, lakini wanachokiangalia ni kupata matokeo ya kuendelea kuwaweka kileleni.
“Huu ni mwaka wa Yanga, hatutaacha kitu iwe mechi za mkoani ama za Dar es Salaam, nimeona changamoto ya viwanja kwa baadhi ya mikoa ambayo tumecheza, ila jambo la msingi kwetu ni pointi tatu,” alisema na akaongeza;
“Niwe mkweli nikicheza Uwanja wa Mkapa, najisikia vizuri zaidi, kwani ni mzuri unaomfanya mchezaji acheze kwa uhuru bila kuhofia kupata majeraha na ufundi na mbinu vinakuwa vinatawala,” alisema.
Hadi sasa Mayele ndiye anaongoza kwa mabao sita na asisti mbili ndani ya kikosi cha Yanga.
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

UBISHI WA MZEE WA KALIUA: Saido anataka kuwaibia Yanga kama 'Auba' kwa Arsenal.​

saido pic 1

NILIACHA kila kitu na kutega sikio langu kwa makini ili nilisikie tena jibu la kocha wa Arsenal, Mikel Arteta. Mwanzoni nilidhani Arteta anatania lakini haikuwa hivyo.
Aliendelea kusisitiza kwamba yeye na Arsenal hawana mpango wa kuendelea kuishi na mshambuliaji raia wa (Gabon), Pierre Emerick Aubamayeng. Kisa? Kwanza ni utovu wa nidhamu. Pili ni kuporomoka kiwango kwa kiasi kikubwa.
Hii sababu ya pili inaweza kumtokea mchezaji yeyote. Kinachowakera zaidi Arsenal ni kwamba Aubamayeng mwenyewe hakuonyesha kujali wala kukerwa na kiwango chake kibovu. Ndiyo sababu walitaka aondoke.
Wanachosahau Arsenal ni kwamba haya maisha walimtengenezea Aubamayeng wenyewe. Mwaka mmoja na nusu uliopita Auba alikuwa katika kiwango bora cha maisha yake na mkataba wake ulikuwa unaelekea ukingoni.
Arsenal walijitutumua kumlazimisha asaini na kweli mwisho wa siku Auba alisaini mkataba mnono zaidi kuwahi kuusaini maishani mwake. Alisaini mkataba wa miaka mitatu unaompatia Pauni 350,000 kila mwisho wa wiki.
Baada ya hapo Auba hajawahi kukamata makali yake tena. Ule uwezo wake uliowahangaisha Arsenal kuharakisha kumpatia mkataba mpya uliondoka na wino aliomwaga kutia saini katika karatasi ya mwisho mkataba wake.
Nini kilitokea ghafla? Ukweli ni kwamba baada ya kupata kandarasi mpya Auba hakuwa na kitu kingine anachohitaji zaidi.
Kabla ya mkataba alijitoa kila alivyoweza ili kuwalazimisha Arsenal kumpatia mkataba wa muda mrefu. Alijua utaisha akiwa amekusanya pesa za kutosha kisha atatokomea zake huko China au Marekani kwenda kumalizia maisha yake ya soka.
Kwa lugha rahisi tunaweza kusema Arsenal walikosea kumpa Aubamayeng mkataba wa miaka mitatu akiwa na umri wa miaka 31. Licha ya hivyo bado hatuwezi kuwalaumu Arsenal. Walichofanya ni kutazama kile Auba alichokuwa anakifanya kwa wakati ule kisha wakampatia walichoona anastahili kupatiwa. Isingekuwa rahisi kutabiri kwamba Auba ataporomoka kiwango kwa kasi kutokana na ubora aliokuwa nao wakati ule.
Ni kama ambavyo ni ngumu kwa sasa kutabiri kwamba, kiungo wa Yanga, Saido Ntibazokinza anaweza kuporomoka kiwango mwaka ujao kutokana na ubora anaouonyesha kwa sasa.
Msimu ulianza vibaya kwa Saido Ntibazonkiza. Hakuwa na furaha ndani ya Yanga kwa sababu hakuwa sehemu ya kikosi cha kwanza. Mara nyingi aliachwa jukwaani au aliwekwa benchi kwa sababu ya ufinyu wa nafasi.

saido pic

Aliumia Yacouba Sogne na ghafla Saido alipata nafasi. Tangu alipopata nafasi Saido hajawahi kufikiria kurudi nyuma. Amekuwa akiongezeka ubora siku baada ya siku na sasa ni mmoja wa wachezaji tegemeo ndani ya Yanga.
Mwisho wa msimu uliopita Yanga waliweka jina lake kwenye ‘red list’ kwamba lazima aondoke. Lakini ghafla idadi ya wachezaji wa kigeni iliongezeka kisha akaondoka Tuisila Kisinda na kujikuta nafasi ya Saido inapatikana. Yanga wakakubaliana wamvumilie kwa msimu mmoja mwingine. Ni msimu huu ambao mkataba wake unakatika ndani ya miezi sita ijayo.
Yanga hawakuwahi kufikiria kama siku moja watamshuhudia Saido katika ubora huu alionao sasa. Saido amepata nafasi na amerudisha swali kwao. Amewaweka katika kizungumkuti.
Je wampe mkataba mpya kutokana na wanachokiona sasa? Lakini vipi kama Saido anawaibia? Vipi kama anawaonyesha ubora huu ili wampe mkataba mpya kisha arudi kule alipokuwa? Ni maswali magumu ambayo Yanga hawajui wanayajibu vipi.
Iliwahi kutokea kwa Haruna Niyonzima pale Simba. Alitumia miaka miwili kukaa benchi au jukwaani baada ya Simba kutumia nguvu kubwa kumng’oa Yanga. Ilipofika miezi ya mwisho ya mkataba wake akawasha moto kuwaaminisha Simba kuwa amezaliwa upya.
Simba wakaanza kutafutana lakini baadaye walikuwa wajanja wakamuacha aondoke. Waligundua Niyonzima alikuwa anawadanganya. Ni kitu kama hiki kitawasumbua Yanga kwa Saido.
Lakini pia unampongeza Saido kwa kuwa mjanja katika kuiuza saini yake. Nyakati ambazo mkataba unaelekea mwisho mchezaji inabidi uzishtue klabu zingine zikutolee macho. Ni kama ambavyo Antonio Rudiger anafanya kwa sasa pale Chelsea kule England.
Kama leo Yanga wataamua kuachana na Saido hawezi kukosa klabu nne au tano ndani ya Ligi Kuu Bara zitakazopigana vikumbo kuipata saini yake.
Ni lazima atavuna pesa zingine nyingi kutokana na usajili wake. Ni akili kama hizi za kina Saido Ntibazonkiza inabidi wachezaji wetu waziige. Mchezaji unamalizaje mkataba na klabu kubwa nchini halafu klabu ndogo hazipiganii saini yako?
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Chico Aandaliwa kwa Kazi Maalum Yanga.​

chico-ushindi-yanga.jpg

PAMOJA na mashabiki wa Yanga kuendelea kuwa na shauku ya kutaka kumuona winga wao mpya raia wa DR Congo, Chico Ushindi akifanya mambo yale aliyokuwa akiyaonesha enzi hizo akiwa na TP Mazembe, unaambiwa kocha wa timu hiyo, Nasreddine Nabi, kumbe anamuandaa kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Winga huyo amejiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo uliofungwa Januari 15, mwaka huu akitokea TP Mazembe.
Chanzo chetu kutoka katika kambi ya Yanga iliyopo Avic Town, Kigamboni, Dar, kimeliambia Spoti Xtra kuwa, malengo ya Nabi ni kumtumia zaidi Chiko katika mzunguko wa pili wa ligi, hivyo kwa sasa anajitahidi kuhakikisha anampa nafasi ya kuzoea mazingira ili aje kuongeza nguvu katika mbio za kuwania ubingwa.
“Ukiambiwa usajili wa kocha wetu Nabi siyo wa kukurupuka basi huna haja ya kubishana na hilo, kwani hadi sasa anadhihirisha kwa Chico Ushindi ambaye amemsajili hivi karibuni kutoka TP Mazembe, kwani amesema hana haraka ya kumpa presha badala yake ataendelea kumuingiza katika mfumo wake taratibu mpaka pale atakapozoea.
“Malengo yake siyo kumuona Ushindi akicheza tu, ila anahitaji kumpa muda mzuri wa kurejea katika ubora wake kwani alikotoka alikuwa hapati nafasi mara kwa mara, hivyo anamuandaa kwa ajili ya mzunguko ujao ambapo wachezaji wengi huwa wanakumbwa na majeraha,” kilisema chanzo hicho.
Hivi karibuni, Nabi alimzungumzia kiungo huyo akisema: “Ninaamini uwezo wa Ushindi uwanjani, hivyo hilo sina hofu nalo kabisa, usajili wake mimi ndiyo nilioupendekeza, ni suala la muda tu kuonesha ubora wake.”
Yanga imebakiwa na mechi mbili kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara ambapo inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 35.
 
mhariri

Mpiga Chabo
Dec 17, 2021
203
0
0

MCHUNGAHELA MWENYEKITI MPYA KAMATI YA UCHAGUZI YANGA.​

AVvXsEgSVquRrx9PoxyNy3y_U6m2PYiM_t8IMxsP6kYhuR8Acne92he5V6Ica1F8I9NSHgi9bicdHDjz0tyH2_QJR32_N20_7ysi31xWVjM3Y2693ORGFxNt5c9xu36EdLpCgp00LDmAeF5S73BPt5g4jFtr3AeJoGNzM9h9aqdlAfgdoKtQDdntWTag9aHX=w640-h366

UONGOZI wa Yanga umemeteua Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Malangwe Ally Mchungahela kuwa Mwenyekiti wake mpya wa Kamati ya Uchaguzi.
AVvXsEhZxK1EEbvz6gfyQnh_5wGBGPNz0y7fOINUD9pDm37JZOlAsGyY-6uBItdxDgEjfKrX43loH9BydzBdawBxzS1dhzV-SCIhvqwoSjMoFfh44CYZAOwUqn2msot_b2wqrB_aTBgbSpPUpJtZf3-mUN3t46GX_9hEr2U_bUtPSdtqLvhVx9XrgdiUwPop=w640-h640
 
vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Tuisila Kisinda Atuma Salamu Yanga.​

269734588_447189670231791_895064827705611607_n.jpg

ALIYEKUWA winga wa Yanga, Tuisila Kisinda, amefunguka kufurahishwa na klabu yake ya zamani kuongoza ligi kwa alama nyingi dhidi ya Simba huku akiweka wazi kuwa matamanio yake ni kuiona Yanga ikitwaa ubingwa msimu huu.
Kisinda ambaye amedumu kwa msimu mmoja pekee ndani ya Yanga, kwa sasa anakipiga katika Klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco inayonolewa na kocha Florent Ibenge.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Kisinda alisema kuwa anajisikia furaha kuona timu yake ya awali ikiwa inafanya vizuri katika msimamo wa ligi kuu huku akiweka wazi kuwa anatamani kuona timu hiyo ikitwaa ubingwa msimu huu mara baada ya msimu uliopita kuukosa.
“Nafurahi kuiona Yanga ikiwa inaongoza mbele ya Simba tena kwa pointi nyingi, msimu uliopita ubingwa haukuwa kwa Yanga lakini kwa hiki ambacho kinaendelea kwa sasa ni dalili nzuri za ubingwa.
“Mimi napenda kuiona Yanga ikifanikiwa mara baada ya kushindwa kutwaa kwa muda mrefu ubingwa wa ligi kuu, hivyo nitafurahi kama ndoto hizo zitakamilika kwa Wanayanga kufurahia ubingwa wao,” alisema mshambuliaji huyo.
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Vigogo Afrika Wagombea Saini ya Fei Toto.​

FEI-TOTO.jpg

KUFUATIA kuwepo kwa taarifa ya klabu kubwa za Afrika kuwa kwenye mchakato wa kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto’, uongozi wa klabu hiyo umeweka wazi kuwa upo tayari kumwachia nyota huyo kama watapokea ofa nono.
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa mpaka sasa baadhi ya klabu kubwa kama Orlando Pirates, Al Masry na TP Mazembe zimeonyesha nia ya kuwasilisha ofa ya kumsajili kiungo huyo mara tu baada ya dirisha kubwa la usajili kufunguliwa.
Kuendana na mtandao wa Transfer Market ambao unajihusisha na tathmini ya thamani za wachezaji, Fei Toto kwa sasa ana thamani ya zaidi ya euro 75,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 195 za Kitanzania.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Mwenyekiti wa Kamati ya ufundi ya Yanga, Dominic Albinus alisema: “Tumekuwa tukisikia kuhusu taarifa za mchezaji wetu Feisal Salum kutakiwa na baadhi ya timu za nje, lakini nikuweke wazi kuwa mpaka sasa hakuna ofa yoyote rasmi ambayo imefika mezani kwa ajili yake.
“Lakini msimamo wetu juu ya suala hilo na uhamisho wa wachezaji kiujumla ni kwamba tuko tayari kumruhusu mchezaji yeyote ikiwa tu makubaliano yatafikiwa.
“Kuhusu thamani yake hilo linatokana na urefu wa mkataba wake, ambapo kwa Feisal bado ana mkataba zaidi ya miaka mitatu hivyo kwa kuongeza na kiwango chake uwanjani lazima klabu ipate ofa ya maana ili kumuachia.”
 
vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Nkane Abakiza Siku 14 tu Kukiwasha Yanga.​

1.jpeg

HABARI nzuri kwa Wanayanga ni kuwa baada ya siku 14 tu watapata kuona maufundi ya kiungo wao mshambuliaji, Denis Nkane ambaye alikuwa nje kwa sababu ya majeraha.
Kiungo huyo kwa muda hakuwa dimbani baada ya kupata majeraha ya kinena kwenye Kombe la Mapinduzi lililofanyika Januari, mwaka huu visiwani Zanzibar.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Dokta wa Yanga, Youssef Mohammed alisema kiungo huyo amebakiza wiki mbili pekee kabla ya kurudi dimbani huku kukiwa na wachezaji wengine nao wakianza mazoezi.
“Kuna baadhi ya wachezaji kama Feisal ambao walikuwa majeruhi tayari wameanza mazoezi lakini kwa upande wa Nkane (Denis) bado ni majeruhi.
“Nkane alikuwa na jeraha la kinena ambalo lilipaswa kumuweka nje kwa muda wa mwezi lakini mpaka sasa amebakiwa na wiki mbili kwa ajili ya kurejea uwanjani.”
 
vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Nabi Amchomoa Kaseke Yanga.​

KASEKE-2.jpg

BAADHI ya mastaa wa Yanga ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu huu ni pamoja na Deus Kaseke ambapo inatajwa kuwa uongozi wa klabu hiyo hauna mpango wa kumuongezea mkataba kutokana
na kushindwa kuonesha makali yake chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Kaseke ambaye alikuwa na kiwango kizuri msimu uliopita wa 2020/21, msimu huu mambo yamekuwa magumu kwake ambapo ameshindwa kumshawishi kocha Nabi kumuanzisha kwenye kikosi chake.
Chanzo kutoka ndani ya Yanga, kimeliambia Spoti Xtra kuwa:
“Kuna baadhi ya wachezaji wa Yanga mikataba yao inaelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu wakiwemo Saidi
Ntibazonkiza ‘Saido’ na Deus Kaseke.
“Saido uongozi upo tayari kumuongezea mkataba kutokana na kiwango chake kuwa bora, pia kocha Nabi (Nassredine) amesema bado anamuhitaji kwenye kikosi chake.
“Jambo zito lipo kwa Kaseke ambaye msimu uliopita aliongezewa mkataba wa mwaka lakini ameshindwa
kuonesha kiwango bora kiasi cha kuwashawishi viongozi na benchi la ufundi.
“Viongozi kwa sasa wamesema hawana mpango wa kumuongezea mkataba wa kuendelea kubaki kwenye timu
lakini pia kuna uwezekano wa timu kuachana na Paul Godfrey ambaye kwenye dirisha dogo alikuwa kwenye orodha ya kuachwa.”
 
vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Beki Avuruga Mipango Yanga.​

270016648_289349469685915_8676774062818196805_n.jpg

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ameweka wazi kuwa, kukosekana kwa baadhi ya wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza akiwemo beki Mkongomani, Djuma Shabani, ni miongoni mwa vitu vinavyowapa changamoto kubwa ya kutimiza malengo yao.
Djuma anaendelea kukosekana kwenye michezo ya Yanga kutokana na kutumikia adhabu ya kufungiwa michezo mitatu baada ya kufanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania. Mpaka sasa amekosa mechi mbili.
Yanga ambao wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zao 35 walizokusanya kwenye michezo 13, jana
Jumamosi walishuka uwanjani kuvaana na Mbeya City katika mwendelezo wa ligi hiyo.
Akizungumzia na Spoti Xtra, Kocha Nabi alisema: “Ni kweli kukosekana kwa baadhi ya wachezaji wetu ambao wanatumikia adhabu na wenye majeraha ni miongoni mwa mambo ambayo kwa kiasi fulani yanatupa wakati mgumu kwa kuwa upo utofauti kati ya mchezaji mmoja na mwingine.
“Lakini licha ya changamoto hizo, kama kikosi hatuwezi kulalamikia hali hiyo, bali tunalazimika kutumia wachezaji waliopo kupata matokeo mazuri.” Mbali na Djuma ambaye anatumikia adhabu hiyo, nyota wengine wa kikosi hicho ni majeruhi akiwemo Kibwana Shomary, Yacouba Songne na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.
 
vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Yanga Yawaandalia Mikataba Minono Mwamnyeto,Yacouba.​

99.png

UONGOZI wa Yanga, umezima tetesi za kuondoka baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na kuweka mazingira ya kuwapa mikataba mirefu.
Chanzo cha ndani kutoka Yanga kimelitonya Championi Jumamosi kuwa: “Ndani ya Yanga hakuna atakayeondoka tena, kwa sababu inataka kujenga timu yenye kikosi kipana, wote ambao mikataba yao ipo ukingoni itaongezwa.”
Championi lilimtafuta Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabity Kandoro ili kujua ukweli wa taarifa hizi ambapo alisema: “Kwa kawaida timu inayotengeneza kikosi bora haiwezi kuacha mchezaji holela.
“Kwa sababu kwa kufanya hivyo inakuwa ni sawa na kurudi nyuma baada ya kwenda mbele, Yanga itawapa mikataba mipya wachezaji wote ambao mikataba yao ipo ukingoni, hakuna atakayeondoka.”
Baadhi ya wachezaji wa Yanga ambao mikataba yao inatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu ni nahodha Bakari Mwamnyeto, Kibwana Shomari, Saidi Ntibazonkiza, Yacouba Songne, Deus Kaseke na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Nabi: Tuliwazidi Mbeya City Kila Kitu.​

nabi-pic-data.jpg

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga, yenye pointi 36 ikiwa nafasi ya kwanza kwenye ligi kuu, amesema kuwa waliwazidi wapinzani wao Mbeya City walio na pointi 23 kwenye kila kitu ndani ya dakika 90, kasoro kuwafunga tu ndio walishindwa.
Juzi, Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 0-0 Mbeya City ambapo jitihada za Fiston Mayele mwenye mabao sita na pasi mbili kuweza kumtungua Deogratius Munishi, ziligonga mwamba.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Nabi alisema kuwa walikwenda uwanjani na mbinu tofauti za kusaka ushindi na walikuwa wakibadilika kila wakati lakini hawakupata matokeo.
“Ukizungumzia mchezo ambao tumecheza mbele ya Mbeya City, tuliweza kuwazidi kwenye kila kitu kasoro tulishindwa kuwafunga, hayo ni matokeo na huwezi kuyabadili kwa kuwa yametokea na wachezaji walipambana, wanastahili pongezi.
“Ukianzia nafasi ambazo tulitengeneza zilikuwa ni nyingi, uwezo wa kumwiliki mpira ulikuwa ni mkubwa lakini ambacho nilikiona ni kwamba kipindi cha kwanza tulikuwa tunapoteza mipira mingi hasa kwenye upande wa viungo.
“Hilo lipo na hainqa maana kwamba wachezaji wetu watakuwa bora muda wote, inatokea hivyo, tunakwenda kuyafanyia kazi makosa yetu ili kuweza kurudi tukiwa imara zaidi,” alisema Nabi.
 
Amir

Mgeni
Dec 10, 2021
736
12
5
tanzania

Mayele Mchezaji Bora wa Mwezi.​

mayele.jpg

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amechaguliwa mchezaji bora Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC mwezi Januari, 2022.
Kikao cha kamati ya Tuzo cha TFF kilichokutana mwishoni mwa wiki kilichokutana mwishoni mwa juma kimemchagua Mayele baada ya kuonyesha kiwango kizuri na kuisadia timu yake kupata ushindi katika mechi mbili.
Mayele anakuwa mcheaji wa tano kushinda tuzo hiyo akiwashinda Realiants Lusajo wa Namungo Fc, Tepsea Evans wa Azam Fc, alioingia nao fainali.
 
vuligate

Mgeni
Dec 17, 2021
395
3
5

Kabwili Yupo Zake Tabata FC.​

KABWILI.jpg

BAADA ya kutoonekana ndani ya kikosi cha Yanga kwa muda mrefu, golikipa Ramadhan Kabwili, ameonekana
akicheza fainali ya Kombe la Ng’ombe akiwa na Tabata FC.
Kabwili ambaye aliondoka kambini tangu Yanga ilipokuwa ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo uliochezwa Novemba 20, 2021, mpaka leo hajaonekana akiwa na kikosi hicho kinachonolewa
na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi.
Juzi Jumapili, Spoti Xtra lilimshuhudia kipa huyo akiwa kwenye kikosi cha Tabata FC ambacho kilicheza
mchezo wa fainali ya kombe la Ng’ombe dhidi ya Tabata Future kwenye Uwanja wa Tabata Shule uliopo Tabata jiji Dar.
Mchezo huo ulimalizika kwa Tabata FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuchukua zawadi ya ng’ombe huku Tabata
Future wakiambulia mbuzi wawili ambao ni zawadi ya mshindi wa pili.